Live Star TV: John Mnyika na Job Ndugai

NGOWILE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
454
258
Wadau asubuhi hii John Mnyika na Job Ndugai watakuwa live kwenye kipindi cha watanzania tuongee asubuhi kinachorushwa live na kituo cha star tv.
Updates: Mtanange umeanza Job Ndugai Dar, Mnyika bado hajafika.

Updates: Mnyika kafika. Ndugai kapigwa maswali na Yvonna Kamuntu badala ya kuyajibu anaanza kupongeza star tv na kutoa historia badala ya kujibu maswali.

Updates: Ndugai na Mnyika wanakubaliana kuwa kanuni zina mapungufu mengi. Mnyika anaenda mbali zaidi anasema wamewahi kutoa mapendekezo ya kubadili kanuni lakini bado kimya. Anasema hata kanuni zilizopo hazifuatwi na kiti.

---------------------------------

Ndugai kaanza kufai kuwa kwanza kanuni ni za 2007 na yeye ndio alikuwa mwenyekiti na akiwa na kina Dr. Slaa, Mwakyembe, Kilindo nk na anadai yeye kama kiongozi kachaguliwa na wabunge hivyo anahitaji kuheshimika

Update; Job anaeleza kuhusu kanuni za bunge za 2007 ambazo bunge linazitumia sasa. Kanuni zilizopo hazikidhi mahitaji ya bunge la sasa

Mnyika; Kanuni zinahitaji kuboreshwa, ila pia kuna upungufu wa utekelezaji wa kanuni zilizopo.
! Kanuni zetu hazifatwi
! Kiti cha spika kinatakiwa kutoa maamuzi, maamuzi ya spika ni sehem ya kanuni.
! Malalamiko ya wabunge juu ya maswala ya kanuni hayashughulikiwi kwa wakati.

Job anakwambia alijua Lissu anadanganya lakini akamwacha tu sababu alikuwa anatafuta umaarufu mbele ya camera.it kiongozi mkubwa wa muhimili kama bunge unaacha watu waseme uongo kweli?. Haiingii akilini.

Update: Job anasema kinachofanyika bungeni ni usanii mtupu, na kwa, maoni yake ni kuwepo kwa kamera ndani ya bunge ndo maana wabunge wanafanya usanii... vielelezo ni kwamba katika kamati ndogondogo hawafanyi vurugu kwa vile kule hamna kamera.

Ndugai anasema Dhana ya demokrasia inakiukwa bungeni na wapinzani. Demokrasia manake wengi wape. Lakini chadema wanataka kila kitu wasikilizwe wao na inapotokea hawajasikilizwa wanaleta vurugu yaani wengi wameamua wao wanapinga.

Job Ndugai kasema wapinzani wanazani yeye ni mnyonge,Mnyika akasema kama umekili wewe kuwa sie tunazani we ni mnyonge basi una inferiority complex,Ndugai kapanic eti Mnyika ananidharau duh mimi ni kaka yake.Huyu mzee anamatatizo

Mnyika: Mh ndugai anakabiliwa na tatizo la Inferiority complex kutokana na mzlezo ya ndugai kuwa wabunge wa upinzani wamekuwa wakimwonea akikalia kiti yeye mbona hawafanyi wakati mwingine vile!!
Ndugai: Bwana mdogo uwe na heshima kwa wakubwa zako? Huwezi kunismbia mimi nina infireority complex! Siku zote wewe umekuwa huna lugha nzuri kwa wakubwa wako!

Mnyika uvumilivu wake ni mdogo bungeni anahitaji muda kujifunza katika bunge

Kimewaka, "Haniheshimu, mimi ni kaka yake, mimi ni mbunge kama yeye, hawaheshimu watu wa Kongwa" Ndungai analalamika baada ya kuambiwa ana inferiority complex.

Mnyika kabeba madesa ya kutosha kama evidence, Ndungai kaja mwenyewe mwenyewe tu na hoja ya vurugu kwa wapinzani.

Katika kipindi cha Tuongee asubuhi cha Star Tv kikibeba mada ya Vurugu bungeni, Naibu spika Job Ndugai amesema wabunge wa upinzani wanachokifanya ni usanii mbele ya kamera wawapo bungeni kwani majadiliano huanzia kwenye kamati ambako hukubaliana vuzuri!
Mnyika namwona anamtolea jicho meza moja!

Mtangazaji wa upande wa Dar amepwaya sana, wakati Ndugai akiongea Mnyika ananyamaza ila akipewa Mnyika nafasi Ndugai anamkatisha kuongea.

Hii inaonyesha wazi kuwa Ndugai anapenda sana Ubabe ndio maana anashindwa kuongoza Bunge. Halafu anadai kuwa eti huwa anajiona kwamba Wabunge wa Upinzani wanamuona Dhaifu.

Kama tu leo pale Star Tv Ndugai ameshindwa kuonyesha uvumilivu wa kumpa Mnyika nafasi ya kujibu hoja zake wakati yeye akipewa kuongea Mnyika ananyamaza,je unadhani inakuaje pale bungeni anapokua kakalia kiti?

Kwa mujibu wa Ndugai, ambaye amekiri kuwa "watu wanadhani yeye ni dhaifu kuliko wote...hivyo anawahakikishia kuwa yeye sio dhaifu..." (a case for inferiority complexity), kuna kanuni zake ambazo huzitumia na alirudia mara nyingi ktk mjadala:

1) Kanuni ya kufuata umri (kanuni ya kumlinganisha Agustine Mrema na F. Mbowe)
2) Kanuni ya kufuata uzoefu wa kuwepo bungeni/mjengoni (yeye ana miaka 15 wakati Mnyika ni mzoefu wa miaka 3)
3) Kanuni ya kuwa kiti cha spika ni untouchable unapproachable kwa Wapinzani (hasa CHADEMA)
4) Kanuni ya kuwa Kamati za Bunge ndio Bunge proper na kila kitu kiwe kinamalizika kule,
5) Kanuni ya kuwa ikiwa wewe si mjumbe wa Kamati husika basi usichangia wala kuzungumzia mambo ya hiyo Kamati
6) Kanuni ya kuwa CHADEMA (literary) wanafanya fujo kwa vile kuna kamera zenye kunasa na kurusha vikao vya bunge, na kwa busara za Ndugai mijadala isirushwe live ili kuondoa "fujo".

Mwisho, Ndugai ameshindwa kabisa kwa mara nyingine kujifunza na kukubali kuwa ana madhaifu mengi na upungufu mkubwa wa hekima na weledi. Kwa kifupi Ndugai ameonesha yeye ni Pinda na Kikwete in ONE!
 
nini kinaendele, manake wengine kisimbuzi utata, jf mambo yote.
 
Wana JF,Habari za asbh,kwa ss Ndugai na mnyika ndio wapo studio za star tv .na Ndugai anawasifia srar tv kuwa ndio kituo cha habari number moja Tz kwa maoni yake.
 
Update; Job anatoa maelezo ya jinsi spika/naibu spika anavyopatikana,... ANACHAGULIWA NA WABUNGE!
 
Dah! Kuna mtu alileta thread ya kumlalamikia huyu dada mapozi yake, nilijua ni chuki tu, leo nimeelewa alikuwa anamanisha nini, maana dada full kufumba fumba macho mbele ya TV, mara kafumbua nusu.

Ninakoma kumwangalia, kutoa sitoi, badala ya kufatilia mjadala mi namwangalia yeye tu, after all siasa zipo tu.
 
Ndugai kaanza kufai kuwa kwanza kanuni ni za 2007 na yeye ndio alikuwa mwenyekiti na akiwa na kina Dr. Slaa, Mwakyembe, Kilindo nk na anadai yeye kama kiongozi kachaguliwa na wabunge hivyo anahitaji kuheshimika
 
Update; Job anaeleza kuhusu kanuni za bunge za 2007 ambazo bunge linazitumia sasa. Kanuni zilizopo hazikidhi mahitaji ya bunge la sasa
 
Mnyika; Kanuni zinahitaji kuboreshwa, ila pia kuna upungufu wa utekelezaji wa kanuni zilizopo.
! Kanuni zetu hazifatwi
! Kiti cha spika kinatakiwa kutoa maamuzi, maamuzi ya spika ni sehem ya kanuni.
! Malalamiko ya wabunge juu ya maswala ya kanuni hayashughulikiwi kwa wakati.
 
Job; Nini kimetokea bungeni, kwa nini bunge limekuwa na vurugu kwa kipindi hiki... jibu, kuna wabunge wengi wapya ambao bado hawazijui, kanuni za bunge.
 
Back
Top Bottom