Luhanjo atoa ripoti, Jairo arudishwa kazini

kama Pinda angekuwa na ujasiri angejiuzulu kwa kuwa alishatamka bungeni kuwa nastahili kufukuzwa kazi kwa kuwa makosa aliyotenda hayawezi kutetewa kwa namna yoyote ile ila hakuwa na malaka hayo kuwa sio yeye aliyemteua.
Nasikia Kikwete aliporudi kutoka SA alimkaripia Pinda kwa kauli yake hiyo hadharani. Hapo wengine tulijua haendi mtu.
 
Inaonesha ni jinsi gani wabunge wa CCM ama wanavyoforge vyeti (kutokujua kusoma), pengine si makini ni wadandia hoja tu, na pengine ni mbumbumbu tu, wanaigaiga. Sijawatusi tafadhali: -


1. Mh. Shelukindo alisoma barua iliyoandikwa kwa kiswahili, nilimshuhudia kwenye luninga akitaja taasisi 20 kupewa agizo a.k.a ombi la kila moja kuchanga 50 milioni, jumla yake bilioni moja.

2. Mh. Ole Sendeka akasema hiyo nakala anayo na anamshukuru Mh. shelukindo kwa kuwahi kuitoa. Tena akaendelea kwa kusema pesa hizo ziliingizwa kwenye akaunti iliyokusudiwa na zimetolewa zote.

Je, waheshimiwa hawa walisoma barua feki, au hawajui kusoma?

Je, kama wafanyakazi (wateule wachache waitwao wataalam) wa wizara moja wanahitaji kwa mujibu wa Luhanjo, shilingi 500 milioni kuitetea bajeti kwa wiki moja pale bungeni, je, serikali yote ya JK inatumia bilioni ngapi kwa ajili tu ya kutetea bajeti yake yote?

Hivi kweli watanzania tunahitaji matumizi hayo makubwa ya pesa za kodi yetu, kwa ajili ya kutetea bajeti tu?

Wataalam wa wizara husika wanawajibika ipasavyo kweli?
 
sasa yule aliyemlipua Jairo si ndo ama zake ama za.....Mh? Nahisi kizungumkuti. Kweli hili ni jukwaa la mastress, puuuu
 
WanaJF tunasahau haraka. Kuna thread humu ndani lieleza sakata la wabunge kumkataa Jairo kuwa ilikuwa ni kwa sababu ya kuwajibu vibaya wakati wanaingia kwenye kikao cha kamati ya wabunge wa ccm kujadili namna ya kupitisha bajeti yao. Sababu haikuwa Jairo kataka kuwahonga kwani hilo ni jambo la kawaida. Utakumbuka barua yake inasema "...kama ilivyo kawaida....." Sababu wala haikuwa kwamba bajeti ya wizara ilikuwa mbaya; kwani hii waliyoiptisha ina uzuri gani - huo umeme wa dharura ambako mtakuja kugundua kuwa ni ufisadi mtupu umefichwa huko!

Ebu jiulize, hiyo idara ya uhasibu ya wizara inapata wapi pesa zote hizo za ziada? Hiyo idara ya mipango - ni vitu gani havikufanyika ili kupatikana fedha hizo? Hii ina maana fedha za bajeti iliyopita hazikutumika ipasavyo ikabakia ziada ya kuhongana?

Kuna thread humu ilieleza kuonekana kwa fomu ya malipo ambapo waziri na naibu wake walipokea 4m kila mmoja. Je hizo nyingine zililipwa kwa akina nani? - si inawezekana ni kwa wabunge haohao wapiga kelele?

Amkeni - kumekucha; pigeni kurazenu vizuri na mzilinde.
 
Hawezi kuondoka wakati bado analinda hisa za Mzee kwenye uchimbaji wa gesi, hawezi kuondoka kwa sababu bado hisa za mzee kwenye kuchimba mafuta zitakosa mwangalizi, hawezi kuondoka kwa sababu miradi ya uchimbaji wa Urani bado hisa za Mzee hazijakaa sawa na sio vizuri kuacha hisa za mzee bila uangalizi makini na wa mtu ambaye anaweza kulinda masilahi ya Mzee.

Wabunge ni Ze comedy ndio maana anarudishwa na mkubwa amekubaliana naye kuwa wabunge hawana maana .

Hata Masaburi anajua kuwa wabunge ni Ze Comedy na ndio maana hajairudisha bodi ya DDC na hakuna wa kumfanya kitu, kumbukeni huyu ni diwani wa kata ya Ikulu na hata Rais ni mpiga kura wake , kwenye vikao vya WDC rais anapaswa kuhudhuria mnataka kumpima akili?

Jana Msekwa kasema hivyo hivyo kuwa kama kuna watu wanataka abakie kuwa makamu mwenyekiti wa chama na aachane na Ngorongoro basi wamuulize aliyemteua kwani alijua kuwa yeye ni Makamu na alimteua . Alisemwa kuwa yeye anatoa maeneo ya ujenzi na kusema katumwa na Rais Kikwete sasa mnategemea nini?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Bora hili lilianzia ccm na sasa linamalizwa na serikali ya wana ccm kwa maslahi ya wenye ccm. Haya ndo aina ya maamuzi magumu wanayotaka yakifanyika tu, tutoe pongeze!
 
Mura Mwita25 kumbe mara moja moja huwa unakuwa na akili timamu. Kama ulikuwa hujafahamu, Rushwa na Ufisadi ndizo sera za chama chetu na serikali yake.
Wapi?Unaweza kuta walikuwa wanavizia hizo nafasi.Plus huyo Rejao.My advice is dont buy it.
 
<br />
<br />

MM,

Tuhuma hizo zilikosa uzito gani? Nadhani kwa sababu hatujui ripoti imesema nini inakuwa vigumu kulizungumzia hili suala.

Ila kutokana na hali halisi, yaani, maneno ya Waziri Mkuu bungeni na kwamba kutakuwa na kutafutana mchawi kati ya Jairo na wafanyakazi wa Wizara si busara kumrudisha wizarani! Waziri Mkuu ni bosi wake! Alimhukumu kabla ya kujua ukweli. Wafanyakazi wa wizara ndio waliomuuza kwa kina Shelukindo. Ni bosi wao!

Hii nchi ina mapungufu kila upande. Kwa wanaotaka mabadiliko na walioko madarakani. Wote wana mapungufu makubwa. Wote wanataka sifa kwa kutotenda au kutekeleza maslahi ya wananchi! Kila mtu anataka aonekane kiongozi bora sio kwamba ni kiongozi bora!

Inakwaza sana kufikiria mwisho wa haya yote!

waziri mkuu siyo bosi wa makatibu wakuu.
 
Juu ya ukweli wa hii taarifa naomba niruhusuwe niwe doughting tomaso, lazima nione viganja ndio ni amini. Ya wezekana ni watu wa idara ya hali ya hewa mko kazini na kipima upepo( you call it barometer sio?). Inasemekana mnatumia mbinu za zamani kupima hali ya hewa. Bali ni furusa ya kuona wachaingiaji ambao wako idara ya hali ya hewa. Ila wafikishiene ujumbe huu mitaa hali ya hewa ni mbaya sana mvua na upepo ni mwingi sana ikiongezeka na hiyo sunami ya jairo tena, si ajabu sunami inayoikumba libya sas ikatokea na hapa kwetu.

Source ni Radio One breaking news.Huo ndo ukweli bwana.Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
 
hii nchi tunaoatakiwa kuanza mapinduzi ni sisi wananchi-hawa watawala wanatuchezea mchezo wa ajabu sana,na sisi tupo tu hatureact,hii ni aibu
KWA MTINDO HUU,HAKUNA ATAKAYE PATIKANA NA MAKOSA-MAANA WANABEBANA KWA KUOGOPA KUTAJANA
 
Kwa hali hii uvumilive unaisha sasa. tutafika tu kama misri na libya. Hawa jamaa kweli hawana huruma kabisa kama wameanza tena mtindo wa kulindana, yaani ni kama vile wamemficha kichwa tu wakati mwili wote uko wazi.
 
Viongozi wanajuwa watanzania hawana jeuri ya kufanya kama yale waliyofanya wananchi wa Libya,tunisia na Egypt.Kwa jinsi mambo yanavyoenda.

Nina amini kuna namna wamejiamainisha kuwa watanzania kamwe hawana cha kufanya.Ni maoni tu.
 
Heeee sasa mnataka ashtakiwe kwa lipi alaaaaaah nyie bana, kwani kati yenu nani ni msafi??????? mnakaaaaaaa kuombea mabaya wenzenu tu. Una uhakika Jairo alichukua hizo hela haujui siasa ni mchezo mchafu na wamaigizo mengi. Eeeeeeeeeeh mwacheni Jairo ajilie bata bwana.
 
Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo,ametoa ripoti na kusema Jairo anarudishwa kazini kuanzia kesho.

===========
UPDATES:

Luhanjo anasema tuhuma zilikuwa za uwongo
Anasema taasisi za Wizara hazizidi 7 na si zaidi ya 20 kama ilivyodaiwa
Taasisi nne tu ndizo zilizochangia na zilichanga karibu TZS 500mil na si zaidi ya 1bil kama ilivyodaiwa
Pesa zilichangwa ili kuwawezesha watendaji watakaoenda kwenye bunge la bajeti
REA walichangia 50mil
TANESCO walichangia 40mil
EWURA waliombwa 40mil lkn hawakutoa, walichangia gharama za chakula na malazi kwa watendaji wa Wizara
Idara ya Uhasibu ya Wizara ilitoa 150mil
Idara ya mipango ya Wizara ilitoa 278mil

More updates to follow

Hizi pesa si zingesaidia kkupunguza mgao wa umeme jamani?! yaani watendaji kwenda Dodoma hapa ghalama zake sawa na kwenda ulaya 500m?! haya bwana!
 
Huo ndio utawala wa sheria. Pelekeni ushahidi ili afikishwe mahakamani kama hamkuridhika na maamuzi ya Serikali.
sasa unataka nani apeleke huo ushahidi wakati tuhuma ziliibuliwana magamba wenyewe, kumbe CCM wakurupukaji
 
Back
Top Bottom