Taasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika Mkoa wa Arusha imemwalika Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa kuwa mgeni rasmi

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Taasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika Mkoa wa Arusha imemwalika Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya kuzaliwa kwa mtume Mohamedi yatakayofanyika Katika Kijiji cha Karangai Wilayani Arumeru,Mkoani hapa.

Aidha Maadhimisho hayo yataenda sanjari na Changizo la Ujenzi wa kituo cha watoto yatima,ambapo viongozi wengine mbalimbali wa chama na serikali wamealikwa kushiriki sherehe hizo.

Akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha katika ,maandalizi ya maadhimisho hayo ya Maulidi ,msemaji Mkuu wa taasisi hiyo sheikh Haruna Hussein amesema kuwa watayatumia maadhimisho hayo kuombea amani taifa la Tanzania linaloelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Taifa.

Amesema maadhimisho hayo yatafanyika februal 22 mwaka huu katika kijiji cha Karangai ambapo waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa ataongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha watoto yatima kitakacho gharimu kiasi cha zaidi ya sh, milioni 150.

Naye mwenyekiti wa Twarika mkoa wa Kilimanjaro,Amin Hatibu Moshi amewataka viongozi wa dini kote nchini kuungana kwa pamoja na kuombea amani katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu wa Taifa.

Moshi amewataka viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini kuungana kwa pamoja na kuombea amani Taifa linaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa viongozi mbalimbali.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa Twarika hapa nchini,Khalifa Omari amesema kuwa maadhimisho ya Maulidi ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtume Mohamedi yataadhimishwa katika Zawiya ya Karangai huku dhima ya maadhimisho hayo ni kuombea amani Taifa la Tanzania .

Ends

IMG-20200123-WA0001.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
mzee Lowasa ingekuwa enzi zile anasaka uraisi hapo angewapa miliomi 100 akisema ni michango toka kwa rafiki zake friends of Lowasa
Sasa hivi rafiki zake ni Polepole, Mangula na wamasai wafugaji jee hawampi support?
Wengi wamemtenga kwa tabia za aina ile aliisema mwl Nyerere (kimalaya Malaya) yaani Leo huku kesho huku
 
"... kuombea amani taifa la Tanzania linaloelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Taifa." Siasa tayari zishaingizwa humo!
 
"... kuombea amani taifa la Tanzania linaloelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Taifa." Siasa tayari zishaingizwa humo!
Kua na akili ya uelewa,kuliombea taifa amani ni siasa? Yaani ukiona thd inayohusu dini usiyoipenda lazima ujipitishe huku unatingisha sio?
 
Kua na akili ya uelewa,kuliombea taifa amani ni siasa? Yaani ukiona thd inayohusu dini usiyoipenda lazima ujipitishe huku unatingisha sio?
... stop quoting me mpuuzi! Nakupotezea lakini naona unajiletaleta kima wewe!
 
Back
Top Bottom