Lowassa ashinda Ujumbe wa NEC (CCM) Monduli kwa Ushindi wa 99.9%!

Lowassa amemaliza yaani kofi la uso haswa! Nina furaha kwa ushindi wake na amejibu wale wote waliokuwa na shaka naye, nusu saa iliyopita nilisoma thread ya pasco mmh alinitia shaka nikawa nadhani labda ccm wanaweza wakamtosa kama Sumaye! Kumbe kutoswa kwa Sumaye ni draft la Lowassa! Well done EL!
Nawashangaa mnaoshangaa fisadi papa huyu kushinda kwa kishindo kura za masai wenzie wa kule Arusha.Binafsi sishangai kwa sababu amechaguliwa na kundi dogo la watu linalonunulika kwa fedha ambayo kibaka
asiye aaibu huyu si tatizo kabisa. Ukweli ni kwamba wigo ukipanuliwa hataweza kuwahonga wapiga kura wote Tanzania nzima!
 
Mwenendo wa Kisiasa wa Mh. Edward Lowassa ndini ya CCM umekuwa mwiba mchungu kwa Katibu Mwenezi wa Chama cha Mafisadi (CCM). Ushindi wa kishindo alioupata Mh. Lowassa wa 99.9% ya kura zilizopigwa na kumpitisha kuwa mjumbe wa NEC-Mafisadi kutoka wilaya ya Monduli umekuwa sawa na kofi la uso kisiasa dhidi ya Nape ambaye alimwandama Lowassa na wenzake kuwa ni miongoni mwa wa chafuzi wa CCM kisiasa na kimwenendo.

Sipati picha, katibu mwenezi huyo yuko hali gani mara aliposikia kimbunga cha Lowassa kikipita mbele yake kwa matokeo hayo! Kijana Nape hana budi kujitokeza hadharani na kumtaka radhi Mh. Lowassa na wana magamba woote. Kwa jinsi Lowassa anavyopaa na kupaishwa na wana-CCM hapana ubishi kwamba kauli za Nape dhidi ya Lowassa zimedharauliwa na kumwagwa jalalani kama mchuzi wa mlenda wa juzi na wana-CCM; kwa mantiki hiyo, Nape hakubaliki na huenda haheshimiki ndani ya wana-CCM.

Ushauri wangu. Nape ajiuzuru nafasi aliyonayo ama amwombe radhi Mh. Lowassa na wana-magamba wote kwa kauli zake alizowahi zisema juu ya Lowassa. Ama la, Nape atakuwa gamba sugu analokufa nalo nyoka.
 
Mpende msipende lowasa atakuwa rais 2015 hakuna wakumpinga heri fisadi mchapakazi,haza ukisingatia kipindi chake akiwa wasiri mkuu nidhamu ilikuwepo.

leo ndo umenigusa mkuu kwa lowasa kuwa rais hata mimi kula yangu ya ndio ashapata.
 
Dr Slaa naye atamgaragaza 2015 kwa asilimia za kutosha. Lowasa hawezi kusafishwa na maaskofu na mashekhe anaowafadhili. Kuanzia unataka mpaka hataki. Huo ndio ukweli.

Ndugu yangu, Slaa ni kichuguu cha mchwa mbele ya Lowassa Mlima Everest. mbona hilo liko wazi? Tafakari vitu vya kulinganisha Moriah.
 
Lowassa hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,ccm hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,wanamonduli hongereni sana mmetupa raha watanzania.
 
Rais in 2015 lazima atoke kaskazini, either oposition or rulling part. Big up maumvi na sera ya taifa la wajinga
 
Hakika hawezi kujibu hii maana atakuwa amepepea vita na lowasa na akijaribu atafukuzwa ukatibu ueneze.
Nape linapokuja swala la Lowasa ana kuwa muoga sana!

Subiri atakuja kukujibu sasa hivi !
 
Lowasa ana sifa kuu 3 1. Hajawahi kukata tamaa au kukatishwa tamaa na binadamu,mzoefu wa fitina za siasa za TZ
2. Silaha ya pesa ni kipaumbele kikubwa kwake
3. Mbishi wa kuhimili Lawama na kashfa .
 
Mkianza haya mambo ya kila kanda kujifagilia na kujipigia kura basi si kaskazini, si kusini, si pwani wala si magharibi bali kanda ya ziwa ndiko atatoka rais.

Embu tuache mambo haya!!

Huyo wa kutoka kanda ya ziwa ni nani?
 
Lowassa kule Mondulu ni Mungu mtu!!! Kwa watanzania wote ni sifuri!! Karibu fisadi 2015 ukagombee Urais!! Kumbuka husafishiki hata kwa maji taka!! Umechafuka mno!! Nape hongera!! SSM Mondulu hawakutambui na debe lako tupu halitiki!! Hivi upoo mkuu sijakusikia kwa press release na matamko!!
 
Lowasa ana sifa kuu 3,
1. Hajawahi kukata tamaa au kukatishwa tamaa na binadamu,mzoefu wa fitina za siasa za TZ
2. Silaha ya pesa ni kipaumbele kikubwa kwake
3. Mbishi wa kuhimili Lawama na kashfa .
 
Pasco na Wana JF: Mnakumbuka mchango wangu kuhusu ile thread ya kumshauri EL kuachana na siasa? Let me quote a paragraph from my contribution nayo ni hii iliyo kwenye red:

"Naona kuna siri kubwa kati ya vigogo wa CCM ikiwa ni pamoja na Lowassa mwenyewe. Anaogopwa ndani ya chama chake mbona hawakuthubutu kumwengua mapema kama walivyomfanya Sumaye? Wanaogopa atamwaga mboga na ugali kwa mpigo au?? Kweli siasa ni mchezo wa ajabu mno especially where transparency is lacking".

This man EL seems to exert high influence within his party for sure. He knows so many secrets of his senior colleagues and for that, they fear him. They can never denounce him publicly like the naive Nape did, no way!! Hata hivyo kwa wilaya ya Monduli na sehemu nyingi za Tanzania bado ujinga ni mtaji na ni fursa nzuri mno kwa Lowassa na CCM kuendelea kutawala kwa sasa. Kutokana na ujinga, watu wengi hawajaweza kutafakari na kutafsiri madhara muda mrefu yatokanayo na ufisadi na rushwa katika maisha yao. Kwa hiyo suala hili haliwasumbui sana. Ushahidi ni yale yaliyojiri Monduli kwa kumpitisha EL kwa kishindo kuwa mjumbe wa NEC wilaya. Na si ajabu anategemewa kitaifa tusubiri. CCM ni wanafiki hili liko wazi. Lakini ikumbukwe kuwa fursa hazidumu bali hubadilika na kuchukua sura tofauti. Pengine hili analijua Lowassa vizuri na analifanyia kazi usiku na mchana bila shaka.

Lowassa hivi karibuni ameonyesha kuwa na msimamo wa kusisitiza suala la elimu kuliko kilimo. Kwa nini? Anajua pengine uchaguzi ujao (2015) CCM kwa kujikita katika ile fursa ya ujinga walioulea kwa manufaa yao ya kisiasa, unaweza ukawa mwisho wa CCM kuchukua dola kilaini. Kwa kuwapatia wananchi elimu baada ya hapo, itakuwa vigumu kwa chama chochote cha kisiasa kuchukua dola kirahisi kama walivyofaidi CCM miaka yote. Kwa mantiki hii atakuwa ameshatimiza ndoto yake na CCM kupata nafasi nzuri ya kujipanga vema katika siasa za ushindani!!!

Mwenendo wa Kisiasa wa Mh. Edward Lowassa ndini ya CCM umekuwa mwiba mchungu kwa Katibu Mwenezi wa Chama cha Mafisadi (CCM). Ushindi wa kishindo alioupata Mh. Lowassa wa 99.9% ya kura zilizopigwa na kumpitisha kuwa mjumbe wa NEC-Mafisadi kutoka wilaya ya Monduli umekuwa sawa na kofi la uso kisiasa dhidi ya Nape ambaye alimwandama Lowassa na wenzake kuwa ni miongoni mwa wa chafuzi wa CCM kisiasa na kimwenendo.

Sipati picha, katibu mwenezi huyo yuko hali gani mara aliposikia kimbunga cha Lowassa kikipita mbele yake kwa matokeo hayo! Kijana Nape hana budi kujitokeza hadharani na kumtaka radhi Mh. Lowassa na wana magamba woote. Kwa jinsi Lowassa anavyopaa na kupaishwa na wana-CCM hapana ubishi kwamba kauli za Nape dhidi ya Lowassa zimedharauliwa na kumwagwa jalalani kama mchuzi wa mlenda wa juzi na wana-CCM; kwa mantiki hiyo, Nape hakubaliki na huenda haheshimiki ndani ya wana-CCM.

Ushauri wangu. Nape ajiuzuru nafasi aliyonayo ama amwombe radhi Mh. Lowassa na wana-magamba wote kwa kauli zake alizowahi zisema juu ya Lowassa. Ama la, Nape atakuwa gamba sugu analokufa nalo nyoka.
Hivi Lowasa na Nape wanauhasama?Upi?si wote ni CCM?
 
........ hakuna jinsi najua watu walitaka yaliyomkuta Sumaye yawe ya Lowassa na yaliyomkuta Lowasa yawe Sumaye mimi Nampongeza kwa ushindi, hii inadhirisha kwamba wananchi wa Monduli ni miongoni wana CCM wanaomkubali

Kwakweli Nape hapo kapigwa kofi la kisiasa na hamuwezi kabisa lowasa!
 
Back
Top Bottom