Maandamano ya wanafunzi St Johns University

We unaonge pumba gani? Kuna nchi zenye police imara kama Marekani, Uingereza na nyinezo zilizoendelea! Lakini kiwango cha uhalifu kwa saa moja ndani ya Newyork kikoje? mauaji yakoje? inamaana nao hawawajibiki? Polisi hawezi kuwa kila mahala kwa kila tukio unless wawe wanapiga ramli! wahalifu nao ni wajanja! wa disclose information ni sisi raia wema sio kila kitu kitazuilika!
Wewe inaelekea ni Polisi unaficha udhaifu wako. Fuatilia vizuri ni matukio mangapi ya uhalifu huko New York kwako ambayo huwa yanapotezewa bila kufuatiliwa kama wanavyofanya polisi wa huku, then fuatilia ni polisi wangapi huko New York wanapokea rushwa, then fuatilia polisi wanaoshirikiana na wezi huko ndo uje uwasifie hawa polisi wenzako ambao ni irresponsible na lazy
 
Hili suala la wanafunzi wa vyuo kufanyiwa haya mambo lipo muda mrefu naa taarifa zinatolewa polisi hazifanyiwi kazi mpaka waandamane.Nafikiri wakuu wa kipolisi wa mikoa yenye vyuo vingine waimarishe ulinzi kwa vyuo hivyo wasingoje mpaka wanafunzi waandamane.

Je Chuo hakina walinzi? Je wanafunzi hawwawezi kujilinda wenyewe? Je Polis wanatosha kumlinda kila mwanafunzi? Je Polis jamii haijafika Vyuoni? TAFAKARI
 
Utashangaa watawapiga risasi
Ivi hawa polisi hawajui kuwa raia awakiamua hawatafua dafu maana idadi ya raia ni kubwa kuliko polisi sio kila wakati ni wakati wa kutumia nguvu
 
Kila kona maandamano, Mtwara, Pwani?!nk. naona haka ka msemo tz nchi ya amani kako ukingoni sasa.
 
Jazba haisaidii,busara inahitajika hapo kwa wanavyuo na polisi.kwakweli utendaji wa polisi unatakiwa umulikwe hali inavyokwenda sio sawa kabisa.
 
Nchi haitawaliki hata kidogo sasa!!! Siku haipiti bila kusikia vurugu za polisi na jamii au maandamano kwa ujumla!! Juzi mwanza, leo kibiti pwani, dodoma, na nina hakika kuna maeneo mengine protests zinaendelea ni vile tu hakuna taarifa!!! Serikali mu wapi? Hao nao ni CDM? Majuzi ilikuwa ni IFM? Na mabomu yalirushwa na virungu kama risasi vile bila hata kuangalia mazingira hatarishi ya karibu na bahari kuwa watu wanaweza hata kudondoka baharini kwa hofu. Shame on you!
 
Ni masikitiko makubwa sana Ndani Ya Chuo Cha St. John's University Of Tanzania Kilichopo Kikuyu Dodoma, Baada Ya Kuliuwawa Mwanafunzi Mtu Mzima Mmama Wa makamo anayefahamika kwa jina la LYDIA LEO MZIMA Usiku alipokuwa akitoka kujisomea alipgwa na kitu kizito na vibaka nyuma ya jengo la hostel ya chuo kisha kubakwa na baadaye fisi kumtafuna.

Wanafunzi wakiwa bado na simanzi na lawama kwenda kwa mkuu wa Chuo Bwana Mtetemela kwa kushindwa kulinda usalama wa wanafunzi na vitendo kama hivi si vigeni katika chuo hicho.

Tukio lingne ni usiku wa kuamkia alhamisi kundi la vibaka kuvamia hostel za wanawake na kuwabaka pamoja na kuwaibia, Wanafunzi wanaishi kwa mashaka ivyo kuamua kufanya maandamo kushnkiza Uongozi wa Chuo kuwatazama kwa macho mawili hata ivyo wakati wanafunzi wanatafuta suruhu Rais wa Chuo Hicho na Baraza Lake Wakawasaliti Na hatimaye kuvuliwa Uongozi wa Hao Waliomchagua; Wanafunzi Hao Wakiwa katika maandamano kuelekea Mjini Huku Nyuma Mkuu wa Mkoa Wa Dodoma Alifika Katika Chuo Hicho Na Kuongea Na Mkuu wa Chuo Hakijafahamika Kipi Kilichoongeleka.


Wanafunzi Wanabakwa Hawana Watetezi Jeshi La Polisi Lipo Kimya Kama Vile Halina Taarifa Hakuna Hatua Inayochukuliwa Juu Ya Wabakaji Na Vibaka Wanaowakosesha Amani Wanafunzi, Ikiwa Chuo Kina Walinzi Wagetini Vibaka Wanapitia wapi??? Au kazi Ya walinzi Hawa Ni Kufungulia Magari Geti??? Zipo Hostel Ambazo Zipo Nje Ya Chuo Na Wanaendelea Kubakwa nakuibiwa.

Serikali Haijali Raia Wake Laiti Ingekuwa Ni Mambo Ya Vyama Basi Mabomu Na Kuuwawa Watu Tungesikia Lakini Raia Wa Tz Hana Mtetezi Ni Vitendo Vya Aibu Sana Nani Wa Kumuokoa Raia Wa Tanzania??? Nani Wa Kumlinda????
 
hvi kubaka kuna mahusiano gani na kuiba jamani!
kwani si uniibie tu uniache na kubaka tena ili kiwe nini?
hii style imetoka wapi hii!
hao wezi wana kisasi gani na wanavyuo?
kuna nini hapa?
leo ST JOHN,juzi ilikuwa IFM kuna nini?
nini kinaendelea zaidi ya hiki?
vyuo vinapofumbia macho swala hl nini athar zake?
polisi wanapoona ni swala binfsi kuna nini?
nini kipo nyuma ya nini hapa SIELEWI!kusema ukweli!serious sielewi!
poleni sana wanachuo na wengine wote
 
2015 chagueni CHADEMA haya yote yataisha vijana wa kazi akina mnyika wakipewa uwaziri mambo ya ndani!
 
hvi kubaka kuna mahusiano gani na kuiba jamani!
kwani si uniibie tu uniache na kubaka tena ili kiwe nini?
hii style imetoka wapi hii!
hao wezi wana kisasi gani na wanavyuo?
kuna nini hapa?
leo ST JOHN,juzi ilikuwa IFM kuna nini?
nini kinaendelea zaidi ya hiki?
vyuo vinapofumbia macho swala hl nini athar zake?
polisi wanapoona ni swala binfsi kuna nini?
nini kipo nyuma ya nini hapa SIELEWI!kusema ukweli!serious sielewi!
poleni sana wanachuo na wengine wote
wanaoingoza hii nchi wanashughulikiwa na mapopobawa kila uchao. unategemea nini??
 
Wanafunzi wapatao 5000 hivi wa chuo cha St John wanaandamana kutaka jeshi la polisi liwajibike kwa mauaji yanayoendelea kutokea ndani ya chuo yanayofanywa na vibaka na majambazi.

Ikumbukwe juzi jumatatu mwanachuo ameuawa kikatili na kuporwa simu,jana hosteli za akina dada zilivamiwa na laptops,simu na fedha kuibwa na wanafunzi kupigwa vibaya.Majambazi hayo ktk tukio la jana waliwabaka na kuwalawiti wanachuo kadhaa.

Maandamano ni makubwa sana,RPC kaingia kwa VICE Chancellor kwa mazungumzo,mbaya zaidi wanafunzi wanaelekea kituo cha polisi na kuna wasiwasi zikatokea vurugu kubwa na msuguano na polisi.

hii ni dom nini maana sasa hivi ni migomo na mipolisi tu duu...

R I P mdada wa SJUT
 
Nchi yetu haina usalama kabisa, wa mipaka yetu na ndani ya nchi yetu, usalama wa raia, mali zao na hata rasilimali za nchi, nchi haina utaratibu kila mtu anafanya anvyoona inafaida kwake kwa wakati huo!

m
 
Back
Top Bottom