Maandamano nchi nzima, yanaweza kutatua kero zetu?

Tuandamane

JF-Expert Member
Feb 2, 2008
1,220
52
Wasalaam wote,

Napenda kuanzisha muamko wa maandamano sasa haya maneno hayatasaidia hata siku moja, maana wao wanamajibu wanayoyataka pindi wanapoulizwa maswali magumu, tuweke UDINI pembeni jamani, tuweke ubishi pembeni sasa.. naomba sasa tuanzishe makakati wa maandamano.. tuwe serios, hatuwezikuendelea kuishi hivi

· je unafurahia bei za bidhaa zinavopanda kiholela?
· Je unapenda unavopata shida mahospitalini ukienda (hospt a serikali)
· Je unaupenda usafiri wa daladala uliopo hapa sasa hivi huku watu wakifanay uhuni kwny UDA?
· Je unapenda kukaa makazi yasio bora tena kwa kupanga kwa bei kubwa huku nyumba za taifa (NHC) ziliwa zinaaiwa kwa wenypesa kubwa na ndugu wa viongozi
· Je unapenda bei za umeme na huduma mbovu zinazotolewa na mamlaka husika
· Je unapenda kutumia maju unayo nunua 800 dumu tena ya chumvi na machafu

  • je unapenda bunge linavoacha kushugulikia mambo yanayolihusu taifa na kumjadili JAIRO kwasbb tu ni rafiki wa kikwete
  • je unapenda unavolipa mamilioni kwa ajili ya ada ya mwanao wa chekechea kwashule za binafsi au kukosa elimu kabisa kwa shule za serikali
Tafadhlini tuwekekila kitu pembeni sasa tuamke..sapoti post hii kama hupendi maisha unayoishi sasa

STRATEGY:

1.Ku establish organising committee ya watu bold na strong katika kila mji mkuu wa Mkoa na Wilaya

2. Kazi mojawapo ya kamati hiyo ni kuandaa matangazo kwa kutumia media ambayo itawafikia wananchi wote kwa urahisi kwa mfano kutafuta gari la matangazo lenye uwezo mkubwa. Hii ni pamoja na kuandaa posters zenye ujumbe utakao mgusa kila atakayesoma na kumpa ujasiri wa kushiriki.

3. Kuandaa key figures za ku address wananchi na ku launch maandamano yatakayo malizika kwa mkutano mkubwa

4. Kutengeneza bajeti na kufanya fund raising kwa ajili ya maandalizi ya hayo maandamano
 
Sipendi hata kimoja wapo. Mimi nipo tayari kwa maandamano siku yoyote wakati wowote nimeshoshwa na hii hali.
 
Sijaona uhusiano wa moja kwa moja kati ya maandamano unayotaka kuanzisha na matatizo uliyoyaorodhesha hapo chini. Je baada ya kuandamana hayo matatizo yatakuwa yamejitatua?
 
Sijaona uhusiano wa moja kwa moja kati ya maandamano unayotaka kuanzisha na matatizo uliyoyaorodhesha hapo chini. Je baada ya kuandamana hayo matatizo yatakuwa yamejitatua?

Ww masabuli tu, kaz kujilovekeza tu kwa wakubwa, jamaa ameorozesha mambo ya msingi kabisa harafu unataka kuleta upupu wako hapa, maandamano yata mtoa anayesababisha haya ambaye ni ccm kwa nguvu ya uma.
 
Nipo tayari kuunga mkono ila nifahamishe baada ya hayo maandamano tunategemea ku achieve nini? Hayo matatizo yataondokaje kwa maandamano? Naomba uhusiano wa hayo matatizo na kuto kuandamana ili nikuunge mkono.
 
Nipo tayari kuunga mkono ila nifahamishe baada ya hayo maandamano tunategemea ku achieve nini? Hayo matatizo yataondokaje kwa maandamano? Naomba uhusiano wa hayo matatizo na kuto kuandamana ili nikuunge mkono.
Hope ni Tz spring na si vinginevyo.
 
Mpwa sipendi hata moja kati ya hayo; sasa kwa pamoja tuweke strategy, mimi naomba kama kuna mtu anaweza kutengeneza strategy nzuri akaiweka hapa jamvini tukaweka mawazo ili kuiboresha na kisha kuitangaza kwa wananchi kwa ajili ya utekelezaji, asante kwa kuja na wazo zuri Mpwa kilio changu ndio hicho, eti hadi bei ya kitimoto imepanda? this is too much
 
tunaweza kuandamana hata mm niko tayari lakini je tunaowaandamania wakitoka madarakani nani wa kushika hatam ikiwa tulio waamini wamekomba posho zote mkuu? kwa ujumla tuliowaamini wameshindwa kusimamia walichokiamini
 
jamani lakini inawezekana tukiwa serious. Tunaweza ku demand rais aondoke kama hawezi kuwafilisi mafisadi akiwemo mwanae. Leteni mawazo how do we start mobilizing.

Kwanza tupate orodha kamili ya mafisadi na kiasi cha pesa kwenye akaunti zao na hata na mali zao tuziweke wazi.

Then ukichanganya na matatizo yaliyopo nchini tunaweza kushawishi jumuiya za kimataifa wasitishe misaada tz hadi clean govt itapopatikana.
Wenye data za ukweli kuhusu hawa corrupt leaders aweke hapa tuanze kuzi compile.

'Let's go Tanzanians, we can'
 
Sijaona uhusiano wa moja kwa moja kati ya maandamano unayotaka kuanzisha na matatizo uliyoyaorodhesha hapo chini. Je baada ya kuandamana hayo matatizo yatakuwa yamejitatua?
wewe ni sehemu ya matatzo, kwa hiyo hauwezi kuna maana ya maandamo.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom