Huu ni mwaka wangu wa 16 kufunga mwezi wa Ramadhani China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
1710462679108.png


1710462688762.png

Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, serikali nyingi zisizo za Magharibi zilianza kuamka na kujua kwamba demokrasia na haki za binadamu za dhana zilizotetewa na nchi za Magharibi zinalenga kuzipendelea nchi hizo tu na kupuuza maslahi ya mataifa mengine mengi ya Kusini, na kwamba dhana hizi zinaonekana katika vitendo mbalimbali vya uingiliaji kati vinavyofanywa na nchi za magharibi ambazo zinajinadi kwamba wao ndio mabingwa wa kutekeleza demokrasia na haki za binadamu.

Nchi hizi za magharibi mara nyingi zimekuwa zikinyooshea vidole nchi nyingine kwamba hawafuati demokrasia ama kukiuka haki za binadamu kwa kuwa tu hazitendi kama vile wanavyotaka wao. Mhanga mkubwa wa shutuma hizi ni China. China ikiwa ni nchi kubwa ambayo ni kama kioo kwa nchi nyingine duniani bila shaka inatekeleza haki za binadamu na demokrasia kamili.

Wahenga wanasema “Usisikie ya kuambiwa subiri ujionee mwenyewe”. Mimi nikiwa nimeishi nchini China kwa takriban miaka 16, nimejionea kinaga ubaga namna China inavyoweka sera zake za kuhakikisha watu wote wanapatiwa haki za msingi. Wanaolalamika kwamba China inakiuka haki za binadamu mara nyingi huwa wanatolea mfano wa mikoa ya makabila madogo kama vile Xinjiang ambako kuna Waislamu wengi.

Nakumbuka mwaka 2021, nilipotembelea mkoa huu wa Xinjiang nilipata fursa ya kujionea mwenyewe Waislamu wanavyoshiriki kwenye ibada mbalimbali za dini kwa uhuru, na hata kupata nafasi ya kuongea na baadhi ya mashekhe na maimamu wa misikiti ya mji huo. Muhtaram Sherif ni Imamu wa Msikiti wa Yanghang, ambao ni mkubwa sana wilayani Urumqi. Anasema wakati wa Ramadhan, Waislamu wa huko wanatekeleza ibada ya kufunga na kusali kama wanavyotekeleza waislamu wa maeneo mengine duniani. Hakuna kizuizi chochote kinachowafanya wasitekeleze ibada, ilimradi tu hawavunji sheria.

Ni sahihi kabisa anavyosema Imamu Muhtaram Sherif. Katika miaka yote 16 ambayo nimebahatika kufunga mwezi wa Ramadhani hapa China, sijawahi kushuhudia kizuizi chochote kilichowekwa na serikali dhidi ya waumini. Kama Waislamu wa Xinjiang wangekuwa wananyimwa haki zao za msingi ikiwemo ya kuabudu, je mbona katika mkoa huo kuna misikiti mingi ipatayo 20,000? Na je mbona katika kipindi hiki cha Ramadhani huwa wanaongeza muda wa kufanya ibada kutoka dakika 10 hadi saa mbili. Kwa maana hiyo ni dhahiri kwamba shutuma hizi hazina msingi wowote ule, na kwa wale wote wanaoifahamu China na Wachina bila shaka wanaelewa kuwa hizi ni propaganda tu za Magharibi.

Ikija kwenye suala la demokrasia, China pia ina njia yake ya kuendesha nchi kidemokrasia ambayo kwa maoni yangu nikiwa mgeni niliyeishi muda mrefu China, naona ni nzuri zaidi labda hata kushinda ile tuliyoizoea katika nchi zetu, ambayo asili yake ni nchi za magharibi. Demokrasia ya China ya mchakato kamili wa watu sio tu inakuja na seti kamili ya taasisi na taratibu zake, bali pia ina ushiriki kamili wa watu, ni pana zaidi, ni ya kweli na yenye ufanisi zaidi. Wakati akihutubia mkutano mkuu wa kazi Oktoba mwaka 2021, rais Xi Jinping wa China alisema demokrasia si pambo tu la kuwekwa ndani, bali itumike kushughulikia masuala ambayo wananchi wanayajali sana.

“Kitu muhimu kwenye demokrasia ya nchi ni kuona kwamba wananchi wanaendesha nchi, na pia inategemea kama wananchi wana haki ya kupiga kura na muhimu zaidi, iwapo wananchi wana haki ya kushiriki kwa mapana zaidi.” Anaeleza Rais Xi

Ni muhimu kuwa na demokrasia inayohusisha watu wote na sio inayohusisha serikali tu. Ni hivi majuzi tu Mikutano Miwili ya China yaani Bunge la Umma na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa ilimalizika hapa Beijing. Katika Mikutano hii demokrasia ilijidhihirisha wazi katika mchakato mzima, hata wageni waliopata fursa ya kushiriki walisifu sana kwa kuona bunge linahusisha wawakilishi wa majimbo na sekta mbalimbali, hata wawakilishi wa makabila madogo na hata wasio wa chama cha CPC pia hawakusahauliwa. Hii ndio maana ya demokrasia ya mchakato kamili wa watu.

Mwandishi wa habari kutoka Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Abubakar Harith, alihudhuria vikao vya bunge na kupata fursa ya kumuuliza swali Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, kwenye mkutano na wanahabari. Yeye anaona kuwa bunge la China ni lenye ufanisi zaidi likilinganishwa na mabunge mengine duniani kwasababu ni jumuishi zaidi na halina vikao vingi.

“Katika mfumo wa China mambo yote yanaratibiwa na kumalizwa majimboni au katika maeneo ya kazi. Na linapofika bunge kukutana kawaida hakuna orodha kubwa ya vikao. Huwa inasomwa ripoti ambayo inaeleza yale yaliyopatikana katika mwaka uliopita, vilevile na kutazama matarajio katika mwaka unaofuata. Hii ni tofauti na mabunge yetu ambapo vikao vinakuwa vingi, majadiliano yanakuwa marefu” anasema Abubakar Harith

Lengo la kufanya vikao vifupi vya bunge, moja ni kupunguza muda wa mijadala na kutoa nafasi ya kuwa na muda mrefu zaidi wa kufanya kazi na pili ni kupunguza gharama za matumizi ya uendeshaji wa vikao. Kwa maana hiyo cha muhimu zaidi demokrasia inapaswa kutekelezwa kulingana na nchi yenyewe na sio kufuata uendeshaji wa demokrasia wa nchi fulani ambazo ndio zinajiona kubwa zaidi.
 
Shida ya Afrika ni roho nyeusi na umimi vinatusumbua, nazani mshaona watu wanajipigia chapuo walipwe kiinua mgongo kwa ajili yawenza wao kustafu.
 
Labda! sasa kama wanapewa uhuru nani analalamika kwa hao wanaolalamika kuhusu kubaguliwa na kunyimwa haki?
 
tukiancha nchi za magharibi je unadhani mashariki ya kati kuna huo uhuru wa kuabudu kama china ?
 
Screenshot_20240315-050654.png
miongoni mwa sababu zilizopelekea Mesut Özil kuondoka Arsenal ni yeye kuwatetea waislamu wa uighurs ambao serikali ya china imewaweka kwenye makambi maalumu kama wafungwa na watoto shuleni wanafunzwa kuikana imani yao halafu mkuu unaleta propaganda katika nchi ambayo waislamu wanapitia magamu waziwazi basi ni china, burma nahis na india ila wao wao wako busy tu marekani ambapo wanauhuru hata wakununua makanisa na kuyafanya misikiti ila china wanavunja misikiti wanajenga vyoo vya umma mkuu yote hayo huyajui 😁
 
According to Chat Gpt:

Serikali ya China imeweka sera kali sana kuhusu uhuru wa dini, na mara nyingi imekuwa ikikandamiza haki za kidini kwa Waislamu na wafuasi wa dini nyingine nchini. Kwa Waislamu, serikali ya China imeweka vizuizi vikali kuhusu ibada na mila zao za kidini, ikiwa ni pamoja na kutowaruhusu kufuata ibada zao kwa uhuru na kwa kiasi wanachopenda.

Hasa katika maeneo ya Xinjiang, ambayo ni makazi ya Waislamu wa Uighur, serikali ya China imekuwa ikichukua hatua kali za kudhibiti ibada za Kiislamu na kuzuia mazoea ya kidini ya Waislamu hao. Wananchi wa Uighur wamekuwa wakikabiliwa na mateso, kufungwa kwa lazima, kulazimishwa kuvunja mila zao za kidini, na hata kufanyiwa vitendo vya mateso na ukandamizaji mkali kutoka serikali.

Kwa ujumla, hali ya uhuru wa kidini nchini China, hasa kwa Waislamu, imekuwa ya wasiwasi na inakiuka viwango vya haki za binadamu. Serikali ya China inaonekana kuona dini kama tishio kwa utawala wao na mara nyingi huchukua hatua za ukandamizaji dhidi ya dini zote, ikiwa ni pamoja na Uislamu.
 
Back
Top Bottom