Analysti......huo wimbo Monduli watauimba...ukitaka kujua jamii ya pale ni Kasuku nenda pale ongelea suala la ufisadi afu umtaje EL....nachelea kusema ndugu zetu wa jamii ya Wafuga Ng'ombe kwa Mtindo wa kuhama hama bado wapo nyuma sana.Samahani kwa wale niliowakwaza lakini ukweli ndo huo[/QUOTE
bila samahani. mi sidhani kama wale ndugu wote ni kasuku, lakini ndo siasa, kuna ujinga na pia kuna suala la kuwa "biased" kwa "mtu" wao EL kwa makusudi, pamoja na kasoro zake..its like washabiki wa mpira na timu zao.....bias..., Tz yetu hii viongozi wasafi ni ndoto kwa sababu system inayowazaa ni chafu. ila sijui una maanisha nyuma sana ya nini kwa ni sitegemei wafugaji waachane na mfumo huo wa maisha kuja "mbele" unayofikiria wewe, its relative {kuwa nyumba -kuwa mbele}, but, well, pastoralist simply is a socio-economic system which will reproduce itself forever.
Wala sishangai Sitta ananguvu kwa sababu ya uspika wa bunge nje ya hapo hana tofauti na wakina Mwakyembe na mama Kilango na kwa sababu bunge limevunjwa inabidi arudishe majeshi nyuma unlike lowassa ambaye ni mwanzo mwisho japokua hayupo kwenye serikali bado ananguvu za ajabu
Inashangaza mbado kuna wananchi misukule bado wanaitetea hii misukule origino pamoja na HASARA KUBWA walituingizia taifani. HII INAGHADHABISHA SANA.
...mzee wapinzani wa mtandawo walikuwa wamejipanga kweli kweli....na aina yoyote ya kujitetea asingeeleweka...na rais alishafanywa behind the scene ashindwe au aogope kumtetea ......so Mwanajijiji in general Taarifa za kijasusi alizopewa Lowassa kuhusu hali halisi zilimshtua sana..na zilikuwa za ghafla....ie Plan B ya kina Mwakyembe ilikuwa tishio kwa utawala mzima...
...naamini kabisa Lowassa angepata taarifa mapema ya kinachopangwa ....angekuwa waziri mkuu hadi leo ...kwani hata angepata taarifa ndani ya masaa 24 au 48 kabla ya tukio ...angekuwa na uwezo wa kubadilisha kabisa..hali ile na kuwapanga watu wa kumtetea na namna ya kujitetea au hata lolote lingeweza kutokea ......ni wazi tume ya Mwakyembe ilichomudu ni USIRI mkubwa!!!
wANA JF, NIMESHINDWA KUMWELEWA HUYU NDUGU KUWA ALIKUWA NA AKILI TIMAMU AU LA, NIMESHINDWA KUELEWA JINSI ANAVYOISIFIA RICHMIOND KAMA NDIYE YEYE KWELI ALISEMA KAONEWA. hABARI KAMILI, TIZAMA TBC1 SAA 2 NA NUSU USIKU HUU MAOJIANAO NA TIDO MUNDA YATARUSHWA LIVE. mLIOKO NYUMBANI TUJUZENI BAADA YA KUTAZAMA
NAJISIKIA UCHUNGU SANA .
hahaha. umenifurahisha, ana manguvu ya ajabu. bora mchapa kazi kuliko mpole anayetupaka mafuta kwa mgongo wa chupa, bora croloquine kali itakayoponya kidonda kuliko sukari tamu itakayokuletea magonjwa na kupooza....EL is far better than most of our leaders in government, including mkuu wetu....akirudi nitafurahi tu...na ninajua hatafanya makosa kwasababu ameshaonja makonzi....Naomba Mungu Pinda asifikiriwe hata kwa ndoto za usiku tu....hata karama ya uwaziri mkuu, Mungu amempa kwengine ndo aende huko, lakini hapo kwenye u pm, hayupo....Mohamed shein kule zanzibar, wameshapoteza CCM kwa kumuweka yeye, ni choice mbaya sana na hatashinda...hata kama atashinda watakuwa wameweka chaguo la mtu wa kumshika masikio kwa upande wa visiwani...atatii chochote atakachoambiwa na bara...so nasikitika kwa hilo....Mungu ibariki Tanzania.
Tatizo la misukule wanategemea master wao awapatie ugali na kila kitu.
Hapo ndo penye tatizo.
Watu wapo tayari kuuza utu wao ilhali wamtumikie SHETANI
mahojiano safi sana yale ..Lowassa hakuwa na kosa na amesema hata leo awe PM atalishugulikia suala la richmond vile vile ...mimi napenda viongozi jasiri wa mtindo ule ..mengine ni chuki binafsi na Lowasaa amesema historia itawahukumu...tuone sasa itakavowahukumu....
Labda nyie wafuasi wa 'shujaa Lowassa' mtuambie HASARA aliyoiingizia taifa yeye na troop lake atailipia nani?? Huo umahiri wenu wa siasa uchwara unalisaidia vp taifa??