Maalim Seif amvaa IGP

Sefu ana laana ya Jumbe.Makao makuu si yapo mtendeni buguruni anataka nini
 
Hii barua umeipata?
14470616_10210251063811509_6260259026217653658_n.jpg
Duh kama IGP tayari anafahamu haya, kuna kipi atakachokipata Maalim huko?hapa kama ana issue aende mahakamani.
 
Duh kama IGP tayari anafahamu haya, kuna kipi atakachokipata Maalim huko?hapa kama ana issue aende mahakamani.

Hilo kundi kinatakiwa lisikanyage buruguruni kumbugudhi mwenyekiti kama hawamtambui waende mahakamani.Lakini wakijitia kwenda kinyume cha sheria yakiwakuta ya kuwakuta wasimpigie yowe mtu
 
mulidai yamekwisha,huyo mnyamwez mtahangaika nae sana,ndio mtapojua nini maana ya mzigo mzito mpe mnyamwez,kahangaika wee kuijenga cuf bara leo mnataka kuwauzia wafuga ng'ombe wa kaskazini!

Kweli kaijenga CUF bara maana miaka 20 ya uongozi wake hakuwahipo kupata zaidi ya wabunge wawili bara.

Wacha zaidi ya wabunge wawili!!!! Hakuwahipo kupata hata diwani mmoja mkoa aliozaliwa.

Bila ya juhudi za wapemba kuipatia wabunge basi katu CUF isingefikia hapo ilipo sasa.

Wapemba wakiisusa leo CUF basi itakufa na kubakia jina kama vile TLP na vyama vyengine vilivyobakia jina tu.
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ametua ofisini kwa kiongozi mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, ili kumueleza mkakati wake wa kutua ofisini kwake, Buguruni jijini Dar es Salaam.

Maalim anakwenda kwa IGP Mangu kumueleza adhima yake ya kufika ofisi kuu ya chama chake kesho Ijumaa, majira ya saa mbili asubuhi.

Hatua ya Maalim kutinga ofisini kwa IGP imetokana na kitendo cha jeshi la polisi kumsindikiza Prof. Lipumba kurejea ofisini; kusaidia uharibifu wa mali na kushambulia wanachama na wafuasi wa chama hicho.

Azma yake ya kwenda ofisini kwake kesho, inatokana na ofisi hiyo kuvamiwa na aliyepata kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba na genge la wafuasi wake.

Prof. Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti wa CUF, 6 Agosti mwaka jana na miezi 11 baadaye akatangaza kurejea katika nafasi yake, amefukuzwa rasmi uanachama wa chama hicho Jumanne iliyopita na Baraza Kuu la uongozi la Taifa (BKT), lililokutana Visiwani.

Hata hivyo, Prof. Lipumba, ameendelea kung’ang’ania kuwa bado mwenyekiti halali wa chama hicho na msimamo wake huo, unadaiwa kuungwa mkono na msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa watu waliokaribu na Maalim Seif zinasema, kiongozi huyo amekwenda kwa IGP Mangu kumtaarifu kuwa yeye na wabunge wa chama hicho, wamepanga kufika Buguruni kwa pamoja.

Anasema, “Maalim Seif anakwenda kumweleza IGP Mangu kwamba, tayari kumekuwepo na viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na watu wa Prof. Lipumba na kwamba chochote kitakachotokea, yeye na jeshi lake, wanapaswa kubeba msalaba.”

Prof. Lipumba alijiuzulu uenyekiti karibu na uchaguzi mkuu mwaka jana, akakimbilia nje ya nchi huku akidai hakufurahishwa na Edward Lowassa kuwa mgombea urais chini ya mwavuli wa vyama vinne ikiwamo CUF.

Ukawa unaundwa na vyama vinne; Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na National League for Democrats (NLD).

Hii ni mara ya pili tangu mfumo wa vyama vingi urejee nchini, kukumbwa na “mbegu mbaya” ndani yake.

Mara ya kwanza ilikuwa pale Augustine Mrema, akiwa mwenyekiti, alipojiapiza kufukuza wanachama thabiti ndani ya NCCR-Mageuzi. Alishindwa. Alifukuzwa mwenyewe.

Chanzo: Mwanahalisi
UBINADAMU KAZI KWELI.YAANI WATU UNAOWATUKANA KILA SIKU MATUSI YA KILO 9000000000000000000000000000000000 KILA SIKU NDO HAO HAO UNAOLAZIMISHA WAKULINDE.HII NCHI IMEJAA MINAfiki
 
Hii nchi itakuja kuendelea CCM itoke madarakani.Kuna figisu nyingi sana,sanaa nyingi sana.
hii inch itakuja kuendelea pale fikra za wanaicnh zitakapojua nani adui yetu katika maendeleo yetu na kupambana naye.. hayataletwa na ccm wana chadema wala act cuf. ni sisi wenyewe.
 
UBINADAMU KAZI KWELI.YAANI WATU UNAOWATUKANA KILA SIKU MATUSI YA KILO 9000000000000000000000000000000000 KILA SIKU NDO HAO HAO UNAOLAZIMISHA WAKULINDE.HII NCHI IMEJAA MINAfiki
Ww ndie mnafiki tena mdhandiki,wao ndio wenye dhamana ya ulinz na usalama,sasa ulitaka seif atumie nguvu km unavofikiri ww kuliko akiri,shame of u
 
Kweli kaijenga CUF bara maana miaka 20 ya uongozi wake hakuwahipo kupata zaidi ya wabunge wawili bara.

Wacha zaidi ya wabunge wawili!!!! Hakuwahipo kupata hata diwani mmoja mkoa aliozaliwa.

Bila ya juhudi za wapemba kuipatia wabunge basi katu CUF isingefikia hapo ilipo sasa.

Wapemba wakiisusa leo CUF basi itakufa na kubakia jina kama vile TLP na vyama vyengine vilivyobakia jina tu.
suala la CUF kupata au ktopata wabunge lilikua suala la mambo mengi ikiwemo mfumo(system) iliona ni chama cha waislamu,kukidhoofisha ni kuwakatisha tamaa kwa ktowapa hata mbunge mmoja,unaamin CUF ya 2005 temeke na ya 2015 ya 2015 ilikua na uungwaj mkono mkubwa!?..2015 system iltikiswa na NYANGUMI,ikahangaika na nyangumi ikaachia hvo viti
 
Unataka kutuaminisha kuwa 2015 CUF ilionekana ni chama kikirsto!?

Na pia unataka tufahamu kuwa system ndio inayovichagulia vyama vya siasa wabunge hivyo haina haja ya raia kuwapigia kura wagombea wake!!!!!!!!??????

Kwa akili hizi ni haki yenu pale mlipo mfananisha J. Nyerere na nabii.
 
Badala ya kwenda Buguruni yeye anarandaranda kwenye ofisi ya IGP na kwa nini asiende kureport kituo cha polisi huko Buguruni?

Kama yeye kidume aende Buguruni siyo kutafuta huruma polisi ilhali juzi tu wametoka kuwaponda kwamba wanatumika.

BTW:Juzi tuliambiwa humu kuwa makao makuu ya CUF yako Mtendeni Zanzibar,kinachomleta Buguruni ni nini?
 
ANAJIHENYESHA YEYE MWENYEWE MAANA WAZENJI SIKU ZOTE WAKO GADO NA WANAJIELEWA.
Si kuna mzenji kaenda kwa IGP kuomba escort ya kwenda ofisini kwake Tanganyika bila kujua kwamba IGP ana nakala ya Msajili. Anajitambuaje sasa huyu! Si aende mwenyewe ofisini kwake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom