Maalim Seif Hamad apinga CUF kuungana na CHADEMA

Wadau,

Taarifa za kuaminika nilizopata kutoka chanzo cha kuaminika huko Zanzibar zinasema kuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amepinga kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama hicho kuingia makubaliano na CHADEMA ili kupinga muswada wa katiba mpya. Maalim Seif amenukuliwa akisema mbele ya baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa uamuzi huo si wa kichama bali ni msimamo wa baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao wamepewa fedha na CHADEMA ili wawe na msimamo wa aina moja. Maalim Seif anasema kuwa wanaoratibu mpango huo ni Naibu Katibu Mkuu, Julius Mtatiro kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge wa chama hicho kutoka Zanzibar. Taarifa zinasema kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Ibrahim Lipumba inaelekea kuwa ameingia kucheza ngoma ambayo haijui na matokeo yake anaonekana kupoteza mwelekeo na kukosa msimamo. Hoja zilizoainishwa na Maalim Seif za kupinga makubaliano hayo ni hizi zifuatazo;

  1. Hakuna kikao chochote cha chombo chochote cha kiutendaji na kimaamuzi cha CUF kilichoketi iwe Zanzibar au Tanzania Bara kujadili jambo hilo na kuweka msimamo wa chama.
  2. Maoni yaliyotolewa na Kambi Rasmi ya Upinzani juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba hayakuwa maoni ya vyama vyote vya upinzani bali yalikuwa ni maoni ya CHADEMA pekee waliyoandaa kwa muktadha wa kujipatia umaarufu Zanzibar
  3. CUF ni moja ya vyama vinavyounda serikali ya umoja wa Kitaifa Zanzibar. Kutokana na ukweli kuwa Serikali hiyo imeshirikishwa na yeye (Maalim Seif) ameshiriki katika kuboresha Muswada huo anaamini kuwa chama hicho kupitia Serikali ya Umoja wa kitaifa ambayo imepewa baraka na Wazanzibari wote kimeshiriki kutoa maoni yake. Hivyo madai kuwa Wazanzibari hawajashirikishwa si ya kweli na ni upotoshwaji mkubwa
  4. Misimamo ya viongozi wa CHADEMA dhidi ya Zanzibar mara zote imekuwa hasi na kwa hali hiyo hali iliyojitokeza ya viongozi wa chama hicho kujipendekeza kwa Wazanzibari imetafsiriwa kuwa ni ulaghai wa kisiasa.
  5. Zanzibar ina viongozi ambao ndio waliopewa dhamana ya kuwasemea Wazanzibari na si mtu mwingine ambaye misimamo yake dhidi ya Wazanzibari inajulikana
  6. Kwa muda mrefu, CHADEMA wamekuwa wakitoa kauli za kuudhi dhidi ya CUF na viongozi wake hasa wale wanaotoka Zanzibar kama vile CUF ni CCM B, CUF ni chama cha Kiliberali ambacho kinasupport ndoa ya jinsia moja na CUF imeolewa na CCM. Kwa kauli hizo, hakika muungano unaosema hasa na CHADEMA si wa kweli bali ni wa maslahi ya upande mmoja.
  7. CHADEMA wanataka kuitumia CUF kama daraja ili kujipatia wafuasi Zanzibar. hii ni kutokana na CHADEMA kuendelea kupoteza mvuto visiwani humo hasa kutokana na viongozi wakuu wa chama hicho kuwa na chuki binafsi dhidi ya Zanzibar. Aibu aliyopata Katibu Mkuu wa CHADEMA alipofanya ziara visiwani humo imechochea viongozi wa chama hicho kuona haja ya kuungana na CUF

Kutokana na hali hiyo, Maalim Seif ametoa msimamo ufuatao ambao anategemea kuuwasilisha kwenye vikao halali vya kiutendaji vya CUF na ambao amesema unaungwa mkono na viongozi wengi wa chama hicho;

  1. Yeye kama katibu Mkuu na mtu anayekubalika na kutumainiwa na Wazanzibari wengi hatashiriki kikao chochote na CHADEMA kujadili jinsi ya kukwamisha mchakato wa Katiba
  2. Yeye kama Katibu Mkuu hatashiriki ziara iliyotangazwa na CHADEMA ya kuzunguka nchi nzima kwa kile kinachodaiwa kuishtaki serikali ya ccm kwa wananchi
  3. CHADEMA wameonywa kutojipendekeza kwa CUF na wamekumbushwa msimamo wao kuwa CHADEMA KITASIMAMA KWA MIGUU YAKE YOYOTE NA HAKIHITAJI MSHIRIKA YEYOTE KATIKA JAMBO LOLOTE

Nawasilisha

Nmesoma heading, nikaingia kusoma habari jinsi ilivyokaa kimajungu.ikabidi niangalie nan muanzilishi nilivyoona jina la Muhusika nikajua alaaa, kumbe ndo maana
 
Back
Top Bottom