Maafisa Elimu Wilaya na Mkoa, utitiri wa mitihani mnahujumu ufundishaji na ujifunzaji?

FAHAMA

New Member
Jan 1, 2023
2
1
Wanajamvi, nimejaribu kufanya uchunguzi wangu nimebaini viongozi wa wanaosimamia elimu yani ma REO na ma DEO ndio chanzo cha wanafunzi kufanya vibaya kwa sababu ya utitiri wa mitihani yao wanayolazimisha ifanyike karibu kila mwezi kwa shule za msingi na sekondari na kuzitafuna siku 194 zinazotengwa kwa ajili ya masomo siku ambazo ni sawa na siku 96 kwa nusu muhula.

Unakuta mtihani mmoja wa mkoa au wilaya wa sekondari unachukua wiki mbili ambazo ni sawa na siku kumi. Ukijumlisha na wiki moja ya masahihisho unakuta mtihani mmoja unatumia siku takriban 15. Mitihani kama hii ikifanyika mara tatu kwa muhula mmoja wenye siku 96 inatumia siku 45 yani 15 X 3.

Katika siku 96 za nusu muhula ukitoa siku 45 zilizopotea kwa kuwafanyisha wanafunzi mitihani mwalimu anabakiwa na siku 51. Hapo sijagusa monthly test na weekly test za mkuu wa shule ambazo nazo unakuta zinatumia siku kumi ukitoa hapo unabakiwa na siku 41.

Kwa kutumia siku hizi eti ndo mwalimu afundishe mambo yote yanayotakiwa kufundishwa kwa muhula wa kwanza. Siku hizi ni chache sana zinasababisha mwalimu afundishe kwa kulipua lipua na mwisho wa siku lazima wanafunzi wafanye vibaya.

Nashauri ma REO na ma DEO wenye tabia kama hizi muache mara moja na kama kuna maslahi mnayapata kupitia mitihani hiyo nashauri mtafute vyanzo vingine vya hayo maslahi na sio kuhujumu muda wa mwalimu na mwanafunzi katika zoezi zima la ufundishaji na ujifunzaji.
 
Back
Top Bottom