Maandamano nchi nzima, yanaweza kutatua kero zetu?

Sijaona uhusiano wa moja kwa moja kati ya maandamano unayotaka kuanzisha na matatizo uliyoyaorodhesha hapo chini. Je baada ya kuandamana hayo matatizo yatakuwa yamejitatua?
Atleast leo umeweza kushirikisha ubongo wako vizuri. Lakini tambua kwamba maandamano yoyote yana ujumbe mzito kwa serikali, ambapo inakuwa ni hatua ya serikali kuamua kuchukua hatua za haraka kutatua matatizo, au kukomaa na ubabe wake kutetea unyanyaswaji na udhalilishaji wa haki na utu wa mwanadamu, ambayo itakuwa ni dhalili mbaya kwa serikali, na dhalili mbaya sana kwa mkuu wa nchi.

Hatua itakayofuata itakuwa ni wananchi kwenda Ikulu moja kwa moja kwa maandamo kumkata kichwa mkulu.
 
Tukiandamana tukumtoa JK na Serikali yake, ni nani wa kushikilia japo kwa kipindi cha mpito?

Vinginevyo, hata Tunisia, Misri, Libya walianza na wazo la mtu mmoja mmoja!
 
je tulishiriki kwenye upigaji kura?

watu wengi hawakushiriki kupiga kura na wengine walipiga kura kwa wale waliowapa kanga na kofia na nadhani matatizo yote uliyoyataja yamesababishwa na watu hao niliowataje..........
 
WanaJF, twende taratibu. Kabla hatufikiria kutekeleza maoni ya mtoa hoja lazima kwanza tujiulizwe maswali haya:
1. Je, hayo yaliyoorodheshwa na MATATIZO yetu au ni MATOKEO tu yanayotokana na tatizo ambalo halijatajwa?
2. Kama ni matokeo, tusianzie juu kwenye matawi ya mti, kuangusha mti. Hapana, twende kwenye mzizi - Ndilo tatizo.
3. Lengo letu ni lipi? Tuwe more specific, tuseme tunaandamana halafu hili litafuata, na hili, lile.....
4. Strategy ni ipi...., tuandamane nchi nzima, wilaya tu, mkoa, kikanda au? Lazima tuje hapa na Strategic intervention ambayo ni clear, very SMART
5. Tuweke utaratibu wa kuongoza nchi... nani atakuwa nani, wapi,... lini.... kwa nini?
 
wasalaam wote,


napenda kuanzisha muamko wa maandamano sasa haya maneno hayatasaidia hata siku moja, maana wao wanamajibu wanayoyataka pindi wanapoulizwa maswali magumu, tuweke UDINI pembeni jamani, tuweke ubishi pembeni sasa.. naomba sasa tuanzishe makakati wa maandamano.. tuwe serios, hatuwezikuendelea kuishi hivi

· je unafurahia bei za bidhaa zinavopanda kiholela?
· Je unapenda unavopata shida mahospitalini ukienda (hospt a serikali)
· Je unaupenda usafiri wa daladala uliopo hapa sasa hivi huku watu wakifanay uhuni kwny UDA?
· Je unapenda kukaa makazi yasio bora tena kwa kupanga kwa bei kubwa huku nyumba za taifa (NHC) ziliwa zinaaiwa kwa wenypesa kubwa na ndugu wa viongozi
· Je unapenda bei za umeme na huduma mbovu zinazotolewa na mamlaka husika
· Je unapenda kutumia maju unayo nunua 800 dumu tena ya chumvi na machafu

  • je unapenda bunge linavoacha kushugulikia mambo yanayolihusu taifa na kumjadili JAIRO kwasbb tu ni rafiki wa kikwete
  • je unapenda unavolipa mamilioni kwa ajili ya ada ya mwanao wa chekechea kwashule za binafsi au kukosa elimu kabisa kwa shule za serikali
tafadhlini tuwekekila kitu pembeni sasa tuamke..sapoti post hii kama hupendi maisha unayoishi sasa

Kwanza naunga mkono hoja 1200%
Tumezidi kulalamika kama wanawake au wasichana walionyimwa mapenzi na waume zao.
sasa natoa rai ni marufuku kwa mwanaume rijali kulalamika bila kuchukua hatua madhubuti.
Tujaribu kuwapa majukumu watu ambao tunawaheshimu humu ndani ya Jamiiforum
ambao watatuongoza bila woga wowote na tukafikia malengo yetu.
Bila kuchagua watu wachache kama watano tuu ambao tuna uhakika wataunda
mkakati wa kuandamana ambao utaratibiwa kila mkoa bila kujali chama chochote
na tukafanikiwa sana.
Hatuhitaji unafiki kwenye jambo la maisha kama hili tunahitaji mtu ambaye anaijua
siasa ya Tanzania na anakubalika pande zote za vyama vya siasa na jamii kwa ujumla
Tunahitaji mtu ambaye si mkabila na mpenda nchi yake,ambaye atakubali kuifia nchi yake.

Kamati hii lazima waunde hoja za msingi ili zipate kuungwa mkono na taasisi zote za serekali
pamoja zisizo-serekali (NGOS)
.na watu mbalimbali wanoheshimika hapa Tanzania na nje ya nchi.
Nani wataweza hii kazi?????
 
Sijaona uhusiano wa moja kwa moja kati ya maandamano unayotaka kuanzisha na matatizo uliyoyaorodhesha hapo chini. Je baada ya kuandamana hayo matatizo yatakuwa yamejitatua?
Hayatapungua ila tutaiondoa serikali hii legelege madarakani
 
Nilikuwa najiandaa kuamini ulichoongea kwenye comment yangu lakini hii imefanya niendelee kuamini huna busara wala hekima.
Hata hapo pia nimeona umeshirikisha ubongo wako vizuri. Si kawaida yako kuzungumzia hekima na busara. Haya nimekurekebishia we si dadake MS.
 
mimi siandamani naogopa kuvunjwa kiuno au mguu! nani? atakaekuja kunilipia matibabu na chakula?

Watu kama ninyi mtakuwa wakusanyaji wa vyakula na maji pale tutakapoweka ngome ya maandamano katika viwanja vya mnazimmoja, dsm. Usiogope maana ulemavu wako utaleta heri kwa wanao wa sasa na kizazi kijacho.
 
Nina wasiwasi na huyu mwita25 anaeza akawa jk nikifananisha na majibu anayotoa akiulizwa maswali
 
STRATEGY:

1.Ku establish organising committee ya watu bold na strong katika kila mji mkuu wa Mkoa na Wilaya

2. Kazi mojawapo ya kamati hiyo ni kuandaa matangazo kwa kutumia media ambayo itawafikia wananchi wote kwa urahisi kwa mfano kutafuta gari la matangazo lenye uwezo mkubwa. Hii ni pamoja na kuandaa posters zenye ujumbe utakao mgusa kila atakayesoma na kumpa ujasiri wa kushiriki.

3. Kuandaa key figures za ku address wananchi na ku launch maandamano yatakayo malizika kwa mkutano mkubwa

4. Kutengeneza bajeti na kufanya fund raising kwa ajili ya maandalizi ya hayo maandamano
 
STRATEGY:
1.Ku establish organising committee ya watu bold na strong katika kila mji mkuu wa Mkoa na Wilaya
2. Kazi mojawapo ya kamati hiyo ni kuandaa matangazo kwa kutumia media ambayo itawafikia wananchi wote kwa urahisi kwa mfano kutafuta gari la matangazo lenye uwezo mkubwa. Hii ni pamoja na kuandaa posters zenye ujumbe utakao mgusa kila atakayesoma na kumpa ujasiri wa kushiriki.
3. Kuandaa key figures za ku address wananchi na ku launch maandamano yatakayo malizika kwa mkutano mkubwa
$. Kutengeneza bajeti na kufanya fund raising kwa ajili ya maandalizi ya hayo maandamano

Sisi wa-Tanzania ni waoga kama mbweha.
Tukitishwa kidogo tuu kila mtu anakimbilia uvunguni mwa kitanda.
Nani anaweza kusimama kuandaa maandamano hapa?au tutaishia kulalamika tuu siku zinaenda.
 
Haya matatizo yanaleta kichefuchefu, hata hivyo siungi mkono hoja hiyo mpaka mtoa hoja atoe majibu ya maswali yafuatayo :

1.Je maandamano ndo njia pekee iliyopo?

2.Kwa kuwa umependekeza maandamano, labda tuelimishane kwa mifano mchache ya nchi ambazo zimefanikiwa kupitia maandamano, sitarajii mfano wa Misri au nchi inayofanana na hiyo kwa kuwa huko hali si shwari kwa sasa.

MAONI YANGU
Maandamano yanaweza kuanzishwa kwa nia njema lakini yakatekwa na watu wenye AGENDA TOFAUTI na waandaaji wa maandamano, ikitokea bahati mbaya watu hao wakawa na financial na political power nchi imekwisha!!!.

WITO
Nakushauri ufanye homework ya ziada ya angalau kufikiri, uje na positive recommendations tukukumbuke nawe kama Mwl. Nyerere!!!! usicheke! unaweza kujijengea rekodi hivi hivi kwa kutumia siku moja kufikiri (critical thinking) kuwasaidia watanzania na watawala. AU UNATAKA KUTAWALA MWENYEWE?
 
Back
Top Bottom