Maalim Seif amvaa IGP

Maalim seif ana akili sana..ni kweli kama katibu mkuu lazima aweke angalizo kwa haya yanayoendelea
 
Maalim seif anajua sana huyu jamaa ni Genius, kesho tutaingia pale Buguruni kwa mbwembwe kabisa
 
Si kuna mzenji kaenda kwa IGP kuomba escort ya kwenda ofisini kwake Tanganyika bila kujua kwamba IGP ana nakala ya Msajili. Anajitambuaje sasa huyu! Si aende mwenyewe ofisini kwake.

Huyo mzenji ambae kaenda kwa IGP hekima ndio imemtuma kwenda huko ili kuweka akiba ya maneno.

Anajua fika IGP hana moja ambalo anaweza kumsaidia.

Hekima ndio ya mzenji huyu ndio inayompa kiburi lipumba na sikwamba ameshindikana kutoka ofisi za CUF buguruni.
 
Huyo mzenji ambae kaenda kwa IGP hekima ndio imemtuma kwenda huko ili kuweka akiba ya maneno.

Anajua fika IGP hana moja ambalo anaweza kumsaidia.

Hekima ndio ya mzenji huyu ndio inayompa kiburi lipumba na sikwamba ameshindikana kutoka ofisi za CUF buguruni.
LIPUMBA hatoki na ndio mwenyekiti halali kwa mujibu wa katiba na ana muda wa miaka mitatu kutoka sasa
 
Huyo mzenji ambae kaenda kwa IGP hekima ndio imemtuma kwenda huko ili kuweka akiba ya maneno.

Anajua fika IGP hana moja ambalo anaweza kumsaidia.

Hekima ndio ya mzenji huyu ndio inayompa kiburi lipumba na sikwamba ameshindikana kutoka ofisi za CUF buguruni.
Alipotoka kwa IGP ikawaje sasa?
 
Seif shariff Hamad Alitakiwa aende peke yake kama katibu mkuu akiwa amebeba makbrasha ya taarifa kumpelekea mheshimiwa mwenyekiti wa CUF taifa mheshimiwa Lipumba.Sasa yeye anasema atakwenda na baraza kuu zima,wabunge,madiwani,wana CUF!!! ebo.Yeye na hilo kundi lake ndio wanaenda leta vurugu kwenye ofisi ya mheshimiwa mwenyekiti wa CUF.Kama kamwita Seif katibu mkuu ofisini hao wengine kinachowapeleka ofisi ya buguruni ni nini? Si wanataka kumfanyia vurugu tu mheshimiwa mwenyekiti wao? Polisi inabidi wamsaidie Lipumba DHIDI YA HILI GENGE LINALOTAKA KWENDA KUFANYA VURUGU BUGURUNI.
Uchonganishi kutoka lumumba
 
NEW....
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ametua ofisini kwa kiongozi mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, ili kumueleza mkakati wake wa kutua ofisini kwake, Buguruni jijini Dar es Salaam.
Maalim anakwenda kwa IGP Mangu kumueleza adhima yake ya kufika ofisi kuu ya chama chake kesho Ijumaa, majira ya saa mbili asubuhi.
Hatua ya Maalim kutinga ofisini kwa IGP imetokana na kitendo cha jeshi la polisi kumsindikiza Prof. Lipumba kurejea ofisini; kusaidia uharibifu wa mali na kushambulia wanachama na wafuasi wa chama hicho.
Azma yake ya kwenda ofisini kwake kesho, inatokana na ofisi hiyo kuvamiwa na aliyepata kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba na genge la wafuasi wake.
Prof. Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti wa CUF, 6 Agosti mwaka jana na miezi 11 baadaye akatangaza kurejea katika nafasi yake, amefukuzwa rasmi uanachama wa chama hicho Jumanne iliyopita na Baraza Kuu la uongozi la Taifa (BKT), lililokutana Visiwani.
Hata hivyo, Prof. Lipumba, ameendelea kung’ang’ania kuwa bado mwenyekiti halali wa chama hicho na msimamo wake huo, unadaiwa kuungwa mkono na msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa watu waliokaribu na Maalim Seif zinasema, kiongozi huyo amekwenda kwa IGP Mangu kumtaarifu kuwa yeye na wabunge wa chama hicho, wamepanga kufika Buguruni kwa pamoja.
Anasema, “Maalim Seif anakwenda kumweleza IGP Mangu kwamba, tayari kumekuwepo na viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na watu wa Prof. Lipumba na kwamba chochote kitakachotokea, yeye na jeshi lake, wanapaswa kubeba msalaba.”
Prof. Lipumba alijiuzulu uenyekiti karibu na uchaguzi mkuu mwaka jana, akakimbilia nje ya nchi huku akidai hakufurahishwa na Edward Lowassa kuwa mgombea urais chini ya mwavuli wa vyama vinne ikiwamo CUF.
Ukawa unaundwa na vyama vinne; Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na National League for Democrats (NLD).
Hii ni mara ya pili tangu mfumo wa vyama vingi urejee nchini, kukumbwa na “mbegu mbaya” ndani yake.
Mara ya kwanza ilikuwa pale Augustine Mrema, akiwa mwenyekiti, alipojiapiza kufukuza wanachama thabiti ndani ya NCCR-Mageuzi. Alishindwa. Alifukuzwa mwenyewe.
Chanzo: Mwanahalisi
 
kichwa cha habari kinaonyesha ameshaenda kwa IGP, ukisoma ndani unaona kuwa ataenda kwa IGP ijumaa!! hata ss wasomaji tumekuwa dili?
 
Kuna kitu sijakielewa,Lipumba na wafuasi wake akisindikizwa na askari walienda kwenye mkutano ambao hawakualikwa fujo ikatokea hakuna hatua waliyochukuliwa,wafuasi wake wameandamana mpaka ofisi za buguruni wakati ikitolewa taarifa ya zuio la maandamano liko palepale wala hawakuchukuliwa hatua yoyote,wamevamia ofisi na kuvunja makufuli hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.katika mambo ambayo naamini yangeweza kuvuruga amani iliyopo ni haya mambo yanayofanywa na PROFESA.na hakuna hatua zilizochukuliwa,hii inaashiria kitu.
 
walipiga Vigelegele....
Werevu wakiwa kimya wanapanga mambo yao..
La profeserii na wahuni wake wakavamia office..
Kesho ndio atajua kua CUF inamamlaka kamili na sio yale ya jaji Mitungii
 
Lipumba ni mwenyekiti hewa, harafu hii tabia ya nataka sitaki siyo nzuri kwa jinsia ya kiume
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom