Lowassa aanza kuwachezea rafu CHADEMA, alazimisha atengewe nafasi 30 za Wabunge

Haha badala hii ingekua furaha kwao CCM nashangaa wanalia!!!

Kila anachofanya Lowassa wanalia mpaka wanasahau kufuli lao!!!!

Waliposema Rais hawezi toka kaskazini si walijiaminisha?? Sasa vilio vya nini??

Mnatufumbua macho sisi WA kusini!tumekuelewa
 
Ukome kutuandikia umbea, tunaamini katika mabadiliko. Liwalo naliwe hatutaki rangi ya mbolea ya mooo.
 
Haha badala hii ingekua furaha kwao CCM nashangaa wanalia!!!

Kila anachofanya Lowassa wanalia mpaka wanasahau kufuli lao!!!!

Waliposema Rais hawezi toka kaskazini si walijiaminisha?? Sasa vilio vya nini??

Kwa hiyo unaconclude Rais keshatoka kaskazini kwa nji hizo tayari? Weka maneno ya akiba mkuu wangu
 
Haha badala hii ingekua furaha kwao CCM nashangaa wanalia!!!

Kila anachofanya Lowassa wanalia mpaka wanasahau kufuli lao!!!!

Waliposema Rais hawezi toka kaskazini si walijiaminisha?? Sasa vilio vya nini??

Wewe endelea kuchekacheka huku mwenyekiti akiendelea kupiga dili kwenye biashara hii ovu ua wafuasi wa UKAWA kuchezewa shere na viongozi wenu,
mpaka EL anabwagwa october mwenyekiti atakua na club nyingine wewe ukiendelea na vicheko vyako.
 
Wadau,amani iwe kwenu.

Taarifa za uhakika kutoka Team Lowasa zinasema kuwa Waziri Mkuu aliyeshinikizwa kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond, Edward Lowasa ambaye pia ni mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA kupitia UKAWA ameanza kuwachezea rafu viongozi wa CHADEMA.

Taarifa hizo zinasema kuwa mwanasiasa huyo amewataka viongozi wa CHADEMA kutenga nafasi 30 za wabunge ambazo anakusudia kuwapa makada wake waliohama na anaoendelea kuwashawishi ili wahame CCM. Taarifa za chini ya kapeti zinasema kuwa Lowasa ameshaandaa baraza lake la Mawaziri na wabunge hao 30 ndio watakaotawala kwenye baraza hilo endapo atafanikiwa kushinda Urais.

Hata hivyo, baadhi ya wagombea ambao amewatengea nafasi wameshinda kwenye mchujo wa CCM na wamesema kuwa hawapo tayari kupoteza nafasi hizo na kumfuata Lowasa.

Mtoa habari hizi ambaye ni miongoni mwa wagombea waliopitishwa na CCM na ambaye yupo kwenye orodha hiyo ya Lowasa anasema kuwa yeye alikuwa anamuunga mkono Lowasa akiwa CCM na hayupo tayari kwenda huko. Anasema kuwa amekuwa akishawishiwa usiku na mchana ili ahamie CHADEMA lakini msimamo wake ni kwamba ataendelea kubaki CCM ambako ndiko kwenye mafanikio.

Miongoni mwa makada walioombewa nafasi hizo ni pamoja na Said Mkumba, Esther Bulaya, James Lembeli, Makongoro Mahanga, Nazir Karamagi nk. Taarifa zinasema kuwa ili kutekeleza agizo hilo la Lowasa, CHADEMA wanalazimika kufanya mazungumzo na vyama washirika wa UKAWA kwa vile baadhi ya majimbo yanayotakiwa na Lowasa yapo kwenye vyama hivyo.

Mathalan, Makongoro Mahanga atateuliwa kugombea jimbo la Ukonga ambalo lilipewa CUF ambapo Julius Mtatiro ndiye aliyetaka kupeperusha Bendera. Hata hivyo, taarifa zinaelezwa kuwa Mtatiro amekubali kuacha jimbo hilo baada ya kuhakikishiwa na Lowasa kuwa atamteua kuwa mbunge ndani ya nafasi kumi anazopewa Rais Kikatiba ikiwa atafanikiwa kushinda nafasi hiyo.

Hiki chama cha chadema kimeuzwa sioni wa kumdhibiti lowasa kama anachukua dola naliona kundi lake la mafisadi likitamalaki ktk utawala wake,
Hapo ndipo watakapoanza kulialia.
 
Mmeanza.nendene mkajadili anguko kuu la ccm.unasikia inavyoporomoka?nyumba hiyo yaungua ng'ang"ania tuu.utateketea!!!
 
Baada ya lowasa na team yake kuhamia cdm, sasa lowasa amelazimisha kupewa viti 50 vya ubunge. Habari za ndani zinasema hata kuchelewa kutoka kwa majina ya wagombea wa ukawa umesababishwa na mvutano huu mkubwa. Wanaotajwa kuwa vinganganizi wa nafasi hizi ni lau Masha ambaye hivi karibuni alifukuzwa pale immma advocates na fatma karume. Sasa ile kamba inaowaunganisha mbowe na lowasa itadumu? Chukua tahadhari wewe kijana kipofu usiyejua kuchambua mambo.
 
Ongea yanayokuhusu ya CHADEMA ya nn wakati yenu yanawashinda!
 
Kipofu ni wewe usiyejua herufi kubwa na ndogo.

Unaongoza na hisia za tumbo,ngoja maana ccm inaanguka ukose kula.
 
Baada ya lowasa na team yake kuhamia cdm, sasa lowasa amelazimisha kupewa viti 50 vya ubunge. Habari za ndani zinasema hata kuchelewa kutoka kwa majina ya wagombea wa ukawa umesababishwa na mvutano huu mkubwa. Wanaotajwa kuwa vinganganizi wa nafasi hizi ni lau Masha ambaye hivi karibuni alifukuzwa pale immma advocates na fatma karume. Sasa ile kamba inaowaunganisha mbowe na lowasa itadumu? Chukua tahadhari wewe kijana kipofu usiyejua kuchambua mambo.

Ma ccm hayajui hata propaganda.
Swissme
 
Back
Top Bottom