Maaskofu Tanzania watoa Tamko, wakemea udini, ukanda na ukabila!

Mbona hizo takwimu ktk makanisa ya RC sijazisikia? Hapo ndo huwa nawapa big up RC
kanisa katolic na wengine walishinda kesi nyingi sana mahakamani kwa kuambiwa wali mtengeneza Yesu wa kubuni ili wadanganye dunia, jamaa wakaja na evidence.FBI na wengine wapo busy sana kufungua Library ya Siri ya kanisa.Pope naye ana kiona mbali cha kuangalia anga za juu(telescope). Makanisa yote yapo hivyo kwa mapana tofauti.
 
Kamanda Molemo, duu!! Pole sana kwa ban muda tumekumisi karibu tena jamvini...sikukuu njema.

Nakushukuru mkuu Ritz tuko pamoja sana.Ninashukuru Mungu tunakula sikukuu tukiwa pamoja jukwaani.Asante sana.
 
Last edited by a moderator:
Udini tayari upo wazi hakuna tena kujificha kama viongozi wa dini wameamua kuongea haya basi tena tujiandae na lolote litakalotokea.

mkuu ni ukweli kabisa ila tulaani kwa nguvu zote wanasiasa wanaotumia dini na ukanda kama mtaji wao kisiasa mkuu
 
Udini tayari upo wazi hakuna tena kujificha kama viongozi wa dini wameamua kuongea haya basi tena tujiandae na lolote litakalotokea.
Usiope mkuu.Tamko limekaa kisomi, kiweledi na limejaa upako wala usipate hofu.Tusubiri tamko la Maulamaa
 
Walisema kuwa watavumilia lakini uvumilivu unamwisho! Kama nchi inaongozwa na waislamu na bado waislamu wanalia kwamba ni mfumo Kristo, wanataka iwe dola ya Kiislamu ili waridhike? Maana mara zote madai ya waislamu kuhusu mfumo Kristo yanapotelewa serikali haijawahi kukanusha!
Unataka ikanushe kuwa hakuna MoU kati ya Serikali na Kanisa?! ikanushe kuwa NECTA haiwahujumu Waislamu? zaidi ya 75% ya wabunge ni Wakristo? zaidi ya 75% ya mawaziri ni Wakristo?!..
 
Ritz umepotea hilo halitokaa litokee maana hata kielimu bado waislamu wako nyuma sana fanya tafiti ndogo tuu utaona. mimi nashangawa kuona chuoni fulani cha nje kina wanafunzi wa masters kama 8, PhDs 10 na hata waajiriwa ila huwezi kumkuta muislamu na kama yupo basi ni mmoja tuu. Huku huwa wanauliza ivi Tz kuna waislamu maana huwa hawawaoni. Fungukeni msome na sio kulalamika kila kukicha
Mkuu Mingoi,
Inasikitisha sana kiongozi wa dini anahoji uwiano wa dini kwenye ofisi za serikali.

Nadhani itasaidia wizara zote ziwe na uwiano wa dini ili twende sawa.
 
ombi la kurejesha taasisi zilizochukuliwa na serikali kwa wenyewe litatusaidia, tutaheshimiana. MoU ivunjwe kama wanavyopendekeza hawa wakristo. labda tutagundua tofauti ya misaada ya tende, nyama ya ngamia, majambia na vifaa vya hospitali, shule, maabara n.k

Hahaa nimejizuia kucheka lakini imeshindika, haahaa duuuh kuna watu mnamaneno!
 
Unataka ikanushe kuwa hakuna MoU kati ya Serikali na Kanisa?! ikanushe kuwa NECTA haiwahujumu Waislamu? zaidi ya 75% ya wabunge ni Wakristo? zaidi ya 75% ya mawaziri ni Wakristo?!..

Ndo mana maaskofu wamesema warudishiwe hospt zao na shule zao, km serikali haitaki kurudisha basi iende kwa uma ikaeleze uzuri ma ubaya wa MoU
 
Kwanza Waislam hawaoni faida ya MoU bora ivunjwe kama anavyosema Askofu Shayo, mie nikiiugua natibiwa kwa pesa yangu.
 
Tamko Zito sana na lenye afya kwa Taifa.

Mkuu wangu Molemo,

Karibu sana. Naona Noeli umeila kutoka Robben Island. Kwa muda uliokuwa kifungoni, tulikosa busara na hekima zako. Hapa St. Peters pia Mhashamu Eusebius Nzigilwa anamalizia kutoa salamu zake za Noeli. Separately, nitaweka ujumbe wake kwa wakristu, lakini kwa Watanzania wote wenye mapenzi mema.
 
Ubaya umeuona baaMda ya Wakristo kuvumilia ma kuchoka?
Mimi binafsi ni mkiristo ila nimekerwa na namna jambo hili lilivyoibuliwa.Jambo hili lilishapoa kwa kiasi fulani na basi ingekuwa jambo zuri kuendeleza mazungumzo kuanzia hapo kulikoni kuanza kusutana hadharani hapa nina maana kwenye mahubiri kama walivyofanya.

Katika hali ya kawaida kwenda kuongelea jambo ambalo bado lina mgogoro kwa namna ya kulalamika tena ukiwa kiongozi badala ya kutumia mwanya wa utulivu uliopo kwa sasa ili kulimaliza maana yake nini ni kama sio kuchochea mgogoro.Wewe kama kiongozi ukilalama mbele ya watu wako unatarajia wao nao wafanye nini kama sio kuendeleza mgogoro.

Machafuko ya kidini jamani sio jambo dogo.Tukifika huko tutakimbiana wenye kwa wenyewe.Haya si mambo ya kushabikia tu kisa alieongea ni kiongozi wa dini yangu.Pima alichoongea kabla ya kumuunga mkono.Kiongozi wa kidini ni binadamu kama wewe kwahiyo anaweza kukosea.

Tukileta utatatibu wa wewe ukimwaga mboga,mimi namwaga ugali kwenye mambo ya dini hakika tutakuja juta vibaya.

Subirini muone nao kesho wakija na tamko lao na malalamiko lukuki.

Viongozi kaeni chini muongee matamko hayasaidii bali yanaongeza mvutano uliopo.
 
Ndo mana maaskofu wamesema warudishiwe hospt zao na shule zao, km serikali haitaki kurudisha basi iende kwa uma ikaeleze uzuri ma ubaya wa MoU

Siyo kuvunja tu MoU mnatakiwa kurudisha pesa yote toka mwaka 1991 mpaka 2013 hesabu zitapigwa. Hakuna mtu anayetibiwa bure kwenye hosptial za makanisa.
 
Wanapendekeza? kitu gani kinachowazuia kujitoa katika makubaliano?


Mkuu sadeeq

Rejea malumbano yetu ya wakati uleeee.

Kujitoa ni jukumu la serikali, mwenye nguvu ndiyo huamua makanisa yameshaamua, je serikali ipo teyari watu wake wateseke?

Kumbuka yawezekana wewe ukawa na uwezo, watanzania waliowengi sivo unavodhani, tukiacha ushabiki wa imani zetu yatupasa kuwaonea huruma wasio na uwezo maskin watanzania wenzetu. Serikali ikikurupuka kuzirejesha shule na mahospitali watakaoumia ni watanzania kaka, shida na maradhi haziangalii iman ya mtu.
 
Mkuu wangu Molemo,

Karibu sana. Naona Noeli umeila kutoka Robben Island. Kwa muda uliokuwa kifungoni, tulikosa busara na hekima zako. Hapa St. Peters pia Mhashamu Eusebius Nzigilwa anamalizia kutoa salamu zake za Noeli. Separately, nitaweka ujumbe wake kwa wakristu, lakini kwa Watanzania wote wenye mapenzi mema.

Nakushukuru sana Kamanda wangu SEBM.Usihofu mkuu kwani hata Mandela alifungwa kwa ajili ya kutetea wanyonge..Ha..Ha..Ha!
 
Last edited by a moderator:
Unataka ikanushe kuwa hakuna MoU kati ya Serikali na Kanisa?! ikanushe kuwa NECTA haiwahujumu Waislamu? zaidi ya 75% ya wabunge ni Wakristo? zaidi ya 75% ya mawaziri ni Wakristo?!..

Wakati mwingine akili ya kuzaliwa ni muhimu sana. Na haya ndio madhara ya kukataa shule. Kama asilimia 75% ya mawaziri ni wakristo, wamechaguliwa na maaskofu? Si huyu huyu Jakaya Mrisho kikwete amewachagua? Au nae mfumo Kristo? Kama wabunge 75% ni wakristo, kwanini nyie waislamu mnachagua wakristo wawaongoze? Huoni kama kuna tatizo? Au hao wamewekwa na mfumo Kristo? Kama ungetumia akili yako ya kawaida kabisa ungetambua kuwa kuna pange mbili kubwa za kidini hapa Tanzania yaani Wakristo na Waislam. Waislamu wanasema serikali inaendeshwa kwa mfumo Kristo, Wakriso wanasema udini unazidi. Sasa lazima sirikali itoe msimamo wake ama kwa kukanusha au kukubali malalamiko hayo toka kwa pande mbili na kutafuta suluhu ya kudumu katika kuleta umoja wa kitaifa.
 
Back
Top Bottom