Arusha: Wadau wa utalii waungana na Jeshi la Polisi kupinga ukatili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Chama cha Wanawake Mawakala wa Utalii Tanzania (TAWTO) kimeungana na Jeshi la Polisi kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia Mkoani Arusha kwa kukarabati Ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya mjini.

Akiongea mara baada ya ufunguzi wa ofisi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema kuwa endapo kutakuwa na Jamii kubwa iliyoathiriwa na vitendo vya ukatili itapelekea usalama kupungua huku akikipongeza chama hicho kwa kuonyesha njia ya kupinga vitendo vya ukatili katika jamii.
WhatsApp Image 2024-02-13 at 14.47.55_0cba597a.jpg

WhatsApp Image 2024-02-13 at 14.47.56_fcb54b4b.jpg
Mongellla ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau wengine wa maswala ya usalama kuungana na Jeshi la Polisi kupinga vitendo vya uhalifu huku akibainisha kuwa Mkoa huo ni kitovu cha utalii hapa nchini ambapo amesema vyombo vya ulinzi na wananchi wanaowajibu wa kuhakikisha Mkoa huo unakuwa shwari.

Kwa upande mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Mawakala Utalii Tanzania (TAWTO) Elizabeth Ayo amesema baada ya kusikia changamoto zinazolikabili dawati la jinsia na Watoto Wilaya ya Arusha waliona ni vyema kutatua changamoto hizo kwa kufanya uakarabati na kununua samani katika dawati hilo.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo Pamoja na kuwashukuru wadau hao kwa ukarabati walioufanya, amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi litahakikisha linakomesha vitendo vya ukatili katika Mkoa huo huku akiahidi kuwa kituo hicho kitaendelea kutumika vizuri na kuatatua changamoto za wahanga.

Awali akisoma taarifa fupi kabla ya uzinduzi wa Ofisi hiyo, Mkuu wa Dawati la jinsia na Watoto Wilaya ya Arusha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ursula Mosha ametaja baadhi ya changamoto zilizokuwa zinaikabili Ofisi hiyo ni pamoja na uchakavu wa paa, uchakavu wa Samani za Ofisi, uchakavu jengo kwa ujumla ambapo kupitia Chama hicho kimefanikisha kutatua changamoto hizo.
 
Back
Top Bottom