Mhandisi 2009
Member
- Feb 5, 2011
- 22
- 4
adolay, JokaKuu,
Matatizo wa Waislam wa Somalia wala hayana uhusiano wowote na Uislam. Unaweza kuwa Muislam lakini kama haufuati mafundisho yake ni kazi bure.
Wasomali wameweka Uislam wao pembeni na kufuata mambo yao ya makabila na koo ndiyo maana unaona kila siku mauaji ya wenyewe kwa wenyewe, kila sehemu kuna kiongozi wa koo fulani kutoka kabila fulani mpaka ukafikia kabila fulani hawapati na kabila fulani. Wakati katika mafundisho ya Uislam hakuna kabila bora wala koo bora, mbora ni yule anayemcha Mwenyezi Mungu.
Hivi mauaji ya Rwanda yamesababishwa na Wakiristo? Mauaji ya Adolf Hitler, ya watu 12,000,000 mwaka 1939-1945 yana uhusiano na Ukiristo. Mauaji ya wa Congo 8,000,00 yaliyofanywa na Leopold II wa Belgium, yana uhusiano na Ukiristo? Mauaji ya Cambodia ya watu 1,700,000 yaliyofanywa na Pol Pot yana uhusiano na Ukiristo?
Huu ni mfano mdogo matatizo ya kibinadamu msitake kuyanasibisha na dini.
Umeongea point mkuu
Last edited by a moderator: