Maandamano ya wanafunzi St Johns University

siku huyu rais ataondoka madarakani,tutashukuru sana,he has failed miserably in every aspect including running his own family.
 
Nchi yetu haina usalama kabisa, wa mipaka yetu na ndani ya nchi yetu, usalama wa raia, mali zao na hata rasilimali za nchi, nchi haina utaratibu kila mtu anafanya anvyoona inafaida kwake kwa wakati huo!Jambo la kuwavamia dada zetu na kuwabaka kisha kuwaibia halikubaliki kabisa! Lakini kinachokela zaidi Polisi wanapewa taarifa lakini hawafuatilii, na pamoja na MaRPC wanakosa umakini kabisa, kwa mfano baada ya kutokea IFM, je MaRPC wa mikoa mingine yenye vyuo vikuu wamechukua hatua gani kuahakikisha haya hayatokea kwao? Naamini hakuna, wangefanya hivyo yasingetokea DODOMA tena kwa muda mfupi kwa kujirudiarudia. Hapa ndipo tunapokosa imani nao, kwani kwenye mikutano ya siasa au mambo yanayofanana nayo wanafika kwa wingi tena kwa nguvu kubwa.Jambo lingine, kwenye nchi yenye utawala bora wenye kujali usalama wa Raia serikali ingehakikisha inatoa ulinzi wa kutosha, wanachofanya sasa wamaliki wa vyuo ni kuajili makampuni yenye sifa za chini kabisa ili kupunguza gharama, matokeo yake hakuna usalama!Tumesikia IFM, SAUT-MWANZA, DODOMA na bado tutaendelea kusikia kwa sababu tu viongozi wetu wamekosa au wamepungukiwa maarifa! Pole sana waathirika wa jambo hili kwa sasa!
 
tena nyie wanavyuo ndo mlikifanya hicho chama kiendelee kuwa madarakani,
mwaka 2015 achanani na hicho chama hakifai.
 
DA! me ni mwanajamvi mgeni jamani, ila kusema ukweli hili suala limenigusa coz kuna ndugu zangu wanasoma hapo St.John yan hapa naona akili yangu inaingia inatoka.
 
nani kawambieni vyombo vya ulinzi na usalama vya TZ vinalinda raia na mali zao? wao wanalinda maslahi ya watawala basiii!
 
Wanafunzi wa chuo kikuu cha st Johns hapa mkoani Dodoma leo wameandamana kupinga vitendo vilivyoshamiri vya wanafunzi kubakwa,kuibiwa mali zao na unyanyasaji mwingine unaofanywa na watu ambao ni vibakaba au wezi.Maandamano haya yanakuja ikiwa ni siku 3 tu zimepita tangu mwanafunzi mmoja abakwe na kuuwawa.Leo hii tena wanafunzi wengine wamevamiwa na hivyo kusababisha maandamano ya leo

RPC na mkuu wa mkoa walifika hapa chuoni ila hata hivyo waliishia kuzomewa na wanafunzi kwani wamekuwa hawachukui hatua zinazostahili tangu matukio ya awali yaliporipotiwa polisi.Kumukuwa na ahadi hewa za kujenga kituo cha polisi pamoja na kuimarisha ulinzi.Hata hivyo yote hayo yamekuwa ni siasa tu.
 
Hao watoto hawajapitia JKT. Ndio matokeo yake. Wanavunjwa bikra mchana kweupe na vibaka. Vibaka wasingejaribu wakati wetu. Tulipitia JKT, tukafundwa sawasawa.
 
Ni matokeonya kufanya kazi kwa propaganda. Serikali imeacha ukweli limekuwa jukwaa la uzushi na majungu na haya ndiyo matokeo.

Tulikuwa na Edward Moringe Sokoine, peke yake Tanzania ilitetemeka na aliweza kusimamia maelekezo yake vema na kwa ufanisi

Tukampata Augustine Lyatonga Mrema kama sokoine nchi ilitulia wezi, vibaka na wabakaji walitulia maana jamaa alifanya kazi

Leo hii, pamoja na maendeleo ya sayansi na technolojia, mambo ndiyo yanazidi kuharibika kila leo afazari ya jana.

Siasa safi imeporomoka imekuwa siasa chafu ya akina mwigulu, Nape na wasira majungu, uzushi na mipasho wala hawakemewi

Afya na elimu bora imekuwa kwa watu wachache wenyefedha na zaidi mafisadi, sehemu kubwa ya watanzania imebaki kutaabika

Usalama na haki kwa watanzania imebaki kwa wenyefedha na mafisadi, masikini, wakinamama, watoto na wanafunzi ni wahanga wa ubakaji na unyang'anyi.

Polisi imebaki kuwa kikundi cha wahuni wa kuitumikia ccm na mafisadi, wameacha misingi ya uwajibikaji kutoka katiba nasasa sio walinzi wa usalama wa raia na mali zao bali wamegeuka kuwa walinzi ccm na malengo yake ya kifisadi.

Katika yote hayo

Kikwete yupo madarakani anachokifanya anakijuwa yeye na inawezekana anafahamam vema malengo ya wahuni hawa.

1. makanisa yamechomwa tena mengi, rais amekaa kimya haiwezekana kwa idadi kubwa kiasi kile asifahamike mchomaji.

2. Askari wake wamemuuwa mwangosi, kikwete kashindwa kumuadhibu kamuhanda anataka ushahidi gani zaidi ya ule?

3. Mwanahalisi katoa habari za kiuchunguzi kuhusiana na mtesi wa Ulimboka, cha ajabu anafungiwa badala ya kumwita awasaidie.

4. Askari polisi wameuwa Songea, morogoro, Arusha nk, kikwete katia pamba masikioni na kuvaa miwani ya mbao

5. Polisi wamekwapuwa mamilioni Dsm, kova kakiri hatua zilizochukuliwa zipo kwenye mabano haijulikani nani kaadhibiwa

Kunamambo mengi sana yanayopingana na utawala bora na uwezo wa Kikwete katika kuiendesha nchi, matokeo yake wahuni

sasa wameingia hadi vyuoni sio wanaiba tu bali wanabaka na kuuwa wanafunzi tena sio chuo kimoja na wala sio mara moja ni

mara kadhaa.


Wenye hekima wanajiuliza

-waziri wa ulinzi yupo wapi?

-Said mwema yupo wapi?

-Kova na mbwembwe zake yupo wapi?

-Manumba yeye yuko ICU lakini alikuwa wapi siku zote?

Mwisho Rais yupo wapi kwanini hawawajibishi hawa watendaji wake kwa kushindwa kuwalinda watanzania? kwakukaa kimya

kikwete bila kuwaadhibu watendaji wake ndipo napata mashaka kwamba inawezekana akawa nyuma ya mpango mzima
.
 
Ingekuwa ni Chadema wanaandamana mapolisi wangesema inelijensia yao imewatahadharisha kwamba kuna uvunjifu wa amani,hivi hii intelijensia ya Kova na wengine ni kwa Chadema tu lakini si kwa wavunjaji wa sheria?
 
Nao wanaliwa kiboga kama wa IFM? Taifa litakuwa la mashoga hili
 
Wanafunzi wapatao 5000 hivi wa chuo cha St John wanaandamana kutaka jeshi la polisi liwajibike kwa mauaji yanayoendelea kutokea ndani ya chuo yanayofanywa na vibaka na majambazi.

Ikumbukwe juzi jumatatu mwanachuo ameuawa kikatili na kuporwa simu,jana hosteli za akina dada zilivamiwa na laptops,simu na fedha kuibwa na wanafunzi kupigwa vibaya.Majambazi hayo ktk tukio la jana waliwabaka na kuwalawiti wanachuo kadhaa.

Maandamano ni makubwa sana,RPC kaingia kwa VICE Chancellor kwa mazungumzo,mbaya zaidi wanafunzi wanaelekea kituo cha polisi na kuna wasiwasi zikatokea vurugu kubwa na msuguano na polisi.
Acha uongo, wanafunzi wote wa Chuo hicho hawazidi 4000, hata vyombo vya habari wameonesha breaking news wanafunzi walioandamana hawakufika robo ya wanafunzi hao 4000.
 
watuhumiwa ni hao polisi.

na si mtuhumiwa mmoja n watuhumiwa tujue kuwa wapo waliouwa na kumbaka Lydia Leo Mzima na wapo waliovamia hostel na kuiba laptop camera pesa na kubaka na kulawiti so hatuwezi kukubali et kuona kakamatwa mmoja kwani ni kundi la watu wanaofanya mambo haya
 
Serikali iwajibike kwa anafunzi wanaotendewa unyama

Tanzania haimlindi Raia bali beba panga rungu ujilinde mwenyewe hivi kwa Nchi zngne Hostel akama ya wanafunzi tena wakike basi inawekwa ulinzi tena sio na wagambo bali na polisi wenye silaha nchu Ya Tanzania Mtu Anabakwa Eti Kisha Ndo Analindwa Kama Jeshi Lingekuwa Na Akili basi baada ya kuwawa Mwanafunzi wangeweka Dolia kali sana hata hili lingne lisingetokea
 
Back
Top Bottom