Maalim Seif: Nikipewa uenyekiti niko tayari kuhamia CCM

Kama ni kweli juu ya ulisemalo,kweli siasa ya tanzania inazidi kudidimia na pia tunaona hakuna changamoto zinazotolewa tena na baadhi ya vyama vya upinzani kwa sababu ya uchu wa vyeo na hili ndo linapelekea kuipa ccm nguvu yakuzidi kutawala,kitu ambacho mabadiliko katika taifa ili la watanganyika itakuwa ni ngumu,cz what we expect ni kwamba kama wangetoa political challenges against the ruling party tungetoa support yakutosha, hata hvyo we cant forfeit easly still we have hope CDM.
 
Hivi ndivyo siasa na (baadhi ya) wanasiasa wa TZ walivyo; wamo ulingoni kwa sababu ya maslahi binafsi tu. Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, ni wangapi walihama na kurudi na kuhama na kurudi CCM na vyama vyengine? Wanafuatia nini?
Mwanasiasa mwenye itikadi thabiti hawezi kuhama chama, kubwa analoweza kufanya ni kuunda chama chake lakini sio kuhama chama ambacho aliingia kwa hiari yake.

Kuhusu huyu "balahau", mimi nilianza kumuona si mtu wa maana pale alipowasaliti wenzake (akina Jumbe). Mkuki kwa nguruwe, yalipomgeukia akajidai yeye ni mkombozi wa Wazanzibari na kuhama CCM, leo yumo ndani ya mlo...kimyaaaaaa! Sitoshangaa kama kasema hivyo kwani mwenzake Mrema amepitia njia hiyo hiyo.

Nakumbuka "quotation" ya mwanasiasa mmoja (jina nimesahau): "Kwenye siasa ni bora uweko nje ukakojo.lea ndani, kuliko kuwemo ndani ukakojo.lea nje" , akiwa na maana huwezi kuwa mkombozi na mtetezi wa wenzako ukiwemo ndani ya mfumo. Seif ameingia katika kundi la hawa waliomo ndani wanaokojo.lea nje, wanawasaliti waumini wao.
 
Huyo ni wale wale cha muhimu zanzibar nao wadai uhuru wao tu sasa hivi maana hakuna chochote huko. maalimu seif anasema hivyo akijua kuwa uenyekiti hawezi kupewa ccm na kwa hiyo si rahisi yeye kwenda ccm. anayekiona ccm ni kizuri hata kama ni kiongozi wa upinzani sisi tunampiga chini na tunaendelea na harakati zetu. hatuwezi yumbishwa na viongozi wa roho wa pesa na madaraka.
 
Chadema alikuwa na haki ya kuikataa kafu kuwa nao bungeni .Viva Mbowe heko Chadema
 
Unategemea Katibu Mkuu wa Chama awe ameshiba Itikadi ya chama kiasi cha kutoweza kushawishika kuhamia chama kingine chenye itikadi tofauti kwa ahadi ya cheo tu. Labda atuambie itikadi ya CUF inafanana na ya CCM na kama hali ni hiyo, basi hakuna haja ya kuwa na vyama viwili(CCM na CUF)-kuwe na chama kimoja tu.

Kauli ya Hamad inaonyesha yuko CUF kwa sababu ya madaraka na sio itikadi, kitu ambacho sio kizuri kwa kiongozi wa chama kikubwa kama hicho. Halafu kesho watu wanashangaa wananchi wanapokipigia kura chama fulani kwa sababu wamepewa t-shirt , kofia, pombe na ubwabwa, wakati siasa za tumbo wamejufunza kwa viongozi wa vyama.
 
Usitake kupotosha watu Mkuu Moses maana hata sisi tumesikia.Alichosema Maalim Seif ni kuwa "walinambia kuwa sasa tuna Serikali ya Umoja wa Kitaifa, si urudi tu CCM?. Mimi niliwambia labda niwe Mwenyekiti" Au words to that effect.Sasa ho ni tofauti kabisa na unavyotaka watu waamini.Nadhani humjui Maalim Seif wewe.
ebu tupe undani wake we unaemjua vizuri!!ni kibaraka wa ccm ee?
 
mnaomponda seif hamjashirikisha brain zenu. Seif anajua kuwa hawezi kuwa mwenyekiti bila ya kuwa rais. Kwa maana nyingine alikuwa anasema atahamia ccm kama atakuwa mgombea urais
 
Usitake kupotosha watu Mkuu Moses maana hata sisi tumesikia.

Alichosema Maalim Seif ni kuwa "walinambia kuwa sasa tuna Serikali ya Umoja wa Kitaifa, si urudi tu CCM?. Mimi niliwambia labda niwe Mwenyekiti" Au words to that effect.
Na wewe huna hakika, usiweke quotes kama huna hakika, just hush!
 
Kwa mujibu wa mahojiano yatakayorushwa Jumatatu na ITV, Maalimu Seif Sharif Hamad (Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar), amesema yuko tayari kujiunga na Chama Cha Mapinduzi, ikiwa tu atapewa nafasi ya Uenyekiti. Na kwa mujibu wake kwa sasa hakuna jambo la Msingi ambalo serikali ya CCM inafanya makosa.

My take:
Historia inajirudia mashaka yangu ipo siku chama kikuu cha upinzani bara, kitaanza kukiona CCM kizuri ilimradi tu kipewe nafasi serikalini

Hii ni dharau kubwa sana kwa CCM na wana CCM wake.
Maalim Seif alikuwa CCM, alilelewa CCM na anaelewa taratibu za CCM.
Kwamba anweza "kupewa" Uenyekiti wa CCM maana yake hao watu waliomo wawe mazuzu na mapunguani.Kufikiria tu kuwa hilo linawezekana ni kipimo cha jinsi CCM inavyofikiriwa na wengine-kwa dharau.
 
Hata kwa ulivyo andika wewe bado ujumbe ni ule ule kuwa katamka kuwa anaweza kurudi CCM. Every man has his price and he just named his. Sasa wewe sijui unataka watu waelewe vipi.

Mkuu humjui Maalim Seif wala mila za Kizanzibari na hivyo ni kazi bure kukuondosha katika mgando ulionao.
 
Sikuwahi kumuamini huyu Seif hata siku 1, watu hasa wa cuf walikuwa wakielezwa kuhusu mtu ni nani wanakuwa wakali. Yale yote mambo ya muafaka yalikuwa ni harakati zake binafsi za kurejesha maslahi yake binafsi ambayo aliyapoteza baada ya kufukuzwa serikalini akiwa Waziri Kiongozi. Sasa keshayapata, na sasa wana cuf ndo wanaziona true colours za Seif. Too late, but we warned them. Mimi sishangai akirudi ccm hata leo kwakuwa ame-accomplish mission yake mwenyewe.
 
Hiyo ndiyo siasa na hao ndio wanasiasa wetu. Madaraka kwao ni muhumu zaidi kuliko kuwatumikia wananchi wao.
 
Cuf ni CCM B, ndo maana huku bara wamekwisha ghafla. Mimi sishangai yeye kurudi CCM A. Mbona sakaya juzi alipinga posho akitetea CCM A?
 
Back
Top Bottom