Lundenga wa Miss Tanzania awaomba radhi watanzania

mbona wanamlaumu anko lunde wakati hata media zilikuwa hazijatanga news yoyote wakati wa ajali wabongo bwana..
 
Unajitetea bahada ya kuona maoni mengi ya watanzania wanatofautiana nanyi.
 
Eti taarifa rasmi kapaipata saa 9 mchana!!!! Huyu mtu ni wa namna gani???!!! Katika Dharura kama ile unasuburi taarifa rasmi????!! Lundenga???? Can't you improvise??? Kama huwezi basi hufai kuwa Kiongozi hata wa Mtaa!!! Alitaka mpaka JK ampigie simu au amuandikia memo ndo achukue hatua??? This is OUTRAGEOUS!!!!!.... Lame!!.
 
Hawakutakiwa kuomba radhi hao akina Lundenga, Kama mnakumbu kumbu Mzee Mwinyi alikwenda mpokea Michael Jackson wakati wa Meli MV Bukoba imezama. Taifa likiwa kwenye msiba mkubwa huyu mzee alikuwa na mzee wa Pop Duniani pale DIA

103815fc9311602b.jpg
[/QUOTE
Acha uongo wewe, MV. Bukoba imezama Mei 12. 1996 na Michael Jackson na Ali Hassan Mwinyi wamekutana Feb 1992
 
walipata taarifa za kuzama meli saa tisa na nusu mchana..........duhhhh
 
HASHIMU HATUONI MOYO WA DHATI KATIKA UOMBAJI WAKO RADHI KWA WAFIWA
NA JAMII YA TANZANIA KWA UJUMLA WETU


Katika taarifa hii kuna kiswahili kingi mno na
mwendelezo wa UBISHI kama si mzaha vile kwa Hashimu kuendelea kutunyooshea kidole kwamba ni kwa nini tumlaumu tu yeye wakati hata fulani na kufani na fulani pia nao walifanya hiki na kile na vile ...

Kwa maoni yangu uombaji radhi kwa ndugu yetu Lundenga ni kitendo cha ki-uungwana na silka ya Mtanzania lakini
UDHATI WA MOYO humu bado ni wa kuunga unga tu.

Hata hivyo, kama mambo yote haya yngelikua watu kupewa maski za darasani vile, mpaka hivi sasa anawazidi kwa mbali sana Uongozi Mzima wa CCM kushikilia mgugumio wao kwa kitendo chao cha kuonelea kwamba uzinduzi wa kampeni Igunga, na kumtafutia Kafumu ukubwa ni wa maana zaidi kuliko kukimbilia visiwani Pemba kwenda kuokoa hata roho ya Mtanzania mmoja tu ambao ndio tunaoleta uhalali na maanaa ya kuhitajika kuwepo viumbe vinavyoitwa viongozi.

Nasema kama mchezo wa kuigiza vile CCM kama kawaida iliendelea na sherehe za kuangushia wanakijiji rushwa ya ubwabwa kwenye mkutano wa kisiasa na kukodisha akina Masanja wa Ze Komedi kukata Mauno Jukwani huku shamrashamra hizo zikisindikizwa na muziki murua wa mirindimo ya muziki wa mwambao wa Pwani (taarab) kwa hisani ya chombo chao binafsi TBC huku hayo yakiendelea bila aibu yoyote kwa kuzingatia kwa watoto ambao ni taifa la kesho wanaendelea kunyng'anywa tu midomoni mwa samaki papa kutokana na msaada finyu wa watu wenye zana duni tu kama vile matumbwi tu huko Nungwi.

Lakini kama ajali kama hii ingetokea nchi nyingine, naweza hata kuelezea kwamba Waziri wangu wa Mambo ya nje, Mhe Membe, angetumia maneno gani kuonyesha masikitiko na majonzi ya taifa letu kwa NCHI RAFIKI hiyo.

Ndio, ni kweli kwamba tunakumbuka busara hizi kwamba Ndugu yako akikuomba radhi na kujiona mnyonge mbele ya jamii yake ya Tanzania na kudhihirisha mbele ya kandamnasi kwamba anajutia matendo yake ambayo kimsingi kabisa jamii yake haikuafi jana, leo na hata kesho lakini wewe mwenye ukafunga milango ya moyo wako, Lundenga bado atakua haja saidika kitu na maombi yake hayo.

Naam, lakini mtu huyu ambaye ni mdhambi mbele ya macho ya jamii yake kwa kukiuka na kudhalilisha UTAMADUNI WA MTANZANIA wakati wa majonzi, majanga na kadhalika, ambao nao hata na yeye kakatwa kitovu chake kwa tamaduni hizo hizo, akiamua kwenda kwa mtu au watu wenye heshma zao katika jamii kumuombea radhi kwa sisi akina kapuku huku na bado tukatia roho ngumu tu hapo nako Lundenga na jopo lake bado litakua halijajinasua katika dhambi hii ya kihistoria hata kama jamii yake hiyo huenda haiheshimiwi na wawekezaji wa nje ya nchi kama vile VODAKOM.

Kama haitoshi vile, huyu mwenzetu akiendelea na udhati wa moyo na kujibidisha kabisa kama mtu ambaye kweli anajihisi kuelekea kukosa kitu chenye thamani kubwa kisichonunulika dukani (kuthaminiwa na kukubalika na jamii yako inayokuzunguka na inayokufanya wewe ujihisi kukamilika kuwa wewe kweli) anaweza kabisa akawafuata hata viongozi wetu wa kiroho kwenda kutubu na kuwasihi wakamuombee samahani ili apate kukubalika tena.

Nasema mabo yakifikia kiwango kama hiki na wananchi bado tu tumeendelea kushikilia mioyo migumu basi haina shaka kwamba ndugu huyo tayari atakua ameshafunguliwa kule mbinguni na makosa yote kuhamishiwa katika mafaili yetu wenyewe hadi hapo.

Lakini kwa hili la Lundenge, UDHATI WA MOYO bado licha ya ukweli kwamba utamaduni wa viongozi kuomba radhi nchini nayo pia siku zote huwa bidhaa hadimu mno midomoni mwao kuliko hata hali halisi ya dhahambu kwa wachimbaji Barricks kule Kahama!!!!!

Hebu tuendelee kusubiri kuja kuona wao CCM watatoka kivipi vile katika sakata hili kuku VODACOM tukiwafuta kabisa katika midaftari zetu kwa kuwa mambo yetu wala haiwahusu kitu hata chembe isipokua tu fedha zetu!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

13 / 09 / 2011


YAH: KUOMBA RADHI KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR .


KUOMBA RADHI

Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza “TUNAOMBA RADHI”

Mwenyezi MUNGU aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,

Amina,


Hashim Lundenga

Mkurugenzi
 
Looks like hiyo so called apology kaandika Mange Kimambi

hivi kuna tatizo gani hawa watu wakanyamaza?
attachment.php
 

Attachments

  • matusi ya Mange.png
    matusi ya Mange.png
    12.8 KB · Views: 186
watoto wa mjini wanakumbia katia kiberiti kichaka...dah..anko..Hash..kama nakuona..vile..kumbuka ulishawahi kupishana kiswahili na waislamu kuhusu miss tanzania?..ukawajibu ...nini vilee
 
Hawakutakiwa kuomba radhi hao akina Lundenga, Kama mnakumbu kumbu Mzee Mwinyi alikwenda mpokea Michael Jackson wakati wa Meli MV Bukoba imezama. Taifa likiwa kwenye msiba mkubwa huyu mzee alikuwa na mzee wa Pop Duniani pale DIA

103815fc9311602b.jpg
[/QUOTE
Acha uongo wewe, MV. Bukoba imezama Mei 12. 1996 na Michael Jackson na Ali Hassan Mwinyi wamekutana Feb 1992

Wewe Juha MV Bukoba imezama May 21, 1996
 
Kama kweli Lundenga umeomba radhi umekosea sana. Haujafanya kosa lolote hata uombe radhi katika Tanzania hii ya kibepali. Alafu msiba umetokea taifa la Zanzibar ambako shindano la mamiss hawalitambui wakati shindano limefanyika katika taifa la Tanzania. Haukufanya kosa lolote Lundenga hata uombe radhi.. Watanzania nasema kwa sauti kuu sana tusimsakame Lundenga hana kosa lolote hapo..
 
Hata kujitetea pia hajui!
eti mie niliwaona majilani zetu wanatoka nje wakiwa utupu na mie nikatoka kwa hiyo naomba radhi, ebo, upuuuuzi mtupu!
Lundenga hajaomba radhi bali amejitetea huku si kuomba radhi kunakotakiwa kwanza sababu alizotoa ni hafifu...
Amesema waliendelea na tamasha lao kwa vile TFF walikuwa wanamchezo what is this...
Waliendelea kwa vile mabaa yalikuwa wazi shit...
Eti wangechelewa kuwasilisha jina kwani alikuwa anakwenda mbinguni kuwa ukichelewa basi.......
Nafikiri utetezi ni hopeless wameongeza machungu badala ya kupunguza, tuseme basi sababu zao ni za kweli kwa hiyo wanaomba radhi ya nini, kuomba radhi ina maana umetenda ndivyo sivyo walichofanya ni kujitetea si kuomba radhi.
 
Ukiandaa tafrija ya harusi kwa mfano. halafu mzazi wako akafa siku moja kabla ya ya tukio....utaendelea na sherehe kisa umetumia gharama nyingi hivyo unaogopa hasara?

vitu vingine tuache ushabiki tu ndo maana umesema mzazi wako akifa na sio jirani yako bwana!!
 
Tuambie wewe Wacko jacko kaja lini naona Moderator amechakachua post zangu ila umesema uongo lazima ukubali.​
  • kati ya mwaka 1992 au 1993..tena kwa mwaliko wa shule ya sinza maalum
 
Lundega has lost legitimacy to organise Miss Tz event, I think he has to quit to protect his reputation. After all he has served this duty for quite some time now so he probably needs someone to spell him.
 
Hawakutakiwa kuomba radhi hao akina Lundenga, Kama mnakumbu kumbu Mzee Mwinyi alikwenda mpokea Michael Jackson wakati wa Meli MV Bukoba imezama. Taifa likiwa kwenye msiba mkubwa huyu mzee alikuwa na mzee wa Pop Duniani pale DIA

hahahahahaha....kama niko sahihi ..mwinyi alienda Airport kumpokea Kanda Bongoman..wakati huo Muhimbili kulikuwa na mgomo wa madaktari na manesi
 
  • kati ya mwaka 1992 au 1993..tena kwa mwaliko wa shule ya sinza maalum

Mkuu Wacko jacko alikuja February 1992 akafikia pale Kilimanjaro Hotel au sasa inaitwa Kempiski. Sasa sijaelewa nia ya Rev Masanilo kusema Mzee Mwinyi alikwenda kumpokea Wacko Jacko ilipotokea ajali ya Mv Bukoba ilipotokea May 1996. Ndio narudia kumuuliza ni Wacko Jacko gani aliyekuja mwaka 1996 Moderators do the needful to Masanilo amemchafua Mzee Mwinyi na hataki kuomba radhi!!!!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI13 / 09 / 2011

YAH: KUOMBA RADHI *KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR

Usiku wa kuamkia Jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba. Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taasisi yetu ilikuwa inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011.

Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko mkubwa sana juu ya tukio hilo, kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:•

Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .

•Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.

•Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.

•Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo

•Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo. Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo.

Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu. Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo.

KUOMBA RADHI

Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na *Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII.

Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza “TUNAOMBA RADHI” Mwenyezi MUNGU *aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.

Hashim Lundenga Mkurugenzi
Hapo kwenye red sijaelewa kama ni kuomba radhi ama ni kujitetea!
 
Back
Top Bottom