Lowassa ashinda Ujumbe wa NEC (CCM) Monduli kwa Ushindi wa 99.9%!

Mpende msipende lowasa atakuwa rais 2015 hakuna wakumpinga heri fisadi mchapakazi,haza ukisingatia kipindi chake akiwa wasiri mkuu nidhamu ilikuwepo.
 
hata akishinda kwa 200% haisadii maana ukiangalia wamasai ujinga ndio kabisa elimu ndio kabisa usijifariji kama akingombea urais atapata 99.9% hizo zitakuwa ni ndoto za kuota kama una bisha ccm wamuweke 2015 ndio uone kama wananchi watanzania ni wajinga kama unavyofikiria atashindwa tena vimbaya sana.
 
Dr Slaa naye atamgaragaza 2015 kwa asilimia za kutosha. Lowasa hawezi kusafishwa na maaskofu na mashekhe anaowafadhili. Kuanzia unataka mpaka hataki. Huo ndio ukweli.
 
Mwenendo wa Kisiasa wa Mh. Edward Lowassa ndini ya CCM umekuwa mwiba mchungu kwa Katibu Mwenezi wa Chama cha Mafisadi (CCM). Ushindi wa kishindo alioupata Mh. Lowassa wa 99.9% ya kura zilizopigwa na kumpitisha kuwa mjumbe wa NEC-Mafisadi kutoka wilaya ya Monduli umekuwa sawa na kofi la uso kisiasa dhidi ya Nape ambaye alimwandama Lowassa na wenzake kuwa ni miongoni mwa wa chafuzi wa CCM kisiasa na kimwenendo.

Sipati picha, katibu mwenezi huyo yuko hali gani mara aliposikia kimbunga cha Lowassa kikipita mbele yake kwa matokeo hayo! Kijana Nape hana budi kujitokeza hadharani na kumtaka radhi Mh. Lowassa na wana magamba woote. Kwa jinsi Lowassa anavyopaa na kupaishwa na wana-CCM hapana ubishi kwamba kauli za Nape dhidi ya Lowassa zimedharauliwa na kumwagwa jalalani kama mchuzi wa mlenda wa juzi na wana-CCM; kwa mantiki hiyo, Nape hakubaliki na huenda haheshimiki ndani ya wana-CCM.

Ushauri wangu. Nape ajiuzuru nafasi aliyonayo ama amwombe radhi Mh. Lowassa na wana-magamba wote kwa kauli zake alizowahi zisema juu ya Lowassa. Ama la, Nape atakuwa gamba sugu analokufa nalo nyoka.
 
Pasco usiliache hilo jembe, hayo ndo majibu kukata hamu za akina nape, Lowassa I salute you.
 
Pasco yuko wapi na ushauri wake?? nilimuambia MOnduli wanamuabudi fisadi kama mungu!!
 
Ushindi ulioupata mzee sasa umepitiliza. Walidhani utafuata nyayo za Sumaye ila kuna tofauti kubwa sana kati yako na yeye!

Kushinda kwa asilimia 99.9 si mchezo NEC hiyo sasa! Hongera Comrade......
Join Date : 14th September 2012
naona ulijiunga maalumu kwa ujira maalumu wa kutetea mafisadi!!
 
Lowassa ni jembe nasubiri nape aje na yake! Chezea Lowassa wewe?
 
Ushindi ulioupata mzee sasa umepitiliza. Walidhani utafuata nyayo za Sumaye ila kuna tofauti kubwa sana kati yako na yeye!

Kushinda kwa asilimia 99.9 si mchezo NEC hiyo sasa! Hongera Comrade......

Mm ndo kawa komred wako??? Ujue io ni kjipendekeza kwa fisadi EL na katu skuungi mkono katu...
 
Rais 2015 atatoka kaskazini iwe ni ccm au cdm

Mkianza haya mambo ya kila kanda kujifagilia na kujipigia kura basi si kaskazini, si kusini, si pwani wala si magharibi bali kanda ya ziwa ndiko atatoka rais.

Embu tuache mambo haya!!
 
Lowassa amemaliza yaani kofi la uso haswa! Nina furaha kwa ushindi wake na amejibu wale wote waliokuwa na shaka naye, nusu saa iliyopita nilisoma thread ya pasco mmh alinitia shaka nikawa nadhani labda ccm wanaweza wakamtosa kama Sumaye! Kumbe kutoswa kwa Sumaye ni draft la Lowassa! Well done EL!
 
Fisadi lowassa kawashika wale wamasai duni monduli,hapa arusha mjini hakohoi.TUMESHAMZIKA KISIASA LONGI
 
Nauliza hivi NEC inaviti vingapi?

Naona maadui wa Lowassa level ya NEC watakuwa wengi halafu msisahau Ridhiwani na Mama Kikwete na influence yao

Mwisho kabisa sitashangaa kama Richmond ikawa gumzo tena. Nani alitarajia suala la sumu kurudia tena kuwa gumzo?
 
Ushindi ulioupata mzee sasa umepitiliza. Walidhani utafuata nyayo za Sumaye ila kuna tofauti kubwa sana kati yako na yeye!

Kushinda kwa asilimia 99.9 si mchezo NEC hiyo sasa! Hongera Comrade......





MONDAY, OCTOBER 01, 2012

MH LOWASSA ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA NAFASI YA UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA WILAYA YA MONDULI





Mh Lowassa akizungumza na kuwashukuru wapiga kura wake waliompatia ushindi wa
kishindo.

Waziri mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,mh. Edward Lowassa akipongezwa mara baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya Wilaya ya Monduli uliofanyika leo katika ukumbi wa chuo cha ualimu Monduli,Mh Lowassa ameshinda kwa kishindo kwa kuwabwaga wapinzani wake kwa idadi ya kura 709,mpinzani mwingine ameta kura 44 na mshindi mwingine aliibuka na kura 7.



Waziri mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,mh. Edward Lowassa akipongezwa mara baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya Wilaya ya Monduli uliofanyika leo katika ukumbi wa chuo cha ualimu Monduli,Mh Lowassa ameshinda kwa kishindo kwa kuwabwaga wapinzani wake kwa idadi ya kura 709,mpinzani mwingine amepata kura 44 na mshindi mwingine aliibuka na kura 7.

MONDAY, OCTOBER 01, 2012 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG








 
mwenendo wa kisiasa wa mh. Edward lowassa ndini ya ccm umekuwa mwiba mchungu kwa katibu mwenezi wa chama cha mafisadi (ccm). Ushindi wa kishindo alioupata mh. Lowassa wa 99.9% ya kura zilizopigwa na kumpitisha kuwa mjumbe wa nec-mafisadi kutoka wilaya ya monduli umekuwa sawa na kofi la uso kisiasa dhidi ya nape ambaye alimwandama lowassa na wenzake kuwa ni miongoni mwa wa chafuzi wa ccm kisiasa na kimwenendo.

Sipati picha, katibu mwenezi huyo yuko hali gani mara aliposikia kimbunga cha lowassa kikipita mbele yake kwa matokeo hayo! Kijana nape hana budi kujitokeza hadharani na kumtaka radhi mh. Lowassa na wana magamba woote. Kwa jinsi lowassa anavyopaa na kupaishwa na wana-ccm hapana ubishi kwamba kauli za nape dhidi ya lowassa zimedharauliwa na kumwagwa jalalani kama mchuzi wa mlenda wa juzi na wana-ccm; kwa mantiki hiyo, nape hakubaliki na huenda haheshimiki ndani ya wana-ccm.

Ushauri wangu. Nape ajiuzuru nafasi aliyonayo ama amwombe radhi mh. Lowassa na wana-magamba wote kwa kauli zake alizowahi zisema juu ya lowassa. Ama la, nape atakuwa gamba sugu analokufa nalo nyoka.
viongozi wa dini wameanza kukataa fedha zake za kifisad atahamishia kampen wapi?
 
Back
Top Bottom