Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

Status
Not open for further replies.
hana tofauti na muuza magazeti, anaongea badala ya

-kuamua
-kukemea
-kupiga marufuku aina ya uchochezi
-hana hatua zozote kuhusu uchochezi, mauwaji na kuchinja

anapiga story kama muuza kahawa

Nakuunga kwa hili Rais katika hotuba yake, ananyesha kujikosha na sio kukemea hali ilivyo na uovu unayotokea, kuhusu kuhudhuria misiba kwani yeye ni lazima afanye hivyo kazi zake huwa anazipitia muda gani? Ndio maana Rais analaumiwa kwa kupewa taarifa zisizo sahihi. Kudhuru msiba wa shekhe au Mchungaji hii sio kazi ya Rais wa JMT, japo wengi wasio jua majukumu ya rais uona ni fahari. RAIS ANATAKIWA KUKEMEA UOVU BILA KUJALI ITIKADI YAKE. Uovu ni uovu, hauna ustaarabu.
 
Mkuu alianza na ziara ya raisi wa CHINA, akaja na JENGO kuanguka and then Ishu ya UDINI. Mimi nimeona kaongea vizuri sana kwenye hoja ya UDINI na hasa ya kuchinja. Amefanya analysis moja nzuri sana, kwamba hivi tukiruhusu kuwa kuwe na mabucha ya wakristo na waislamu itakuwaje kwenye Restaurant? Hotel? Mama/Baba Ntilie nk. Je itakuwaje kwenye Harusi, Misiba nk? Nadhani inapaswa kufikiri kwa kina kwenye hili. Moja ya vitu vinavyokwenda kuangamiza taifa letu si mfumo UKRISTO wala UISLAMU nchini. Hili la kuchinja ndio linakwenda kutugawa kabisa na kutumaliza.

Hoja ya ziara ya raisi wa CHINA ameshindwa kutueleza faida za maana sana tunazokwenda kuzipata, na ishu ya majengo namuomba akajipange sana, maana hakuna shaka kuna uzembe na kulea uzembe kwenye halmashauri zetu. Haiwezekani jengo linanyanyuka bila wahusika kufahamu.


Baada ya kuongea yote hayo hapo kwenye blue mkuu wangu amehitisha vipi? yaani what was his conclusion?

Je ameliacha hewani? amewaacha wananchi waamue nini hasa ...........
 
Invisible,

Kama inawezekana tuwekee hotuba ya rais tuisome.
 
Last edited by a moderator:
Suala la kuchinja wakristo tunakurupuka, Biblia iko wazi. Hakuna mahala popote inapotoa kanuni za kuchinja na nani achinje. Sheria inakataza kula kibudu, na damu. Vinginevyo ni kutaka kuendeleza vurugu na mabishano yasiyo na mchango chanya kwa jamii.
 
JK anashindwa kabisa ku balance udini alionao na anaouamini na kuwapa confidence jeshi lake la msaada lililo nyuma yake!!!ana hoja zisizo na mashiko,kukojolea quraan,mabucha nguruwe!!amesahau tu kusema biashara inadoda sana wakati wa mfungo!!
 
Inawezekana tatizo ni kubwa kuliko tunavyofikiria na kuliona, kama uongozi wa nchi haupo au umelele usingizi fofofo au pengine kuna policy zilizopandikizwa kitambo kidogo ambazo zimedumaza kila kitengo!...Pengine Leadership ndo ingekwamua huko kudumaa, Grrrrrr......Hivi kuna mtu capable presidential material aliebaki CCM baada ya kufariki J.K.Nyerere?...Akina majebele, Ritz na Utaifakwanza mwaweza kunisaidia hili swali ili niendelee kuchangia vema badala ya kuzungumzia matatizo yanayotokea...
 
Baada ya kuongea yote hayo hapo kwenye blue mkuu wangu amehitisha vipi? yaani what was his conclusion?

Je ameliacha hewani? amewaacha wananchi waamue nini hasa ...........

Yah!!! Nadhani hapo ndio tatizo, mimi nimedhani ndio lile tatizo wanalomlalamikia kuwa hana historia ya kufanya MAAMUZI MAGUMU. Ifike kipindi aseme nini ndio msimamo wa serikali, nakubaliana na wewe hili ndilo tatizo kubwa kwa JK.
 
Wakati muafaka, hongera rais hii hotuba ya leo ni bomba saanaaaaaa umewapa ukweli pande zote mbili hasa upande flani ambao unalisha waumini wao chuki dhidi yako, serikali na dini yako, umesema ukweli juu ya mauji ya buserere maana taarifa ilikuwa inatolewa za upande mmmoja tu, vrg za mbagala, znz nk BIG UP JK

Unaonyesha kuwa wewe ni shabiki wa mipasho, kama Rais akitoa mipasho na sio kukemea. Kumbuka huyu ni rais wa Watanzania wote, na nchi yetu haina dini, inasheria zake ambazo ndizo zinalenga kulinda haki ya kila raia bila kujali itikadi yoyote ile
 
kampeni zake 2010

unamjua vizuri mwasisi wa udini tanzania lakini kwa kuwa unampenda huwezi kumsema...huo mwaka ulioutaja ndio mara yake ya kwanza kuutaka urais na mapadre wenzake na wachungaji walitangaza wazi na kuhubiri madhabahuni waumini wao wamuunge mkono na kumpa kura..huu ndio ukweli mchungu.
 
Suala la kuchinja wakristo tunakurupuka, Biblia iko wazi. Hakuna mahala popote inapotoa kanuni za kuchinja na nani achinje. Sheria inakataza kula kibudu, na damu. Vinginevyo ni kutaka kuendeleza vurugu na mabishano yasiyo na mchango chanya kwa jamii.

Mkuu mimi ninachojua ni kuwa Wassira ndo alileta all these contradictions kwa kusema waislam wachinje kwa kunogeza na neno "IBADA" hapo ndipo wakristu waka react. Mbona toka kitambo wao ndo walikuwa wachinjaji wakubwa na hakukuwa na tatizo. Tatizo ni kuwa wakristu hawataki kuwa involved in ibada zao.
 
Hiki ndo kipimo cha urais wake kwanini hakemei mashehe wake wanaohujuma nchi yetu. Watu kama shehe ilunga dvd zilishazagazwa muda ktk misikiti kuhimiza wachukue hatua za kutetea jihad . Kimsingi suala la buseresere lina uhusiano mkubwa ambalo analiita ni la hapo kijijini limejengwa na hotuba mbaya za shehe ilunga hasan kapunga na ndo maana walimuua mchungaji kutokana na hotuba yake ya fitna dhidi ya anaowaita makhafiri. Hivi kikwete anamdanganya nani. Eti kasomewa itikafu. Sasa tunakuambia wakristo wanakuombea ndo maana itikafu zote tatu zimebaunsi labda kama sio itikafu . Kama kweli itikafu ndo hizo mtu jua halizama umeshaondoka. Washukuru wachungaji waliozuia maasi ya itikafu vinginevyo unekuwa ulishazikwa muda. Heshimu haki za watu
 
Mimi hapa nadhani issue kubwa ilikuwa udini na ambalo ameendekea "kusihi" tusikubali kugawanywa na watu tusiowajua ajenda zao.

Mi sijakubaliana naye kuhusu vyombo vyabusalama kwamba pale vinaposhindwa ku act timely ni uzembe wa mtu na sio sera ya serikalo..then what do you do? Kuwaacha tu waendelee na uzembe huku mhemko wa udini ukizidi?

Some one must act swiftly....and stop this nonsense.
 
Wakati muafaka, hongera rais hii hotuba ya leo ni bomba saanaaaaaa umewapa ukweli pande zote mbili hasa upande flani ambao unalisha waumini wao chuki dhidi yako, serikali na dini yako, umesema ukweli juu ya mauji ya buserere maana taarifa ilikuwa inatolewa za upande mmmoja tu, vrg za mbagala, znz nk BIG UP JK

Kama Rais wa URT anatakiwa aende kwenye chanzo na mizizi ya tatizo na si kulalama kama anasoma taarifa ya magazetini kama akina Yahya Mohamed...Rais hatakiwi kuwa shallow minded! anatakiwa aonyeshe Leadership!...
 
Nilitarajia kama rais mwenye maamuzi ya mwisho pamoja na maelezo ya utangulizi kwa kila jambo angehitisha namna hii.

1. Tatizo la kuchinja kuanzia leo uchinjaji ni ........... na atakaye kwenda kinyume na hivyo ata.......

2. Tatizo la uchochezi hasa wa kidin kuanzia leo ..........atakayepatika anahubili kwa misingi ya ........ achukuliwe hatua .....atakaekamatwa na kanda, dvd, cd, vcd nk za uchochezi mara moja a.........atakayebainika kutengeza na kusabaza vitu hivi mara moja ......

3. Kuhusu uchomaji wa makanisa kuanzia leo mkowa au eneo uhalifu huu ukitokea ndani ya muda flani wahalifu wawe wamepatikana bila hivyo mkuu wa mkowa, Rpc na afisa upelelezi mkowa waachie ngazi mara moja kwa uzembe.

4. tatizo la kushuka kwa elimu pamoja na ............ mwisho wahusika wajitathimi kama wanafaa kuendelea kubakia wizarani .......maana taifa lolote linasimama kupitia elimu.

5. Kuhusu vyombo vya habari na wamiliki wake...........



Cha ajabu kikwete ameporomoa story kama muuza kahawa asiye na maamuzi wala mamlaka ilimradi anawaburudisha wateja wake kahawa yake iendelee kunyweka.

Nasikitika upuuzi wa uchochezi, upuuzi wa kogombea kuchinja, nk vitaendelea maadamu mwenye nyumba bado amelala fofofo na hana cha kumua na hatua za kudhibiti ujinga huu.

Mfano leo hakuna kuchinja mfugo mtu yeyote mpaka pale atakapo patikana mchinjaji. Kwa hiyo leo Tunduma(mbeya) nyama ni adimu
 
Adolay,

Hii nchi inafuata utawala wa sheria. Rais hana mamlaka hayo ya kuwa hakimu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom