Luhanjo atoa ripoti, Jairo arudishwa kazini

Itabidi sasa hata viongozi wanaotuhumiwa na ufisadi watengwe na jumuiya za dini zao na kufanyiwa maombi maalumu Mungu awaadhibu na familia zao, maana hii kusafishana kwa serikali ya ****** sijui kutaisha lini.

Mimi nasema hata kama hakuna taasisi 20 ila zilichangwa hela ambazo nikijumlsha haraka haraka naona kama ni mil 518. Ambazo kwa haraka haraka ni kama madawati 3,453 (518m/150,000) tena madawati ya kisasa kabisa.
 
kama pinda aliweza kutoa hukumu palepale, na Shelukindo aliweza kuongea kwa machungu namna hiyo basi mimi binafsi nawaomba hawa waheshimiwa watoe tamko lao kuwa wao watashikilia msimamo wao huo wa jairo kufukuzwa kazi...vinginevyo wajiuzulu na waachane na siasa maana hawatatufaa kama ndio wanaongea kwa hasira halafu wanageukwa na KikweteKikwete
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo,ametoa ripoti na kusema Jairo anarudishwa kazini kuanzia kesho.

===========
UPDATES:

Luhanjo anasema tuhuma zilikuwa za uwongo
Anasema taasisi za Wizara hazizidi 7 na si zaidi ya 20 kama ilivyodaiwa
Taasisi nne tu ndizo zilizochangia na zilichanga karibu TZS 500mil na si zaidi ya 1bil kama ilivyodaiwa
Pesa zilichangwa ili kuwawezesha watendaji watakaoenda kwenye bunge la bajeti
REA walichangia 50mil
TANESCO walichangia 40mil
EWURA waliombwa 40mil lkn hawakutoa, walichangia gharama za chakula na malazi kwa watendaji wa Wizara
Idara ya Uhasibu ya Wizara ilitoa 150mil
Idara ya mipango ya Wizara ilitoa 278mil

More updates to follow


yeah nimesikia kwenye habari zilizovunjikavunjika za ITV mida ya mchana... hivi jamani niambie haya tuseme kuwa haikuwa rushwa ni kuchangia watendaji wa wizara kwenda kushughulika na bajeti bingeni.. hivi ndio zichangwe milioni 500.....

Kha hivi kwa matumizi gani ya kufikia pesa hiyo.. hata hao watendaji wangekuwa 100 na hata kama hilo bunge lingefanyika uswis bado gharama zisingefika huko.. haya sasa masikhara yaani gharama za kwenda kusoma bajeti kwa watendaji wa wizara zifikie milioni 500.

Yaani kama wamemchomoa jairo huko. basi wizara nzima pamoja na waziri wake waadabishwe kwa ufujaji wa makusudi.. watoe takwimu za matumizi ya hizo mil 500 walitumiaje au watazitumiaje.....

HII INCHI NAHISI TULIVAMIA ENEO LA MAKABURI HAIWEZEKANI WATU WANAJIFANYIA MAMBO WANAVYOTAKA TUINAWAANGALIA HKU SIO KULALA NI KUWA MFU.. ngoja nikaangalie ramani ya AFRIKA vizuri pengine hili eneo lilitengwa kwa ajili ya makaburi na ss tumelivamia nakuweka makazi ndio maana tunakuwa mazezeta kiasi hiki.
 
I have no comment! kila mtu ni kula tu kwa kwenda mbele. Naota vurugu zaja nchini.
 
Hii serikali inatupeleka wapi sasa. Mtu ambaye ametuhumiwa kwa uwazi kabisa anarudishwaje tena kazini. It beats me!

Leo imekuaje tena Mwita25 tuko pamoja kwa hili? sababu wewe kila kitu chenye manufaa hua unapinga,hongera na uendelee hivi hivi,issue hapa lipigwe dude nchi nzima kushinikiza gvt iwachukulie hatua wezi wote wa nchi hii
 
Hao ndio viongozi wa Bongland! kama kweli ucchunguzi wa kina ungepita jairo asinge survive maana anazo tuhuma nyingi za wizi na ufisadi achilia hizo tuhuma za Mhe. Beatrice Shellukindo.

Vyombo vyetu haviko makini kabisa ndio maana kila mtu anafanya anavyotaka! Hivi Luhanjo anastaafu lini? JK kwanini anambeba huyu mzee? Kila siku anaongezewa mikataba ina maana hatuna young blood kushika nafasi hiyo?

Tumemchoka Mzee Luhanjo anatupeleka kubaya! yeye na jairo lao moja na wanakula pamoja ndio maana kesi ya ngedere haiamuliwi na nyani.
 
Ningekuwa mimi namfukuza kazi mara moja - PM

Naunga mkono hoja, lazima baraza la mawaziri livunjwe na kumuondoa PM. Huwezi kukaa na PM anayetoa matamshi ya rejareja ya jinsi hii tena bila kufanya utafiti wa kina. Kuendelea kubaki naye rais atakuwa anajitukanisha mbele ya anaowaongoza na mbele ya jairo.
 
Mods naomba ruhusa nitukane kidogo tu, japo kidogo tu nisjekufa kwa presha....pls nasubiri.
 
"...Jairo ambaye yuko chini yake, analazimika kwenda likizo kuanzia juzi ili kupisha uchunguzi wa awali ambao unalenga kubaini iwapo ametenda kosa la kinidhamu kwa mujibu wa sheria zinazoongoza Utumishi wa Mmma.(Philemon Luhanjo kwa mujibu wa nukuu ya Gazeti la Mwananchni)

Kwa mijibu wa hii kauli ya Luhanjo uchunguzi unaofanyika hauna haja na ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwa sababu makosa aliyofanya Jairo yameshapindishwa na si ya rushwa tena na hamna uchunguzi wowote wa rushwa dhidi yake, hivyo kamsafisha na tuhuma za rushwa, wanachofanya sasa ni kumpaka mafuta tu!

Kwa mujibu wa Sheria Na.6 ya 2001 (Public Finance Act) hakuna kosa watakalo mkumba nalo Katibu Mkuu wa Wizara maana yeye ndio Accounting officer wa Wizara na fedha yote ya serikali katika wizara husika ipo chini yake, yeye ndiye mwenye VOTE ya ku-control fedha hizo na matumizi yake hivyo matumizi yeyoye atakayofanya ili mradi yawe na lisiti halali ni sahihi na haki; swali lililo baki hapo na wanalotaka kuja nalo ni kama hayo matumizi si halali au la! Ni kazi rahisi sana, kuwa na lisiti za soda na hotel walizolipa zenye gharama sawa na matumizi yaliyofanyika sidhani kama inawashinda hawa watu ambao hawana hata chembe ya aibu katika nyuso zao.

View attachment 34348
Wanacho angalia watu wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu ni kile kinachoitwa "General accepted accounting practice" yaani kama matumizi yaliyofanyika yakitunzwa vyema ki-hasibu na gharama zake ni bei halali ya soko huo ndio utakao kuwa mwisho wao, swali kwanini hawaku institute uchunguzi wa tuhuma ya rushwa? badala yake Luhanjo anaenda mbali hadi kusema kosa la kinidhamu! Kusema kosa la kinidhamu tayari ni kumsafisa na makosa ya kijinai ambayo ni fraud na corruption.

Ushauri wangu kwa serikali, badala ya kupoteza fedha zaidi kumpaka mafuta Jairo, rais atangaze kuwa Jairo hana kosa na kuwa anampangia kazi nyinge maana haina jinsi yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu na Majeshi yote bado yana mtii na kumpigia Mizinga hasiwe na shaka apunguze matumizi yasiyo lazima katika uchunguzi ambao tayari wameshau elekeza katika dimbwi, awe wazi na atangaze maamuzi yake juu ya Jairo, Pia Pinda kwa mujibu wa maelezo yake bunge alisema Jairo ni wakufukuza tu, ila anamsubiri rais sasa asimamie maneno yake ajiuzulu kama kweli hana unafki katika maneno yake na matendo yake akae pembeni maana ukitofautiana mtazamo na mawazo kiasi cha kuoneka kama hivi ni bora kupisha hili husiwe sehemu ya usafi au uchafu huo unao upinga.


Now i can agree with you
 
? Jamani ni kweli nime confirm hapa Tbc1 Jairo kesho anarudi kazini kwamba tuhuma zilikua si za kweli,dah! najisikia tumbo kuuma kabisa,hivi kweli tutafika ndugu na hii hali
 
Wabunge wa CDM, CUF NCCR , TLP jitokezeni mseme mkiwa bungeni huko zaidi ya wizara ya Jairo mmepokea na kuvuta pesa za "mawasiliano ya bajeti " za wizara gani. Mkisubiri serikali ijipange jinsi ya kujibu mapigo na jinsi ya kuremba hiyorushwa mtaumbukaaaaaaa
 
Nasubiri kibali toka kwa Mods nitoe dukuduku langu japo tuko kwenye mwezi mtukufu
 
Sasa source wako nani??? Na kwanini unaongea issue sensitive namna hiyo kwa ufupi kiasi hicho bila details? Yaani umeniharibia siku yangu leo mara mbili, kwanza kwa kuandika jambo zito kwa ufupi sana, pili kama ni ukweli basi siku yangu leo ndo imekuwa mbaya zaidi!
JF jukwaa la siasa halina uzushi umbea ni michuzi huko na viblog vya udaku pole sana aisee
 
Back
Top Bottom