Viongozi mnaosimamia elimu tumienzi Lowasa tukijiuliza yeye aliwezaje kwenye elimu nyie mnashindwaje kwenye elimu

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
4,451
9,374
Kifo cha lowasa kimeibua mijadala ya mazuri yake na mabaya yake katika safari yake ya maisha katika siasa zake, uzuri wa siye wabantu marehemu asemwi kwa mabaya ni mwiko marehemu anasemwa kwa mazuri tu hata kama mabaya yapo basi mnatasemea gizani

Kuna jambo zuri kuhusu marehemu linasemwa la kuhusu elimu ya sekondari kuhakikisha kila kata nchi hii inakuwa na shule ya sekondari ya kata hili suala alisimamia marehemu lowasa na kweli shule zilijengwa kwa michango ya wanainchi ikiwa sambamba na serikali kweli shule zikajengwa, maswali yakaja je walimu watatoka wapi

Serikali ikatangaza clush program kwa wahitimu wa kidato cha sita waende vyuo vya uwalimu wakapewe zile skills za uwalimu kwa mwezi mmoja kisha waende kufundisha kwa kibali maalum na wakambiwa kabisa ndani ya miaka mitatu wawe wamejiendeleza kimasomo kweli shule zikapata walimu hili ni jambo zuri la mh Lowasa katika uhai wake akiwa kama waziri mkuu matunda ya shule za kata tunayaona shule zinaimalika kila siku

Pili kipindi cha mbio za urais 2015 mh lowasa alisema wazi elimu elimu elimu na alisema endapo atakuwa Rais wa nchi hii elimu itakuwa bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu kuna kundi lilimbeza likasema haiwezekani shule zipo nyingi uzuri wa hoja hii hata chama tawala nao wakaja nayo kuwa elimu ya msingi itakuwa bure minongono ikawa mingi je itawezekana kweli

Ukweli ukaja bainika kumbe inawezekana magufuri alipoingia madarakani elimu ya msingi imekuwa bure kuanzia chekechea mpaka kidato cha sita hakuna ada kwa sasa kitu ambacho tunataka viongozi wa sasa wajifunze kwa mh lowasa ni kama wazo la shule la kata lilikuja shule zikajengwa na walimu wakapatikana na kama aliwaza elimu bure inawezekana inchi hii na wazo hilo chama tawala wakawa nalo na likawezekana leo elimu bure sote mashahidi

Swale je

Kwanini sasa shule zipo nyingi na walimu wapo wengi wenye sifa za uwalimu lakini serikali haitaki wajiri je pamoja na kuwa aitaji ajiri haiwezi kuja na mpango wowote kuhakikisha hawa wahitimu wa uwalimu wanaenda kuziba nafasi za upungufu wa walimu kwa makubaliano furani kwa malipo furani uku wakiwa katika mpango wa kuwapatia ajira za kudumu je wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, Wakurugenzi mnakosa ulowasa furani kuhusu elimu yani kuwa wabunifu

Mfano kila halmashauri ikaja na uhitaji wa walimu kwa kila shule kisha serikali kupitia mafungu ya elimu bure ikaongeza fungu pengine asilimia 20 ya pesa ambayo shule inapokea itoe kama posho kwa walimu wanaojitolea pia halmashauri katika mapato yake ya ndani itoe asilimia 20 kwa kila shule kulipa walimu wanaojitolea kisha vijana hawa wawepo katika mashule wafundishe watoto ukuwakilipwa kiasi hicho cha pesa ambayo imepatikana na kipindi cha ajira zikitoka hawa hawa vijana ndio wapewe kipaumbele serikali iwajiri kwa zone yani ukanda mfano serikali ikitaka kutoa ajira tayali walimu hao wapo inangalia ukanda upi mapungufu ni mengi na walimu wanaojitolea ni wengi basi inajiri walimu wote eneo hilo kama kanda ya kati basi awamu ya kwanza inatoa ajira awamu ya kati tu kisha zile asilimia 20 inaongezea walimu wengine tena kwenye mpango wa kujitolea kweli viongozi wetu haya mnashindwa waza

Tumuenzi lowasa kwa kutatua hizi changamoto za ukosefu wa walimu hayo mambo ya sijui kufundisha kwa njia ya video eti mwalimu mmoja afundishe nchi nzima jamani watalamu wetu tokeni semeni ukweli teaching is not only kutoa material tu kuna vitu vingi hivi huyo mwalimu wa dodoma anayemfundisha mtoto wa maswa anajua changamoto ya wanafunzi mmoja mmoja je anaweza simamia malezi ya mtoto so tuache siasa kwenye elimu walimu bado wanaitajika kuingia darasani kuonana watoto pamoja na technology kukuwa ila hiyo technology ifanyike watoto wanamuona mwalimu wao physical

R.I.P LOWASA
 
Kampeni hizo hamna jipya, mwalimu mmoja kufundisha tanzania nzima? Kwa umeme upi na hizo video?

Hapa mjini umeme ni wa kuvizia.

Kijiji ninachotoka mimi hakunaga umeme, miaka yote tunatumiaga solar, wakati wa mvua Tv tunaangalia kwa masaa machache sana.

Sasa huyo mwalimu atakae fundisha tanzania nzima kwa wakati mmoja, atafundisha na wanafunzi wa vijijini?

Hapa tumepigwa.

N.b. walimu mjiandae kujiajiri maana hamtokuwa na kazi, kama mwalimu mmoja atafundisha Tanzania mzima nyie wengine mna kazi gani?

Kila kipindi mwalimu mmoja anapiga kipindi Tanzania nzima huku wengine vijijini wamekaa chini, wanafundishwa kwa video, nyie itakuwa balaa.

R.I.P LOWASSA.
 
Kampeni hizo hamna jipya, mwalimu mmoja kufundisha tanzania nzima? Kwa umeme upi na hizo video?

Hapa mjini umeme ni wa kuvizia.

Kijiji ninachotoka mimi hakunaga umeme, miaka yote tunatumiaga solar, wakati wa mvua Tv tunaangalia kwa masaa machache sana.

Sasa huyo mwalimu atakae fundisha tanzania nzima kwa wakati mmoja, atafundisha na wanafunzi wa vijijini?

Hapa tumepigwa.

N.b. walimu mjiandae kujiajiri maana hamtokuwa na kazi, kama mwalimu mmoja atafundisha Tanzania mzima nyie wengine mna kazi gani?

Kila kipindi mwalimu mmoja anapiga kipindi Tanzania nzima huku wengine vijijini wamekaa chini, wanafundishwa kwa video, nyie itakuwa balaa.

R.I.P LOWASSA.
Kazi sana viongozi wetu wajaribu uthubutu wakuu wa mikoa wakuu wa wilaya wakurugenzi hatuoni wala kusikia halmashauri furani haina upungufu wa walimu wote wamekaa wanasubilia maagizo ya mchengelwa inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom