Lundenga wa Miss Tanzania awaomba radhi watanzania

Hivi jamii forums ni taarifa rasmi?Hashimu amezungumzia tamko rasmi la serikali,hautuwezi kutumia jf kama tamko rasmi mkuu.Tunatakiwa kuwa na upeo wa kufikiri japo kidogo.
 
CCM, TFF, TBC, Maharusi, Kumbi zote za burudani na mabaa yote yalifanya shughuli the same day Miss TZ inafanyika pia yameomba radhi? Wabongo tu dhaifu sana kukaripia mamlaka, tumejua hatuna courage ya kuzisakama mamlaka husika hivyo tumempata mnyonge wa kumtolea hasira zetu na ideal candidate amekua miss tz. Haya maisha yaendelee sasa
 
Ujinga sana, mnajidai kuomba radhi baada ya kustarehe!
Wanapaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu hawa
ili iwe fundisho.
 
Usitishe watu na vitu ambavyo huvijui, hutaki kujua, bali kiherehere kivisemea..soma kwanza uko shallow sana mkuu kuhusu sharia..

Sharia law is most JUST law on Earth..
wewe endelea kuka uchi mpaka upauke
 
Ukiandaa tafrija ya harusi kwa mfano. halafu mzazi wako akafa siku moja kabla ya ya tukio....utaendelea na sherehe kisa umetumia gharama nyingi hivyo unaogopa hasara?
kwani harusi inadhaminiwa?, au ni tukio la kibiashara?. BE RELEVANT!
 
Lundenga hajaomba radhi bali amejitetea huku si kuomba radhi kunakotakiwa kwanza sababu alizotoa ni hafifu...
Amesema waliendelea na tamasha lao kwa vile TFF walikuwa wanamchezo what is this...
Waliendelea kwa vile mabaa yalikuwa wazi shit...
Eti wangechelewa kuwasilisha jina kwani alikuwa anakwenda mbinguni kuwa ukichelewa basi.......
Nafikiri utetezi ni hopeless wameongeza machungu badala ya kupunguza, tuseme basi sababu zao ni za kweli kwa hiyo wanaomba radhi ya nini, kuomba radhi ina maana umetenda ndivyo sivyo walichofanya ni kujitetea si kuomba radhi.
 


13 / 09 / 2011


YAH: KUOMBA RADHI KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR .


Usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba .

Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taaasisi yetu ilikuwa inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011.



Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko mkubwa sana juu ya tukio hilo .
kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-


• Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .


• Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.


• Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.


• Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo


• Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo.


Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo.


Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu.


Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo.


KUOMBA RADHI


Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza "TUNAOMBA RADHI"


Mwenyezi MUNGU aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,


Amina,



Hashim Lundenga


Mkurugenzi




source: hakingowi blog
Kwa jinsi Hashim alivyoomba huu Msamaha ni bora angenyamaza kimya kabixa. Anachotaka kuuaminisha Ulimwengu ni kuwa Tanganyika a.k.a Tanzania Bara hatukuguswa kabisa na haya madhila. Na ndio maana utaona kataja mazingira tofautitofauti..hivi kweli Nchi hii lini tulitangaza msiba wa kitaifa tukaamriwa kufunga Baa??..Si wakati wa Nyerere au Kawawa..baa zilipiga mzigo kama kawaida..sioni mantiki ya kosa kutetewa kwa kosa.
Lakini ukirudi kwa Mizania ya Nani anastahili Lawama nadhani bado Wizara ya Nchimbi inastahili kuwajibishwa..kumuacha Lundenga na baadhi ya watu kuamua aidha kufanya mashindano au lah..ni kuwatwika lawama tu..Serikali from the spoti walitakiwa ileile asubuhi kuutangazia Umma kwamba kuna msiba wa Kitaifa na watu wangeelewa..vinginevyo tumeeamua kumfanya Hashim na Voda yake ''scapegoats''
 
Kama ameomba msamaha asamehewe bila masharti wala masimango, regardless amekuwa mnafiki au vipi!
si imeandikwa samehe saba mara sabini?
La msingi kaomba msamaha.
Tosha naungana na Mr Toyo nimewasamehe.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

13 / 09 / 2011


YAH: KUOMBA RADHI KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR .


Usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba . Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taaasisi yetu ilikuwa inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011.

Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko mkubwa sana juu ya tukio hilo. Kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
  • Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .
  • Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.
  • Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.
  • Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo.
  • Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo.
Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo. Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu.

Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo.

KUOMBA RADHI

Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza “TUNAOMBA RADHI”

Mwenyezi MUNGU aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,

Amina,


Hashim Lundenga

Mkurugenzi

Aisee umeamsha hasira kichizi! Kweli naona kama umekurupushwa mtu yeyote mwenye akili aliyesoma hii barua yako anajua wazi hujaomba RADHI hata kidogo.
 
kwa nini shindano la wakaa uchi lisingesitishwa<br />
shariah law ina umuhimu wake

Okay! Unataka Shariah weye?! Kumbuka nayo ni msumeno, leo utawakatia akina Hashim, siku na wewe yakikukuta utulie vilevile ikukate na wala usilalame kuwa ni mfumo dume.
.
 
Lundenga fanya press na waandishi wa habari ili umma wa watanzania wajue ni kweli kwahaya uliyoyaandika kwenye hiyo Blog kama ni ukweli! kwaupande fulani naona kama hiyo barua niyakizushi haina hata saini wala muhuri wa kamati ya Miss Tanzania naona hii nikama sinema ya kina Kanumba na Ray Kigosi!
 
Yupo Clouds Fm, anasema kuwa wamegundua kuwa wamekosea sana. Kwahiyo alikuwa hajui kama si uungwana kuendelea na maonesho wakati wa msiba?
 
Back
Top Bottom