Maalim Seif Hamad apinga CUF kuungana na CHADEMA

Msimamo mzuri ndugu yangu Maalim Seif mpenda madaraka sema umeongea point za msingi chadema walikuwa hawapendi cuf na wanasema cuf ni chama cha zanzibar kwahiyo sio chama cha tanzania cuf imefunga ndoa na ccm matusi mingi sana leo mnataka support ya cuf?huyu Maalim Seif I used to like him before lakini nilikuja kugundua kama anapenda madaraka tu sio kama yupo kwa maslahi ya wazanzibar iwezekani miaka yote yeye tu ndie anataka kugombea Urais kama hakuna watu wengine tafakari
chaguo la wananchi ndio maana anagombania urais, sasa kama una masuala mengi kamuulize Queen Uwengereza ? Ambae anaitawala Uwengereza toka mababu na mabibi zake hadi leo anatawala ufalme wake, iweje maalim seif ? Mwache agombee urais bwana anakubalika kisiasa.
 
Huyo anaeandika upuuzi
huo ni muongo, viongozi wa cuf wanaunga mkono msimamo wa wabunge wake
kuungana na chadema, hata jussa juzi katika mkutano KAMPONGEZA TUNDU
LISSU.

mkuu, ulipaswa kusoma kwa makini uzi huu badala ya kukimbilia kuandika kitu usichokijua. Maalim Seif ametoa msimamo wake na wala si msimamo wa chama
 
OK! twende kwa hoja;kutokana na hoja zako mimi nina mashaka na uelewa wako na unachokiandika kama ifuatavyo;
1.Unasahau kuwa wabunge wamechaguliwa na wananchi ili kuwawakilisha na sio cuf, sasa katika jambo lolote linalogusa maslahi ya wananchi lililojadiliwa bungeni si la chama ni la wananchi na wabunge hao wanatekeleza majukumu waliotumwa na wananchi na si chama kwahiyo wa kuhoji ni wazanziibar waliowatuma sio maalim seef wala cuf kwa sababu katiba inayotengenezwa ni ya wananchi na si ya cuf.
2.Hoja yako ya pili haina mashiko na kama ni maalim seef amekutuma useme hivyo mwambie amelewa madaraka na anataka kuwasaliti wa zanzibar kwa sababu hoja si kwamba, hoja hiyo imetolewa na nani au chama gani, hoja ni kwamba hoja iliyotolea bungeni ina maslahi gani kwa wananchi(wazanzibar) kwa hiyo hoja za chadema zilikuwa na maslahi kwa uma ndo maana wabunge wote wa upinzani wakiwemo wa cuf waliwaunga mkono.
3.Kwa hoja ya tatu ndo aibu kabisa coz inshu ya katiba mpya inahitaji uwakilishi mpana, yeye anasema alishirikishwa eti kwa sababu yeye yumo ndani ya serikali sasa amesahau kuwa katiba haikuwa ni ya serikali ni yawananchi wote na serikali haikuwa na mamlaka kisheria ya kuingilia mchakato wa katiba mpya bali wananchi wote ndo walipaswa washiriki kama ilivyokuwa kwa upande wa bara.
4.Kwa hoja ya nne ni kwamba kama chadema imekuwa na kauli hasi dhidi ya hoja za wanzanzibar,je kwa hoja ambazo zinagusa maslahi ya wazanzibar zinazo tolewa na chadema na wabunge wote wa zanzibar wakaunga mkono kwa niaba ya wa zanzibar maalim seef anatoa wapi mamlaka ya kupinga? sasa alitaka wapinge maslahi ya wazanzibar? inamaana adui yako akitaka kukuokoa usiliwe na simba utakataa eti kwa sababu ni adui yako au utamshukuru kwa kuokoa uhai wako?
5.Kwa hoja ya tano, maalim seef anataka kusema sikuhizi katiba ya tanzania inakataza mtu au kikundi chochote kuwa na uhuru wakutoa maoni mpaka awe mwakilishi wa kundi fulani?eti anasema misimamo ya chadema dhidi ya waanzibar inajulikana mbona hakuitaja kama kweli anawapenda wazanzibar?
6.Kwa hoja ya sita,inshu ya katiba mpya na wafuasi wa kisiasa ni wapi na wapi? sasa maalim seef anataka kusema kama jambo ni la msingi kwa maslahi ya wazanzibar hata chadema isipoungana na cuf anataka kusema wazanzibar watakataa jambo jema kwao eti kwa sababu tu limeletwa na chadema na kuwaunga cuf ambao wataleta jambo ambalo halina maslahi kwa wazanzibar eti kwa sababu tu limeletwa na cuf?
NB.Wazanzibar tuwakatae viongozi kama maalim seef anaewaza maslahi yake pekee badala ya maslahi ya wazanzibar.
 
Aliyefukuzwa (kwa kutolewa
nje ya ukumbi wa bunge kwa amri ya kiti) ni KUB ambaye ni Mbowe -
Chadema! Vyama vingine vya upinzani vilifuata na kutoka nje kuonesha
kuungana mkono na Chadema; Sasa napata shaka moja wanaosema Chadema
inajipendekeza kwa CUF naombeni ufafanuzi nahisi nimepotea hapa.

Lakini pia nadhani Maalim angekuwa na point hasa kama angeitisha chombo
husika cha chama chake na kupitia chombo hicho wakaja na maelezo haya.
Lakini ikiwa mleta habari amepata habari ya uhakika ni wazi hapo hakuna
chama bali ni Maalim ndiye CUF na CUF ndiye maalim. Hii ni hatari sana
ni jambo ambalo limekuwa likinipa shaka sana juu ya umakini wa CUF kama
chama hasa inapokuja uchaguzi mkuu, kila uchaguzi mkuu tangu kuwepo kwa
CUF mgombea kwa upande wa Zanzibar ni Maalim sina hakika kwa bara kama
tangu wakati huo ni Lipumba.

Hii kwa wenye akili ya kawaida tu ina maana kwamba CUF haina mtu makini
yeyote zaidi ya Maalim!

Mwisho napenda kuamini kwamba Maalim ni mwoga tu anahofia kwa kete hii
ya katiba Chadema itaweza kusimamisha miguu yake sawia huko Zanzibar na
ndio unaweza kuwa mwisho wa CUF na 'kamuhogo' ka Maalim. Woga huu si
mbaya hata hivyo kwa mtu mwenye kujali maslahi binafsi kwa uwazi kama
Maalim

mkuu, katika ulimwengu wa sasa, jambo la uazi ni la muhimu sana. kwangu maalim seif simuoni kama mwoga bali ameeleza yale ya moyoni. na ukipitia uzi huu kwa umakini utagundua kuwa yale yaliyosema na maalim seif ni kweli tupu
 
OK! twende kwa hoja;kutokana
na hoja zako mimi nina mashaka na uelewa wako na unachokiandika kama
ifuatavyo;
1.Unasahau kuwa wabunge wamechaguliwa na wananchi ili kuwawakilisha
na sio cuf, sasa katika jambo lolote linalogusa maslahi ya wananchi
lililojadiliwa bungeni si la chama ni la wananchi na wabunge hao
wanatekeleza majukumu waliotumwa na wananchi na si chama kwahiyo wa
kuhoji ni wazanziibar waliowatuma sio maalim seef wala cuf kwa sababu
katiba inayotengenezwa ni ya wananchi na si ya cuf.
2.Hoja yako ya pili haina mashiko na kama ni maalim seef amekutuma
useme hivyo mwambie amelewa madaraka na anataka kuwasaliti wa zanzibar
kwa sababu hoja si kwamba, hoja hiyo imetolewa na nani au chama gani,
hoja ni kwamba hoja iliyotolea bungeni ina maslahi gani kwa
wananchi(wazanzibar) kwa hiyo hoja za chadema zilikuwa na maslahi kwa
uma ndo maana wabunge wote wa upinzani wakiwemo wa cuf waliwaunga mkono.
3.Kwa hoja ya tatu ndo aibu kabisa coz inshu ya katiba mpya
inahitaji uwakilishi mpana, yeye anasema alishirikishwa eti kwa sababu
yeye yumo ndani ya serikali sasa amesahau kuwa katiba haikuwa ni ya
serikali ni yawananchi wote na serikali haikuwa na mamlaka kisheria ya
kuingilia mchakato wa katiba mpya bali wananchi wote ndo walipaswa
washiriki kama ilivyokuwa kwa upande wa bara.
4.Kwa hoja ya nne ni kwamba kama chadema imekuwa na kauli hasi dhidi
ya hoja za wanzanzibar,je kwa hoja ambazo zinagusa maslahi ya
wazanzibar zinazo tolewa na chadema na wabunge wote wa zanzibar wakaunga
mkono kwa niaba ya wa zanzibar maalim seef anatoa wapi mamlaka ya
kupinga? sasa alitaka wapinge maslahi ya wazanzibar? inamaana adui yako
akitaka kukuokoa usiliwe na simba utakataa eti kwa sababu ni adui yako
au utamshukuru kwa kuokoa uhai wako?
5.Kwa hoja ya tano, maalim seef anataka kusema sikuhizi katiba ya
tanzania inakataza mtu au kikundi chochote kuwa na uhuru wakutoa maoni
mpaka awe mwakilishi wa kundi fulani?eti anasema misimamo ya chadema
dhidi ya waanzibar inajulikana mbona hakuitaja kama kweli anawapenda
wazanzibar?
6.Kwa hoja ya sita,inshu ya katiba mpya na wafuasi wa kisiasa ni
wapi na wapi? sasa maalim seef anataka kusema kama jambo ni la msingi
kwa maslahi ya wazanzibar hata chadema isipoungana na cuf anataka kusema
wazanzibar watakataa jambo jema kwao eti kwa sababu tu limeletwa na
chadema na kuwaunga cuf ambao wataleta jambo ambalo halina maslahi kwa
wazanzibar eti kwa sababu tu limeletwa na cuf?
NB.Wazanzibar tuwakatae viongozi kama maalim seef anaewaza maslahi yake
pekee badala ya maslahi ya wazanzibar.

mkuu, kama umetumwa sawa, ila kama ni muono wako hakika wewe hujui kabisa siasa za Zanzibar. Maalim Seif ni Mtu makini sana na ameshika nafasi mbalimbali zanzibar. kule zanzibar vyama vya siasa vinavuta hisia kubwa kuliko serikali kwa vile vina historia ndefu.
 
Sasa ngoma imeingia patamu. Sijui CHADEMA watakuja na lipi la kutueleza

Anayetaka kumfahamu maalimu Sefu amwulize Mapalala. Huyu ni mdini anayetaka kumbagua Itatiro. Halafu wakiambiwa CUF ni chama cha Zanzibar wanabisha.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Anayetaka kumfahamu
maalimu Sefu amwulize Mapalala. Huyu ni mdini anayetaka kumbagua
Itatiro. Halafu wakiambiwa CUF ni chama cha Zanzibar wanabisha.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Mkuu, hilo suala la udini ni tatizo la vyama vya cuf na chadema. ndo maana kule chadema zitto kabwe ananyanyasika sana kwa sababu ya uislam wake
 
image.jpg Kweli ulipoandika ni sahihi.....na hapa walikuwa wanafanya nini leo? Hotel ya courtyard ? Tamko umelisoma ....
 
[*]Kwa muda mrefu, CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli za kuudhi dhidi ya CUF na viongozi wake hasa wale wanaotoka Zanzibar kama vile CUF ni CCM B, CUF ni chama cha Kiliberali ambacho kinasupport ndoa ya jinsia moja na CUF imeolewa na CCM. Kwa kauli hizo, hakika muungano unaosema hasa na CHADEMA si wa kweli bali ni wa maslahi ya upande mmoja.
[
Kwa uzoefu wangu naamini Seif hawezi kuongea hivyo,umemlisha maneno
 
Msimamo mzuri ndugu yangu Maalim Seif mpenda madaraka sema umeongea point za msingi chadema walikuwa hawapendi cuf na wanasema cuf ni chama cha zanzibar kwahiyo sio chama cha tanzania cuf imefunga ndoa na ccm matusi mingi sana leo mnataka support ya cuf?huyu Maalim Seif I used to like him before lakini nilikuja kugundua kama anapenda madaraka tu sio kama yupo kwa maslahi ya wazanzibar iwezekani miaka yote yeye tu ndie anataka kugombea Urais kama hakuna watu wengine tafakari

hapo umenena ndugu
 
[*]Kwa
muda mrefu, CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli za kuudhi dhidi ya CUF na
viongozi wake hasa wale wanaotoka Zanzibar kama vile CUF ni CCM B, CUF
ni chama cha Kiliberali ambacho kinasupport ndoa ya jinsia moja na CUF
imeolewa na CCM. Kwa kauli hizo, hakika muungano unaosema hasa na
CHADEMA si wa kweli bali ni wa maslahi ya upande mmoja.

[
Kwa uzoefu wangu naamini Seif hawezi kuongea hivyo,umemlisha
maneno

mkuu, wengi tuliposoma uzi huu tulijawa na mshangao. hata hivyo tumeamini kuwa ni kweli maalim kaongea hayo na hata kama hakuwahi kutamka hayo kabla, basi katamka leo
 
Sasa ngoma imeingia patamu. Sijui CHADEMA watakuja na lipi la kutueleza

Binafsi naamini CUF wanaihitaji zaidi CDM kuliko CDM inavyoihitaji CUF, hofu ya Maalimu Seif hapa sio hicho alichokieleza, nadhani hofu yake ipo hivi, kama CDM ikiingia hadi Zenji then CUF na yeye binafsi ndio basi tena, so hapo issue ni maslahi zaidi na sio hicho kilichosemwa naye.
 
"Waliopo madarakani tumewachoka na hatuwataki, na mnaotaka kuingia madarakani hatuwaamini!" Nchi ya majuha hii, hivi wapinzani msipoungana mtawezaje ing'oa ccm wehu wakubwa nyie! Ndio maana wenzenu ktk salamu zao wanasema mapinduzi daima! mtapinduliwa hadi kiama, mazuzu nyie!!!
 
Huyo Maalim Seif kachoka akae pembeni,hicho kiinua mgongo chake asiwe na shaka ataendelea kupata kwa sheria za sasa.
Hapa kinachoangaliwa ni maslahi ya vizazi vijavyo na sio yeye aliyejiishia na hakati jamaa.
 
hii kali inaonekana aliyeanzisha uzi alikuwa ana timu iko tayari kuchangia kwa namna anavyotaka maana michango imeporomoka kila dakika mara baada ya uzi kuanzishwa!

nashawishika kuamini kuwa muanzisha uzi na wenzake wameshtushwa na ushirikiano walionesha Chadema CUF na NCCR kwa jambo ambalo ni muhimu!
 
Nimepata kushauri kwamba CUF ishirikiane na CHADEMA kuondoa Chama cha Mafisadi madarakani: Katika mpangilio huo, Lipumba angegombea Ubunge Tabora badala ya kuendelea na taaluma yake ya kugombea u-Rais. Tukishinda angekuwa Spika. Maalim angekuwa Naibu Waziri Mkuu wa JMT.

Kama pendekezo sasa ni CHADEMA na CUF kuungana na kuwa chama kimoja, mambo yatanoga zaidi kwa vile muungano huo utashinda. Hata kama CCM itaendelea kuongoza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, itawezekana kuendelea kushirikiana na Serikali ya Muungano kama ilivyo sasa.
Mzee Mtei , wazo la Chadema kushirikiana na CUF ni butu na halina tija wala mashiko.

1. CUF ni chama kilichopoteza maana halisi ya chama cha kisiasa. Hakuna anayeweza kueleza msimamo wa CUF kimebaki kuwa chama cha personality zaidi ya wanachama
a) Msimamo wa CUF kuhusu mchakato wa katiba nadhani unaufahamu. Waliofikisha rasimu yao hata bila kujua nini maana ya mchakato ni akina Mtatiro wala siyo Lipumba au Seif. Ni kundi la watu kila mtu na lake.

b)Wakati maalim Seif anakataa ushirikiano wa CUF na CDM, ni maalimu huyo huyo ana ushirikiano na kamati ya maridhiano, BAKAZA na Uamsho. Msimamo wake kwenye muungano ni mkataba tofauti na chama chake.
Leo anapata wapi ushujaa wa kusema wapo viongozi wa CUF waliofanya mashauri kinyume na taratibu za chama!!!

c)Kamati ya maridhiano ya akina Jusa pamoja na BAKAZA ya Profesa Shariff zinasema znz haikushirikishwa katika marekebisho ya mswada, Seif anasema wao walishirikishwa kama GNU. Sasa hapa Maalim anasimamia nini, msimamo wa GNU au wabunge wake waliotoka ndani ya Bunge au kamati anazohusiana nazo.

d) Wakati Chadema wakiwa katika maziko kule Arusha, CUF waliomba nafasi rasmi ya upinzani.
Tunafahamu ndoa ya CCM na CUF na kwamba CUF haina uaminifu linapokuja suala la ndoa.

Kama amekorofishana na mwenzi wake CCM sijui CDM wanajiridhisha vipi kuwa wanaweza kupanga nyumba moja. Kumbuka CCM wamewapa kila ushirikiano lakini CUF wanaingia wanachomoa.
CDM inatafuta nini kama si kujiletea balaa!!

CDM iliwahi kufanya makosa ya mchakato kuanzia mwanzo. Nilidhani wangejifunza kutokana na makosa hayo. Nafasi ya CDM kuishtaki CCM mbele ya umma ipo wazi na wanaweza kufanya hivyo bila CUF.
Jambo muhimu ni kuwa na ujumbe mahususi na utolewe kwa watu kwa njia muafaka ukifika kila kona ya nchi.

Hili wazo la kushirikiana na CUF chama ambacho kinamtegemea mtu mmoja hata mwenyekiti akiwa hana kauli ni hatari sana. Hakuna shaka maoni ya Seif yanaonyesha mpasuko wa kukimaliza chama kabisa.
Kwanini CDM idhani kuwa inaihitaji CUF iliyosambaratika na isiyo na uelekeo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom