Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

Status
Not open for further replies.
Suala la kuchinja wakristo tunakurupuka, Biblia iko wazi. Hakuna mahala popote inapotoa kanuni za kuchinja na nani achinje. Sheria inakataza kula kibudu, na damu. Vinginevyo ni kutaka kuendeleza vurugu na mabishano yasiyo na mchango chanya kwa jamii.
Wame kuelewa mkuu. Tatizo wengi wa Wacristo hawaijui dini yao nini inaamrisha na kipi ina kikataza. Ndio maana usishangae mchungaji kalewa viroba anawaambia waumini wake kuwa waislamu wana taka kulipua makanisa siku ya mkesha wa pasaka.
 
Wame kuelewa mkuu. Tatizo wengi wa Wacristo hawaijui dini yao nini inaamrisha na kipi ina kikataza. Ndio maana usishangae mchungaji kalewa viroba anawaambia waumini wake kuwa waislamu wana taka kulipua makanisa siku ya mkesha wa pasaka.

Kwan ustaadhi Ilunga aliwapa maelekezo gani? Au unajisahaulisha alichofanya makame huko zanzibar kwa padri mushi!
 
Msisitizo hapa ni uleule Wacristo muendelee kula nyama iliyo chinjwa na Waislamu.


Nyie ndio mnafanya Rais aendelee kubezwa na kudharauliwa. Kikwete hajasema, hajahitimisha wewe unamuwekea maneno mdomoni. unadhani yeye haijui katiba?

Juu yako kuchangia kishabiki au ukweli wa hotoba ya kikwete. ukiingiza ushabiki ukweli hutauona kamwe na kulifanya

janvi/mkeka kupoteza weledi kwa michango dhaifu.
 
MHE Rais wa Jamhuri ya muungano ameamua kutoa dukuduku lake ndani ya nafsi yake, kama ilivyo kawaida yake kusoma taarifa ya mwezi kwa wananchi wake wapendwa wa TZ kwa kutumia screen kubwa ambayo huwa iko mbele yake yenye kuonesha hotuba anayoisoma hakufanya hivyo mwezi huu ameamua kutoa dukuduku lililo ndani ya moyo wake,angalizo kwa viongozi wa dini,haya ni mawazo yangu, MAASKOFU NA MASHEIKH KUWENI SANA MAKINI NYIE NDIO MTKAOTUMIKA KAMA INITIATORS WA VURUGU NDANI YA NCHI,PIA WALE MASHEIKH WAJINGA WASIOPENDA SHULE WALIOMSOMEA ITKAF JK WALAANIWE WAO WENYEWE MPAKA KIZAZI CHA NNE.
 
Wakristo wameonesha uvumilivu mkubwa sana muda mrefu ndo maana wameamua kutoa tamko. Kuna mambo mengi ambayo anataka kuidhihirishia dunia kuwa yeye ni makini kufuatilia masuala yanayondelea. Ananikera sana anapowahusisha wakristo na vurugu zinazofanywa na waislamu dhidi ya wakristo.aseme ni wapi wakristo wamechoma msikiti kwa jambo lolote? Ukristo hauna sera ya malipizo. Kwahiyo rais tutake radhi . Suala la kukojolea quruan for god's sake sidhani kama lina uzito anaotaka kulipa. Unaambiwa watoto walikuwa wanabishana mmoja anatishia mwenzake kuwa utageuka nyoka ukikamata quruan mtoto wa pili akawa inquistive kama kweli anachoambiwa ni cha kweli akaamua kukojolea ili aone muujiza huo na akahakiki hakuna lolote. Kitendo alichokifanya hakikuwa cha kiungwana hata kidogo more or less ulikuwa ni utoto na ukosefu wa uchaji wa kuheshimu dini nyingine, lakini ummat wa dini ukahamaki wakti serkali inachukua hatua. Wakachoma makanisa na kuiba vitu kanisani sijui hili la kuiba vitu nalo ni agizo la dini ama vipi. Normally christian are so rational on ahandling of matter while asking their god on what next to do. We would like our counterpart to copy this merit in theri approach to solving problems

unaonekana ni mwerevu lakini unakosa kitu kimoja tu, neutrality and fairness, uko biased na unaegemea upande mmoja.. Ndio mana unaona mkosaji muislam tuu na mkristo ni malaika.....penye moja sema moja na penye tatu sema tatu.
 
Tufani limetikisa Mfumo Kristo povu zinawatoka mlozoea kupeleka Vimemo vya uteuzi Ikulu na kudandia misafara ya viongoz nchi za nje!

Amka wewe kumeshakucha acha kuota asubuhi asubuhi. Yaan wewe na umri wako unakubali kushikiwa akili na Hasan ILunga? Mwenzio sasa hivi anatibiwa na madaktari wakristo India katuliza vitenesi vyake shobo yote chali! Kama vipi angeenda saudi arabia kutibiwa
 
wakristo hawakurupuki na wala wao hawakuwa na shida ya kuchinja miaka yote ni pale tu walipofumbuliwa macho na Wasira kuwa waislamu kuchinja ni ibada,na wakristo kwa imani yao hawawezi kushiriki ibada ya miungu wengine.
kajifunze maana ya Neno Ibada kwa Muislam, Kila jambo jema ni Ibada hata mie nipo hapa kutekeleza Ibada ya kukuelimisha japo hutaelimika, Ibada sio kuombea mapepo na kukusanya sadaka za maskini pekee. Waambieni watoto wenu wazibe masikio akiingia mwalim mwislam ili wasimskie maana hata kufundisha ni Ibada kubwa kwa Muislam, hata Dereva muislam anawasha gari kwa Bismillah so mkifika kituo cha basi msipande kabla ya kujua dini ya dereva!
 
wakristo hawakurupuki na wala wao hawakuwa na shida ya kuchinja miaka yote ni pale tu walipofumbuliwa macho na Wasira kuwa waislamu kuchinja ni ibada,na wakristo kwa imani yao hawawezi kushiriki ibada ya miungu wengine.

Naendelea kutafuta andiko la Mtume Paulo akiwaandikia Wakorintho kuhusu kula nyama iliyotolewa kwa mizimu...alisema.." Kama una imani kubwa, na ukala nyama ambayo imetolewa kwa mizimu basi usihukumiwe kwa hilo, na akasema wale wenye imani ndogo, wanaokuwa na shaka na nyama zinazotolewa kwa mizimu nao wasihukumiwe kwa dhamira yao. Nikipata sura na mstari nitaweka hapa JF. Nachotaka kusema, hivi hao waislamu wakifanya ibada baada ya kuchinja uwa wanaifanyaje ile nyama? Maana kama wakisema "awakbari" au kugeukia Makka sijui ina madhara gani kwa mlaji? Na je, wakristo tunafanya mangapi machafu ambayo yanakwenda kinyume na ibada zetu? Ndugu zangu wakristo, tusidanganyike twendeni tusome neno, tuje hapa tubishane kwa neno. Maana Paulo anaonyesha kuwa wakati wa wakorintho kulikuwa na hoja kama hii ya leo, na yeye rulling yake ilikuwa "KAMA MTU ANA IMANI KUBWA AKAAMUA KULA NYAMA ILIYOKUWA INATOLEWA KWA MIZIMU WAKATI HUO AACHWE ALE, MAANA YEYE HANA SHIDA NA NYAMA HIYO, LAKINI KAMA MTU ANA IMANI NDOGO NA MASHAKA MENGI, PIA ASILAZIMISHWE KULA NYAMA ILIYOTOLEWA KWA MIZIMU"
 
Siamini anaweza kutoa mfano huu kwamba wakristu wamekojolea kuraani, haki ya Mungu hatuna Rais,
Wacristo mikikalia dhana kuwa JK yupo kuli pigania kanisa kama watangulizi wake, mume umia. Yeye kachoshwa na tabia ya kanisa kuwa ndio kila kitu ndani ya nchi hii. Nawashauri muendelee kumchukia, ila sidhani kama atafanya kazi/kutawala kwa matakwa yenu.
 
Rais wa mipasho, misemo, kutalii nk

Tatizo la kutoa maamuzi hana nikama bendera upepo unakoelekea huko huko.

Lakini kwa dhati kabisa anajuwa anachokifanya na kwasababu anajiona mjanja kwa kuweka mambo yake sirini nakuongoza kwa mizengwe nchi imemshinda na muda si mrefu atajutia usanii wake.

waswahili walisema Samaki mkunje angali mbichi - Matatizo hutatulia kwa urahisi na kwa haraka mapema kabla hajakomaa

1. Amezembea suala la ucchomaji makanisa limewakupusha wakristo nasasa wanatishia kuiasi serikali rejea tamko la maasikofu. Yeye anadhani wanafanya mchezo.

2. Amezembea suala la kuchinja ambalo lilikuwa la kipuuzi na dogo kabisa na bado anaendekeza hadithi watanzania wanapalaganyika.

3. Polis wanauwa raia anachagua aongelee misiba gani kwa maslahi ya chama (cc) na mingine mfano wa Mwangosi hapana hili ni tatizo kubwa kwa raia.

Tusubiri mwisho wa tamthilia hii nani atatoka.
 
Amka wewe kumeshakucha acha kuota asubuhi asubuhi. Yaan wewe na umri wako unakubali kushikiwa akili na Hasan ILunga? Mwenzio sasa hivi anatibiwa na madaktari wakristo India katuliza vitenesi vyake shobo yote chali! Kama vipi angeenda saudi arabia kutibiwa
mbona hushangai Pengo na genge lake la kina slaa kuongozwa na Rais Mwislam!
 
wakristo hawakurupuki na wala wao hawakuwa na shida ya kuchinja miaka yote ni pale tu walipofumbuliwa macho na Wasira kuwa waislamu kuchinja ni ibada,na wakristo kwa imani yao hawawezi kushiriki ibada ya miungu wengine.
We, muongo. Wacristo walianza kudai kuchinja kabla ya Wassira kwenda kutoa kauli hiyo. Uwe mstaarabu na mwenye kumbukumbu pindi uchangiapo jambo lenye rejea. Kumbuka hapa sio kanisani kila asemalo Padri ni ndio tu hakuna aseme sio wala kuhoji.
 
Kama rais hajasema nani anastahili kuchinja kwenye hotuba yake basi ameonyesha dharau kubwa kwa maaskofu waliomtaka afanye hinyo ili kulinda katiba aliyoapa kuilinda. Ninaomba Rais ajue kuwa ile sauti ya maaskofu si sauti ya wao kama binadamu ila nia sauti ya Mungu mwenyewe aliye hai. Majanga yanayoipata tanzania si bure bali ni adhabu tuliyopewa kutokana na kumkana Mungu wa israel na kufuata/kutenda mambo yasiyo haki. Ninaomba nimwambie Rais wangu mpendwa kutoa kauli hiyo si hiari yake bali nilazima afanye hivyo kwa mamlaka tuliyompa na kama ameshindwa kufanya hivyo basi ajue kuwa Mungu wa Mussa, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Yusufu atainuka na kutoa pigo ambalo siyo tu litahusu watanzania wasio na hatia bali hata yeye binafsi/familia yake itahusika pia. Kukwepa pigo hilo lisimpate anatakiwa afanye kitu kimoja tu, kujibu hoja zote alizoambiwa na maaskofu azijibu. Binafsi nakutakia Rais wangu utekelezaji mwema wa majukumu uliyopewa juu ya nchi hii lakini usijisahau kuwa na wewe ni mwanadamu kama mimi na utaonja mauti kama mimi.


sauti ya maaskofu ni sauti ya mungu na unga wanaouza ni unga wa......
[siku chadema ikishika nchi najinyonga]
 
Utaanza kulaaniwa wewe kwanza kwa kutofuatilia mambo kwa kina nakuja na matusi ya nguoni kwa viongozi wa dini za watu, nadhani hivyo ndio mnavyofundishwa huko kanisani kwenu. Naanza kuwa na wasiwasi na ELIMU yako naomba eweke CV yako kwa sababu mtu aliyeelimika hawezi kuzungumza maneno ya kashfa kiasi hicho eti walaaniwe mpaka kizazi cha nne, Fikiria kabla ya kuzunguza.
 
mbona hushangai Pengo na genge lake la kina slaa kuongozwa na Rais Mwislam!

Umenchekesha sana! Raisi gani huyo unayesema muislam? Huyu tunayekula naye bia ambaye kitimoto anagonga kama hana akili nzuri? Au uislam ni jina? Ihusishe akili yako kidogo tu acha kuendeshwa na GUBU kama mke mwenza ambaye ni tasa! Ulishamsikia pengo anawaambia watu wapige watu risasi na AK47?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom