Lowassa na Kiingereza chake!

I frankly do not see any problem with his English relative to other Tanzanians who claim to know this language. Its OK.
 
Rais wa Uchina haongei Ki Ing ereza.

Rais a Uchina hakutumia Kiingereza kama lugha ya kujifunzia shule ya upili mpaka University. Huyu baba kasoma shule kiingereza primary mpaka University tena ana mpaka shahada ya pili. Besides, amefanya kazi kwenye higher positions ukiwemo uPm, how come ana kidhungu kibovu kiasi hiki na composure hamna kabisa wakati vitu vyenywe anasoma? What if angekuwa anatoa kichwani directly?
 
Hawezi hata kuongea sentensi mbili kwa kiingerez. Bora hata Mr dhaifu mzee wa the the the the.....
 
Kuna jamaa aliandika watanzania nani katuloga???? Kuna shida gani hapo na kiingereza cha Rais ajae, umeshamsikia Putin, Raisi wa china, raisi wa korea kaskazini. Acha uzuzu wewe, kama vip na hutaki hama nchi kama unaweza.

Haya sasa....Timu ubwabwa ipo kazini!!!
 
rais a uchina hakutumia kiingereza kama lugha ya kujifunzia shule ya upili mpaka university. Huyu baba kasoma shule kiingereza primary mpaka university tena ana mpaka shahada ya pili. Besides, amefanya kazi kwenye higher positions ukiwemo upm, how come ana kidhungu kibovu kiasi hiki na composure hamna kabisa wakati vitu vyenywe anasoma? What if angekuwa anatoa kichwani directly?
si anaumwa....
 
Lowasaa anapiga ngeli vixurii tuuuu hata kiswahili hajui kama english ndio maana hana maneno mengi kama mzaramoo😆

Yeye ni mtu wa vitendo na kwa mara ya kwanza tutakuwa na kiongozi makini kam dikteta👮🏿
 
Akiwa raisi hajui kiingereza vizuri wakija wageni kutoka nje itakuwaje?
 
Mdau kwenye mikutano ya kimataifa ataongea kimasai au? Badala ya kumpenda kupita kupita kiasi na kutetea ujinga ni vema mngemshauri akajifunza hiyo lugha vizuri,mbona diamond platnumz now anakiongea vizuri tu na hajasoma uingereza kama lowassa

Mkutano upi wa kimataifa unalazimisha mtu aongee kungereza? Rais wa china, Rusia, German, Italy, spain, uarabunii, korea nk mikutano yote ya kimataifa huzungumza kwa Lugha zao mama hawana ulimbukeni wa Lugha ya kingereza
 
Akiwa raisi hajui kiingereza vizuri wakija wageni kutoka nje itakuwaje?

Nini kazi ya mkalimani? Rais si lazima ajue kingereza wapo marais kibao hawajui kingereza hata juzi Rais wa msumbiji kahutubia Bunge Dodoma kwa kireno, huu ujinga wa kudhani kingereza ni bora utakwisha lini? Hivi Rais wa Ufatansa anaongea English?
 
Mdau umewahi kumsikia Lowassa akizungumza kiingereza????hebu mtazame hapa rais wetu huyu mpya halafu just imagine siku yuko cnn anahojiwa na Larry King na hivi vingereza vya kuandika kwanza then kukariri

We vipi..hapo hakuna kingereza? Labda wewe ndio kingereza hakuna. Edward kasoma vizuri sio nyinyi wa leo wenye elimu za kukariri.
 
Last edited by a moderator:
bila ushabiki ni kweli kabisa EL kwa kingereza hajiwezi kabisa

Wananchi wa Tz wanatawaliwa kwa kutumia Lugha ya Taifa Kiswahili hotuba zote ni Kiswahili na si lazima Rais aongee English kwani hii ni Nchi huru Rais anaamua aongee lugha ya Taifa hakuna wa kumuuliza.
 
Mkutano upi wa kimataifa unalazimisha mtu aongee kungereza? Rais wa china, Rusia, German, Italy, spain, uarabunii, korea nk mikutano yote ya kimataifa huzungumza kwa Lugha zao mama hawana ulimbukeni wa Lugha ya kingereza

Kwani hapo Kilimanjaro kwenye hiyo video alilazimishwa na nani kujikakamua namna hiyo kuongea kiingereza?Si ni mazingira ndio yalimpelekea " alazimike" kuongea English,na hapo alikua pm tu,akiwa rais( mungu apishie mbali) mazingira ya namna hiyo ya "kulazimika" kusema kiingereza yatamkuta sana tu,hasa ikizingatiwa amewahi kusomea uingereza elimu ya kiwango cha shahada tofauti na Putin au rais wa China.Lowassa afanyie kazi mapungufu,kujaribu kuficha udhaifu ni kujidanganya
 
You're missing a bigger picture of it.

Kiingereza ndiyo lugha ya kufundishia Tanzania. Kutoka Secondary hadi chuo kikuu.

Lowassa ni msomi wa kiwango cha shahada. Hivyo amesoma kwa kutumia kiingereza hadi kupata hiyo shahada.

The BIG question is, kama hajui Kiingereza aliwezaje kufaulu masomo yake hadi kupata shahada.

kama Kiswahili ndiyo kingekuwa lugha ya kufundishia tusingekuwa na matatizo na Lowassa kutojua Kiingereza, kama tusivyokuwa na matatizo na Wachina, Wajapan, Warussia, Wakorea etc kutojua Kiingereza because it is not their lingual fracas

Kwahiyo kipimo cha elimu ya mtu ni kujua sana kiingereza kwa sababu tunasoma kwa kutumia kiingereza? kuna tofauti ya kutokujua kabisa lugha na kuongea kwa shida.
 
Kwani hapo Kilimanjaro kwenye hiyo video alilazimishwa na nani kujikakamua namna hiyo kuongea kiingereza?Si ni mazingira ndio yalimpelekea " alazimike" kuongea English,na hapo alikua pm tu,akiwa rais( mungu apishie mbali) mazingira ya namna hiyo ya "kulazimika" kusema kiingereza yatamkuta sana tu,hasa ikizingatiwa amewahi kusomea uingereza elimu ya kiwango cha shahada tofauti na Putin au rais wa China.Lowassa afanyie kazi mapungufu,kujaribu kuficha udhaifu ni kujidanganya

Wazungu huwa wanajua kuwa English si Lugha mama ya waafirika ndiyo maana wao hata ukichapia kingereza kibaya kibovu hawana shida na hawakushangai kwani wanajua ww si mzaliwa wa London, Mkosoaji Mkubwa wa Lugha hii ni ya kigeni ni Mswahili huyu huyu malimbukeni wanaodhani kujua kingereza ni Usomi ! Tambua wapo wasomi wana Phd ni wanasansi wakubwa na hawajui kingereza, Taaluma na Lugha ni vitu tofauti kwani Taaluma hupatikana kwa Lugha mbali mbali, Wapo wazaliwa wa Uingereza ambao hawakwenda shule na wanaongea kingereza je? Na hao ni wasomi? Rais wa china na mataifa kama German, holand, Belgium viongozi wa huko hawajui kingereza hata wakienda UN hutoa hutuba kwa Lugha zao tu.
 
Yaani wewe hujui umuhimu wa Rais wako kujua kiinereza!!? You must be kidding me ................ Kiingereza ni lugha ya Taifa kama kilivyo kiswahili. Hata unapoajiliwa serikalini unafanyiwa interview kwa kiingereza!! Hivi hizo kazi wengine mmezipataje. Kwa Tanzania tunatakiwa kizimaster lugha zote mbili meaning; Kiswahili na Kiingereza. Kushindwa kwetu ni aibu na ni ku-fail kwa mfumo wetu wa elimu!! Labda ndiyo maana Lowasa amedai kwake itakuwa ni ELIMU KWANZA!!

However, kwa Lowasa ambaye hakufundishwa na Walimu wa UPE ni aibu kuongea kiingereza cha kuunga unga sentence kiasi hicho na kurudia rudia points. Kama anashindwa kujieleza kwenye kitu ambacho amejiandaa kukizungumzia atawezaje kujieleza kama atakalishwa kiti moto kwenye HARD TALK au akikutana na Christine Amanpour, Hala Golani au Richard Quest!!?

Mkuu suala la kuongea kiingereza kwa shida haina maana kuwa huyo mtu hajui kiingereza,maana hiyo elimu aliyonayo ameipata kwa lugha ya kiingereza,sasa ukiniambia hajui kiingereza nitakushangaa. Kuongea kiingereza kwa shida ni tatizo la wengi ila halina maana kuwa hawajui.
 
Lowasa si lazima ajue English na mtu ukiwa Rais unaweza kuweka wakalimani kokote aendako Duniani, kingereza si muhumu sana kwa maisha ya watanzania kwani watu wanataka maendeleo ya haraka hii lugha ya Mkoloni isomeni nyie wengine lakini Rais si lazima aijue, wapo marais wengi sana Duniani hawajui kingereza na hata wakiongea wakakosea hakuna wa kuwashangaa, Tatizo la watanzania ni kujidai wanakijua kingereza kuliko hata wenye Lugha yao, Wazungu wao hawana shida hata ukiongea ukakosea hawashangai wala kucheka kwani wanajua si Lugha mama ya waafirika, Lowasa komaa na Lugha ya Taifa achana na malimbukeni ya kudhani kila cha mzungu ni bora kuliko cha mweusi.
 
Akiwa raisi hajui kiingereza vizuri wakija wageni kutoka nje itakuwaje?

Kutokujua kiingereza vizuri maana nini kwa mtu ambaye teyari ni msomi? tatizo mnachanganya kuongea kiingereza kwa shida na kutokujua kiingereza. Mara nyingi imekuwa wanasemwa humu viongozi kuwa hawajui kiingereza hadi Jk rais wa nchi anaambiwa hajui kiingereza pengine kwa makosa wanayoyafanya pindi wanapoongea,sasa sijui hizo elimu wamezipataje kama kweli hawajui kiingereza!!
 
Mbona kaongea vizuri kbs.Ulitaka aongee kama Hashim Thabit wabongo tunawadudu na funza kichwani sio bure.

T
 
Mkuu, nmegundua kuna vilaza wengi sana humu jamvini na ndio maana badala ya kuwajenga wagombea wao wamebaki na kumjenga Lowassa wakifikiri wanambomoa!! kwanini nasema hivi, jamaa anawashangaa Wachina kuongozwa na Raisi asiyejua kiingereza, lkn unjiuliza hivi huyu hayajui MAENDELEO MAKUBWA YA KIUCHUMI NA KITEKNOLOJIA YA CHINA?? jibu ni kwamba watanzania wengi kwao kiingereza ndio Usomi na uwezo wa kutenda wa akili ya kiongozi! Tubadilike tujenge hoja za maana!

Wapo Raia kibao wa Uingereza wazawa hawajaenda shule lakini wanaongea kingereza je? Hao ni wasomi? Huu ulimbukeni wa kudhani ukiongea kingereza ni Usomi utakwisha lini? Tambueni kuwa Taaluma hupatikana kwa lugha mbali mbali wapo wasomi kibao hawajui kingereza na kazi zao zinaendelea vizuri tu.
 
Back
Top Bottom