Luhanjo atoa ripoti, Jairo arudishwa kazini

jamani kwani kutuhumiwa ni kukutwa na hatia? si alituhumiwa, akawekwa kando kupisha uchunguzi huru na umekamilika na kuonekana hana hatia (kama ndivyo alivyoonekana)

mi nafikiri kwa mchakato wa utawala bora wako sawa, ila wasiwasi wangu ni sawa na wa wengine, kama suala la jairo halikuwa la rushwa/ufisadi, sasa suala la rushwa/ufisadi ni la aina gani? kama hata jairo kapenya, atakayenaswa ni nani tena?

kwa kweli mi naona kama serikali inaji-disqualify yenyewe katika ku-lead hii vita ya rushwa/ufisadi

bado nasubiri kupata taarifa kamili kabla siaongeza maoni yangu mengine

mbarikiwe sana

YES hana hatia; wachunguzi walikuwa wanashinda naye clubs na kwenye makasino!
 
jamani kwani kutuhumiwa ni kukutwa na hatia? si alituhumiwa, akawekwa kando kupisha uchunguzi huru na umekamilika na kuonekana hana hatia (kama ndivyo alivyoonekana)

mi nafikiri kwa mchakato wa utawala bora wako sawa, ila wasiwasi wangu ni sawa na wa wengine, kama suala la jairo halikuwa la rushwa/ufisadi, sasa suala la rushwa/ufisadi ni la aina gani? kama hata jairo kapenya, atakayenaswa ni nani tena?

kwa kweli mi naona kama serikali inaji-disqualify yenyewe katika ku-lead hii vita ya rushwa/ufisadi

bado nasubiri kupata taarifa kamili kabla siaongeza maoni yangu mengine

mbarikiwe sana

Mamie Miss; ufisadi ni nguzo muhimu katika utawala wa chama cha magamba so unajidanganya sana kuwa wanaopatikana kama waweza adhibiwa na nitakupa sababu chache tu;


1. Ukimwadhibu huyo mkuu unatoa somo kwa wakuu wote wa idara na mashirika kuwa siku nyingine wakitakiwa kutekeleza kale kautamaduni ketu kaku wa facilitate waheshimiwa (nukuu ya barua iliyowekwa hadharani) basi wasikubali asilani kwani wanaingia katika matatizo wao binafsi.

2. Hili likitokea basi ujue basi hata chaguzi zetu zote tata zitakoma kwani unatoa somo kuwa kawaida/mazoea inaweza vunjika na mhusika ukabeba msalaba wako peke yako.

Sasa jaribu kufikiri hii cost ilivyokubwa kwa wenzetu hawa kwani mambo yao mengi hayaendi bila 'facilitation fee' yaani mhimili mkuu wa ufisadi ndiyo inayoyasukuma zaidi kuliko mfumo wa kawaida wa malipo. Kama nawsingizia si uliwasikia wenyewe vijana wa magamba ambao walikuwa wanadai kukabidhiwa bakuli la nyama maana ni amu yao sasa kula?

Walisema nukuu isiyo rasmi; nizamu yetu sisi kula.... Mungu isaidie Tanzania!
 
sasa source wako nani??? Na kwanini unaongea issue sensitive namna hiyo kwa ufupi kiasi hicho bila details? Yaani umeniharibia siku yangu leo mara mbili, kwanza kwa kuandika jambo zito kwa ufupi sana, pili kama ni ukweli basi siku yangu leo ndo imekuwa mbaya zaidi!

Ni kweli kasafishwa huyu house boy wa kikwete kwa muda mrefu sasa hakuacha aaibike huyo alikuwa kibaraka wa mungwana tangu wizarani huko so tulitegemea ataoshwa tu na bunge ndo hilo linakwenda.

IIa kitu kimoja watu wa CHADEMA watumie Igunga wawambie mnaona Kikwete hampendi Rostam na wema aliomtendea kubeba na mbeleko hadi Ikulu kashindwa kumsafisha huuuu jamani ni mtaji wa chadema wakienda nao kule igunga ccm bwana kila wanapo jalibu kuficha ndio wanachokoza bandora box.
 
Sikupenda kuamini kama haya yangetokea lakini nalazimika kusema kuwa ukombozi wa waTanzania upo mikononi mwetu, hawa wazee wameamua kulindana na kuacha watanzania wafe njaa.

Tujitaidi kutoa maoni yetu katika mchakato wa katiba ili tuwe na katiba huru itakayotuwezesha kuleta mabadiliko kiuchumi, kisiasa na kijamii. Tutashuhudia mengi mwaka 2016 kama Mungu akitujalia uzima, tutaona kina Luhanjo, Ottu na mafisadi wengine wakinyongwa kwa makosa ya kuhujumu uchumi, Mungu yupo analiona hili
 
well.. I know I was right on this one. Shelukindo na wenzake hawakuwa na mkakati wa kweli wa kumlipua Jairo it was just the same theatrics of political triangulation. This one was easy.

Mzee Mwanakijiji niliisoma vizuri sana ile makala yako. Wasiwasi wangu sijui viongozi wa CDM wameilewa?
 
Iko wapi heshima ya mbunge wa kilindi kwa Jairo kurudishwa kazini?

Iko wapi serikali sikivu inayofumbia Rushwa na kutetea Mafisadi?

Je ni yupi aliyechangia bajeti ya nishati na madini isipitishwe kwa mara ya kwanza?

Wanawafundisha nini wabunge kwa kumrudisha jairo kazini?

Ni vigezo vipi wametumia kumrudisha jairo kazini?
Je uchapakazi?

Kukwepa kuvuja kwa siri za wizara?
Au ni mchango wake uliotukuka katika kuhakikisha Tanzania yenye mgao inazidi kushamiri kwa giza totoro?

Nani shujaa?
Jairo au shelukindo?
 
Nadhani Jakaya for once ametenda jambo la busara! Ingewezekana vipi kumtosa mtu ambaye wamekuwa pamoja tangu akiwa Wizara ya Nishati na hatimaye akawa Private Secretary wakr kwa miaka yake mitano ya kwanza. Si angechekwa sana?

Hao watumishi ni wengi kiasi gani hadi watumie shs. Milioni 500 ndani ya nchi kuhudhuria vikao vya bajeti kwa siku mbili tu? Hawa ni Kama Mwinyi na Rio de Janeiro nini? Napita tu!
 
Fedha zote hizo zilkuwa ni za nini, mbona hakuna mchanganuo????? Walistuka nini in the first place hao ndio maghmba's.

Lakini huo nimtaji tosha kwa CDM, WACHA WAENDELEE KUFANYA WATANZANIA WOTE NI MBUMBUMBU!!!!!!!! Jibu lao lipo linakuja.
 
Hii serikali inatupeleka wapi sasa. Mtu ambaye ametuhumiwa kwa uwazi kabisa anarudishwaje tena kazini. It beats me!

Kumbe na wewe unakuaga kinyume na serikali maana kila kitu we ni mpinzani.
Wacha arudi maana ndiyo nchi yetu hiyo.
 
jamani kwani kutuhumiwa ni kukutwa na hatia? si alituhumiwa, akawekwa kando kupisha uchunguzi huru na umekamilika na kuonekana hana hatia (kama ndivyo alivyoonekana)

mi nafikiri kwa mchakato wa utawala bora wako sawa, ila wasiwasi wangu ni sawa na wa wengine, kama suala la jairo halikuwa la rushwa/ufisadi, sasa suala la rushwa/ufisadi ni la aina gani? kama hata jairo kapenya, atakayenaswa ni nani tena?

kwa kweli mi naona kama serikali inaji-disqualify yenyewe katika ku-lead hii vita ya rushwa/ufisadi

bado nasubiri kupata taarifa kamili kabla siaongeza maoni yangu mengine

mbarikiwe sana

YES hana hatia; uchunguzi wa kilevi levi, wachunguzi wenyewe utakuta wako kwenye payroll yake, wanashinda naye clubs na kwenye makasino unategemea nini?
 
uwiiiiiii jamani tunaenda wapi kweli tunafanywa mazuzu kweli
JAIRO.jpg
 
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote....
Nasubiri tu ndege ituwe.....
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote....
 
Ningeshangaa sana kama Jairo angefukuzwa. Hata yule Mkurugenzi wa Wanyama pori itabidi arudishwe kazini na kulipwa fidia ya kuchafuliwa na Shellukindo huyohuyo. Anayestahili kutimuliwa ni JK pekee na sio mwingine

Wananchi ndio wenye uwezo wa kuwatimua muda wao ukifika, lakini watatufanya kitu mbaya saana mpaka muda hou ufike!

Tuendelee kuomba tuu!!
 
Napenda kurudia kauli yangu ya awali ya kutaka Mizengo Pinda ajiuzulu wadhifa wake wa uwaziri mkuu, hakuna jambo ata moja ambalo Pinda ameweza kusimamia zaidi ya majonzi ya uongo mbele za macho ya wananchi.

Ni matukio mengi ambayo yanatokea yanayopelekea kuitwa kwa waziri mkuu, Pinda afikapo huongea kwa hisia na kuwapa moyo walengwa lakini hakuna suluhisho la maana, mfano ubadhirifu wa fedha UDOM, aliongea sana na kutoa machozi lakini mwishowe CAG aliwasafisha UDOM, la Jairo aliongea kwa simanzi na kusema kama lingekuwa mikononi mwake angelitolea uamuzi lakini ndiyo hivyo tene.

Kama anaona makosa yapo na wenzake wanayafunika na kama kweli yeye ni mtoto wa mkulima aache unafiki ajitoe kwenye matope abaki mbunge wa kawaida. Umuhimu wake haupo tena.
 
Shelukindo ndiye aliyeharribu sakata zima; kuhamisha fedha za serikali kwenda kwenye akaunti za serikali ni ngumu sana kuifanya iwe ufisadi Kama wezi wa EPA wangechukua zile bilioni 133 na kuziingiza kwenye akaunti ya wizara ya afya au elimu sidhani kama watu wangesema ni ufisadi.

Labda improper yes lakini corruption the bar is very high. Shelukindo hakutaka watu wakamatwe.. vinginevyo angesubiri wabambishwe.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
kama Pinda angekuwa na ujasiri angejiuzulu kwa kuwa alishatamka bungeni kuwa nastahili kufukuzwa kazi kwa kuwa makosa aliyotenda hayawezi kutetewa kwa namna yoyote ile ila hakuwa na malaka hayo kuwa sio yeye aliyemteua.

Ndicho nnachokisubiri sasa hv maana aliongea kwa kujiamin nadhani baada ya kujiridhisha na hali halisi' hana budi ajiengue maana Luhanjo na CAG wamethibitisha Pinda aliropoka na haiwezekani kuwa na waziri mkuu anayeropoka hovyo! Kinyume chake wamegundua Jairo atamwaga mboga kama wao watamwaga ugali.
 
Ni rahisi sana kuwasubiria 2015 simple tuanze na Igunga pale...manake hawa jamaa wasipoharibu wataendelea kuonekana wanafaa kumbe hamna kitu!! hii ndio nzuri waache wamrudishe kazini hakuna shida we take Note...
 
Back
Top Bottom