Maalim Seif amvaa IGP

Huyo SEIF vipi alitakiwa aende kwa Msajili wa vyama akamalizane naye kwanza sio aelekee Buguruni wala kwa IGP.IGP asikupotezee muda huyo mwambie aende kwa msajili wa vyama wakamalizane mambo yao kwanza kama akiona kuna mgogoro wa Kisheria na Lipumba aende mahakamani sio polisi wala buguruni
Akamalizane na msajili uliambiwa wanadaiana,vikao halali vya chama vinajulikana,na vikao vya wahuni pia vinajulikana,muhuni aliendoka kwa hiari yake Leo anataka kurudi kwa kutumia uhuni wake alafu eti aachwe kwa lipi.
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ametua ofisini kwa kiongozi mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, ili kumueleza mkakati wake wa kutua ofisini kwake, Buguruni jijini Dar es Salaam, anaandika Pendo Omary.

Maalim anakwenda kwa IGP Mangu kumueleza adhima yake ya kufika ofisi kuu ya chama chake kesho Ijumaa, majira ya saa mbili asubuhi.

Hatua ya Maalim kutinga ofisini kwa IGP imetokana na kitendo cha jeshi la polisi kumsindikiza Prof. Lipumba kurejea ofisini; kusaidia uharibifu wa mali na kushambulia wanachama na wafuasi wa chama hicho.

Azma yake ya kwenda ofisini kwake kesho, inatokana na ofisi hiyo kuvamiwa na aliyepata kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba na genge la wafuasi wake.

Prof. Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti wa CUF, 6 Agosti mwaka jana na miezi 11 baadaye akatangaza kurejea katika nafasi yake, amefukuzwa rasmi uanachama wa chama hicho Jumanne iliyopita na Baraza Kuu la uongozi la Taifa (BKT), lililokutana Visiwani.

Hata hivyo, Prof. Lipumba, ameendelea kung’ang’ania kuwa bado mwenyekiti halali wa chama hicho na msimamo wake huo, unadaiwa kuungwa mkono na msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa watu waliokaribu na Maalim Seif zinasema, kiongozi huyo amekwenda kwa IGP Mangu kumtaarifu kuwa yeye na wabunge wa chama hicho, wamepanga kufika Buguruni kwa pamoja.

Anasema, “Maalim Seif anakwenda kumweleza IGP Mangu kwamba, tayari kumekuwepo na viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na watu wa Prof. Lipumba na kwamba chochote kitakachotokea, yeye na jeshi lake, wanapaswa kubeba msalaba.”

Prof. Lipumba alijiuzulu uenyekiti karibu na uchaguzi mkuu mwaka jana, akakimbilia nje ya nchi huku akidai hakufurahishwa na Edward Lowassa kuwa mgombea urais chini ya mwavuli wa vyama vinne ikiwamo CUF.

Ukawa unaundwa na vyama vinne; Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na National League for Democrats (NLD).

Hii ni mara ya pili tangu mfumo wa vyama vingi urejee nchini, kukumbwa na “mbegu mbaya” ndani yake.

Mara ya kwanza ilikuwa pale Augustine Mrema, akiwa mwenyekiti, alipojiapiza kufukuza wanachama thabiti ndani ya NCCR-Mageuzi. Alishindwa. Alifukuzwa mwenyewe.
Mungu mbariki Maalim Seif
 
Akamalizane na msajili uliambiwa wanadaiana,vikao halali vya chama vinajulikana,na vikao vya wahuni pia vinajulikana

Kikao halali ni kile ambacho kinatambuliwa kisheria na pia kinatambuliwa na msajili.Huwezi kukusanya tu watu ukasema hiki ni kikao halali eti kwa kuwa tu mmekusanyika.Msajili wa vyama kasema Lipumba kwa mujibu wa sheria ni mwenyekiti sio kwa mujibu wa vikao vyenu okoteza !!!!! Kama mnabisha nendeni mahakamani kwanza mkamalizane na mahakama ambayo itasema hicho mlichofanya kama kilikuwa kikao cha chama au kikao cha send off au kitchen party na pia kama Lipumba ni mwenyekiti au la kwa mujibu wa sheria sio kwa mujibu wa vikao koko mlivyofanya.
 
Kweli nime Amini, Huyu Le Proffeseri ni msomi wa hali ya juu mbooh, yaani hawa kina Maalim badala ya kufuata sheria kum tii kiongozi wao wao wana taka Kupindua? !!
Hapana hai kubalika,
 
Mpwa welcome back...
thank-you-cartoon.png

swissme
 
Huyo SEIF vipi alitakiwa aende kwa Msajili wa vyama akamalizane naye kwanza sio aelekee Buguruni wala kwa IGP.IGP asikupotezee muda huyo mwambie aende kwa msajili wa vyama wakamalizane mambo yao kwanza kama akiona kuna mgogoro wa Kisheria na Lipumba aende mahakamani sio polisi wala buguruni
aende huko kwani amekuambia anaenda sajiri chama mgogoro wa ndani ya chama hautatuliwi na msajili unatatuliwa na mahakama pekee lipumba kafanya makosa ya jinai kuvunja na kupiga kuandamana na kufanya mkusanyiko pamoja na kufanya mkutano wa kisiasa ambao umekatazwa na polisi sasa hapo msajiri anahusikaje
 
Tunaomba Ufafanue Kauli yako. Ni kwa vipi polisi wanatumika? wanatumika katika mambo/masuala gani na wanatumiwa na nani na kwa faida ya nani? Nomba ufafanue ili nikuelewe maana umesema "polisi wanatumika"..
Polisi ni tawi la CCM wanapokeya maagizo kutoka CCM
 
Ifike kipindi Lipumba aone aibu na yeye.

Maana anadhalilisha wasomi pamoja na familia yake.
 
Lipumba akigoma kuachia ofisi mahakama itamn'ngoa tu..maana hakuna namna tena

We ushakuwa mahakama naona ushaandika hata hukumu itakavyokuwa wakati hata kesi haijaenda mahakamani.Mwanasheria koko wewe unatisha na umebobea kwa sheria koko!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom