Maandamano kupinga uuwaji wa polis Tanzania kufanyika Washington DC. Marekani

baajun

Senior Member
May 19, 2012
199
6
MAANDAMANO KUPINGA MAUWAJI YA KINYAMA YANAYO FANYWA NA JESHI LA POLISI TANZANIA KUFANYIKA WASHINGTON DC. MAREKANI


Mandamano ya kupinga mauwaji ya kinyama yanayofanywa na Jeshi la Polisi Nchini Tanzania, yatafanyika Washington DC. Baadhi ya waTanzania waishio Maryland, District of Columbia na Virginia (DMV), wamedhamiria kufanya maandamano kupinga kitendo cha Mauwaji dhidi ya raiya yanayofanywa na Jeshi la Polisi kwa raiya pinzani, na haswa kitendo cha hivi karibuni cha kumuua mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.


Tetesi hizo zinaendelea kubaini kwamba vitendo hivyo vyakinyama vilivyofanywa na serikali havitovumiliwa kamwe na wanaDiaspora waishio nje ya nch. Tarifa za maandamano hayo tutawaletea zaidi pindi maandalizi ya kikamilika zaidi kwa mwenye machungu ya vitendo hivyo mnaombwa kujumuika zaidi.

TAFADHARI KAMA UTAHUZURIA MAANDAMANO, NJOO NA PICHA YOYOTE INAYO HUSU MAUAJI NA VITENDO VYA KIKATILI VINAVYO FANYWA NA SERIKALI NA PLISI WA TANZANIA.

TEGA SIKIO.
View attachment 64295
 
Mtakuwa mumefanya jambo la mbolea sana maana tifu likianzia kwa wakubwa hawa viongozi wetu huufyata
Big up for sucha brilliant idea
 
Ni jambo zuri, tena JK akija Marekani/UK mumpokee na Mabango yenye ujumbe wa "Police Killers" This time muhakikishe JK anaichukia Marekani na UK, na aape kutokanyaga tena.
 
It is a good idea but such demonstration was to begin here in Tz extending abroad!
 
Tanzania ni yetu sote, tunapinga vikali kitendo cha ccm MAFISADI/WAUAJI kujimilikisha hii nchi kana kwamba wamerithishwa na wazazi wao. Wameshindwa kutatua matatizo ya ukosefu wa huduma muhimu za kijamii huku wao, familia zao na jamaa zao wakiishi maisha ya anasa utadhani wao tu ndo wanastahili kuishi. Hii inauma sana. Leo kimepatikana chama kingine ambacho kimeonyesha uwezo wa kuleta mabadiliko, wanaanza FITINA NA UHUNI WA KUZUIA MIKUTANO YA CHAMA HICHO KWA HILA HUKU WAKIUA WATU HOVYO.
Wakuu andamaneni kwa nguvu zote, tunaamini huo ni mchango muhimu mno kwa watanzania wenzenu tulioko huku nyumbani tunaonyanyasika na hii DHULUMA inayofanywa na hawa wezi wa rasilimali za nchi yetu Tanzania. Tuko pamoja wakuu.
 
Unaitwa Nani? Kuchanana? Tafuta kiwanja Kwazulu Natal watakupatia. Sera na jina lako vimekaa kisauz sana unajua. Makaburu walikuwa watawala Wasauz kwa nguvu ya Polisi kama CCM inavyofanya dawa ikawa kuchanana tu. Leo pana Uhuru pale. CCM haijawa tofauti na Makaburu kwa mwenendo ulipo hapa nchini leo. Mimi kwa kweli naunga mkono sera yako. Zipigwe tu. Tulikuwa tunawatia moyo wasauz huwezi kuua nyuki wote kwenye mzinga hata kwa mabomu. wengine watapona tu. Zipigwe hapa tuone kama watamaliza watanzania wote. Mara Mtu kauliwa Igunga, Mara mtu kakatwakatwa Mwanza, Mara Mtu kauliwa Arumeru, Mara Daktari katupwa msituni akiwa mahututi, Mara mtu kauliwa Morogoro, Mara Mwandishi kapigwa bomu Iringa. Hiki ni kichaa kama kilekile cha Makaburu, na hakuna kichaa anaelewa logic. Zipigwe tu. Amani imewachosha
 
nyie wenyewe wote huko mnaishi kimagendo, hao wamarikani watawasikiliza kweli. Msije mkakusanywa na kusafirishwa kwenye kontena tu.
 
Mkuu ni uuaji wa polisi, au uuaji wa raia unaofanywa na jeshi la polisi, iko ambiguous kidogo!!!! wazo zuri, jumuiya ya kimataifa ilione hili.
 
Veri guudi, tusaidieni wakuu wa huko maana hapa bongo tumezidi kudumaa!
 
nauli yakuja nakurudi ni sh ngapi ili na mimi nijiunge na nyie kwa sababu maandamano huku ni sawa na kuchezea kifo.
 
Watanzania sisi ni makondoo sana, mmeshindwa kuandamana kwenye nchi yenu, badala yake mnaandamana kwenye nchi za watu mkitegemea kuonewa huruma na hao wazungu ambao ni marafiki wa ccm. huu sio ufumbuzi.
 
Back
Top Bottom