Uteuzi wa Makonda kuwa Katibu wa NEC itikadi na uenezi: Utakiimarisha Chama kwa nje lakini unaweza kukisababishia ufa ndani. Nini kifanyike?

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Huu ndio mtazamo wangu juu ya uteuzi wa Makonda kama Katibu wa NEC wa itikadi na uenezi wa CCM ambao umefanywa leo na Halmashauri kuu ya CCM Taifa chini ya Mwenyekiti wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwanza ,naipongeza sana NEC kwa kufanya mabadiliko ya mara kwa mara yenye lengo la kukiimarisha chama kwa nafasi mbalimbali na kuondoa udhaifu ,kurekebisha , kufikia mashimo na kuziba nyufa. Na hapa ndio inapoonekana tofauti kubwa kati ya CCM na vyama vingine.

Pili, nina imani mabadiliko yote yana lengo la kutatua matatizo ya Sasa na ya baadae ya kisiasa ndani ya Chama na nchini kwa ujumla Kwa sababu NEC ndio chombo Cha juu chenye kutoa dira na muelekeo wa siasa za CCM kwa nchi yetu.

Kama nilivyokwisha kusema hapo awali na kugusia juu ya uteuzi wa Paul Makonda kama Katibu wa NEC wa itikadi na uenezi ni vyema tukapata wasaa wa kumjadili katika sura mbili, sura ya kukusaidia chama Kwa siasa za nje na ndani ya Chama.

Tukianza na upande wa kwanza, kusaidia kujenga Chama kwa nje. Makonda anatajwa kama mtu mwenye uwezo wa juu wa kupambana na Upinzani na kuwashinda. Kwa tafsiri ya haraka kazi ya kueneza sera na itikadi ya CCM kupitia Makonda haitakuwa ngumu na itafanikiwa kwa kiwango kisichotia shaka.

Upande wa pili wa kazi ya Makonda ndio wenye kuleta tafakuri pana zaidi na kuibia swali la Je, Makonda ni asset au liability?

Kwa Sasa ni mapena sana kuwa na jibu sahihi la swali lakini ukiniuliza nijibu Kwa mtazamo wangu nitasema Makonda anaweza kuwa ni liability kama asipofanikisha baadhi ya mambo, na baadhi ya hayo mambo ni:

Makonda ana historia ya uhusiano na viongozi wengine waandamizi wa Chama ambayo kidogo inatia shaka. Je, ni vipi wanaweza kushirikiana ili kujenga Chama ? Maana yake kama wasipoweza kukubaliana ina maana ni ufa Kwa chama tena unajengwa kutokea ndani.

Ni vipi Makonda atamtazama Katibu Mkuu wa Chama Ndg.Chongolo ambaye kimsingi Kwa Sasa ni bosi wake? Je, anamtazama kama bosi wake au atamtazama kama msaidizi wake wa zamani akiwa ni RC na Chongolo kipindi hiko akiwa ni DC?

Je, ni Kwa vipi wengine wamepokea uteuzi wake ndani ya Chama hususani wale wanaomuona Makonda kama adui na kikwazo kwao? Je, hayo hayataibua mgongano wa kimaslahi ?

Nina imani na Katibu mkuu sana na utendaji kazi bila shaka unavutia ndio maana makatibu wa NEC wa uenezi wamebadlishwa mara tatu lakini yeye Bado yupo.

Na nina imani Makonda atamtazama Chongolo kama mkuu wake na Kwa pamoja watashirikiana Kwa ujenzi wa Chama chama Mapinduzi.

Kama Makonda ataweza kuimarisha mahusiano na viongozi wengine na wanachama ndani ya Chama, atarekebisha makosa na kusimama vema katika nafasi yake basi ni suala la muda Makonda kutambuliwa kama Katibu wa NEC wa itikadi na uenezi Bora kabisa katika historia ya CCM.
 
Kafara la kukimbiza moto linavyoligharimu Taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uteuzi wa hovyo! CCM leo inaenezwa na Makonda!?
Taarifa ya Mike Pompeo haikukanushwa na hata Makonda hajajisafisha!
CCM chini ya Samia sasa inaendekeza kujuana bila kujali uwezo, uadilifu wala maarifa!
Sisi wengine yetu macho ila ivumayo haidumu!
Kwa mwendo wa Samia atagota muda si mrefu!
 
Makonda ndio alie sumbua wafanya biashara kwa kuwabambikiza kesi halafu makonda huyo huyo ndio atawafata wafanyambiashara wachangie kampeni za CCM. Hizi ni dharau kubwa sana
 
7922f88c-3569-43e2-a084-8981be45e440.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uteuzi wa hovyo! CCM leo inaenezwa na Makonda!?
Taarifa ya Mike Pompeo haikukanushwa na hata Makonda hajajisafisha!
CCM chini ya Samia sasa inaendekeza kujuana bila kujali uwezo, uadilifu wala maarifa!
Sisi wengine yetu macho ila ivumayo haidumu!
Kwa mwendo wa Samia atagota muda si mrefu!
Huna akili wewe..pompeo au Hilo zuio Lina faida au linazuia Nini kwa chaguzi zijazo.

Idiot
 
Back
Top Bottom