Lowassa mgeni rasmi harambee Jimbo Katoliki Ifakara

Ninachoamini, EL hakushiriki mpango wa ukwapuaji pesa hizo. Kwa kuilinda nchi isitikisike, isiyumbe, isianguke ndipo akajitoa muhanga kuiokoa serikali yake.
Kanisa/Misikiti inajua fika juu ya kushiriki au kutoshiriki kwa huyu EL, uonapo hususan Catholics wanathubutu kumualika...jua wameshajiridhisha.
RC wanazo system za habari kuliko hata Usalama wetu wa Taifa hapa, wanavyo vyanzo vikubwa na vyenye kuaminika kwa chochote wanachokitafuta. Mafundisho wapatayo katika kusomea upadri, na ngazi nyingine ktk mtiririko wao kimafundisho...ni zaidi ya course za usalama. Hivyo, naimani kubwa kabisa kuwa EL ameshabainika kuwa ni kafara kwa kuinusuru nchi, japo tunakataa kuamini ila AMA mwaka huu kipindi cha chaguzi za ndani za CCM tutamsikia akifunguka AU mwaka mmoja kabla ya 2015 atafunguka tena kwa ushahidi mpana kabisa.

mkuu kuna post humu nimejibu mtu na kumueleza umakini wa kanisa katoliki kwa kila jambo, kama kanisa wangeona EL anatatizo kwa hakika wasingethubutu kumualikana hata siku moja. Viongozi wa kanisa langu huwa hawakurupuki hata siku moja na kama kuna jambo ni lazima walijadili na wakijiridhisha ndio utaona matokeo. Nina imani kubwa sana na kanisa langu na viongozi wake wote pamoja na maamuzi yao pia
 
nipe ushahidi ni lini na wapi EL alikwenda kuomba kuhudhuria harambee? yaani hata ujenzi wa kanisa mnataka tuende kuomba misaada Europe? hapana ni wakati wakujitegemea. Kwapamoja tunaweza kuchangishana na kufikia malengo.
Kwani huo mtambo wa fedha za kuchangia makanisa na asasi za kidini yeye ameutoa wapi? Haijalishi anachangia makanisa, misikiti na hata masikini na wenye shida, kwa maana Mungu hahongeki wala kudanganyika. Nawasikitikia sana viongozi wa dini wanaotumika kama fagio la kumsafisha mhalifu huyu. Mungu atawatendea kwa kadiri ya haki wanayostahili.
 
Sioni tatizo hapo. Mh. Lowasa kualikwa kwenye fundraising ya Catholic church, kwangu siyo dhambi. Mheshimiwa Lowasa kugombea Uraisi wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania siyo dhambi, tena hiyo ni haki yake Kikatiba. Kwa nini zinatolewa judgement kwa huyu mzee kuwa hatafaa kuliongoza taifa hili? I think binadamu we learn through mistakes, Kwa upande wangu naona he is well experienced na mistake tulizozifanya kwa hiyo atazirekebisha mara atakapokuwa mkuu wa nchi , na nchi itakwenda vizuri sana.
 
Siku hizi makanisa yamebaki kutukuza pesa. Hayaangalii tena masuala ya uadilifu ndio maana jamaa anayatumia kujisafisha, na kwa kweli kafanikiwa makanisani.

Tusubiri sanduku la kura.

Duh! Umeongea jambo ambalo wengine hawajaua hilo. Makanisa yanashindana kuinua majengo makubwa na si kujenga imani kwa waumini wao! Kaazi kweli kweli!
 
Nimeamini sasa PESA NDO KILA KITU.Yaani ukiwa na haka kajitu kila mtu atapiga magoti mbele yakoHongera El njia nyeupe hiyo magogoni
 
After reading this thread, I must say I am a proud Atheist.

Tuliambiwa JK ni "chaguo la Mungu", watu wakamchagua kwa sababu hiyo. Leo we all know where he has taken us. With EL, it's De Javu once again, muda si mrefu tutaambiwa ni "Chaguo la Mungu". Hivi ni lini tutaacha kutumia mawazo ya hawa wanaojiita viongozi wa dini na kuanza kutumia utashi wetu vizuri? Time will tell, awaulize waliopo madarakani watamwambia Tanzania aliyoiacha 2008 siyo ya leo na ikifika 2015 itakuwa tofauti kupita kiasi.
 
Sioni tatizo hapo. Mh. Lowasa kualikwa kwenye fundraising ya Catholic church, kwangu siyo dhambi. Mheshimiwa Lowasa kugombea Uraisi wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania siyo dhambi, tena hiyo ni haki yake Kikatiba. Kwa nini zinatolewa judgement kwa huyu mzee kuwa hatafaa kuliongoza taifa hili? I think binadamu we learn through mistakes, Kwa upande wangu naona he is well experienced na mistake tulizozifanya kwa hiyo atazirekebisha mara atakapokuwa mkuu wa nchi , na nchi itakwenda vizuri sana.
Kugombea urais ni haki yake ya kuzaliwa na kikatiba. Kwenda kanisani ni haki yake kikatiba na kiimani kama walivyo watanzania wengine.

Kwenda makanisani kutafuta political support ni kosa, tena kosa kubwa. Kiongozi mwadilifu hawezi kutumia imani kujisafisha kwa kulitia taifa hasara na matatani. Kiongozi mwadilifu hana sababu ya kuwagawa wananchi kwa imani.
Kiongozi mwadilifu hapaswi kuomba radhi kanisani au msikitini, amuombe radhi mungu wake na aliowakosea.

ENL hakufanya makosa, alidhamiria kufanya makosa na hilo ataishi nalo hadi siku mungu atakapompenda.
Hutuhitaji kumpa nafasi kiongozi aliyefanya makosa nafasi nyingine ya kuliumiza taifa kama alivyofanya EL

Alipewa nafasi bungeni atueleze ukweli, hakufanya hivyo alitokwa na mapovu.
ENL hafai si kugombea bali kutajwa katika medani za siasa za nchi hii. Huyu ni mhalifu na haosheki.
ENL ni mchafu wa roho, na sasa anatumia imani kujisafisha ili alitumbukize taifa katika hasara nyingine ya udini hata kabla hatujamaliza kulipa hasara alizosababisha akiwa Waziri mkubwa. Hafai na ni wa kuogopa kama ukoma!
 
nipe ushahidi ni lini na wapi EL alikwenda kuomba kuhudhuria harambee? yaani hata ujenzi wa kanisa mnataka tuende kuomba misaada Europe? hapana ni wakati wakujitegemea. Kwapamoja tunaweza kuchangishana na kufikia malengo.

mbombongafuuu
 
wito wa Narubongo ni kuwahimiza watanzania wote wenye nia njema kujitokeza kwa wingi 7th march 2012 @ diamond jubilee pasipo kujali itikadi za udini, ukabila, uraia na personal issues ili tukamilishe kazi hii ya kulieneza neno la mungu na kuijenga tanzania yetu yenye maadili



Mimi ni muumini mzuri sana wa Kanisa Katoliki, lakini siwezi kushawishika kwenda katika hiyo hafra. Na kwa mpango huu napenda nitangaze nia ya kuwa "HATA UKIITISHWA MCHANGO / SADAKA PAROKIANI KWANGU KWA AJILI HII SITOCHANGIA, NI HERI NIKAWAPE OMBAOMBA BARABARANI"

Kanisa letu linaanza kuchanganya dini na Siasa, kwani hakuna waumini wanaoweza kuwa wageni rasmi????

nakumbuka kwenye Jumuiya yangu tulinyimwa Ibada ya Misa mwaka jana tu na Paroko kwa sababu tulimualika MBUNGE ambaye ni wa CDM kushiriki nasi. Paroko akatuambia kuwa katika shughuli za Dini haturuhusiwi kualika viongozi wa Siasa. Tunapaswa kualika viongozi wa Dini (mfano Padre, Askofu au baba mtakatifu) paroko akasema "tusichanganye Dini na Siasa"

hii imenitokea ukweli si kusimuliwa kwani mimi kama kiongozi wa hiyo jumuiya ndiye nilikuwa nafuatilia. Huenda paroko yule ni wa CCM ndio maana alikakataa tumualike Mbunge wa eneo letu ambaye ni CDM.


Sasa iweje kama mimi nilinyimwa haki yangu ya msingi kiimani kupata Ibada ya Misa katika Jumuiya na leo E. L. kiongozi wa Siasa anaalikwa kanisani.

OMBI: KANISA KATOKI TUSICHANGANYE DINI NA SIASA


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
JF Senior Expert Member Array


Join Date : 14th December 2010
Posts : 990
Rep Power : 470


[h=2]
icon1.png
Re: Vote for eddo 2015!![/h]
Nadhani ccm wanahitaji kuangalia nje ya kundi la hao waliopo ktk ulingo wa siasa, kwani naamini kuwa wapo tena wenye uwezo kuliko hata hao tunaowaona ulingoni. Hawahitaji kuuzwa/kunadiwa kwa kuwapitisha wakanisani wala misikitini, bali jamii itawakubali na kuwaunga mkono. tatizo linakuja tu pale hao waliotangulia wameziba milango ya wale wanofaa, huku wakitambua vema yakuwa historia inawanyima kibali cha kuiongoza jamii, ndiyo maana wamejikita makanisani kwa makusudi kwani wanaitambua nguvu ya imani za dini ambavyo waumini huwa hawaoji kinachoendelea bali ni kupokea tuu kila litokalo kwa viongozi wao wa kiroho,mwisho wa siku hushindwa kujipeleleza ili watatue matatizo yao ya kimwili kwa kuweka mifumo inayoamua mistakabali ya mahitaji yao ya kimwili.
Ole wao viongozi wa dini kwa kujua ama kutokujua wanawaongoza kondoo wa bwana kuelekea upotevuni.RAI YANGU KWA VIONGOZI WA DINI, kuna uhusiano wa karibu sana kati ya mwili na roho maana hivi vitu vipo pamoja ktk uhai wa mtu, ninyi kama wahudumia roho hampaswi kutofautishwa na aneye hudumia mahitaji ya kimwili, mnapo amuwa kuwa ma kuwadi wa viongozi wa kushughurikia mahitaji ya kimwili ya hao waumini wenu huku mkijua kuwa kazi hiyo hawataitimiza, basi hata ninyi kazi yenu ya huduma za kuroho hugeuka na kuwa ubatili mtupu nayo haina kibali machoni pa BWANA!

Bulesi likes this.



Edit Post Reply Reply With Quote
 
Tumepewa akili na Mungu tuzitumien jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! hu!, fikirini nje ya hapo tunaweza kwenda nje ya ccm na cdm, ni swala la uamzi tu na tukafanya vyema!
 
Hivi Kanisa litaunga mkono SLAA CHADEMA au LOWASA wa CCM ikitokea mpambano 2015?
 
Nasikitika sana kanisa langu katoliki kuwa ni sehemu ya kupigia magoti na kupokea hela hz chafu za E.L sisi waumini tuwe na tumaini gani na kanisa ili?kua sasa limeamua kupinga na imani zake na kuwaangukia wezi na wenye pesa?hata Yesu alisema hawezi kuwatumikia mabwana wawili,PESA na Mungu,lazma uchague moja
 
lowasa na mwinyi wapo ifakara katika sherehe za kumsimika askofu wa jimbo jipya la ifakara mwenye taarifa zaidi atujuze nini kinachoendelea muda uhu.....
 
umesema wapo kanisani sasa kinachoendelea mi nafikiri ni misa tu au sijakuelewa...
 
Naam! Shughuli ya kumsimika Askofu Libena ndo imeisha..baadhi ya viongozi waliopewa nafasi ya kuzungumza wakati wa ibada ni pamoja na rais mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ally Hassan Mwinyi, na waziri mkuu aliyejiuzulu bwana Edward Lowossa. Wakati mzee mwinyi alipokuwa akiingia msafara wake ulikuwa na viongozi kama waziri wa sheria na katiba bi Celina Komboni,waziri wa afya Dr Hadji Mponda,mbunge wa kilombero Abduli Mteketa kwa kutaja wachache. Wakati wakiondoka, msafara ulikuwa na viongozi wawili tu. Mzee mwinyi na EL. Swali ni EL huwa anapewa 'eskoti' ya polisi? Au amedandia msafara wa mzee mwinyi?
 
Back
Top Bottom