Dorothy Semu: Hotuba ya Kassimu Majaliwa haina majibu kwa changamoto za wananchi

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
semu.jpg

Hoja saba (7) za Waziri Mkuu Kivuli ACT Wazalendo Ndg. Dorothy Manka Semu kufuatia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu Mapitio ya kazi na mwelekeo wa Serikali na makadirio ya matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2023/2024.

Utangulizi
Juzi Jumatano tarehe 05 April 2023 Waziri Mkuu aliwasilisha Bungeni mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa Fedha wa 2022/2023 jijini Dodoma. Katika kuendeleza wajibu wetu wa kuisimamia Serikali, nikiwa Msemaji Mkuu wa Kamati ya Kuisimamia Serikali ya ACT Wazalendo (Waziri Mkuu Kivuli) ninatoa kwenu maoni machache kuhusu Hotuba ya Waziri Mkuu aliyeitoa Bungeni.

Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu Waziri Mkuu ndiye msimamizi wa shughuli za kila siku za Serikali. Kwa hiyo ni matarajio ya wengi kuwa hotuba ya Waziri Mkuu ingekuja na mwelekeo na majawabu ambayo yangesaidia kutatua changamoto mbalimbali ambazo nchi yetu inakabiliana nazo kwa sasa zikiwemo changamoto za hali ya kiuchumi, mwenendo wa kisiasa na hali ya usalama.

Hivyo basi kutokana na uchambuzi wetu, tumeona yapo masuala makubwa saba (7) yanayohusu maisha ya watu ya kila siku hayajaguswa kwa kupatiwa ufumbuzi.

i. Hali ngumu ya maisha
Suala la hali ya maisha ya wananchi (hususani mfumuko wa bei na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu) bado Serikali haijaweka mkazo kujiandaa kukabiliana na mwenendo huu kiasi cha kutoa nafuu kwa wananchi.

Licha ya kuwepo kwa vilio kutoka kwa wananchi kila kona ya nchi yetu kwa miaka miwili mfululizo. Hotuba ya Waziri Mkuu inataja takwimu za kitaalamu (ambazo hazigusi uhalisia) kuonyesha kama hali ni nzuri.

Hofu yetu ni kuwa mwelekeo huu wa Serikali unaweza kupelekea kipindi kijacho tena kuwa kwenye hali ngumu zaidi kwakuwa hakuna hatua madhubuti za kutoa nafuu kwa wananchi.

Tulipohitimisha ziara ya mikutano ya hadhara tulieleza na kuishauri Serikali ichukue hatua kadhaa kujiandaa na kukabiliana na mwenendo huu mbaya.

Aidha, tulitoa rai kwa Serikali kuchukuwa wajibu wake badala ya kuendelea kulalamika au kutoa tu maelezo ya kwamba hali hii ni duniani kote.

Waziri Mkuu kwenye hotuba yake ambayo inatoa mwelekeo wa Serikali inaacha hofu kubwa kwamba Serikali haijajiandaa na wala kuwawezesha wananchi kukabiliana na mwenendo huu hali itaendelea kuwa hivi hivi au itegemee neema za maulana bila jitihada za makusudi.

ACT Wazalendo tunaielekeza Serikali kununua na kuhifadhi chakula cha kutosha angalau miezi 3 kutokana na chakula kitachovunwa mwaka huu ili kujilinda na upungufu wa chakula. Kutokana na ukweli kuwa kwa maeneo mengi nchini uzalishaji unaweza kuwa sio mzuri kwa mwaka huu.

Hatua hii itawezakana kwa Serikali kujenga uwezo wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa kutenga bajeti ya kutosha ya kununua chakula (Tani Milioni 1.5 za Mahindi, Tani laki 5 za Mpunga, Maharagwe tani Milioni 1). Aidha, kuwezeshwa Bodi ya mazao mchanganyiko kununua na kusambaza chakula kwenye eneo linaloonyesha uhaba/upungufu wa chakula.

Mwisho, Serikali iweke mazingira bora kwa wakulima wadogo ili kuongeza uzalishaji zaidi; kwa kuendelea kutoa ruzuku katika mbolea na kusimamia usambazaji wake; kuhakikisha usalama wa ardhi kwa Wakulima wadogo kwa kushughulikia migogoro ya ardhi.

ii. Suala la hali ya ukosefu wa ajira na maslahi ya wafanyakazi nchini.
Ofisi ya Waziri Mkuu inahusika moja kwa moja na masuala ya ajira na uwezeshaji kupitia Wizara ya Vijana, kazi na ajira.

Mwenendo na hali ya ukosefu wa ajira nchini inazidi kuwa tata sana, uchumi wetu unazidi kupunguza uwezekano wa kuzalishaji ajira zenye staha na shughuli za kueleweka za kuwapatia vijana vipato ili kumudu maisha yao. Takwimu zinaonyesha ukweli kwa namna tofauti tofauti.

Athari za janga hili ni kubwa sana katika jamii yetu kwa sasa, ikiwemo; kuongezeka kwa wimbi la umasikini na utegemezi, kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili na uhalifu nchini ikiwemo vitendo vya wizi, ukahaba, unyang’anyi, uporaji.

Kuongezeka kwa upendeleo, kujuana, rushwa katika utolewaji wa kazi, kuongezeka kwa utumikishaji wa watoto kwa ujira mdogo au bila malipo hususani; mashuleni, viwandani, majumbani, migodini nk kwa kigezo cha kupatiwa ajira.

Katika hotuba ya Waziri inaonyesha wazi Serikali haitoi kipaumbele kushughulikia janga la ajira. Tunashuhudia mahitaji makubwa ya wafanyakazi na watumishi tena kwenye sekta nyeti kama vile elimu, afya na kilimo.

Lakini Serikali haijaweka mkazo kabisa kwenye kuhakikisha sekta hizo zinapata wataalamu na watumishi, licha ya kuwepo kwa wataalamu waliosomeshwa kwa gharama kubwa, Serikali ina waacha mtaani. ACT Wazalendo tunaitaka Serikali isikwepe wajibu wake wa kutoa ajira kwa vijana ili kwenda kuimarisha huduma za elimu, afya na kilimo na maeneo mengine yenye uhitaji.

Pili, Malalamiko ya wafanyakazi wa vyeti vya darasa la saba kutorudishwa kazini au kutopatiwa stahiki zao. Kwa mwaka huu tumepokea malalamiko ya waliokuwa watumishi wa TANESCO, Shirika la Maendeleo Dar es Salaam (DDC), Shirika la Bima la Taifa na maeneo mengi ya halmashauri.

Malalamiko yao kuondolewa kazi kimakosa lakini wengine kurudishwa kazini na wengine kuachwa mtaani. Wapo pia ambao wamefikia umri wao wa kustaafu lakini hawajapata stahiki zao.

Katika hotuba ya Waziri Mkuu ilitarajiwa kuona umetolewa utaratibu mzuri wa kushughulikia matatizo ya kundi hili kubwa ambalo halijui hatima yake na hivyo kuachwa wakining'inia.

Tatu, kuhusu kikotoo cha mafao (pensheni) bado wafanyakazi wanalalamikia kanuni mpya za ukokotoaji wa mafao ambazo zimeanza kutekelezwa mwaka jana Julai.

Kikotoo hiki kilipigiwa kelele sana na wafanyakazi kwakuwa hazingatii maslahi ya wastaafu wa nchi hii. Kanuni hizi zinawaumiza kwa sana wastaafu kwa kuwapunja mafao yao karibia nusu ya kiinua mgongo kinashikiliwa na Serikali, kinafupisha muda wa kuhudumiwa na kupoteza kiasi kikubwa cha mafao.

ACT Wazalendo tulizipinga kanuni hizi na kutoa rai kwa Serikali kurejesha kanuni za mwaka 2017 ambao zilikuwa zinamwezesha mfanyakazi angalau kupata kiwango cha kuishi kwa staha na kumudu maisha yake baada ya kulitumikia taifa.

Nne, kuhusu hali ya wafanyakazi katika sekta binafsi (usafirishaji); kuna malalamiko ya muda mrefu ya madereva wa masafa marefu kuhusu kupunjwa posho za kujikimu, kutopatiwa mikataba ya kazi na hali mbaya ya usalama wakati wanasafirisha mizigo.

Ingawa Serikali imeweka kima cha chini cha mishahara kwa madereva bado wanalipwa kiduchu na bila kufuata utaratibu wa ajira na maslahi yao.

ACT Wazalendo tunatoa wito kwa Serikali kuitazama sekta ya uchukuzi na usafirishaji kwa umuhimu mkubwa kwa kuwasimamia kupata haki na stahiki zao.

iii. Kuhamishwa kwa wananchi (jamii ya wafugaji) Ngorongoro
Katika hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri mkuu ameleza kuwa mchakato wa kuwahamisha kwa hiyari wananchi wa jamiii ya wafugaji katika hifadhi ya Ngorongoro limefanyika kwa kuzingatia haki za wanaohama, Waziri Mkuu anasema katika hotuba yake ukurasa wa 39 anasema” zoezi hilo limefanyika kwa umakini mkubwa na kwa kuzingatia haki za wanaohama.

Hadi kufikia Januari, 2023 jumla ya kaya 1,524 zenye watu 8,715 na mifugo 32,842 zilikuwa zimejiandikisha kwa ajili ya kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera. Kati ya kaya hizo, kaya 551 zenye39 watu 3,010 na mifugo 15,521 tayari zimehamishwa kwa hiari kwenda Msomera.”

Jambo hili si kweli, Serikali imewahamisha wananchi wa Ngorongoro kwa nguvu kubwa, ukweli ni kwamba tarehe 10 Juni 2022 katika Kijiji cha Loliondo kulijitokeza mapigano kati ya askari wa jeshi la Polisi dhidi ya wananchi kutoka katika vijiji 14. Taarifa zinaonyesha kuwa Juni 7, 2022 vikosi vya ulinzi viliwasili Loliondo kwa magari mengi na silaha.

Jeshi la polisi, FFU, mgambo, na watu waliovalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania walionekana wakielekea kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita mraba 1,500 lilalokusudiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba.

Na katika kusimika vigingi kwa kuingiza eneo la vijiji katika pori la akiba wananchi waliungana na kuingilia zoezi hilo ikapelekea Mapigano baina ya Jeshi la Polisi yalipelekea kujeruhi wananchi wapatao 14 kati yao wanawake ni wanane (na vikongwe wawili (2) na askari polisi mmoja ameuwawa.

Suala la ngorongoro ni sehemu tu ya matukio ya mamlaka za hifadhi kutumia nguvu katika kupora maeneo ya wananchi na kuleta madhara makubwa kwa jamii.

Ni wakati sasa wa Serikali kuwalipa fidia stahiki kwani kuna uharibifu walioufanya na kuwahamisha makazi yao bila matakwa yao ambayo imepelekea kukwamisha shughuli zao za kimaendeleo pia wengine kupoteza baadhi ya mali zao.

iv. Kukosekana kwa uratibu wa kukabiliana na maafa.

Ofisi ya Waziri inashughulikia na uratibu wa maafa na kukabiliana na majanga mbalimbali. Pamoja na hotuba ya Waziri Mkuu kuanzisha hatua za kufanya mapitio ya sheria na kutungwa kwa sheria kadhaa mwaka uliopita bado tunaona Ofisi ya Waziri Mkuu haijakuwa na uratibu mzuri wa kukabiliana na maafa.

Mifano ya kuendelea kutokea kwa matukio ya kuungua kwa masoko ya Wafanyabiashara hapa nchini ni moja ya mifano ya kuonyesha kuwa bado hakuna jitihada madhubuti za kukabiliana na maafa. Matukio ya ajali kadhaa yanayonyesha uwezo wa wizara na taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu bado ni mdogo kwenye shughuli za uokoaji.

Kwenye hotuba, hatujaona hatua za makusudi za kujenga uwezo wa kibajeti kununua vifaa vya kisasa vya uokoaji, kujenga uwezo wa Idara ya maafa na taasisi zilizo chini yake. ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kutenga bajeti (fedha) za kutosha ili kujenga uwezo wa idara ya maafa na kuongeza ufanisi wa usimamizi wa idara hiyo. Pia ni muhimu Kujenga uwezo kwa kutumia teknolojia juu ya kufuatilia maafa sehemu mbalimbali za nchi.

Jambo jingine, kuwepo kwa malalamiko ya kupunjwa na kutolipwa fidia wahanga (1361) wa mabomu ya Mbagala tangu mwaka 2009.

Hata hivyo, ni jambo la kusikitisha kuona licha ya kunyimwa kucheleweshewa kwa haki zao wamekuwa wakipokea majibu ya kukatisha tamaa, kejeli na vitisho toka kwa watumishi wa Serikali ikiwemo watumishi toka Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa.

ACT Wazalendo inatoa rai kwa Waziri Mkuu kuhakikisha mwaka huu wanafuatilia suala hili na kuwafuta machozi wahanga hao kwa kuwalipa fidia ya haki.

v. Kucheleweshwa kwa Miradi Mikakati na kutokamilika kuondoa umaskini wa wananchi.
Katika uelekeo wa jumla wa Serikali, hotuba ya Waziri Mkuu imeelezea azma ya kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchini.

Tunatambua jitihada hizo za kuendeleza na kukamilisha miradi hiyo kwa hatua mbalimbali. Ingawa, ACT Wazalendo inasikitishwa sana na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi hii jambo linalopelekea hasara kwa taifa kwa kulipa fedha za ziada kwa wakandarasi.

Mathalani Mradi wa Bwawa la Nyerere ulipaswa kukamilika 2022 umeongezewa muda wa miaka miwili zaidi hadi 2024 na kulitia taifa hasara ya Shilingi Bilioni 327.93. Mradi SGR kipande cha Dar- Morogoro kilipaswa kukamilika Novemba 2019.

Ongezeko la muda wa siku 1414 kwa mujibu wa ripoti ya CAG imetusababishia hasara ya Shilingi za kitanzania Bilioni 26.37 ambazo anapaswa kulipwa mkandarasi Mshauri.

Aidha kuandaliwa na kuwezeshwa kikamilifu wazawa kushiriki na kufaidika na uwekezaji (local contents); hatujaona hatua madhubuti za kuhakikisha Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inawaandaa vijana (Watanzania) kuipokea miradi hii.

Miradi ya Reli ya kisasa (SGR), Mradi wa Bomba la Mafuta, Mradi wa kusindika Gesi asilia Lindi (LNG) bado yapo malalamiko ya kutoandaliwa kwa wazawa uwezo wa kuendesha, kupata ajira na kunufaika na miradi hii.

Hotuba ya Waziri Mkuu haijagusa kabisa namna ya kutatua changamoto wanazo kabiliana nazo vijana kwenye kupata ajira kwenye miradi hii, kuandaliwa ili kuendesha na kusimamia kwa siku za usoni na viwango vya ujira wao wanapopata kazi.

Mwisho, malalamiko ya wananchi wanaopisha miradi kutolipwa fidia za haki au kucheleweshewa kwa malipo ya fidia. Rai yetu kwa Serikali kuwa ije na Sera mpya ya fidia kwa wananchi wanaopisha maeneo ya uwekezaji.

Sera itakayobeba utaratibu wa ardhi kwa uwekezaji (Land for Equity) uanze kutumika katika miradi yote nchini ambapo ardhi ya wananchi itumike kama mtaji katika mradi na hivyo kuzipa Serikali za mitaa za maeneo husika umiliki katika miradi.

Wananchi wajengewe makazi mbadala maeneo yaliyopimwa na yenye huduma zote za kijamii na vile vile wapewe shughuli mbadala za kiuchumi kama vile ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kilimo.

vi. Hali ya usalama wa wananchi
Hali ya usalama wa raia kwenye baadhi ya maeneo kuonekana kuwa ni mbaya. Tulipokuwa kwenye ziara kwenye mikoa tisa (9) tuliwaeleza waandishi kwamba tulikutana na malalamiko ya matukio ya utekekaji, kupotea kwa watu kwenye baadhi ya maeneo kama vile Kasulu, Kigoma Mjini na kuwepo kwa tishio kwa wananchi katika ukanda wa Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

Hata hivyo, tulipokea taarifa ya matukio ya namna hiyo pia kwenye mkoa wa Simiyu. Hata Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Ndg. Shamsha Mohammed kupata ujasiri wa kumweleza Waziri Mkuu alipokuwa kwenye ziara yake tarehe 25 Machi 2023.

Taarifa zinaonyesha kuwa wananchi wanapotea, wanauwawa na kuokotwa kwenye mifuko ya Rambo. Jeshi la Polisi halishughulikii masuala haya kwa weledi badala yake linapotosha ukweli huu.

Kwenye hotuba ya Waziri Mkuu hatujasikia hatua zilizochukuliwa hadi sasa na Serikali kukabiliana na madhila haya. Hivyo tunaitaka Serikali ichukue hatua zifuatazo ili kuhakikisha nchi yetu inarejea kwenye usalama na amani;

Mosi, kulitaka Jeshi la Polisi kushughulikia vijana wanne (4) waliotekwa Kigoma Mjini na mmoja Kasulu Mjini.

Pili, Serikali iondoe ukanda wa MKIRU kama ukanda wa Kijeshi (Urejeshwe utawala wa kirai) iwaondoe watumishi (watendaji, Maafisa maendeleo) wanajeshi kwenye vijiji na ngazi za Wilaya.

Tatu, Tume inayoshughulikia mfumo wa haki jinai iongezewe jukumu la kufanya uchunguzi wa matukio yote ya utekaji na mauaji ya raia wasio na hatia, waliohusika wachukuliwe hatua ili iwe funzo kwa wengine.

Nne, familia (wategemezi) zilizopoteza ndugu zao au kupata hasara yoyote zilipwe fidia ili kuwasaidia watumbukie kwenye umaskini.

Mwisho, Serikali ipanue majukwaa ya maridhiano hadi kwa ngazi za chini kwa wananchi, viongozi na vyama siasa ili kurejesha hali ya kuaminiana, kuheshimiana na umoja.

vii. Mageuzi ya kidemokrasia
Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia mchakato wa mageuzi ya sheria za kisiasa nchini. Tume Huru ya Uchaguzi ambayo inapaswa sasa hivi kuanza kuandaa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio huru.

Katika Hotuba ya Waziri Mkuu amezungumzia marekebisho ya Sheria badala ya mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi ili kuifanya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa huru kwa kuajiri wafanyakazi wake yenyewe na kusimamia chaguzi zote nchini ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.

Hotuba yake imetoa utaratibu wa kawaida wa Tume na Ofisi ya Waziri Mkuu wa kupitia sheria kila baada ya muda fulani bila kuzingatia maoni ya wadau kuhusu maridhiano yanayotaka kutungwa upya kwa sheria zote zinahusu masuala ya Uchaguzi.

Hivyo, tunaitaka Serikali kuharakisha hatua za utekelezaji wa masuala haya kwa kuchukua hatua zifuatazo;

Mosi, tunarudia wito wetu kuwa Serikali itoe ratiba ya utekelezaji wa mageuzi ya kisiasa kama ilivyo kwenye mapendekezo ya kikosi kazi hatua kwa hatua ili itakapofika mwezi Novemba mwaka huu (2023) tuwe na Sheria mpya ya vyama vya Siasa, Sheria mpya ya uchaguzi na kwamba marekebisho ya Sheria ya mchakato wa Katiba mpya yawe yamefanyika na kuundwa kwa kamati ya wataalamu watakaowianisha rasimu ya katiba ya Warioba na Katiba pendekezwa ili kupata rasimu mpya ya katiba itakayopigiwa kura na wananchi.

Hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu ieleze lini muswada wa Sheria ya vyama vingi vya Siasa 2023 na Muswada wa Sheria ya Uchaguzi 2023 utafikishwa Bungeni.

Tunakata muswada wa kuhuisha mchakato wa Katiba Mpya (amendment to constitutional review act 2011) ili kukwamua mchakato wa Katiba mpya kwa mujibu wa mapendekezo ya Kikosi Kazi.
Imetolewa na;

Ndg. Dorothy Semu
Waziri Mkuu Kivuli,
ACT Wazalendo
07 April, 2023.
Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu Waziri Mkuu ndiye msimamizi wa shughuli za kila siku za Serikali. Kwa hiyo ni matarajio ya wengi kuwa hotuba ya Waziri Mkuu ingekuja na mwelekeo na majawabu ambayo yangesaidia kutatua changamoto mbalimbali ambazo nchi yetu inakabiliana nazo kwa sasa zikiwemo changamoto za hali ya kiuchumi, mwenendo wa kisiasa na hali ya usalama. Hivyo basi kutokana na uchambuzi wetu, tumeona yapo masuala makubwa saba (7) yanayohusu maisha ya watu ya kila siku hayajaguswa kwa kupatiwa ufumbuzi.

i. Hali ngumu ya maisha
Suala la hali ya maisha ya wananchi (hususani mfumuko wa bei na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu) bado Serikali haijaweka mkazo kujiandaa kukabiliana na mwenendo huu kiasi cha kutoa nafuu kwa wananchi. Licha ya kuwepo kwa vilio kutoka kwa wananchi kila kona ya nchi yetu kwa miaka miwili mfululizo.

Hotuba ya Waziri Mkuu inataja takwimu za kitaalamu (ambazo hazigusi uhalisia) kuonyesha kama hali ni nzuri.
Hofu yetu ni kuwa mwelekeo huu wa Serikali unaweza kupelekea kipindi kijacho tena kuwa kwenye hali ngumu zaidi kwakuwa hakuna hatua madhubuti za kutoa nafuu kwa wananchi. Tulipohitimisha ziara ya mikutano ya hadhara tulieleza na kuishauri Serikali ichukue hatua kadhaa kujiandaa na kukabiliana na mwenendo huu mbaya. Aidha, tulitoa rai kwa Serikali kuchukuwa wajibu wake badala ya kuendelea kulalamika au kutoa tu maelezo ya kwamba hali hii ni duniani kote.

Waziri Mkuu kwenye hotuba yake ambayo inatoa mwelekeo wa Serikali inaacha hofu kubwa kwamba Serikali haijajiandaa na wala kuwawezesha wananchi kukabiliana na mwenendo huu hali itaendelea kuwa hivi hivi au itegemee neema za maulana bila jitihada za makusudi.
ACT Wazalendo tunaielekeza Serikali kununua na kuhifadhi chakula cha kutosha angalau miezi 3 kutokana na chakula kitachovunwa mwaka huu ili kujilinda na upungufu wa chakula. Kutokana na ukweli kuwa kwa maeneo mengi nchini uzalishaji unaweza kuwa sio mzuri kwa mwaka huu.

Hatua hii itawezakana kwa Serikali kujenga uwezo wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa kutenga bajeti ya kutosha ya kununua chakula (Tani Milioni 1.5 za Mahindi, Tani laki 5 za Mpunga, Maharagwe tani Milioni 1). Aidha, kuwezeshwa Bodi ya mazao mchanganyiko kununua na kusambaza chakula kwenye eneo linaloonyesha uhaba/upungufu wa chakula.
Mwisho, Serikali iweke mazingira bora kwa wakulima wadogo ili kuongeza uzalishaji zaidi; kwa kuendelea kutoa ruzuku katika mbolea na kusimamia usambazaji wake; kuhakikisha usalama wa ardhi kwa Wakulima wadogo kwa kushughulikia migogoro ya ardhi.

ii. Suala la hali ya ukosefu wa ajira na maslahi ya wafanyakazi nchini.
Ofisi ya Waziri Mkuu inahusika moja kwa moja na masuala ya ajira na uwezeshaji kupitia Wizara ya Vijana, kazi na ajira. Mwenendo na hali ya ukosefu wa ajira nchini inazidi kuwa tata sana, uchumi wetu unazidi kupunguza uwezekano wa kuzalishaji ajira zenye staha na shughuli za kueleweka za kuwapatia vijana vipato ili kumudu maisha yao. Takwimu zinaonyesha ukweli kwa namna tofauti tofauti.

Athari za janga hili ni kubwa sana katika jamii yetu kwa sasa, ikiwemo; kuongezeka kwa wimbi la umasikini na utegemezi, kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili na uhalifu nchini ikiwemo vitendo vya wizi, ukahaba, unyang’anyi, uporaji. Kuongezeka kwa upendeleo, kujuana, rushwa katika utolewaji wa kazi, kuongezeka kwa utumikishaji wa watoto kwa ujira mdogo au bila malipo hususani; mashuleni, viwandani, majumbani, migodini nk kwa kigezo cha kupatiwa ajira.

Katika hotuba ya Waziri inaonyesha wazi Serikali haitoi kipaumbele kushughulikia janga la ajira. Tunashuhudia mahitaji makubwa ya wafanyakazi na watumishi tena kwenye sekta nyeti kama vile elimu, afya na kilimo. Lakini Serikali haijaweka mkazo kabisa kwenye kuhakikisha sekta hizo zinapata wataalamu na watumishi, licha ya kuwepo kwa wataalamu waliosomeshwa kwa gharama kubwa, Serikali ina waacha mtaani. ACT Wazalendo tunaitaka Serikali isikwepe wajibu wake wa kutoa ajira kwa vijana ili kwenda kuimarisha huduma za elimu, afya na kilimo na maeneo mengine yenye uhitaji.

Pili, Malalamiko ya wafanyakazi wa vyeti vya darasa la saba kutorudishwa kazini au kutopatiwa stahiki zao. Kwa mwaka huu tumepokea malalamiko ya waliokuwa watumishi wa TANESCO, Shirika la Maendeleo Dar es Salaam (DDC), Shirika la Bima la Taifa na maeneo mengi ya halmashauri. Malalamiko yao kuondolewa kazi kimakosa lakini wengine kurudishwa kazini na wengine kuachwa mtaani. Wapo pia ambao wamefikia umri wao wa kustaafu lakini hawajapata stahiki zao.

Katika hotuba ya Waziri Mkuu ilitarajiwa kuona umetolewa utaratibu mzuri wa kushughulikia matatizo ya kundi hili kubwa ambalo halijui hatima yake na hivyo kuachwa wakining’inia.
Tatu, kuhusu kikotoo cha mafao (pensheni) bado wafanyakazi wanalalamikia kanuni mpya za ukokotoaji wa mafao ambazo zimeanza kutekelezwa mwaka jana Julai.

Kikotoo hiki kilipigiwa kelele sana na wafanyakazi kwakuwa hazingatii maslahi ya wastaafu wa nchi hii. Kanuni hizi zinawaumiza kwa sana wastaafu kwa kuwapunja mafao yao karibia nusu ya kiinua mgongo kinashikiliwa na Serikali, kinafupisha muda wa kuhudumiwa na kupoteza kiasi kikubwa cha mafao. ACT Wazalendo tulizipinga kanuni hizi na kutoa rai kwa Serikali kurejesha kanuni za mwaka 2017 ambao zilikuwa zinamwezesha mfanyakazi angalau kupata kiwango cha kuishi kwa staha na kumudu maisha yake baada ya kulitumikia taifa.

Nne, kuhusu hali ya wafanyakazi katika sekta binafsi (usafirishaji); kuna malalamiko ya muda mrefu ya madereva wa masafa marefu kuhusu kupunjwa posho za kujikimu, kutopatiwa mikataba ya kazi na hali mbaya ya usalama wakati wanasafirisha mizigo. Ingawa Serikali imeweka kima cha chini cha mishahara kwa madereva bado wanalipwa kiduchu na bila kufuata utaratibu wa ajira na maslahi yao.
ACT Wazalendo tunatoa wito kwa Serikali kuitazama sekta ya uchukuzi na usafirishaji kwa umuhimu mkubwa kwa kuwasimamia kupata haki na stahiki zao.

iii. Kuhamishwa kwa wananchi (jamii ya wafugaji) Ngorongoro
Katika hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri mkuu ameleza kuwa mchakato wa kuwahamisha kwa hiyari wananchi wa jamiii ya wafugaji katika hifadhi ya Ngorongoro limefanyika kwa kuzingatia haki za wanaohama, Waziri Mkuu anasema katika hotuba yake ukurasa wa 39 anasema” zoezi hilo limefanyika kwa umakini mkubwa na kwa kuzingatia haki za wanaohama.

Hadi kufikia Januari, 2023 jumla ya kaya 1,524 zenye watu 8,715 na mifugo 32,842 zilikuwa zimejiandikisha kwa ajili ya kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera. Kati ya kaya hizo, kaya 551 zenye39 watu 3,010 na mifugo 15,521 tayari zimehamishwa kwa hiari kwenda Msomera.”

Jambo hili si kweli, Serikali imewahamisha wananchi wa Ngorongoro kwa nguvu kubwa, ukweli ni kwamba tarehe 10 Juni 2022 katika Kijiji cha Loliondo kulijitokeza mapigano kati ya askari wa jeshi la Polisi dhidi ya wananchi kutoka katika vijiji 14. Taarifa zinaonyesha kuwa Juni 7, 2022 vikosi vya ulinzi viliwasili Loliondo kwa magari mengi na silaha.

Jeshi la polisi, FFU, mgambo, na watu waliovalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania walionekana wakielekea kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita mraba 1,500 lilalokusudiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba. Na katika kusimika vigingi kwa kuingiza eneo la vijiji katika pori la akiba wananchi waliungana na kuingilia zoezi hilo ikapelekea Mapigano baina ya Jeshi la Polisi yalipelekea kujeruhi wananchi wapatao 14 kati yao wanawake ni wanane (na vikongwe wawili (2) na askari polisi mmoja ameuwawa.

Suala la ngorongoro ni sehemu tu ya matukio ya mamlaka za hifadhi kutumia nguvu katika kupora maeneo ya wananchi na kuleta madhara makubwa kwa jamii.
Ni wakati sasa wa Serikali kuwalipa fidia stahiki kwani kuna uharibifu walioufanya na kuwahamisha makazi yao bila matakwa yao ambayo imepelekea kukwamisha shughuli zao za kimaendeleo pia wengine kupoteza baadhi ya mali zao.

iv. Kukosekana kwa uratibu wa kukabiliana na maafa.
Ofisi ya Waziri inashughulikia na uratibu wa maafa na kukabiliana na majanga mbalimbali. Pamoja na hotuba ya Waziri Mkuu kuanzisha hatua za kufanya mapitio ya sheria na kutungwa kwa sheria kadhaa mwaka uliopita bado tunaona Ofisi ya Waziri Mkuu haijakuwa na uratibu mzuri wa kukabiliana na maafa.
Mifano ya kuendelea kutokea kwa matukio ya kuungua kwa masoko ya Wafanyabiashara hapa nchini ni moja ya mifano ya kuonyesha kuwa bado hakuna jitihada madhubuti za kukabiliana na maafa. Matukio ya ajali kadhaa yanayonyesha uwezo wa wizara na taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu bado ni mdogo kwenye shughuli za uokoaji.

Kwenye hotuba, hatujaona hatua za makusudi za kujenga uwezo wa kibajeti kununua vifaa vya kisasa vya uokoaji, kujenga uwezo wa Idara ya maafa na taasisi zilizo chini yake. ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kutenga bajeti (fedha) za kutosha ili kujenga uwezo wa idara ya maafa na kuongeza ufanisi wa usimamizi wa idara hiyo. Pia ni muhimu Kujenga uwezo kwa kutumia teknolojia juu ya kufuatilia maafa sehemu mbalimbali za nchi.

Jambo jingine, kuwepo kwa malalamiko ya kupunjwa na kutolipwa fidia wahanga (1361) wa mabomu ya Mbagala tangu mwaka 2009. Hata hivyo, ni jambo la kusikitisha kuona licha ya kunyimwa kucheleweshewa kwa haki zao wamekuwa wakipokea majibu ya kukatisha tamaa, kejeli na vitisho toka kwa watumishi wa Serikali ikiwemo watumishi toka Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa. ACT Wazalendo inatoa rai kwa Waziri Mkuu kuhakikisha mwaka huu wanafuatilia suala hili na kuwafuta machozi wahanga hao kwa kuwalipa fidia ya haki.
v. Kucheleweshwa kwa Miradi Mikakati na kutokamilika kuondoa umaskini wa wananchi.
Katika uelekeo wa jumla wa Serikali, hotuba ya Waziri Mkuu imeelezea azma ya kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchini.

Tunatambua jitihada hizo za kuendeleza na kukamilisha miradi hiyo kwa hatua mbalimbali. Ingawa, ACT Wazalendo inasikitishwa sana na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi hii jambo linalopelekea hasara kwa taifa kwa kulipa fedha za ziada kwa wakandarasi. Mathalani Mradi wa Bwawa la Nyerere ulipaswa kukamilika 2022 umeongezewa muda wa miaka miwili zaidi hadi 2024 na kulitia taifa hasara ya Shilingi Bilioni 327.93. Mradi SGR kipande cha Dar- Morogoro kilipaswa kukamilika Novemba 2019. Ongezeko la muda wa siku 1414 kwa mujibu wa ripoti ya CAG imetusababishia hasara ya Shilingi za kitanzania Bilioni 26.37 ambazo anapaswa kulipwa mkandarasi Mshauri.

Aidha kuandaliwa na kuwezeshwa kikamilifu wazawa kushiriki na kufaidika na uwekezaji (local contents); hatujaona hatua madhubuti za kuhakikisha Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inawaandaa vijana (Watanzania) kuipokea miradi hii. Miradi ya Reli ya kisasa (SGR), Mradi wa Bomba la Mafuta, Mradi wa kusindika Gesi asilia Lindi (LNG) bado yapo malalamiko ya kutoandaliwa kwa wazawa uwezo wa kuendesha, kupata ajira na kunufaika na miradi hii.

Hotuba ya Waziri Mkuu haijagusa kabisa namna ya kutatua changamoto wanazo kabiliana nazo vijana kwenye kupata ajira kwenye miradi hii, kuandaliwa ili kuendesha na kusimamia kwa siku za usoni na viwango vya ujira wao wanapopata kazi.
Mwisho, malalamiko ya wananchi wanaopisha miradi kutolipwa fidia za haki au kucheleweshewa kwa malipo ya fidia. Rai yetu kwa Serikali kuwa ije na Sera mpya ya fidia kwa wananchi wanaopisha maeneo ya uwekezaji. Sera itakayobeba utaratibu wa ardhi kwa uwekezaji (Land for Equity) uanze kutumika katika miradi yote nchini ambapo ardhi ya wananchi itumike kama mtaji katika mradi na hivyo kuzipa Serikali za mitaa za maeneo husika umiliki katika miradi.

Wananchi wajengewe makazi mbadala maeneo yaliyopimwa na yenye huduma zote za kijamii na vile vile wapewe shughuli mbadala za kiuchumi kama vile ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kilimo.
vi. Hali ya usalama wa wananchi
Hali ya usalama wa raia kwenye baadhi ya maeneo kuonekana kuwa ni mbaya. Tulipokuwa kwenye ziara kwenye mikoa tisa (9) tuliwaeleza waandishi kwamba tulikutana na malalamiko ya matukio ya utekekaji, kupotea kwa watu kwenye baadhi ya maeneo kama vile Kasulu, Kigoma Mjini na kuwepo kwa tishio kwa wananchi katika ukanda wa Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

Hata hivyo, tulipokea taarifa ya matukio ya namna hiyo pia kwenye mkoa wa Simiyu. Hata Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Ndg. Shamsha Mohammed kupata ujasiri wa kumweleza Waziri Mkuu alipokuwa kwenye ziara yake tarehe 25 Machi 2023. Taarifa zinaonyesha kuwa wananchi wanapotea, wanauwawa na kuokotwa kwenye mifuko ya Rambo. Jeshi la Polisi halishughulikii masuala haya kwa weledi badala yake linapotosha ukweli huu.
Kwenye hotuba ya Waziri Mkuu hatujasikia hatua zilizochukuliwa hadi sasa na Serikali kukabiliana na madhila haya. Hivyo tunaitaka Serikali ichukue hatua zifuatazo ili kuhakikisha nchi yetu inarejea kwenye usalama na amani;

Mosi, kulitaka Jeshi la Polisi kushughulikia vijana wanne (4) waliotekwa Kigoma Mjini na mmoja Kasulu Mjini.
Pili, Serikali iondoe ukanda wa MKIRU kama ukanda wa Kijeshi (Urejeshwe utawala wa kirai) iwaondoe watumishi (watendaji, Maafisa maendeleo) wanajeshi kwenye vijiji na ngazi za Wilaya.
Tatu, Tume inayoshughulikia mfumo wa haki jinai iongezewe jukumu la kufanya uchunguzi wa matukio yote ya utekaji na mauaji ya raia wasio na hatia, waliohusika wachukuliwe hatua ili iwe funzo kwa wengine.
Nne, familia (wategemezi) zilizopoteza ndugu zao au kupata hasara yoyote zilipwe fidia ili kuwasaidia watumbukie kwenye umaskini.

Mwisho, Serikali ipanue majukwaa ya maridhiano hadi kwa ngazi za chini kwa wananchi, viongozi na vyama siasa ili kurejesha hali ya kuaminiana, kuheshimiana na umoja.

vii. Mageuzi ya kidemokrasia
Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia mchakato wa mageuzi ya sheria za kisiasa nchini. Tume Huru ya Uchaguzi ambayo inapaswa sasa hivi kuanza kuandaa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio huru. Katika Hotuba ya Waziri Mkuu amezungumzia marekebisho ya Sheria badala ya mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi ili kuifanya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa huru kwa kuajiri wafanyakazi wake yenyewe na kusimamia chaguzi zote nchini ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Hotuba yake imetoa utaratibu wa kawaida wa Tume na Ofisi ya Waziri Mkuu wa kupitia sheria kila baada ya muda fulani bila kuzingatia maoni ya wadau kuhusu maridhiano yanayotaka kutungwa upya kwa sheria zote zinahusu masuala ya Uchaguzi.

Hivyo, tunaitaka Serikali kuharakisha hatua za utekelezaji wa masuala haya kwa kuchukua hatua zifuatazo;
Mosi, tunarudia wito wetu kuwa Serikali itoe ratiba ya utekelezaji wa mageuzi ya kisiasa kama ilivyo kwenye mapendekezo ya kikosi kazi hatua kwa hatua ili itakapofika mwezi Novemba mwaka huu (2023) tuwe na Sheria mpya ya vyama vya Siasa, Sheria mpya ya uchaguzi na kwamba marekebisho ya Sheria ya mchakato wa Katiba mpya yawe yamefanyika na kuundwa kwa kamati ya wataalamu watakaowianisha rasimu ya katiba ya Warioba na Katiba pendekezwa ili kupata rasimu mpya ya katiba itakayopigiwa kura na wananchi.
Hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu ieleze lini muswada wa Sheria ya vyama vingi vya Siasa 2023 na Muswada wa Sheria ya Uchaguzi 2023 utafikishwa Bungeni.

Tunakata muswada wa kuhuisha mchakato wa Katiba Mpya (amendment to constitutional review act 2011) ili kukwamua mchakato wa Katiba mpya kwa mujibu wa mapendekezo ya Kikosi Kazi.
Imetolewa na;

Ndg. Dorothy Semu
Waziri Mkuu Kivuli,
ACT Wazalendo
07 April, 2023.
Dar es Salaam.
Hiki chama cha kidini nacho hovyo sana

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 2579863
Hoja saba (7) za Waziri Mkuu Kivuli ACT Wazalendo Ndg. Dorothy Manka Semu kufuatia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu Mapitio ya kazi na mwelekeo wa Serikali na makadirio ya matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2023/2024.

Utangulizi
Juzi Jumatano tarehe 05 April 2023 Waziri Mkuu aliwasilisha Bungeni mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa Fedha wa 2022/2023 jijini Dodoma. Katika kuendeleza wajibu wetu wa kuisimamia Serikali, nikiwa Msemaji Mkuu wa Kamati ya Kuisimamia Serikali ya ACT Wazalendo (Waziri Mkuu Kivuli) ninatoa kwenu maoni machache kuhusu Hotuba ya Waziri Mkuu aliyeitoa Bungeni.

Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu Waziri Mkuu ndiye msimamizi wa shughuli za kila siku za Serikali. Kwa hiyo ni matarajio ya wengi kuwa hotuba ya Waziri Mkuu ingekuja na mwelekeo na majawabu ambayo yangesaidia kutatua changamoto mbalimbali ambazo nchi yetu inakabiliana nazo kwa sasa zikiwemo changamoto za hali ya kiuchumi, mwenendo wa kisiasa na hali ya usalama.

Hivyo basi kutokana na uchambuzi wetu, tumeona yapo masuala makubwa saba (7) yanayohusu maisha ya watu ya kila siku hayajaguswa kwa kupatiwa ufumbuzi.

i. Hali ngumu ya maisha
Suala la hali ya maisha ya wananchi (hususani mfumuko wa bei na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu) bado Serikali haijaweka mkazo kujiandaa kukabiliana na mwenendo huu kiasi cha kutoa nafuu kwa wananchi.

Licha ya kuwepo kwa vilio kutoka kwa wananchi kila kona ya nchi yetu kwa miaka miwili mfululizo. Hotuba ya Waziri Mkuu inataja takwimu za kitaalamu (ambazo hazigusi uhalisia) kuonyesha kama hali ni nzuri.

Hofu yetu ni kuwa mwelekeo huu wa Serikali unaweza kupelekea kipindi kijacho tena kuwa kwenye hali ngumu zaidi kwakuwa hakuna hatua madhubuti za kutoa nafuu kwa wananchi.

Tulipohitimisha ziara ya mikutano ya hadhara tulieleza na kuishauri Serikali ichukue hatua kadhaa kujiandaa na kukabiliana na mwenendo huu mbaya.

Aidha, tulitoa rai kwa Serikali kuchukuwa wajibu wake badala ya kuendelea kulalamika au kutoa tu maelezo ya kwamba hali hii ni duniani kote.

Waziri Mkuu kwenye hotuba yake ambayo inatoa mwelekeo wa Serikali inaacha hofu kubwa kwamba Serikali haijajiandaa na wala kuwawezesha wananchi kukabiliana na mwenendo huu hali itaendelea kuwa hivi hivi au itegemee neema za maulana bila jitihada za makusudi.

ACT Wazalendo tunaielekeza Serikali kununua na kuhifadhi chakula cha kutosha angalau miezi 3 kutokana na chakula kitachovunwa mwaka huu ili kujilinda na upungufu wa chakula. Kutokana na ukweli kuwa kwa maeneo mengi nchini uzalishaji unaweza kuwa sio mzuri kwa mwaka huu.

Hatua hii itawezakana kwa Serikali kujenga uwezo wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa kutenga bajeti ya kutosha ya kununua chakula (Tani Milioni 1.5 za Mahindi, Tani laki 5 za Mpunga, Maharagwe tani Milioni 1). Aidha, kuwezeshwa Bodi ya mazao mchanganyiko kununua na kusambaza chakula kwenye eneo linaloonyesha uhaba/upungufu wa chakula.

Mwisho, Serikali iweke mazingira bora kwa wakulima wadogo ili kuongeza uzalishaji zaidi; kwa kuendelea kutoa ruzuku katika mbolea na kusimamia usambazaji wake; kuhakikisha usalama wa ardhi kwa Wakulima wadogo kwa kushughulikia migogoro ya ardhi.

ii. Suala la hali ya ukosefu wa ajira na maslahi ya wafanyakazi nchini.
Ofisi ya Waziri Mkuu inahusika moja kwa moja na masuala ya ajira na uwezeshaji kupitia Wizara ya Vijana, kazi na ajira.

Mwenendo na hali ya ukosefu wa ajira nchini inazidi kuwa tata sana, uchumi wetu unazidi kupunguza uwezekano wa kuzalishaji ajira zenye staha na shughuli za kueleweka za kuwapatia vijana vipato ili kumudu maisha yao. Takwimu zinaonyesha ukweli kwa namna tofauti tofauti.

Athari za janga hili ni kubwa sana katika jamii yetu kwa sasa, ikiwemo; kuongezeka kwa wimbi la umasikini na utegemezi, kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili na uhalifu nchini ikiwemo vitendo vya wizi, ukahaba, unyang’anyi, uporaji.

Kuongezeka kwa upendeleo, kujuana, rushwa katika utolewaji wa kazi, kuongezeka kwa utumikishaji wa watoto kwa ujira mdogo au bila malipo hususani; mashuleni, viwandani, majumbani, migodini nk kwa kigezo cha kupatiwa ajira.

Katika hotuba ya Waziri inaonyesha wazi Serikali haitoi kipaumbele kushughulikia janga la ajira. Tunashuhudia mahitaji makubwa ya wafanyakazi na watumishi tena kwenye sekta nyeti kama vile elimu, afya na kilimo.

Lakini Serikali haijaweka mkazo kabisa kwenye kuhakikisha sekta hizo zinapata wataalamu na watumishi, licha ya kuwepo kwa wataalamu waliosomeshwa kwa gharama kubwa, Serikali ina waacha mtaani. ACT Wazalendo tunaitaka Serikali isikwepe wajibu wake wa kutoa ajira kwa vijana ili kwenda kuimarisha huduma za elimu, afya na kilimo na maeneo mengine yenye uhitaji.

Pili, Malalamiko ya wafanyakazi wa vyeti vya darasa la saba kutorudishwa kazini au kutopatiwa stahiki zao. Kwa mwaka huu tumepokea malalamiko ya waliokuwa watumishi wa TANESCO, Shirika la Maendeleo Dar es Salaam (DDC), Shirika la Bima la Taifa na maeneo mengi ya halmashauri.

Malalamiko yao kuondolewa kazi kimakosa lakini wengine kurudishwa kazini na wengine kuachwa mtaani. Wapo pia ambao wamefikia umri wao wa kustaafu lakini hawajapata stahiki zao.

Katika hotuba ya Waziri Mkuu ilitarajiwa kuona umetolewa utaratibu mzuri wa kushughulikia matatizo ya kundi hili kubwa ambalo halijui hatima yake na hivyo kuachwa wakining'inia.

Tatu, kuhusu kikotoo cha mafao (pensheni) bado wafanyakazi wanalalamikia kanuni mpya za ukokotoaji wa mafao ambazo zimeanza kutekelezwa mwaka jana Julai.

Kikotoo hiki kilipigiwa kelele sana na wafanyakazi kwakuwa hazingatii maslahi ya wastaafu wa nchi hii. Kanuni hizi zinawaumiza kwa sana wastaafu kwa kuwapunja mafao yao karibia nusu ya kiinua mgongo kinashikiliwa na Serikali, kinafupisha muda wa kuhudumiwa na kupoteza kiasi kikubwa cha mafao.

ACT Wazalendo tulizipinga kanuni hizi na kutoa rai kwa Serikali kurejesha kanuni za mwaka 2017 ambao zilikuwa zinamwezesha mfanyakazi angalau kupata kiwango cha kuishi kwa staha na kumudu maisha yake baada ya kulitumikia taifa.

Nne, kuhusu hali ya wafanyakazi katika sekta binafsi (usafirishaji); kuna malalamiko ya muda mrefu ya madereva wa masafa marefu kuhusu kupunjwa posho za kujikimu, kutopatiwa mikataba ya kazi na hali mbaya ya usalama wakati wanasafirisha mizigo.

Ingawa Serikali imeweka kima cha chini cha mishahara kwa madereva bado wanalipwa kiduchu na bila kufuata utaratibu wa ajira na maslahi yao.

ACT Wazalendo tunatoa wito kwa Serikali kuitazama sekta ya uchukuzi na usafirishaji kwa umuhimu mkubwa kwa kuwasimamia kupata haki na stahiki zao.

iii. Kuhamishwa kwa wananchi (jamii ya wafugaji) Ngorongoro
Katika hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri mkuu ameleza kuwa mchakato wa kuwahamisha kwa hiyari wananchi wa jamiii ya wafugaji katika hifadhi ya Ngorongoro limefanyika kwa kuzingatia haki za wanaohama, Waziri Mkuu anasema katika hotuba yake ukurasa wa 39 anasema” zoezi hilo limefanyika kwa umakini mkubwa na kwa kuzingatia haki za wanaohama.

Hadi kufikia Januari, 2023 jumla ya kaya 1,524 zenye watu 8,715 na mifugo 32,842 zilikuwa zimejiandikisha kwa ajili ya kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera. Kati ya kaya hizo, kaya 551 zenye39 watu 3,010 na mifugo 15,521 tayari zimehamishwa kwa hiari kwenda Msomera.”

Jambo hili si kweli, Serikali imewahamisha wananchi wa Ngorongoro kwa nguvu kubwa, ukweli ni kwamba tarehe 10 Juni 2022 katika Kijiji cha Loliondo kulijitokeza mapigano kati ya askari wa jeshi la Polisi dhidi ya wananchi kutoka katika vijiji 14. Taarifa zinaonyesha kuwa Juni 7, 2022 vikosi vya ulinzi viliwasili Loliondo kwa magari mengi na silaha.

Jeshi la polisi, FFU, mgambo, na watu waliovalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania walionekana wakielekea kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita mraba 1,500 lilalokusudiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba.

Na katika kusimika vigingi kwa kuingiza eneo la vijiji katika pori la akiba wananchi waliungana na kuingilia zoezi hilo ikapelekea Mapigano baina ya Jeshi la Polisi yalipelekea kujeruhi wananchi wapatao 14 kati yao wanawake ni wanane (na vikongwe wawili (2) na askari polisi mmoja ameuwawa.

Suala la ngorongoro ni sehemu tu ya matukio ya mamlaka za hifadhi kutumia nguvu katika kupora maeneo ya wananchi na kuleta madhara makubwa kwa jamii.

Ni wakati sasa wa Serikali kuwalipa fidia stahiki kwani kuna uharibifu walioufanya na kuwahamisha makazi yao bila matakwa yao ambayo imepelekea kukwamisha shughuli zao za kimaendeleo pia wengine kupoteza baadhi ya mali zao.

iv. Kukosekana kwa uratibu wa kukabiliana na maafa.
Ofisi ya Waziri inashughulikia na uratibu wa maafa na kukabiliana na majanga mbalimbali. Pamoja na hotuba ya Waziri Mkuu kuanzisha hatua za kufanya mapitio ya sheria na kutungwa kwa sheria kadhaa mwaka uliopita bado tunaona Ofisi ya Waziri Mkuu haijakuwa na uratibu mzuri wa kukabiliana na maafa.

Mifano ya kuendelea kutokea kwa matukio ya kuungua kwa masoko ya Wafanyabiashara hapa nchini ni moja ya mifano ya kuonyesha kuwa bado hakuna jitihada madhubuti za kukabiliana na maafa. Matukio ya ajali kadhaa yanayonyesha uwezo wa wizara na taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu bado ni mdogo kwenye shughuli za uokoaji.

Kwenye hotuba, hatujaona hatua za makusudi za kujenga uwezo wa kibajeti kununua vifaa vya kisasa vya uokoaji, kujenga uwezo wa Idara ya maafa na taasisi zilizo chini yake. ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kutenga bajeti (fedha) za kutosha ili kujenga uwezo wa idara ya maafa na kuongeza ufanisi wa usimamizi wa idara hiyo. Pia ni muhimu Kujenga uwezo kwa kutumia teknolojia juu ya kufuatilia maafa sehemu mbalimbali za nchi.

Jambo jingine, kuwepo kwa malalamiko ya kupunjwa na kutolipwa fidia wahanga (1361) wa mabomu ya Mbagala tangu mwaka 2009.

Hata hivyo, ni jambo la kusikitisha kuona licha ya kunyimwa kucheleweshewa kwa haki zao wamekuwa wakipokea majibu ya kukatisha tamaa, kejeli na vitisho toka kwa watumishi wa Serikali ikiwemo watumishi toka Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa.

ACT Wazalendo inatoa rai kwa Waziri Mkuu kuhakikisha mwaka huu wanafuatilia suala hili na kuwafuta machozi wahanga hao kwa kuwalipa fidia ya haki.

v. Kucheleweshwa kwa Miradi Mikakati na kutokamilika kuondoa umaskini wa wananchi.
Katika uelekeo wa jumla wa Serikali, hotuba ya Waziri Mkuu imeelezea azma ya kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchini.

Tunatambua jitihada hizo za kuendeleza na kukamilisha miradi hiyo kwa hatua mbalimbali. Ingawa, ACT Wazalendo inasikitishwa sana na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi hii jambo linalopelekea hasara kwa taifa kwa kulipa fedha za ziada kwa wakandarasi.

Mathalani Mradi wa Bwawa la Nyerere ulipaswa kukamilika 2022 umeongezewa muda wa miaka miwili zaidi hadi 2024 na kulitia taifa hasara ya Shilingi Bilioni 327.93. Mradi SGR kipande cha Dar- Morogoro kilipaswa kukamilika Novemba 2019.

Ongezeko la muda wa siku 1414 kwa mujibu wa ripoti ya CAG imetusababishia hasara ya Shilingi za kitanzania Bilioni 26.37 ambazo anapaswa kulipwa mkandarasi Mshauri.

Aidha kuandaliwa na kuwezeshwa kikamilifu wazawa kushiriki na kufaidika na uwekezaji (local contents); hatujaona hatua madhubuti za kuhakikisha Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inawaandaa vijana (Watanzania) kuipokea miradi hii.

Miradi ya Reli ya kisasa (SGR), Mradi wa Bomba la Mafuta, Mradi wa kusindika Gesi asilia Lindi (LNG) bado yapo malalamiko ya kutoandaliwa kwa wazawa uwezo wa kuendesha, kupata ajira na kunufaika na miradi hii.

Hotuba ya Waziri Mkuu haijagusa kabisa namna ya kutatua changamoto wanazo kabiliana nazo vijana kwenye kupata ajira kwenye miradi hii, kuandaliwa ili kuendesha na kusimamia kwa siku za usoni na viwango vya ujira wao wanapopata kazi.

Mwisho, malalamiko ya wananchi wanaopisha miradi kutolipwa fidia za haki au kucheleweshewa kwa malipo ya fidia. Rai yetu kwa Serikali kuwa ije na Sera mpya ya fidia kwa wananchi wanaopisha maeneo ya uwekezaji.

Sera itakayobeba utaratibu wa ardhi kwa uwekezaji (Land for Equity) uanze kutumika katika miradi yote nchini ambapo ardhi ya wananchi itumike kama mtaji katika mradi na hivyo kuzipa Serikali za mitaa za maeneo husika umiliki katika miradi.

Wananchi wajengewe makazi mbadala maeneo yaliyopimwa na yenye huduma zote za kijamii na vile vile wapewe shughuli mbadala za kiuchumi kama vile ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kilimo.

vi. Hali ya usalama wa wananchi
Hali ya usalama wa raia kwenye baadhi ya maeneo kuonekana kuwa ni mbaya. Tulipokuwa kwenye ziara kwenye mikoa tisa (9) tuliwaeleza waandishi kwamba tulikutana na malalamiko ya matukio ya utekekaji, kupotea kwa watu kwenye baadhi ya maeneo kama vile Kasulu, Kigoma Mjini na kuwepo kwa tishio kwa wananchi katika ukanda wa Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

Hata hivyo, tulipokea taarifa ya matukio ya namna hiyo pia kwenye mkoa wa Simiyu. Hata Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Ndg. Shamsha Mohammed kupata ujasiri wa kumweleza Waziri Mkuu alipokuwa kwenye ziara yake tarehe 25 Machi 2023.

Taarifa zinaonyesha kuwa wananchi wanapotea, wanauwawa na kuokotwa kwenye mifuko ya Rambo. Jeshi la Polisi halishughulikii masuala haya kwa weledi badala yake linapotosha ukweli huu.

Kwenye hotuba ya Waziri Mkuu hatujasikia hatua zilizochukuliwa hadi sasa na Serikali kukabiliana na madhila haya. Hivyo tunaitaka Serikali ichukue hatua zifuatazo ili kuhakikisha nchi yetu inarejea kwenye usalama na amani;

Mosi, kulitaka Jeshi la Polisi kushughulikia vijana wanne (4) waliotekwa Kigoma Mjini na mmoja Kasulu Mjini.

Pili, Serikali iondoe ukanda wa MKIRU kama ukanda wa Kijeshi (Urejeshwe utawala wa kirai) iwaondoe watumishi (watendaji, Maafisa maendeleo) wanajeshi kwenye vijiji na ngazi za Wilaya.

Tatu, Tume inayoshughulikia mfumo wa haki jinai iongezewe jukumu la kufanya uchunguzi wa matukio yote ya utekaji na mauaji ya raia wasio na hatia, waliohusika wachukuliwe hatua ili iwe funzo kwa wengine.

Nne, familia (wategemezi) zilizopoteza ndugu zao au kupata hasara yoyote zilipwe fidia ili kuwasaidia watumbukie kwenye umaskini.

Mwisho, Serikali ipanue majukwaa ya maridhiano hadi kwa ngazi za chini kwa wananchi, viongozi na vyama siasa ili kurejesha hali ya kuaminiana, kuheshimiana na umoja.

vii. Mageuzi ya kidemokrasia
Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia mchakato wa mageuzi ya sheria za kisiasa nchini. Tume Huru ya Uchaguzi ambayo inapaswa sasa hivi kuanza kuandaa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio huru.

Katika Hotuba ya Waziri Mkuu amezungumzia marekebisho ya Sheria badala ya mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi ili kuifanya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa huru kwa kuajiri wafanyakazi wake yenyewe na kusimamia chaguzi zote nchini ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.

Hotuba yake imetoa utaratibu wa kawaida wa Tume na Ofisi ya Waziri Mkuu wa kupitia sheria kila baada ya muda fulani bila kuzingatia maoni ya wadau kuhusu maridhiano yanayotaka kutungwa upya kwa sheria zote zinahusu masuala ya Uchaguzi.

Hivyo, tunaitaka Serikali kuharakisha hatua za utekelezaji wa masuala haya kwa kuchukua hatua zifuatazo;

Mosi, tunarudia wito wetu kuwa Serikali itoe ratiba ya utekelezaji wa mageuzi ya kisiasa kama ilivyo kwenye mapendekezo ya kikosi kazi hatua kwa hatua ili itakapofika mwezi Novemba mwaka huu (2023) tuwe na Sheria mpya ya vyama vya Siasa, Sheria mpya ya uchaguzi na kwamba marekebisho ya Sheria ya mchakato wa Katiba mpya yawe yamefanyika na kuundwa kwa kamati ya wataalamu watakaowianisha rasimu ya katiba ya Warioba na Katiba pendekezwa ili kupata rasimu mpya ya katiba itakayopigiwa kura na wananchi.

Hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu ieleze lini muswada wa Sheria ya vyama vingi vya Siasa 2023 na Muswada wa Sheria ya Uchaguzi 2023 utafikishwa Bungeni.

Tunakata muswada wa kuhuisha mchakato wa Katiba Mpya (amendment to constitutional review act 2011) ili kukwamua mchakato wa Katiba mpya kwa mujibu wa mapendekezo ya Kikosi Kazi.
Imetolewa na;

Ndg. Dorothy Semu
Waziri Mkuu Kivuli,
ACT Wazalendo
07 April, 2023.
Dar es Salaam.
Waziri mkuu hawezi kutatua changamoto zozote kama rais hajaridhia huu ni uchambuzi wa kilazi ndio ataelewa tu.
 
iii. Kuhamishwa kwa wananchi (jamii ya wafugaji) Ngorongoro
Katika hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri mkuu ameleza kuwa mchakato wa kuwahamisha kwa hiyari wananchi wa jamiii ya wafugaji katika hifadhi ya Ngorongoro limefanyika kwa kuzingatia haki za wanaohama, Waziri Mkuu anasema katika hotuba yake ukurasa wa 39 anasema” zoezi hilo limefanyika kwa umakini mkubwa na kwa kuzingatia haki za wanaohama.

Hadi kufikia Januari, 2023 jumla ya kaya 1,524 zenye watu 8,715 na mifugo 32,842 zilikuwa zimejiandikisha kwa ajili ya kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera. Kati ya kaya hizo, kaya 551 zenye39 watu 3,010 na mifugo 15,521 tayari zimehamishwa kwa hiari kwenda Msomera.”

Jambo hili si kweli, Serikali imewahamisha wananchi wa Ngorongoro kwa nguvu kubwa, ukweli ni kwamba tarehe 10 Juni 2022 katika Kijiji cha Loliondo kulijitokeza mapigano kati ya askari wa jeshi la Polisi dhidi ya wananchi kutoka katika vijiji 14. Taarifa zinaonyesha kuwa Juni 7, 2022 vikosi vya ulinzi viliwasili Loliondo kwa magari mengi na silaha.

Jeshi la polisi, FFU, mgambo, na watu waliovalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania walionekana wakielekea kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita mraba 1,500 lilalokusudiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba. Na katika kusimika vigingi kwa kuingiza eneo la vijiji katika pori la akiba wananchi waliungana na kuingilia zoezi hilo ikapelekea Mapigano baina ya Jeshi la Polisi yalipelekea kujeruhi wananchi wapatao 14 kati yao wanawake ni wanane (na vikongwe wawili (2) na askari polisi mmoja ameuwawa.

Suala la ngorongoro ni sehemu tu ya matukio ya mamlaka za hifadhi kutumia nguvu katika kupora maeneo ya wananchi na kuleta madhara makubwa kwa jamii.
Ni wakati sasa wa Serikali kuwalipa fidia stahiki kwani kuna uharibifu walioufanya na kuwahamisha makazi yao bila matakwa yao ambayo imepelekea kukwamisha shughuli zao za kimaendeleo pia wengine kupoteza baadhi ya mali zao.
Naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom