Lundenga wa Miss Tanzania awaomba radhi watanzania

Sijui nani anastahili kuombwa na kupokea msamaha, maana watu wanamrukia Lundenga wa watu. Kwa kweli taasisi nyingi binafasi na za serikali pamoja na watu binafsi hawakuonekana kuheshimu maisha ya watu waliopotea. Nadhani wengi tunahitaji kuomba msamaha, ila sijui kwa nani.
 
Looks like hiyo so called apology kaandika Mange Kimambi

hivi kuna tatizo gani hawa watu wakanyamaza?
attachment.php
Huyu mwingine hakuwa na haja ya kuandika upupu wake wakati baadhi ya familia zimepoteza ndugu zaidi ya watano.Sishangai maana huyu bibie wanachokisema Makambas nae lazima afuate mkumbo
@JMakamba January Makamba

Siku ya msiba, CCM ilizindua kampeni kwa shamra Igunga, Ligi Kuu iliendelea, mabaa yalijaa, but kuna watu wamekomalia shughuli ya vichupi!
 
Mwenzetu you made my day; hata siku moja sikuwahi kusoma wazo lolote la maana kutoka kwako katika uzi wowote ule. Kama kuna ka-ufunuo vile kwako leo hii FaizaFoxy.

Hili nali naliingiza kwenye kitabu changu cha kumbukumbu.

Mambo ya Kishetani toka lini yakawa na jema?
 
Aisee umeamsha hasira kichizi! Kweli naona kama umekurupushwa mtu yeyote mwenye akili aliyesoma hii barua yako anajua wazi hujaomba RADHI hata kidogo.
<br />
<br />
KANIUDH HAPO KWENYE MAJNA YA MISS TZ,UTAFKIRI TZ NI YA MUHIM SANA HUKO WKT MARAZOTE WANAIDHALILISHA BENDERA YETU! HUYU LUNDENGA IS SOO CHEAP!!! CRAP AND SHAME ON YOU!!!!!
 
Mosi:Kwenye vyombo vya kijamii na umma kila kitu kilikuwa wazi huitaji akili ya ziada kulitambua hilo;

Pili: Uzalendo Kwanza... Kuwahi kupeleka jina ni sababu hasi na haina mantiki ...kwanza mrembo wenu asilimia 99.999 wanakuwa ni wasindikizaji tu;

Tatu; Kulinganisha TFF na shindano hili ni kuchanganya machungwa na maepo(apple). Shindano lako lilikuwa na usambazwaji uliowafikia watanzania na dunia yote ndani ya sebule yao; timu yako na mdhamini wenu mkuu mmeteleza kwa hili

Ni mengi ya kusema lakini mwisho, tafutuni watu waliobobea katika mambo ya mawasiliano wawasaidie kuandika hizi taarifa.

NB: NDO MAANA HILI SHINDANO NI MARUFUKU HUKO ZENJI KWANI HALINA TIJA KATIKA JAMII!

Kamati ya Miss Tanzania yawaomba radhi Watanzania 13/09/2011

136817025.png

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
13 / 09 / 2011

YAH: KUOMBA RADHI KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR

Usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba.

Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taaasisi yetu ilikuwa inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011.

Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko mkubwa sana juu ya tukio hilo .

kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
  • Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .
  • Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.
  • Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo
  • Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo.
Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo.
Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu.

Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo.

KUOMBA RADHI

Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza "TUNAOMBA RADHI"

Mwenyezi MUNGU aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,

Amina,

Hashim Lundenga
Mkurugenzi

source: Wavuti - Habari

Yaliyojiri Danganyika Bara ndani ya siku moja! 13/09/2011

340979423.jpg

source: Wavuti - Habari
 
Imetulia na inatosha. Mbona serikali haijaomba radhi yoyote? Kuna chombo chochote ambacho kimeomba radhi kwa tukio la kuzama meli?

Hakuna zaidi ya Kamati ya Ms Tz lakini nayo inaonekana kuna ka 'element' ka VTL kushinikiza wawasafishe kishkaji katika hii press release.
 
Nashangaa lundenga anasema amepata taarifa rami sa tisa mchana wakati issue tangu asubuhi ilikuwa hadharani. Anyway amekuwa muungwana kuomba radhi.
 
Yaani nimesoma nikacheka baada ya kukasirika eti wanasema taarifa "rasmi" waliipata saa tisa na nusu mchana (9:30) yaani kwamba sasa ni kweli meli/boti imeuwa watu......hivi kulikuwa na taarifa rasmi? Kama ilikuwepo ni chombo gani kilitoa hio taarifa "rasmi"? waiipata kwa njia gani? Huu ni uongo na ujinga na upuuzi, nadhani elimu ina-matter sana hapa.

Pili, Waliangalia sehemu nyinngine wakakuta TFF wanaendelea na mechi kama kawaida na kigezo kingine ilikuwa kumbi za starehe eti watu waliendelea kuserebuka kama kawa!! Sasa hapa ndio nimewaita hawa jamaa ni wapuuzi kwa maana ya upuuzi kwa sababu hapo juu wanasema taarifa waliipata saa tisa mchana na kwamba wasingeweza kuahirisha lakini hapa chini wanasema "wenzao' waliendelea kula raha wakaona wawaunge mkono; ninachojiuliza ni kwamba; je Kulikuwa na muda kiasi gani tangu wapate taarifa "rasmi" ya msiba na mchezo wa TFF kuendelea? Walikaa saa ngapi tena wakatafakari haya na kuamua kuendelea na Umisi? Je kuna kumbi gani za starehe zilikuwa wazi saa tisa baada ya wao kupata taarfia rasmi hadi kuamua kuendelea na umisi? Hawakupanga vizuri utetezi wao wa kijinga.

Langu la mwisho ni hili; je kamati hii inaendeshwa na matukio ya "wengine" hususani yale mazuri tu (mechi, kumbi za starehe) hadi wakaamua kuwaunga mkono au wana katiba yao na mambo yao na misimamo yao? kama jibu ni hapana; iweje waangalie "wengine" wanafanya nini ili nao ndio waamue kufanya la kwao? Mengine naona niyaache kwa wenzangu. Ila next time noi heri kukaaa kimya tu kuliko kuandika kitu ambacho kinawechekesha watu hata kuanza kuhoji uwezo wa elimu yako na urazini wako.
 
kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
  • Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .
  • Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.
  • Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo
  • Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo.
Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo.
Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu.

HAYA MANENO HAYAKUTAKIWA KABISA, HAPO NDIPO KWENYE KOSA
BARAU YA KUOMBA RADHI WAMEITWANGA NDEFU MNO NDIO MAANA WANAWEKA NA PUMBA
WAO WANGESEMA WANAOMBA RADHI KAMA KUNA WENGINE WAMAKOSEA BADO HAIWAFANYI WAO KUWA NA HAKI YA WALICHOFANYA
NA YAWEZEKANA HAO WENGINE WANANCHI HAWAKUTEGEMEA WEMA WOWOTE KUTOKA KWAO.
KUNA VITU VIWILI KATIKA BIASHARA AU SHUGHULI KAMA MTU HAKIKUPA FEEDBACK INA MAANA ANAKUPENDA NA NAITAJI/TEGEMEA IMPROVEMENT
LAKINI AKIKAA KIMYA HIYO NI KWAMBA ANA MATUMAINI NA WEWE MISS TANZANIA WALIPASWA KUJIONGEREA WAO WENYEWE KAMA WATU WANAOJITEGEMEA NA WENYE AKILI TIMAMU.

KUOMBA RADHI

Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza “TUNAOMBA RADHI”

Mwenyezi MUNGU aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,

Amina,

Hashim Lundenga
Mkurugenzi

hiyo RED haikutakiwa wanaonekana wanaomba RADHI bora liende lakini sio maamuzi ya utashi wao
hapa ndipo makapuni ya TANZANIA yapo fail PR
na kama hawalioni ili basi wamekwisha, kuna TEMPLE kibao kwenye internet walishindwa kudesa?

hii nimeipenda MUUNGANO una kasoro

kwa ujumla wameshemsha
 
Imetulia na inatosha. Mbona serikali haijaomba radhi yoyote? Kuna chombo chochote ambacho kimeomba radhi kwa tukio la kuzama meli?

MZEE MWANAKIJIJI

KOSA LA SERIKALI halifanyo VODACOM kuwa sahihi
hizi ni mamlaka/organisation mbili tofauti
hisitoshe wewe unategemea nani serikali aombe radhi?
ina maana siku hizi unaamini tuna serikali ya wawajibikaji?
 
Ndug yangu kwani "Tume" imeshatoa majibu yake kwamba kulikuwa na makosa?? Tz kila kitu tume... tume ..tume... ni chache sana zinazokujaga na majibu ya kuridhisha!! I am tired of this Country...
 
duh inatosha kwa watakaoelewa maana kama kutolewa kwa tamko la siku tatu za maombolezo limetoka jumapili .... je bado watu wanawalaumu vodacom????
 
MZEE MWANAKIJIJI

KOSA LA SERIKALI halifanyo VODACOM kuwa sahihi
hizi ni mamlaka/organisation mbili tofauti
hisitoshe wewe unategemea nani serikali aombe radhi?
ina maana siku hizi unaamini tuna serikali ya wawajibikaji?

CCM wameomba radhi?
Original Comedy wameomba radhi?
TFF wameomba radhi?
TBC1 wameomba radhi?

Sijaelewa kwanini hata Miss Tanzania wameomba radhi. I mean watu wanaweza kuwa na moral issue dhidi ya Miss Tanzania that is their prerogative lakini kufanya Miss Tanzania the fall guy kana kwamba ndio object of our anger is highly unfair and unwarranted. HIvi, nchi nzima Jumamosi hakukuwa na madisko, sinema, muziki n.k isipokuwa mashindano ya Miss Tanzania au ni Miss Tanzania peke yake ndio ilitakiwa kuahirishwa?

Hivi hata maana ya national mourning ni nini hasa? Kwanini serikali zilitangaza maombolezo rasmi kuanza Jumapili badala immediately jumamosi? Kwa kifupi ni kuwa yeyote ambaye alikuwa anahirisha jambo lake siku ya jumamosi was purely discretionary and optional. Toka mwanzo nilitarajia kuwa Miss Tanzania ingeahirishwa not out of demand ya serikali au kundi jingine lolote isipokuwa out of sensitivity tu. Lakini kuifanya kuwa ni lazima inashangaza.

Tangu lini watu wanalazimishwa kuomboleza? Wamesema walivaa alama za kuonesha maombolezo, kwamba walisimama kwa dakika moja (which is standard worldwide) kuonesha heshima kwa wafu; na wakaja na kutoa rambirambi lakini zote hazikuwa zinatosha. Na sasa hata kuomba radhi kwao -which to tell you the truth was unneeded - kunabezwa.

Kuna nini zaidi ya hili? Mwanzoni tulisikia "mashindano ya vichupi" is this about dada zetu kuonesha urembo ndio imekuwa very offensive? is that it?
 
Yaani nimesoma nikacheka baada ya kukasirika eti wanasema taarifa &quot;rasmi&quot; waliipata saa tisa na nusu mchana (9:30) yaani kwamba sasa ni kweli meli/boti imeuwa watu......hivi kulikuwa na taarifa rasmi? Kama ilikuwepo ni chombo gani kilitoa hio taarifa &quot;rasmi&quot;? waiipata kwa njia gani? Huu ni uongo na ujinga na upuuzi, nadhani elimu ina-matter sana hapa.<br />
<br />
Pili, Waliangalia sehemu nyinngine wakakuta TFF wanaendelea na mechi kama kawaida na kigezo kingine ilikuwa kumbi za starehe eti watu waliendelea kuserebuka kama kawa!! Sasa hapa ndio nimewaita hawa jamaa ni wapuuzi kwa maana ya upuuzi kwa sababu hapo juu wanasema taarifa waliipata saa tisa mchana na kwamba wasingeweza kuahirisha lakini hapa chini wanasema &quot;wenzao' waliendelea kula raha wakaona wawaunge mkono; ninachojiuliza ni kwamba; je Kulikuwa na muda kiasi gani tangu wapate taarifa &quot;rasmi&quot; ya msiba na mchezo wa TFF kuendelea? Walikaa saa ngapi tena wakatafakari haya na kuamua kuendelea na Umisi? Je kuna kumbi gani za starehe zilikuwa wazi saa tisa baada ya wao kupata taarfia rasmi hadi kuamua kuendelea na umisi? Hawakupanga vizuri utetezi wao wa kijinga.<br />
<br />
Langu la mwisho ni hili; je kamati hii inaendeshwa na matukio ya &quot;wengine&quot; hususani yale mazuri tu (mechi, kumbi za starehe) hadi wakaamua kuwaunga mkono au wana katiba yao na mambo yao na misimamo yao? kama jibu ni hapana; iweje waangalie &quot;wengine&quot; wanafanya nini ili nao ndio waamue kufanya la kwao? Mengine naona niyaache kwa wenzangu. Ila next time noi heri kukaaa kimya tu kuliko kuandika kitu ambacho kinawechekesha watu hata kuanza kuhoji uwezo wa elimu yako na urazini wako.
<br />
<br />

kumbe umeona eeeh! Mimi naona hawa hawaombi radhi bali wanajitetea! Kuomba radhi kunamanisha kwamba unakubali kuwa umekosea kwa uliyoyafanya!
 
CCM wameomba radhi?
Original Comedy wameomba radhi?
TFF wameomba radhi?
TBC1 wameomba radhi?

Sijaelewa kwanini hata Miss Tanzania wameomba radhi. I mean watu wanaweza kuwa na moral issue dhidi ya Miss Tanzania that is their prerogative lakini kufanya Miss Tanzania the fall guy kana kwamba ndio object of our anger is highly unfair and unwarranted. HIvi, nchi nzima Jumamosi hakukuwa na madisko, sinema, muziki n.k isipokuwa mashindano ya Miss Tanzania au ni Miss Tanzania peke yake ndio ilitakiwa kuahirishwa?

Hivi hata maana ya national mourning ni nini hasa? Kwanini serikali zilitangaza maombolezo rasmi kuanza Jumapili badala immediately jumamosi? Kwa kifupi ni kuwa yeyote ambaye alikuwa anahirisha jambo lake siku ya jumamosi was purely discretionary and optional. Toka mwanzo nilitarajia kuwa Miss Tanzania ingeahirishwa not out of demand ya serikali au kundi jingine lolote isipokuwa out of sensitivity tu. Lakini kuifanya kuwa ni lazima inashangaza.

Tangu lini watu wanalazimishwa kuomboleza? Wamesema walivaa alama za kuonesha maombolezo, kwamba walisimama kwa dakika moja (which is standard worldwide) kuonesha heshima kwa wafu; na wakaja na kutoa rambirambi lakini zote hazikuwa zinatosha. Na sasa hata kuomba radhi kwao -which to tell you the truth was unneeded - kunabezwa.

Kuna nini zaidi ya hili? Mwanzoni tulisikia "mashindano ya vichupi" is this about dada zetu kuonesha urembo ndio imekuwa very offensive? is that it?

Hivi tulivyosema hapa jana Lundenga kufungwa Kengele kumbe haikueleweka kabisa. Si LINO aliyeomba Radhi Mkuu. Shinikizo hilo nikipata detail ntakupa kupitia P.M hapa JF
 
Imetulia na inatosha. Mbona serikali haijaomba radhi yoyote? Kuna chombo chochote ambacho kimeomba radhi kwa tukio la kuzama meli?

Exactly! Aliyepaswa kuwa wa kwanza kuomba radhi ni SMZ kwa kushindwa kutimiza wajibu wake hadi kusababisha maafa haya makubwa. Hivi usalama wa maisha ya raia na mali zao si ndio kazi ya kwanza na ya msingi ya Serikali yoyote duniani? Unless, leo hii tuambiwe kwamba jukumu hili la serikali limebadilika; pengine kazi yake ya kwanza ni kujipanga kupokea cheques baada ya tukio!

Tuache kutekwa fikra zetu na wanasiasa kutaka kujivua wajibu wao na kuhamisha matatizo kwa wengine wasiohusika moja kwa moja kama Vodacom. Serikali ilipaswa iombe radhi kwanza na iwajibike, zifuate mamlaka nyingine (bandari, SUMATRA, n.k.), wamiliki wa meli, kisha wengine.

Mwisho hata mimi raia nitaomba radhi kwa sababu kama raia nina mchango wangu kwa matatizo yanayoikumba nchi yetu. Na radhi yangu nitaiombea kwenye sanduku la kura.
 
Mosi:Kwenye vyombo vya kijamii na umma kila kitu kilikuwa wazi huitaji akili ya ziada kulitambua hilo;

Pili: Uzalendo Kwanza... Kuwahi kupeleka jina ni sababu hasi na haina mantiki ...kwanza mrembo wenu asilimia 99.999 wanakuwa ni wasindikizaji tu;

Tatu; Kulinganisha TFF na shindano hili ni kuchanganya machungwa na maepo(apple). Shindano lako lilikuwa na usambazwaji uliowafikia watanzania na dunia yote ndani ya sebule yao; timu yako na mdhamini wenu mkuu mmeteleza kwa hili

Ni mengi ya kusema lakini mwisho, tafutuni watu waliobobea katika mambo ya mawasiliano wawasaidie kuandika hizi taarifa.

NB: NDO MAANA HILI SHINDANO NI MARUFUKU HUKO ZENJI KWANI HALINA TIJA KATIKA JAMII!

Kamati ya Miss Tanzania yawaomba radhi Watanzania 13/09/2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
13 / 09 / 2011

YAH: KUOMBA RADHI KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR

Usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba.

Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taaasisi yetu ilikuwa inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011.

Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko mkubwa sana juu ya tukio hilo .

kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
  • Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .
  • Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.
  • Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo
  • Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo.
Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo.
Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu.

Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo.

KUOMBA RADHI

Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza "TUNAOMBA RADHI"

Mwenyezi MUNGU aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,

Amina,

Hashim Lundenga
Mkurugenzi

source: Wavuti - Habari

Yaliyojiri Danganyika Bara ndani ya siku moja! 13/09/2011

340979423.jpg

source: Wavuti - Habari

saaafi kwa mara nyingine...Baadaye zitahama wacha tuseme KABLA Hawajaamka
 
Back
Top Bottom