Mwinjilisti Mkweli
Member
- Nov 21, 2023
- 10
- 24
Mbunge wa Jimbo la Kawe na mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Askofu Gwajima leo tarehe 22 Februari 2024 amekabidhi ambulance kwenye kituo cha afya Kawe Ukwamani Dar es Salaam.
Akikabidhi gari hiyo ikiwa ni utimizaji wa ahadi yake kwa wananchi wa Kawe, Askofu Gwajima amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh Dkt Samia Suluhu Hassan inalenga kukabiliana na matatizo mengi yanayosababishwa na kukosekana kwa miundombinu rafiki ya afya.
Aidha Askofu Gwajima amewasihi wananchi wa kata ya Kawe kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali kuwaletea maendeleo na kuboresha hali za maisha.
Askofu Gwajima ameongozana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.