Lowassa, Malecela na Sitta kunyimwa nishani maana yake nini?

Huu uzi upo tayari ni vizuri zikaunganishwa......maana ile nyingine ishafika page za kutosha.
 
Mantiki ya hizi nishani nini hasa?. Maana ichague baadhi ya vyeo tu?, Kwa nini na marais wastaafu nao wasiwemo? au JK anamuogopa Mkapa?, maana kama kigezo ni hicho alichosema basi Mkapa na Mwinyi wote walikuwa wanakosa kwa upande wa rais.

Kwa mantiki hiyo the whole thing of nishani ni usanii mwingine kati ya sanaa zilezile. Nafikiri na waliotoswa nao wanaweza kuandaa nishani yao kwa ujumla wao na kuwakabidhi marais walio hai, au waliokufa na kumyima Kikwete na kuwapatia Mkapa na wengineo kwa kigezo kuwa rais alichaguliwa kwa kura halali bila kuchakachua na asiye mwoga kuwashughulikia vigogo wala rushwa.
 
JK ana chuki binafsi na hawa jamaa.

Hana sababu za msingi za kuwanyima nishani hizo. Ni uzezeta na ujinga kwa mfano kumpa nishani ANNA MAKINDA spika wa kutetea MAFISADI ambaye ana mwaka tu kwenye nafasi hiyo na kumnyima SAMMY SITTA aliyeliongeza Bunge lililopita kwa umahiri mkubwa akitumia falsafa yake SSSS( Samwel Sitta's Standard and Speed).

Kiwete kwa mara nyingine amethibitisha uzezeta wake! Pambafuuuuuuuuuu
 
Mzee Jumbe kawakosea nini?

Hata mm nasangaa sn, hata kama ana yake(INGAWA SIYAJUI) lkn ukweli utabaki palepale kuwa ni yeye muasisi wa demokrasia visiwani kwa kuanzisha BARAZA LA WAWAKILISHI wongo jamani ????????? hata hivyo mzee asijali HISTORIA ina tabia moja HAIPINDISHWI KONA. Historia ITAMKUMBUKA TUUUU wapende wasipende.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Makinda?, JK kafanya nishani alizotoa kutokuwa na maana kwa hilo, umechemka MKULU
Heshima ya nishani inajengwa na watu wanaopewa. Ana Makinda amechafua maana yote. Hizo zinaitwa nishani za Kikwete na wala hazina maana yoyote!!!!Kikwete aliweka wazi kwamba, nishani hizo zimetolewa kwa Makamu Rais na Mawaziri Wakuu wastaafu walio hai ama waliokufa, walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka kwao madaraka, wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya ofisi yao.

Hivi huyu Bibi aliwahi kuwa Makamu Rais siyo?Uwaziri mkuu je?Labda kama alistaafu kwenye hizi nafasi hapo kale ndio anastahili nishani,hata Msekwa pia.Maana aliowataja kwenye red hapo panahusika,sijaona Spika kama nao walistahili nishani.
Otherwise Sitta kukosa sio issue,Lakini hata EL hakustaafu bali alijiuzuru!!!!!
 
"walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka kwao madaraka, wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya ofisi yao



.

Saturday, 10 December 2011 19:57
jk-kunakichwa.jpg


Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Na Leon Bahati

RAIS Jakaya Kikwete amewatunuku nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili wanasiasa mbalimbali waliowahi kushika nyadhifa za Uwaziri Mkuu na Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Muungano wa Tanzania, huku akiwatosa Edward Lowassa, John Malecela na Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambao nao, waliwahi kutumikia nafasi hizo.Vilevile, amemtunuku nishani hiyo spika wa zamani wa bunge, Pius Msekwa na wa sasa, Anne Makinda na kumtosa Samuel Sitta ambaye aliongoza Bunge la Tisa, kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, Oktoba mwaka jana.


Katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam juzi, kama sehemu ya maadhimisho ya kilele cha kumbukumbu ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, Rais Kikwete alitunuku nishani za aina tatu kwa Watanzania 57 waliotoa michango mbalimbali ya kutukuka kwa maendeleo ya nchi katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru wake.


Kikwete aliweka wazi kwamba, nishani hizo zimetolewa kwa Makamu Rais na Mawaziri Wakuu wastaafu walio hai ama waliokufa, walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka kwao madaraka, wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya ofisi yao.

Katika kundi hilo, Rais Kikwete aliwatunuku watu 10 na kuwaacha Malecela, Lowassa na Mzee Aboud Jumbe Mwinyi aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kujiuzulu mwaka 1984, kufuatia kile kilichoelezwa kuwa, machafuko ya hali ya hewa kisiasa Zanzibar.

Waliotunikiwa nishani hizo ni Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Mzee Abeid Aman Karume, Hayati Rashid Mfaume Kawawa, Hayati Edward Moringe Sokoine, Hayati Idrisa Abdul Wakili na Hayati Dk Omary Ali Juma.

Wengine ni Rais wa sasa wa Zanzibar ambaye aliwahi pia kuwa Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana , Dk Ali Mohamed Shein, na mawaziri wakuu wastaafu, Cleopa Msuya, Joseph Warioba, Dk Salim Ahmed Salim na Fredereck Sumaye.

Malecela akosa
Malecela alikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1990 hadi 1994, wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi.

Mbali na nyadhifa hizo za juu serikalini, mwanasiasa huyu pia aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM mwaka 1995 hadi 2007, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (1964-1966), Waziri wa Mambo ya Nje (1972-1973), Waziri wa Jumuia ya Afrika Mashariki (1975-1976), Mkuu wa Mkoa wa Iringa (1980-1984) , pia amekuwa Balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali ikiwemo Uingereza.

Akiwa katika kilele cha siasa za Tanzania, Malecela alionekana kuwa mwanasiasa mwenye nguvu na kuaminiwa katika Serikali ya Awamu ya Pili, hatua iliyompa nafasi kubwa kwamba huenda angemrithi Rais Mwinyi baada ya kumaliza muda wake kikatiba mwaka 1995.

Hata hivyo, rekodi yake ilichafuliwa wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kutunga kitabu alichokiita ‘Uongozi wetu na hatma ya uongozi Tanzania' kilichoainisha udhaifu kadhaa kisiasa wa kiongozi huyo na kumkosoa.


Kitabu hicho kilizima ghafla ndoto ya Malecela kuzidi kukwea milima ya kisiasa na kuwaacha njiapanda wachunguzi wa mambo ya kisiasa walioamini kuwa alikuwa kete muhimu ya Rais Mwinyi kurithi kiti chake, bila kujua mtu wa kurithi nafasi hiyo, kabla ya Rais Mkapa kuibuliwa na kuwa Rais ambaye hakutarajiwa na wengi.


Lowassa atoswa
Kwa upande wake Lowasa alikuwa Waziri Mkuu tangu mwaka 2005 hadi Februari mwaka 2008, katika Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete .

Lowassa ambaye ni mshirika wa siku nyingi kisiasa wa Rais Kikwete, alijiuzulu kufuatia kashfa ya utoaji zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa kampuni tata ya Richmond Development LCC.

Hivi karibuni kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kilichofanyika mjini Dodoma, Lowassa alijaribu kujitetea dhidi ya kashfa hiyo lakini hata hivyo wachunguzi wa mambo wanasema bado hajawa safi mbele ya serikali inayoongozwa na swahiba wake Rais Kikwete.

Lowassa alisema hakuhusika moja kwa moja katika hilo lakini alilazimika kujiuzulu kwa sababu waliozembea na maofisa walioko chini yake.

Alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa dhamira yake ilikuwa kuvunja mkataba wa Richmond jambo alilomjulisha pia mkubwa wake(Rais Kikwete) kwa simu akiwa nje ya nchi, lakini Rais alimwambia asubiri kwanza kwani alipata ushauri kutoka kwa makatibu wakuu kuhusu jambo hilo.

Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa gazetini kwa kile walichoeleza nafasi zao nyeti ndani ya serikali, walisema utetezi wa Lowassa bado haujakidhi kumfanya awe safi, ndio maana hakuweza kutunukiwa tuzo hiyo.

Walitoa mfano kwamba kwenye sherehe hizo, Rais Kikwete alimtunuku Nishani ya Juu ya Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ingawa naye aliwahi kujiuzulu kutokana na kashfa ya mauaji ya vikongwe mkoani Shinyanga wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Mwalimu Nyerere. Kwa uwajibikaji huo, Rais Kikwete aliutaja kuwa ni moja ya mambo ambayo yalionyesha kuwa Mwinyi ni mwadilifu.

Wachunguzi wa mambo haya siasa wanadai kitendo cha Mzee Mwinyi kujiuzulu na leo anatunukiwa nishani hiyo ni changamoto muhimu kwa Lowassa kutambua kuwa pamoja na maelezo yake ndani ya NEC, bado usafi kwa kashfa zinazomwandama unatia shaka, kwani yeye alijiuzulu baada ya Bunge kuunda tume iliyochunguza na kutoa mapendelezo ya ‘kupima' lakini Mzee Mwinyi alipima mwenyewe uzito wa tukio na kuamua kuachia ngazi.

Mzee Aboud Jumbe Mwinyi
Mzee Jumbe ambaye alikuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais katika kipindi cha mwaka 1972 hadi 1984 naye ni mmoja wa watu ambao hawakutunukiwa nishani hiyo mbali na kutumikia nafasi hizo kutokana na dosari zilizojitokeza wakati wa utumishi wake.

Aboud Jumbe lijiuzulu mwaka 1984 kutokana na kile kilichoelezwa, machafuko ya hali ya kisiasa visiwani Zanzibar yakihusisha chokochoko zilizokuwa na viashirio vya kuvunja Muungano.

Samuel Sitta
Kwenye sherehe hizo pamoja na kutunuku Msekwa na Makinda wengi wamejiuliza sababu za kutoswa kwa ‘Spika wa Bunge la Kasi na Viwango', Samuel Sitta.

Baadhi ya wanasiasa wazoefu waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa wameshangazwa na kitendo cha maspika hao kutunukiwa nishani na Sitta ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kuachwa.

Mmoja wa wanasiasa hao kutoka CCM ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema huenda Sitta hakupewa zawadi kutokana na chama hicho tawala kumtuhumu kuwa anaongoza makundi ya upinzani ndani ya chama, jambo ambalo mara kadhaa mwanasiasa huyo amekuwa akilikanusha.

Alisema huenda kutokana na msimamo wake imara usioyumba wa kupambana na vitendo vya ufisadi bila woga ndilo jambo ambalo linalokera wenzake ndani ya chama hicho nakutafsiri kwamba ni kukigawa chama .

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alisema hajui vigezo vilivyotumika kutoa nishani hizo lakini yeye anaamini Sitta aliweza kulifanya Bunge kuendesha mambo kiuwazi kiasi cha kuwafanya wananchi wengi kuwa na imani nalo.

"Alisema tangu awali Bunge lake litakuwa la ‘standard and speed' (kasi na viwango ) na liliweza kuonyesha hilo… lakini mimi Napata kigugumizi cha kusema sababu sijui vigezo vilivyotumika," alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na alihudhuria sherehe hizo.

Alisema ingawa yeye alichelewa kufika kwenye sherehe hizo, alishangazwa kusikia kuwa Makinda amepata tuzo hiyo wakati kipindi chake cha uspika hakijamalizika.

Spika mwingine ambaye hakutajwa kwenye orodha hiyo ni Yule aliyekuwa wa kwanza baada ya Tanzania kupata uhuru, Chifu Adam Sapi Mkwawa (1964-1973 na 1975-94) na Erasto Mang'enya (1973-75).

Nishani ya juu kabisa iliyotolewa ni ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo walitunukiwa maraisi wa awamu zote tatu zilizopita, Hayati Mwalimu Nyerere ambayo ilipokelewa na Mama Maria Nyerere kwa niaba yake, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

"walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka kwao madaraka, wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya ofisi yao".
 
Lowasa ni fisadi lililokubuhi nishani ya nini tena!!!!!!!??!????????

Mkuu sijui kwa nini watu wengi hawauoni ukweli huo kuwa Lowasa ni Mchafu wa maadili ya uongozi, sasa atapewaje Tunzo wakati sifa zake zina mapungufu ambayo yeye mwenyewe ameyathibitisha kwa kujiuzulu. Na cha kushangaza wanategemea ati Fisadi huyo awe Raisi wao!
 
Mie nimeshangaa katika list ile sikuliona jina la aliyewahi kuwa spika wakati wa enzi za chama kimoja, Chief Adam S. Mkwawa huyu naye alikuwa spika mzuri sana bungeni sijui amesahaulika au hakustahili kupata nishani ile.
 
Mie nimeshangaa katika list ile sikuliona jina la aliyewahi kuwa spika wakati wa enzi za chama kimoja, Chief Adam S. Mkwawa huyu naye alikuwa spika mzuri sana bungeni sijui amesahaulika au hakustahili kupata nishani ile.

Mkuu BAK siadhani kama Composition iliyopo IKULU leo hii ina Qualify kutoa nishani yoyote ya uongozi kwa viongozi wastaafu. Nafikiri wale walioachwa wametunziwa heshima zaidi na hakuna haja ya kulalamika. The whole tuzi was a joke. History will tell that sooner or later.

Serikali haiwezi kuweka vigezo vya kupima viwango vya uongozi wakati yenyewe pia ikiendelea kuonekana imelala fofo. Mchakato wa kutafuta majina haya ulitakiwa ufanyike kwa miezi sita kwa kuwashirikisha wananchi kwa njia ya polls za kisayansi. Kinachoonekana hapa ni JK na kundi la IKULU wameona watumie advantage ya kuwa IKULU Occupants kutuma vijembe kwa maadui zao. Huwezi kutafuta wachezaji bora 10 wa mpira duniani Halafu Leon Messi ukamwacha kwenye list. Kitendo cha kumuweka nje A.S Mkwawa au Samuel Sitta kama maspika bora zaidi kwa nyakati zao waliowahi kuliendesha bunge la Tanzania unakuwa ume-contaminate mchakato mzima. Yaani kinachooneka ni siasa na usanii at its best. Ikulu is rewarding failure instead of success hasa kwa upande wa maspika. Ila wananchi ndiyo tunajua ukweli.
 
Mkuu BAK siadhani kama Composition iliyopo IKULU leo hii ina Qualify kutoa niashani yoyote ya uongozi kwa viongozi wastaafu. Nafikiri wale walioachwa wametunziwa heshima zaidi na hakuna haja ya kulalamika. The whole tunzio was a joke. History will tell that sooner or later.

Serikali haiwezi kuweka vigezo vya kupima viwango vya uongozi wakati yenyewe pia ikiendelea kuonekana imelala fofo. Mchakato wa kutafuta majina haya ulitakiwa ufanyike kwa miezi sita kwa kuwashirikisha wananchi kwa njia ya polls za kisayansi. Kinachoonekana hapa ni JK na kundi la IKULU wameona watumie advantage ya kuwa IKULU Occupants kutuma vijembe kwa maadui zao. Huwezi kutafuta wachezaji bora 10 wa mpira duniani Halafu Leon Messi ukamwacha kwenye list. Kitendo cha kumuweka nje Samuel Sitta kama spika bora zaidi aliyewahi kutokea katika bunge la Tanzania unakuwa ume-contaminate mchakato mzima. Yaani kinachooneka ni siasa na usanii at its best.


Ahsante sana Mkuu Hofstede. Ninachoomba mimi kitokee ni hao maadui wa JK na kundi lake waongeze mashambulizi makali dhidi ya JK na Serikali yake ili kama ikiwezekana aachie ngazi kabla ya 2015, maana mimi naamini kabisa kwamba itakuwa ni janga kubwa sana kwa nchi yetu kama ataachiwa kubaki madarakani mpaka 2015, athari itakayofanywa na Serikali yake kwa nchi yetu itakuwa kubwa sana.
 
Awape asiwape sio kwamba ndo kakabiliana na mafisadi bali litabaki kuwa ni suala lisilokuwa na maslahi kwetu raia, kama maPHD na madegree wanapeana tu siwezi shangaza ktk hilo
 
Hakumainishi chochote - au + Kupewa tunzo yoyote kunahitaji ukamilifu wa sifa na vigezo fulani/kadhaa Wizi na Ubadhirifu ni mapungufu waliyonayo viongozi wengi tuliokuwa nao na tulionao. Wewe na mimi huenda tuna sifa kuliko baadhi ya waliopata hiyo Tunzo na wako waliotoa mchango mkubwa kwenye taifa hili na hata majina yao hayatajwi wamebaki kuwa "SILENT HEROES and WITNESES."
 
Tofautisha Waziri Mkuu mstaafu na Waziri Mkuu aliyefukuzwa. Warioba hakustaafu kwa kashfa, na hata baada ya kuondoka madarakani ameendelea kutumiwa vizuri sana Kimataifa. Hebu tueleze huyu fisadi Lowasa anatumiwa na nani baada ya kufukuzwa?
Ungejua Zigo la Ufisadi Mwananchi na Mereta Linamwelemea Mzee Warioba kama mwenyekiti wa Bodi!
 
Mimi "nadhani "kwa wawili hawa kukosa kupewa Nishani, Rais labda alitaka kuwaonyesha wote wawili kuwa hafurahishwi na mienendo yao katika chama.
 
MIMI Rais kanishangaza na kuniacha na maswali magumu
1.kutoa hotuba ambayo kaoengelea lami tu kama ndo issue kubwa lenye hadhi ya kuongelea katika miaka hamsini???
2.ktunuku wastaafu nishani ya heshima ya mwal. Nyerere ktika viwanja vya ikulu mbele ya wateule wachache? badala ya mbele ya watanzania waliokwenda uwanjani na kupigwa na jua huku wakiambulia gwaride la kila mwaka na hotuba ya dk 15 yenye kusema issue za lami

hili linatueleza nini?????????????????????????????????????

Kwamba Rais wetu anapenda kudili na ishu nyepesi nyepesi
 
Jamani pamoja na Yote,mie Mkweche nitafanya-SUPU ya Uraia ila mbona Mtwa wete Adam Sapi Mkwawa spika alieongoza bunge kwa Muda Mreefu kuliko wote karukwa akakubukwa wa Chini ya mwaka!Nishani hizi kama hazina Mzengwe basi zina Bahati Mbaya!
Mie Mkweche nilikuwa namwona Lowasa ni waziri mkuu mchapa kazi ile mbaya!Hivi mpaka kesho naona ngoyai Lowassa ni Kiongozi bora!Bado sijaona prime minister ka EL Hapa unafiki na ushabiki Kando!
 
[h=2]
icon1.png
Re: Lowassa, Malecela na Sitta kunyimwa nishani maana yake nini?[/h]
Mimi kwa upande wangu nafikiri Sitta alistahili tuzo maana wakati akiwa spika Bunge lake lilikuwa bunge lenye haki bila upendeleo wa chama tawala pia sijaona umuhimu kwanini Anna Makinda amepewa tuzo wakati ni puppet na ameshindwa kumudu Bunge? Naamini Aboud Jumbe Mwinyi alistahili tuzo la heshima ya juu kama marais wastaafu kwa sababu zifuatazo ni yeye aliyeleta demokrasia zaidi Zanzibar kuruhu baraza la wawakilishi kuwepo, kuwa na Waziri Kiongozi wa kwanza mwenye mamlaka Brigedia Ramadhani Haji pia kukubali maoni ya mwalimu kuunganisha TANU na ASP na kuzaliwa CCM

Karume alikuwa dikteta hakustahili hilo tuzo kwanza alikuwa muujai aliwaua Kassim Hanga na wengine, pia kutaka kumuua Professa Abrahman Babu pia hakuruhusu bunge isipokuwa kulikuwa na kundi la watu wanane likiongozwa na Kanali Seif Bakari ndilo lilikkuwa linatunga sheria za nchi. Na hata kama watu wanasema aliwezesha Tanganyika na Zanzibar kuungana hakuwa na jinsi maana ni Nyerere alliyemuweka madarakani baada ya kufanya juu chini na kumpokonya madaraka John Okello aliyefanya mapinduzi

Lakini Jumbe aliruhusu wabunge wawakilishi kuwepo, akaruhusu ASP kuungana na TANU na kuzaliwa CCM wakati Karume alikataa aliogopa nguvu zake kumalizwa na Nyerere. hata kama wanasema machafuko ya kisiasa ya mwaka 1984 Jumbe alikuwa upande wa wengi wenye kutaka serikali tatu kwani ni dhambi kusema vile? hata kama CCM wanaona ni dhambi aliyoyafanya ni mengi kuliko hilo leo ASP na TANU zisingeungana na kuzaliwa CCM sijui kama Tanzania ingekuwepo maana sasa hivi wabara huwacontrol wazanzibar kupitia vikao vya CCM kwahiyo ni Jumbe ndio kafanya Muungano uzidi kuwepo na anastahili tuzo la juu na yeye ni bora kuliko Karume

Pia ni kwanini Spika Adam Sapi Mkwawa hakupewa tuzo hilo wakati utumishi wake ni wa kutukuka? unaweza kumlinganisha Mkwawa na Anna Makinda? hizi nishani hazikuwa na umaana wowote isipokuwa ziligubikwa na siasa za makundi zaidi ya utumishi bora wa umma

 
Back
Top Bottom