Android 00
JF-Expert Member
- May 23, 2013
- 774
- 221
Maalimu kashindwa kutmaka neno vunja muungano, kuna mbunge gani atakayethubutu?
Unajua baada ya hoja ya Seif ya serikali 3 kudadavuliwa hapa JF alijiona dhalili, sijui iliishia wapi.
Sasa wanataka mkataba. Nakuhakikishia siyo Maalim, Ahmed, Jusa au awaye atakayeweza kutamka hata jambo moja la huo mkataba.
Siri kubwa ya mkataba ni kutaka kujificha nyuma ya mgongo wa Tanganyika.
Maalimu amesema eti bidhaa za ZNZ zinatozwa ushuru zikiingia bara. Alichotaka ni kuwa ziingie ZNZ, SMZ ichukue kodi halafu ziingie bara kama zimetoka Tabora. Kwamba soko la Waarabu lisiwe na kodi huku bara.
Seif anafahamu kuwa soko la ZNZ ni Tanganyika, nje ya muungano ni maumivu.
Tena soko si la biashara, ni pamoja na ardhi. ajira n.k.
Hakuna taifa lolote duniani lililowabeba WZN wengi kama Tanganyika.
Hakuna taifa linaloajiri WZNZ kwa upendeleo kama Tanganyika
Hakuna taifa linalosemesha WZNZ bure kama Tanganyika
Hakuna taifa linalotoa nishati ya bure ZNZ kama Tanganyika.
Hakuna taifa linalogharamia ulinzi na usalama wa ZNZ kama Tanganyika
Ikifika hapo, wote wananywea in fact wanaufyata kutamka neno vunja muungano kama alivyoufyata Seif.
Tanganyika ni ya ajabu sana, tumewabeba hawa watu halafu tunawapa muda wa kucheza msewe mgongoni.
LET THEM GO! Period.
Tanganyika inanufaika na nini na serikali 3 ua mkataba na ZNZ!
Maalim Seif Sharif Hamad Mshirazi, bado unauma maneno tena sana. Toa neno mkataba katika hotuba zako weka neno vunja muungano! hapo tutakuelewa kinyume chake unakula matapisha yale yale.
Mwisho wa mkataba ni Chumbe, baada ya kuvuka hapo nidhamu na adabu mbele!
Sasa kama wewe ni msemaji wa serikali ya Tanganyika na ccm tunakuomba liambie jeshi lako unaloliita la muungano liondoke hapa ZnZ uone kitakachofata.
Usijinape kwakua unajua kuwa Waznz wamedhibiwa lkn Fanya utajua kama kweli waznz wanaihitaji Tanganyika au la. fyoo..ko ww