Lowassa, Malecela na Sitta kunyimwa nishani maana yake nini?

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
Baada ya sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kumalizika ktk uwanja wa Taifa (Uwanja wa Uhuru), kulifanyika sherehe nyingine ktk viwanja vya Ikulu Dar es salaam, sherehe hiii ilikuwa ni ya kuwatunuku NISHANI viongozi mbali mbali wastaafu waliolitumikia Taifa hili.

Nishani hii yenye HESHIMA kubwa iliyopewa jina la Mwl. J. K. Nyerere ilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete. Aliwatunuku Marais wote wastaafu, Makamo wa Rais wote wastaafu, Mawaziri Wakuu wote wastaafu, na viongozi mbali mbali. Idadi ya Nishani zilizotolewa ilikuwa ni 40.

Sherehe hizi zilizoanza majira ya saa kumi jioni zilifana sana ktk viwanja hivyo vya Ikulu, nyuso za waliotunukiwa zilionekana kujaa furaha kubwa sana, na ni dhahiri zilionesha ni kiasi gani pengo la Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere lilivyo.

JAMBO lililoushtua umati mkubwa ulioalikwa kuhudhuria na kupamba sherehe hii ilikuwa ni pale jina la Mh. Edward Ngoyai Lowasa kutokuwepo ktk orodha ya viongozi hao. Watu waliokuwa wamejikusanya ktk makundi mbali mbali walisikika wakisema kuwa "huu ndio mwisho wa Lowasa ktk medani za siasa". Wengine walisikika wakisema kuwa "Lowasa hakupaswa kukimbilia ktk kipindi maalum kilichorushwa na TBC1", kwani kufanya hivyo ni kuonesha Umma wa Watanzania kuwa anashindana na viongozi wake Wakuu, yaani Waziri Mkuu na Rais.

Baada ya mahojiano na TBC1, wananchi wengi kutoka ktk viunga vyote nchini walilipuka kwa mshangao dhidi ya kituo hiki cha habari kinachomilikiwa na Serikali kutojua au kwa makusudi kuvunja itifaki. Wengi wamekosa imani na chombo hiki, na kuona kama ni cha Mh. Edward Lowasa.

Ninaamini kuwa tutapata mawazo mengi mazuri juu ya matukio hayo mawili yaliyotokea jana, na hasa ukizingatia kuwa, mara kadhaa Mh. Lowasa amekuwa akitamba hadharani kuwa Rais Kikwete ni rafiki yake aliyetoka nae mbali, na wawili hao hawakukutana mitaani. Lakini jambo jingine hapa ni kuwa, CCM inajiandaa na uchaguzi wa viongozi wake ktk nafasi mbali mbali mwaka kesho. Uchaguzi huu utaunda timu ya ushindi wa chama hicho kikongwe utakaofanyika mwaka 2015. Kuna tetesi kuwa Mh. Lowasa anautamani saana URAIS, na hivyo ANAJIANDAA KUGOMBEA.

Viongozi wastaafu ambao bado wanaendelea na nyadhifa nyingine serikalini nao hawakupewa nishani maana si wastaafu, na Lowassa si mstaafu ni "mjiuzulu".

Jana katika kuazimisha miaka 50 pamoja na mambo mengine Rais alitoa nishani kwa watu mbali mbali waliolitumikia taifa. Kwa upande wa maspika wa Bunge wamepewa Pius Msekwa na Anna Makinda.

Swali ninalojiuliza, hivi Sitta hakustahili kupata nishani? Kwa nini amenyimwa yeye aliyekuwa spika kwa miaka mitano akapewa Anna Makinda ambaye ametumikia nafasi hiyo kwa mwaka mmoja tu sasa?

Kutoka gazeti la Mwananchi Disemba 11, 2011:

Malecela akosa

Malecela alikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1990 hadi 1994, wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi.

Mbali na nyadhifa hizo za juu serikalini, mwanasiasa huyu pia aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM mwaka 1995 hadi 2007, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (1964-1966), Waziri wa Mambo ya Nje (1972-1973), Waziri wa Jumuia ya Afrika Mashariki (1975-1976), Mkuu wa Mkoa wa Iringa (1980-1984) , pia amekuwa Balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali ikiwemo Uingereza.

Akiwa katika kilele cha siasa za Tanzania, Malecela alionekana kuwa mwanasiasa mwenye nguvu na kuaminiwa katika Serikali ya Awamu ya Pili, hatua iliyompa nafasi kubwa kwamba huenda angemrithi Rais Mwinyi baada ya kumaliza muda wake kikatiba mwaka 1995.

Hata hivyo, rekodi yake ilichafuliwa wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kutunga kitabu alichokiita ‘Uongozi wetu na hatma ya uongozi Tanzania' kilichoainisha udhaifu kadhaa kisiasa wa kiongozi huyo na kumkosoa.

Kitabu hicho kilizima ghafla ndoto ya Malecela kuzidi kukwea milima ya kisiasa na kuwaacha njiapanda wachunguzi wa mambo ya kisiasa walioamini kuwa alikuwa kete muhimu ya Rais Mwinyi kurithi kiti chake, bila kujua mtu wa kurithi nafasi hiyo, kabla ya Rais Mkapa kuibuliwa na kuwa Rais ambaye hakutarajiwa na wengi.

Lowassa atoswa

Kwa upande wake Lowasa alikuwa Waziri Mkuu tangu mwaka 2005 hadi Februari mwaka 2008, katika Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete .

Lowassa ambaye ni mshirika wa siku nyingi kisiasa wa Rais Kikwete, alijiuzulu kufuatia kashfa ya utoaji zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa kampuni tata ya Richmond Development LCC.

Hivi karibuni kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kilichofanyika mjini Dodoma, Lowassa alijaribu kujitetea dhidi ya kashfa hiyo lakini hata hivyo wachunguzi wa mambo wanasema bado hajawa safi mbele ya serikali inayoongozwa na swahiba wake Rais Kikwete.

Lowassa alisema hakuhusika moja kwa moja katika hilo lakini alilazimika kujiuzulu kwa sababu waliozembea na maofisa walioko chini yake.

Alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa dhamira yake ilikuwa kuvunja mkataba wa Richmond jambo alilomjulisha pia mkubwa wake(Rais Kikwete) kwa simu akiwa nje ya nchi, lakini Rais alimwambia asubiri kwanza kwani alipata ushauri kutoka kwa makatibu wakuu kuhusu jambo hilo.

Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa gazetini kwa kile walichoeleza nafasi zao nyeti ndani ya serikali, walisema utetezi wa Lowassa bado haujakidhi kumfanya awe safi, ndio maana hakuweza kutunukiwa tuzo hiyo.

Walitoa mfano kwamba kwenye sherehe hizo, Rais Kikwete alimtunuku Nishani ya Juu ya Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ingawa naye aliwahi kujiuzulu kutokana na kashfa ya mauaji ya vikongwe mkoani Shinyanga wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Mwalimu Nyerere. Kwa uwajibikaji huo, Rais Kikwete aliutaja kuwa ni moja ya mambo ambayo yalionyesha kuwa Mwinyi ni mwadilifu.

Wachunguzi wa mambo haya siasa wanadai kitendo cha Mzee Mwinyi kujiuzulu na leo anatunukiwa nishani hiyo ni changamoto muhimu kwa Lowassa kutambua kuwa pamoja na maelezo yake ndani ya NEC, bado usafi kwa kashfa zinazomwandama unatia shaka, kwani yeye alijiuzulu baada ya Bunge kuunda tume iliyochunguza na kutoa mapendelezo ya ‘kupima' lakini Mzee Mwinyi alipima mwenyewe uzito wa tukio na kuamua kuachia ngazi.

Mzee Aboud Jumbe Mwinyi

Mzee Jumbe ambaye alikuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais katika kipindi cha mwaka 1972 hadi 1984 naye ni mmoja wa watu ambao hawakutunukiwa nishani hiyo mbali na kutumikia nafasi hizo kutokana na dosari zilizojitokeza wakati wa utumishi wake.

Aboud Jumbe lijiuzulu mwaka 1984 kutokana na kile kilichoelezwa, machafuko ya hali ya kisiasa visiwani Zanzibar yakihusisha chokochoko zilizokuwa na viashirio vya kuvunja Muungano.

Samuel Sitta
Kwenye sherehe hizo pamoja na kutunuku Msekwa na Makinda wengi wamejiuliza sababu za kutoswa kwa ‘Spika wa Bunge la Kasi na Viwango', Samuel Sitta.

Baadhi ya wanasiasa wazoefu waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa wameshangazwa na kitendo cha maspika hao kutunukiwa nishani na Sitta ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kuachwa.

Mmoja wa wanasiasa hao kutoka CCM ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema huenda Sitta hakupewa zawadi kutokana na chama hicho tawala kumtuhumu kuwa anaongoza makundi ya upinzani ndani ya chama, jambo ambalo mara kadhaa mwanasiasa huyo amekuwa akilikanusha.

Alisema huenda kutokana na msimamo wake imara usioyumba wa kupambana na vitendo vya ufisadi bila woga ndilo jambo ambalo linalokera wenzake ndani ya chama hicho nakutafsiri kwamba ni kukigawa chama .

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alisema hajui vigezo vilivyotumika kutoa nishani hizo lakini yeye anaamini Sitta aliweza kulifanya Bunge kuendesha mambo kiuwazi kiasi cha kuwafanya wananchi wengi kuwa na imani nalo.

"Alisema tangu awali Bunge lake litakuwa la ‘standard and speed' (kasi na viwango ) na liliweza kuonyesha hilo… lakini mimi Napata kigugumizi cha kusema sababu sijui vigezo vilivyotumika," alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na alihudhuria sherehe hizo.

Alisema ingawa yeye alichelewa kufika kwenye sherehe hizo, alishangazwa kusikia kuwa Makinda amepata tuzo hiyo wakati kipindi chake cha uspika hakijamalizika.

Spika mwingine ambaye hakutajwa kwenye orodha hiyo ni Yule aliyekuwa wa kwanza baada ya Tanzania kupata uhuru, Chifu Adam Sapi Mkwawa (1964-1973 na 1975-94) na Erasto Mang'enya (1973-75).
 
... Hao viongozi wawili hawana afya ya kutosha kuzozana kwa muda mrfeu ... hakuna shaka afya zao ndizo zitakzo amua mwisho wa sakata hili muda sio mrefu ... stay tuned!!!!
 
Jana katika kuazimisha miaka 50 pamoja na mambo mengine Rais alitoa nishani kwa watu mbali mbali waliolitumikia taifa. Kwa upande wa maspika wa Bunge wamepewa Pius Msekwa na Anna Makinda.

Swali ninalojiuliza, hivi Sitta hakustahili kupata nishani? Kwa nini amenyimwa yeye aliyekuwa spika kwa miaka mitano akapewa Anna Makinda ambaye ametumikia nafasi hiyo kwa mwaka mmoja tu sasa?
 
Labda tungeanza kwanza kwanini Lowassa apewe nishani ametoa mchango gani ? maana kuwa rafiki na rais sio sababu ya yeye kupewa nishani.

Pia sitta kwa lipi alilofanyia taifa hili?
 
Kuna kitu ambacho sikielewi hapa.Hili jina na Lowassa!Amekuwa akiitwa waziri mkuu mstaafu na watu wamepinga sana tu yeye kutambulika hivyo kitu ambacho binafsi pia nilielewa kwani ni kweli Lowassa hakuwahi kustaafu!Sasa hapa tena ameachwa kwenye orodha ya kupewa nishani viongozi wastaafu inaonekana hajatendewa haki!Nilitegemea rais apongezwe hatimaye kwa kuonyesha kutomtambua mstaafu Lowassa!Lakini bado kuna lawama tena!Duh!Huyu Lowassa anaonekana anao uwezo wa kuwafanya watu wawe vichaa...!
 
Sometimes vitu vingine tuviache vipite tu. Hivi mtu amekuwa Prime Minister for about two years, na ameondoka in disgrace baada ya kusaini mkataba na Kampuni "hewa". Apewe nishani ya nini tena? Mbona hamjauliza na Makamba?

Na unapongelea urafiki wa JK na EL, kwani nishani zilikuwa kwa marafiki wa JK?
 
Jana katika kuazimisha miaka 50 pamoja na mambo mengine Rais alitoa nishani kwa watu mbali mbali waliolitumikia taifa. Kwa upande wa maspika wa Bunge wamepewa Pius Msekwa na Anna Makinda.

Swali ninalojiuliza, hivi Sitta hakustahili kupata nishani? Kwa nini amenyimwa yeye aliyekuwa spika kwa miaka mitano akapewa Anna Makinda ambaye ametumikia nafasi hiyo kwa mwaka mmoja tu sasa?

Sitta na Lowassa sasa wamewekwa kundi moja na vigogo wa CCM na huenda wote wakatoswa pamoja.
 
Baada ya sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kumalizika ktk uwanja wa Taifa (Uwanja wa Uhuru), kulifanyika sherehe nyingine ktk viwanja vya Ikulu Dar es salaam, sherehe hiii ilikuwa ni ya kuwatunuku NISHANI viongozi mbali mbali wastaafu waliolitumikia Taifa hili.

Nishani hii yenye HESHIMA kubwa iliyopewa jina la Mwl. J. K. Nyerere ilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete. Aliwatunuku Marais wote wastaafu, Makamo wa Rais wote wastaafu, Mawaziri Wakuu wote wastaafu, na viongozi mbali mbali. Idadi ya Nishani zilizotolewa ilikuwa ni 40.

Sherehe hizi zilizoanza majira ya saa kumi jioni zilifana sana ktk viwanja hivyo vya Ikulu, nyuso za waliotunukiwa zilionekana kujaa furaha kubwa sana, na ni dhahiri zilionesha ni kiasi gani pengo la Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere lilivyo.

JAMBO lililoushtua umati mkubwa ulioalikwa kuhudhuria na kupamba sherehe hii ilikuwa ni pale jina la Mh. Edward Ngoyai Lowasa kutokuwepo ktk orodha ya viongozi hao. Watu waliokuwa wamejikusanya ktk makundi mbali mbali walisikika wakisema kuwa "huu ndio mwisho wa Lowasa ktk medani za siasa". Wengine walisikika wakisema kuwa "Lowasa hakupaswa kukimbilia ktk kipindi maalum kilichorushwa na TBC1", kwani kufanya hivyo ni kuonesha Umma wa Watanzania kuwa anashindana na viongozi wake Wakuu, yaani Waziri Mkuu na Rais.

Baada ya mahojiano na TBC1, wananchi wengi kutoka ktk viunga vyote nchini walilipuka kwa mshangao dhidi ya kituo hiki cha habari kinachomilikiwa na Serikali kutojua au kwa makusudi kuvunja itifaki. Wengi wamekosa imani na chombo hiki, na kuona kama ni cha Mh. Edward Lowasa.

Ninaamini kuwa tutapata mawazo mengi mazuri juu ya matukio hayo mawili yaliyotokea jana, na hasa ukizingatia kuwa, mara kadhaa Mh. Lowasa amekuwa akitamba hadharani kuwa Rais Kikwete ni rafiki yake aliyetoka nae mbali, na wawili hao hawakukutana mitaani. Lakini jambo jingine hapa ni kuwa, CCM inajiandaa na uchaguzi wa viongozi wake ktk nafasi mbali mbali mwaka kesho. Uchaguzi huu utaunda timu ya ushindi wa chama hicho kikongwe utakaofanyika mwaka 2015. Kuna tetesi kuwa Mh. Lowasa anautamani saana URAIS, na hivyo ANAJIANDAA KUGOMBEA.

Viongozi wastaafu ambao bado wanaendelea na nyadhifa nyingine serikalini nao hawakupewa nishani maana si wastaafu, na Lowassa si mstaafu ni "mjiuzulu".

Lowasa sio waziri mkuu mstaafu..ni waziri mkuu aliyejiuzulu...kwa hiyo astahili kupewa tuzo,Sitta kwa lipi? Lakini TBC1 wanaonekana wanamaslahi ya EL maana kila siku wao ni kumuweka hewani...nadhani kamshika mtu mmoja pale ofisi ya uhariri au chumba cha habari...
 
MIMI Rais kanishangaza na kuniacha na maswali magumu
1.kutoa hotuba ambayo kaoengelea lami tu kama ndo issue kubwa lenye hadhi ya kuongelea katika miaka hamsini???
2.ktunuku wastaafu nishani ya heshima ya mwal. Nyerere ktika viwanja vya ikulu mbele ya wateule wachache? badala ya mbele ya watanzania waliokwenda uwanjani na kupigwa na jua huku wakiambulia gwaride la kila mwaka na hotuba ya dk 15 yenye kusema issue za lami

hili linatueleza nini?????????????????????????????????????
 
Back
Top Bottom