Maalim Seif: Nikipewa uenyekiti niko tayari kuhamia CCM

wasomi wa vyuo vya kata hawajui lugha. hawajui hypothetical questions na hypothetical answers.

ccm haiwezi kumpa hamad kuwa mwenyekiti kwahiyo hawezi kurudi ccm. vyuo vya kata vimeharibu ubongo wa vijana. kichwani wanachojua ni siasa tu. watu kama hawa hata rwanda tu hawawezi kupata kazi. kichwani ni watupu mno.
 
Mkuu humjui Maalim Seif wala mila za Kizanzibari na hivyo ni kazi bure kukuondosha katika mgando ulionao.

Haya bwana. Kwanza ni nchi yenu kwa hiyo hao wanasiasa wenu hawaniumizi kichwa sana. Maadam Maalim siyo kiongozi wa kitaifa (Tanzania) to me he is a non factor kwangu. Ilimradi wenye nchi yenu mmeridhika nae mie wala sina shida.
 
Hii naifananisha na mtu aliyekwisha chumbiwa akasema ''ukinitwanga ndoa tu nahamia kwako''. Yupo ccm tayari anasubiri ndoa kamili.nadhani kanogewa na madaraka!

nimeikubali hii mkuu. so maalim keshachumbiwa, mahari ishalipwa na sasa yupo yupo anasubiri ndoa arudi zake kimagamba. kwa mpemba kama yeye huu ni ujumbe muruwa kabisa, yakhe vp u tayari sasa tuite shehe ndoa ifungwe...? hata ya mkeka yafaaa tu yakhe, ubani upo hapa
 
Huyu Self kweli alikuwa anatafuta ulaji na nyie wanzanzibar nadhani hili mlione kwa makini,,,huyu tayari kawasahau wananchi kama alivyokuwa anajinadi,,,ama kweli njaa ni mbaya sana ila huyu njaa yake imezidi...
 
Kwa mujibu wa mahojiano yatakayorushwa Jumatatu na ITV, Maalimu Seif Sharif Hamad (Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar), amesema yuko tayari kujiunga na Chama Cha Mapinduzi, ikiwa tu atapewa nafasi ya Uenyekiti. Na kwa mujibu wake kwa sasa hakuna jambo la Msingi ambalo serikali ya CCM inafanya makosa. My take:Historia inajirudia mashaka yangu ipo siku chama kikuu cha upinzani bara, kitaanza kukiona CCM kizuri ilimradi tu kipewe nafasi serikalini
Mkuu, mbona umeamua kupotosha kwa makusudi nimekiona kipindi cha Dakika 45 ITV, Maalim Seif, baada ya kujibu swala la msingi alisema ni ndoto yeye kuondoka Cuf, hayo maneno yalikuwa ni jokes, punguza porojo au wewe ni Magamba nini
 
Siku zote Seif yupo kimaslahi zaidi, sijawahi muamini na siku zote msimamo wangu kuhusu yeye ni negative. Ishara za mwanzo ni pale alipokubaliwa kurudishiwa marupurupu yake kama Waziri Kiongozi Mstaafu, ni kuanzia pale msimamo wake ukawa wazi, hakuwa tena kelele.

Seif aliondoka CCM baada ya kukorofishana na magamba wenzake kwenye maslahi na sio kitu kingine, ndipo akakimbilia CUF alikokaribishwa vijana waanzilishi wakiwemo kina Msabaha. Amepata alichokuwa akikihangaikia miaka yote,a nacho ni maslahi yake, utukufu.

Kina Mangula waliuliza hivi serikali haiwezi mrudishia marupurupu yake, kwani walishabaini kuwa tatizo ni maslahi yake, wakakubaliana arudishiwe naye aliporudishiwa akalainika. Ikaja zamu ya JK, CCM wakathibitisha ulafi wa jamaa, wakamtengezea cheo, akakimbilia pasipo kuhoji, na kama ilivyoshuhudiwa baada ya kuapishwa tu akikimbilia DSM, kuwakoga kwamba sasa yeye ni Makamu wa Rais, ha ha ha!!!!

Huyo ndo Maalim Seif!
 
Back
Top Bottom