Maandamano ya wanafunzi St Johns University

CHRISTURKER

JF-Expert Member
Nov 24, 2012
266
54
Wanafunzi wapatao 5000 hivi wa chuo cha St John wanaandamana kutaka jeshi la polisi liwajibike kwa mauaji yanayoendelea kutokea ndani ya chuo yanayofanywa na vibaka na majambazi.

Ikumbukwe juzi jumatatu mwanachuo ameuawa kikatili na kuporwa simu,jana hosteli za akina dada zilivamiwa na laptops,simu na fedha kuibwa na wanafunzi kupigwa vibaya.Majambazi hayo ktk tukio la jana waliwabaka na kuwalawiti wanachuo kadhaa.

Maandamano ni makubwa sana,RPC kaingia kwa VICE Chancellor kwa mazungumzo,mbaya zaidi wanafunzi wanaelekea kituo cha polisi na kuna wasiwasi zikatokea vurugu kubwa na msuguano na polisi.
 
Nchi haitatawalika......haya yalikuwa maneno mazito lakini watawala hawakuyaona .........aliyesema alikuwa na nia njema wakampuuza.......
 
Hili suala la wanafunzi wa vyuo kufanyiwa haya mambo lipo muda mrefu naa taarifa zinatolewa polisi hazifanyiwi kazi mpaka waandamane.Nafikiri wakuu wa kipolisi wa mikoa yenye vyuo vingine waimarishe ulinzi kwa vyuo hivyo wasingoje mpaka wanafunzi waandamane.
 
Maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu cha st Johns yanaendelea kwa sasa bila ya kibali cha polisi.Sababu ni kukithiri kwa vitendo vya ubakaji na wizi wa mali za wanafunzi na kibaya zaidi ni polisi kuonekana kuzembea hali hiyo.Mkuu wa mkoa na RPC wazomewa na wanafunzi baada ya kuwasili maeneo ya chuo ili kuongea na wanafunzi
 
Polisi dodoma wanashughulikia mambo ya kisiasa, mambo ya usalama wa raia hayatiliwi mkazo
 
Waandamane mpaka kwenye medula zao sio mnaandamana leo kesho wanachagua nyinyiem ni ujinga wabadlishe mitazamo yao serkal ya ccm haiwezi kutatua matatzo yao mapinduzi daima
 
Hili suala la wanafunzi wa vyuo kufanyiwa haya mambo lipo muda mrefu naa taarifa zinatolewa polisi hazifanyiwi kazi mpaka waandamane.Nafikiri wakuu wa kipolisi wa mikoa yenye vyuo vingine waimarishe ulinzi kwa vyuo hivyo wasingoje mpaka wanafunzi waandamane.
Hii nchi ni kama haina jeshi la Polisi, mtapiga kelele, mtaandamana lakini kwa kuwa mkuu wa Jeshi anajiona ni SHEMEJI na sio IGP atakaa kimya bila kuchukua hatua. Jeshi la polisi limepoteza dira na mwelekeo, polisi wako busy na kukamata bodaboda na sio kulinda usalama wa raia na mali zao.
 
Sasa kwa nini wamewazomea, na wanaandamana kuelekea wapi kuwasilisha hayo madai yao? Mi nadhani ipo haja ya kutumia busara zaidi katika kuyapatia ufumbuzi hayo madai yao kuliko kutumia jazba ambazo mara nyingi huwa hazitoi ufumbuzi stahiki.
 
Bado kidogo vibaka wa Mwanza nao watagundua kuna deal kwa wanavyuo (laptops, simu na cameras); nafikiri publicity ina kanegative influence kwenye hili.
 
busara itumike kumaliza tatizo hilo,chuo kina private security,inatia shaka kwa vipi watu wasio husika na chuo waingie ndani ya chuo bila walinzi kufahamu,poleni sana wana chuo,lkn pia uchunguzi wa kina juu ya hili ufanyike haraka iwezekanavyo.
 
Nchi haitawaliki kabisa, Huku Arusha kuawanafunzi wa Lema nao wanataka kulianzisha, wanataka wapeelekwe kwenye shule zingine wakasome,
 
Polisi ni janga la Taifa.
Hawajui matumizi sahihi ya kutumia nguvu. Popote hutumia nguvu tuu.
bom.jpg
 
Inasikitisha kuona hali ya utendaji wa vyombo vya dola, haukidhi haja ya jamii. Jana taarifa ya habari ITV, ilishangaza kuona wananchi wameamua kufanya kazi ya dola, na kukamata wahamiaji haramu na kuwakabidhi kwa mkuu wa wilaya, naye bila hata aibu akaonesha kuahidi kushughulikia suala hilo wakati lina muda mrefu, kana kwamba amekumbushwa kitu kipya. Katika hali kama hii, nchi nyingine tungemwomba IGP, kwa kulinda heshima yake na heshima ya mkuu wa kaya, ajiuzuru.
 
Hii nchi ni kama haina jeshi la Polisi, mtapiga kelele, mtaandamana lakini kwa kuwa mkuu wa Jeshi anajiona ni SHEMEJI na sio IGP atakaa kimya bila kuchukua hatua. Jeshi la polisi limepoteza dira na mwelekeo, polisi wako busy na kukamata bodaboda na sio kulinda usalama wa raia na mali zao.

Tunahitaji kuzidisha maombi kwa Mungu wetu atunusuru na haya majanga
 
Nchi haitawaliki kabisa,
Huku Arusha kuawanafunzi wa Lema nao wanataka kulianzisha, wanataka
wapeelekwe kwenye shule zingine wakasome,

Nchi isitawalike kwa nini,? mbona Police wameshamkamata mtuhumiwa na yuko Rumande? Yani watu kwa kupenda vurugu na polisi bana! hadi kero!
 
wana st john angalieni vitu virukavyo vyenye ncha kali...vinaweza ruka mda wowote kuanzia sasa
 
Back
Top Bottom