Lowassa mgeni rasmi harambee Jimbo Katoliki Ifakara

Mkuu, sio kwamba EL anawaandaa wananchi, ukweli ni kwamba EL anaandaliwa kuwa prezdaa wa Tz 2015. Hiyo ndiyo Vatcan kama ulikuwa hujui.

inaelekea hata huelewi kuwa Vatcan ni makao makuu ya kanisa katoliki na sio lutheran ambalo huyo fisadi ndio muumini wake!!halafu unajiita great thinker!!!!
 
Hakunaga anayefaa kuwa rais wa JMT 2015 kama Lowassa.Time will..
Kama nchi imelaaniwa basi mkuu wa wezi EL atachaguliwa, lakini ajue kanisa katoriki la mitume haliwezi kwenda kusujudu mafisadi na wezi wanaoongozwa na EL
 
Jamii Forum: Wonders shall never end!
JF Never ceased to amaze me!

Kama JF Tunazungumzia mipira iliyokufa, watanzania wengine watafanyaje?
 
ni mungu pekee ajuaye nani atakuwa rais wetu ajae,,halaf el kualikwa kwa kutoa msaada makanisan n jambo la heri,watanzania mbna hatufikirii jaman,mnataka apeleke wapi?wanaomwalka wanajua n mtoaji mzuri,mwachen jaman,na kwann misaada yake inahusishwa na mbio za urais,kwan yy kasema kama anataka?
 
Hapa hakuna chaguo la Mungu watu wasidanganye kwani kuna mungu mwingine abudiwae kwa fedha na atoae fedha aabudiwe. watanzania wakitaka kumpata kiongozi atokae kwa Mungu wa kweli waangie Makanisani na Misikitini kwa nguvu ya mioyo yao waombe raisi atokae kwake, tusidanganye kuwa anatoaye misaada ndani ya kanisa au mikitini ndiye anayetufaa, au ni hongo inayotumika kuahadaha mioyo yetu, tutumie macho ya ziada na masikio ya ziada, Kumbukeni hata katika maandiko shetani alimuahidi Yesu ya kuwa akimuabudu atampatia ulimwengu wote na vilivyopo. WATANZANIA WAKITAKA KIONGOZI BORA LAZIMA WAO NDIYO WAMUOMBE MUNGU NA SIO ANAYETAKA URAISI NDIYE ANAYEOMBA NA KUCHANGISHA KATIKA MAKANISA
 
Kama nchi imelaaniwa basi mkuu wa wezi EL atachaguliwa, lakini ajue kanisa katoriki la mitume haliwezi kwenda kusujudu mafisadi na wezi wanaoongozwa na EL

Sikatai kwamba Nyerere hakuwa nabii,lakini alikuwa rais na mwenyekiti wa ccm na aliwafahamu waadilifu,sasa kama alimfungia EL ASIPATE MADARAKA MAKUBWA YA NCHI JE SISI TULIOHAI NDIO TUUE MAADILI HIVIHIVI? Labda manazi wa EL WAMWELEZE KUWA AJIBU SIRI YA UTAJIRI WAKE,NANI MHUSIKA WA RICHMOND,KAGODA,EPA,BARICK?AKIFANYA HIVYO HATA MM NITAMWALIKA KWENYEHARAMBE YA UBARIKIO WA MWANANGU
 
Ali Hassan Mwinyi raisi mstaafu alikuwa mwenyekiti wa CCM wakati haya JK Nyerere akitoa hoja za kwanini Lowasa hafai kabisa kuwa Rais bora JK aliambiwa asubiri na sababu alizotoa Nyerere bado zipo wazi and they stilll stand, tunamuomba wnyekiti huyu na wajumbe ambao walikuwepo na wengi wao bado wapo ndani ya chama waje waweke mezani hasa kama sehemu ya kumbkumbu za mawazo ya busara na kumuenzi Nyerer wapige chini huyu fisadi Lowasa kabla hajaja kwetu wapiga kura tumsulibishe
 
Hakuna shaka sasa Maaskofu nao wameingia kwenye mikono ya EL. sijui watahubiri nini tena makanisani. Hizo fedha zitawatoka puani. Tafakarini sana mnayoyatenda. Kama hamkuwa na fedha za kuanzisha jimbo kwanini mlilianzisha?
Pengo analipeleka kubaya kanisa lenye heshima kubwa hapa nchini,anadhani anamkomoa kikwete hapana,anatukomoa sisi wapinga ufisadi wote tanzania wakiwemo waumini wa kanisa hilo.Anatakiwa kutoka na kutoa tamko kama walvyowahi kufanya walutheri kuzikataa pesa za lowassa na rostam walizokipatia kikundi cha kwaya
 
Hayo mabadiliko ya juzi hakuna kitu!, hiyo ngoma bado mbichi, utaniambia!.

ngoma mbichi kivipi wewe acha propaganda zako hapa,hii kitu inamtesa mzee na sasa amezidisha dozi ya pombe kali wewe unajifanya unakufa na tai shingoni,hebu niambie mhimili wa EL utakuwa wapi tena maana mlikua mnatuaminisha NEC ndiko anazo nguvu,sasa NEC inafumuliwa na kuundwa upya huku kukiwa na kibano cha yeye ama na watu wake ama achague kuwa nec au ubunge?

Hapa lazima mkubali na mkikataa itabidi tuwakubalishe kwamba ndio yametimia,lowassa njia nyeupe cck kama anautaka urais maana chadema nao hawamtaki,aende cck tena nasikia sasa wako arusha kwake huko.
 
Yohana 8 mstari 3 -12 Waandisi na mafarisayo wakamleta mwanamke aliefumaniwa katika uzinzi , wakamueka katikati. wakamuambia mwalimu mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini . Basi katika torati Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii nawe wasemaje ? Nao wakasema neno hlo wakimjaribu ili wapate sababu ya kumshtaki . lakini Yesu akainama akaandika kwa kidole chake ktk nchi . Nao walipozidi kumhoji alijiinua akawaambia yeye asie na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe . Akainama tena akaandika kwa kidole chake katika nchi . Nao waliposikia wakashtakiwa na dhamira zao wakatoka mmoja mmoja wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao. akabaki Yesu pekee yake , na yule mwanamke amesimama katikati . Yesu akajiinua asimuone mtu ila yule mwanamke akamuambia , mwanamke , wako wapi wale washtaki wako ? hakuna aliekuhukumu kuwa na hatia ? akamuambia hakuna bwana . Yesu akamuambia wala mimi sikuhukumu . Enenda zako wala usitende dhambi tena.

TAFAKARI CHUKUA HATUA.
 
Baba wa Taifa sio Mungu!. Mapenzi ya Mungu yatatimia!.


hakuna mungu anaeelekeza kuwapa sumu watu hata kama mnatofautiana kimtazamo;mungu huyo hayupo labda munge wa freemasons ambae hata hivyo simjui..!
 
Kuna watu wanapolisikia jina la Edward Lowassa wanaingiwa uoga sijui kwanini! Lowassa ni mchapakazi na kiongozi jasiri. Ufisadi upi kafanya? Ushahidi uko wapi? Nani hasiye pokea/toa rushwa nchi hii?
 
adui namba moja wa mchawi wa kiafrika ni maendeleo. Yes you are <--bold umeandika ushirikina mtupu kama ulivyo, wewe 2012 hii bado unaimani za mkibuyu??? makanisa mengine bana yani wao kazi yao nikuwajaza waumini wao vitisho badala ya kuwajenga jinsi ya kuishi maisha ya kumpendeza mungu, nyinyi ndio wale wa yale makanisa ambayo katika masaa 3 ya ibada mnatumia masaa 2:45 kumuongelea shetani na matendo yake kwa hiyo mkitoka huko mnakuwa na uelewa mpana zaidi juu ya shetani kuliko mungu kama unavyojionesha hapa.

WITO: Tujitokeze kwa wingi katika harambee ya kuijenga himaya ya mungu.. sambaza ujumbe huu kwa wengine viongozi wa kanisa katoliki ni makini sana na kama wangeona EL ana tatizo wasingemuita

hata jk aliitwa chaguo la mungu na viongozi haohao,pesa inaongea EPA iliwalainisha ma padri na maaskof!!
 
adui namba moja wa mchawi wa kiafrika ni maendeleo. Yes you are <--bold umeandika ushirikina mtupu kama ulivyo, wewe 2012 hii bado unaimani za mkibuyu??? makanisa mengine bana yani wao kazi yao nikuwajaza waumini wao vitisho badala ya kuwajenga jinsi ya kuishi maisha ya kumpendeza mungu, nyinyi ndio wale wa yale makanisa ambayo katika masaa 3 ya ibada mnatumia masaa 2:45 kumuongelea shetani na matendo yake kwa hiyo mkitoka huko mnakuwa na uelewa mpana zaidi juu ya shetani kuliko mungu kama unavyojionesha hapa.

WITO: Tujitokeze kwa wingi katika harambee ya kuijenga himaya ya mungu.. sambaza ujumbe huu kwa wengine viongozi wa kanisa katoliki ni makini sana na kama wangeona EL ana tatizo wasingemuita

Nafurahi umenihukumu pia,lakini fahamu sauti yangu ni Mungu kama yako!je wewe mtakatifu unafikiri kasi hii ya kuchangisha angefanya kwenye dispensari na shule za kata alizohamasisha Mungu angempa baraka gani? Acha upopombo na uhabithi kabwela mkubwa wewe! think great ebooo
 
Jamaa anarudisha mara dufu ya zile alizodhulumu kama yule Zakayo. Naona jamaa anakwenda na strategy ya mkoa kwa mkoa. Punde utamsikia Iringa, mara Mbeya mwishoni KYELA kufanya sala ya toba. Sisi tutazipokea, tutazitakasa kisha tutazila...
 
Kumbe kanisa la Roma limeishiwa hivi kiasi cha kuwa kitanda kimoja na mafisadi! Wanangu hakika dunia hii ni tambara bovu au tuseme guni. Haina wema wala maana kama mafisadi wanaweza kuchangia kazi ya Mungu hawamfanyi naye kuwa fisadi? Papa wa 16 uko wapi hapa?
 
Back
Top Bottom