Lissu: Makampuni yaliyotunyonya tangu 90's hayapo kwenye sheria ya madini

Limepita, una uhakika? Unaona Acacia wanakokwenda?

Update on Developments in Tanzania
04 Jul 2017

Acacia announces that today Notices of Arbitration were served in Tanzania on behalf of Bulyanhulu Gold Mine Limited (“BGML”), the owner of the Bulyanhulu mine, and Pangea Minerals Limited (“PML”), the owner of the Buzwagi mine. These Notices refer the current disputes between the Government of Tanzania and each of BGML and PML to arbitration. This is in accordance with the dispute resolution processes agreed by the Government of Tanzania in their Mineral Development Agreements with BGML and PML.

The serving of the Notices at this time is necessary to protect the Company, but, this notwithstanding, Acacia remains of the view that a negotiated resolution is the preferable outcome to the current disputes and the Company will continue to work to achieve this.

The Government of Tanzania has informed Barrick Gold Corporation (“Barrick”) that at this stage it wishes to continue their dialogue, and therefore Acacia will not participate directly in these discussions when they commence. Any potential resolution that might be identified as a result of such discussions will be subject to approval by Acacia, and the Company will work with Barrick as necessary to support such discussions.

All three of our mines are continuing to operate in line with previous announcements, and we will provide an update on developments, including the proposed mining legislation, once the legislative process is complete.
Acacia in this issue only bears the risk of tainted brand, whereas Barrick Gold bears the real risk of 73.9% shares. To that end, other than facts in the information herein provided, this Acacia's statement is relatively ineffectual.
 
Acacia wangetushataki kama hiyo sheria mpya ingetumika kwao. Ndiyo maana TL alisema toka mwanzo ili kuwashughulikia hawa waliopo ni lazima tujiondoe MIGA and other bilateral trade agreements na ndiyo maana ukiosoma hapo kina sehemu anasema jpm kashindwa kama alivyotabiri. Hii ndiyo wazungu husema means justify ends, TL aliona means na intention za jpm akaona lazima tutaangukia kushtakiwa, JPM kukwepa hilo kasema hawa sheria haiwagusi. Kijana fungua akili yako
Mnahamisha magoli eeeh. Sasa hivi hiyo MIGA ni kwamba TL alikuwa nabii alijua kuwa JPM ataganya mabadiliko ya sheria za maliasili, kweli mahaba niue nyie na lissu!!
 
lissu haeleweki yupo upande gani kutwa nzima anaongea na CEO wa acacia alafu anajifanya kuishauri serikali,lissu ni kibaraka wa acacia!sioni mashiko yoyote kwenye andiko lake,
Aliwaambia muweke recording ya hayo maongezi. Acheni kuropoka tu
 
Haya ulitakiwa kuyaeleza bungeni kabla hamjapitisha. ..kuyasema baada ya kupitisha ni sawa na kujigeuza chombo cha habari tu..Ulitakiwa KUPINGA KWA NGUVU ZOTE HUKOHUKO Bnafsi sihitaji taarifa ya mlichokipitisha na wenzio labda unambie umehusikaje kuzuia msipitishe FULLSTOP
 
Huyu Bwana ni mwongo. Kama ni mkweli angezungumza haya bungeni badala ya kupiga/kuendesha kampeini binafsi kwenye mitandao ya kijamii. Kwa nini asitumie fursa ya jukwaa rasmi la kujadili sera za serikali (Bunge) kuwasilisha hoja (kama ni hoja kweli) kushawishi wabunge wenzake ili wabadilishe maudhui ya muswada husika?


Lakini tafsiri ya maneno ya kejeli na kutukana yanayosheheni kwenye hoja ya Lissu ni dhahiri kuwa amekata tamaa, sasa anazungumza chochote kinachotokea kinywani mwake.


Kwa mantiki ya kawaida, na hata kwa mtu asiyekuwa mwanasheria lakini amesoma na kuelewa miswada husika anajua kuwa mara baada ya kupitishwa jana na kisha kusainiwa na Rais [hata Prof. Kabudi jana alithibitisha hivyo mara baada ya kupitisha miswada ya jana], Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohusu Maliasili za Nchi, 2017 (someni vifungu PART III kifungu cha 6 na 7] ikisomwa kwa pamoja na Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali, 2017, ndio itakayotumika ku-review mikataba ili kui-harmonize na sheria hizi mahsusi kwa ajili ya kurekebisha makosa yaliyofanyika huko nyuma katika ulinzi na udhibiti wa rasilimali za nchi.


Pengine kwa faida ya wasomaji na kuthibitisha uongo wa Tundu Lissu, hebu tusome kwa pamoja kifungu cha 10 cha Muswada wa kutungwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali – Sheria ya Madini, Sheria ya Petroli, Sheria ya Kodi ya Mapato, Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, na Sheria ya Bima, 2017 unaojadiliwa Bungeni leo na ambao Lissu ana uzungumzia;

"The principal Act (hapa ni sheria ya madini inayorekebishwa) is amended by repealing sections 11 and 12 and substituting for them the following, [review and renegotiation of development agreements] '11. Notwithstanding the provisions of this Act and any other written law, all development agreements concluded prior to the coming into force of this section shall, subject to the provisions of the Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Renegotiation of Unconscionable Terms) Act 2017, remain in force'"


Tafsiri ya kifungu hiki ni kuwa mikataba ya madini ambayo taifa liliingia huko nyuma na ambayo inaendelea kuishi hadi sasa imewekewa sharti la kufanyiwa marekebisho ili kuendana na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohusu Maliasili za Nchi, 2017 iliyopitishwa bungeni jana. Soma PART III kifungu cha 6 na 7 katika sheria hiyo.


Ni bahati mbaya kuona kuwa rafiki yangu Lissu ameamua kuji-intoxicate, na pengine bila kujali hadhi yake kitaaluma.
We jamaa unaelewa kizungu?
 
Makampuni ya madini kama Barrick na mtoto wao Acacia walishaingia mkataba na Tanzania.Ili Tanzania iweze kubadili mikataba iliyosainiwa huko nyuma ni lazima kwanza ubadili baadhi ya vifungu vya sheria inayosimamia sekta ya madini. Hiki ndicho kitachofuata baada ya muswada kuwa sheria, kwamba Tanzania itaanza majadiliano na makampuni ya madini kuhusu TERMS OF BUSINESS. Huwezi kufanya mazungumzo - negotiate new terms of business - kama sheria zako hazikupigi wigo wa kufanya hivyo.

Wakati mwingine inatia kinyaa kuona arrogance ya Lissu so publicly displayed. Ni kwanini Lissu anakosa mipaka ya kudharau Watanzania (kwa ujumla wao) kwa kujiona kuwa yeye ndiye anayelewa mambo zaidi ya wengine.

Kama kweli alikuwa mwerevu, ni kwanini tangu ashike usukani CHADEMA, kama Chama kimekosa mwelekeo? Zitto pamoja na mapungufu yake bado ameweza kuongoza ADC kuchambua miswada na kuwasilisha michango yao. CHADEMA na huyo 'learned brother' wao wamebakia kubuni rangi ya mavazi ya kuvaa bungeni! Very unfortunate. Hata kwenye hili?
Ukichagua kufumba macho hasara ni yako mwenyewe. Wenye kuona hatuambiwi tazama.
 
Lisu mnafiki kilichomzuia kutoa maoni take bungeni no nini au alizuiwa?
Kama alijua kuna tatizo halafu aknyamaza ili wapitishe hiyo sheria yenye makosa nani mzalendo? Na alinyamaza kwa maslahi ya nani?
Ule usemi wa kuna watu wanapinga juhudi hizi kwa sababu wamehongwa ninaanza kuuamini.
Lisu alinyamaza ili wafanye makosa spate ulaji si ajabu akawa miongoni mwa jopo la mawakili wa utetezi upande wa acacia.
I hate Lisu.
 
Nilitegemea Tundu Lisu kama Rais wa chama cha wanasheria angeongea tofauti na alivyofanya, amejikita ku-criticize kama kawaida yake. Waziri wa sharia alisema kuwa sharia mpya huanza kuwa applied pale inapotungwa na kupishwa (haiendi nyuma), na kuwa kwa mikataba ya madini iliyokwishaingiwa kabla ya sharia hii (miswada ya madini iliyo ktk mjadala) basi itabidi waongee na hao wawekezaji ili kukubaliana na baadhi ya mambo.

Kwa hiyo Rais wa wanasheria baada ya kuisoma hiyo miswada na kuzingatia kauli ya waziri wengi tulitegemea angekuja na hoja za kisheria (kutokana na weredi wa members wa hicho chama) ambazo zingeonyesha au kuhalalisha sharia mpya kutumika hata kwa mikataba ya huko nyuma. Kwa ufupi angeshauri ni nini cha kufanya ili maoni hayo yahusishwe ndani ya sharia kabla haijapitishwa.

Badala yake amekuja kuongea kama watu wengine wa kawaida tu. Hapo ndo huwa nashindwa kumwelewa kabisa Lisu; anapenda kuonyesha makosa na umbumbu wa wengine akijichukulia kama ndo mwanasheria mahiri pekee hapa nchini.
Kwann kila mnapojibu hoja zake mnahisi anajichukulia kuwa mwanasheria makini zaidi nchini?

Kimjazacho mtu ndicho kimtokacho. Mnamkubali rohoni, mdomoni mnaongea tofauti. Lahaula!! Sura zenu zinawakana
 
Ripoti aliyopewa rais itakuwa ni fake yakutuzuga. Wabunge wetu nao ni vilaza, ilikuwaje wakakubali kujadili na kubadilisha sheria kwa hati ya dharura pasipokuiona ripoti ili warekebishe mapungufu katika sheria na mengineyo?
Ukisikia nyumbu ndo kama hivyo
 
Kuifuta mikataba iliyokwisha sainiwa na viongozi waliopita si jambo jepesi la kulifanya kwa haraka.
Ni jambo linalohitaji sio tu umakini bali pia kuwapata wataalamu wa kushauri kama mheshimiwa Lisu, kuhusu kipengele gani kinaweza kuondolewa, kusahihisha au kuongezwa kwenye mikataba hiyo.
Jambo hilo inabidi lifanyike kwa makubalino na hao wawekezaji kama tulivyokubaliana
nao awali.
Ikumbukwe kuwa biashara ni makubaliano ya pande mbili na mwisho mikataba
inasainiwa.
Kama mikataba hiyo inatoa mwanya wa nchi kuibiwa au kuwapa faida kubwa wawekezaji hapo haijalishi kwani mikataba hiyo ilishasainiwa.
Lisu angefanya vizuri kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu nini kifanywe kwa sasa ili kurekebisha mikataba hiyo na sio kilawakati
kulaumu.
Viongozi waliopita ndo walisha tuingiza kwenye mikataba mibovu na tukijawa na jazba za kuwazuia wasifanya kazi sheria za kimataifa zita tubana maana tulishawaruhusu wenyewe kufanya
biashara.
Tuki amua kutaifisha miradi hiyo pia tutaonekana wakosaji na itatulazimu kama nchi kuwalipa wawekezaji kwa hasara tuliowasababishia.
Ndo maana,
sheria ya mpya ya madini iliyopelekwa Bungeni na mheshimiwa waziri Paramagamba Kabudi haiwezi kuingilia taratibu za makampuni ambayo yanafanya kazi
kabla ya hapo.
Kampuni kama Geita Gold Mine, inafanya kazi kwa taratibu na kanuni zilizosainiwa kwenye mikataba ya awali, hapa inabidi tungoje mpaka muda wa mkataba utakapoisha, watakapo omba ku re-new leseni zao hapo ndipo tunaweza kuwaingiza kwenye sheria mpya za
Kabudi.
Kama lawama tuwalaumu viongozi wetu waliopita kwa kukosa umakini kwenye mikataba ya awali.
Yaliyopita si ndwele hata hizi juhudi za kupeleka Bungeni sheria mpya za mikataba ni jambo la kujivunia na linapaswa kuungwa mkona na sisi sote pamoja na mheshimiwa
Tundu Lisu.
Lisu akumbuke kuwa sheria mbovu za mikataba hazijaanza juzi.
Udhaifu huu upo toka enzi za Chifu Mangungo, alipo ingia mikataba na wajerumani ya kutoa Almasi akibadilishana na Nguo, Mbegu za mazao, Magari na pesa,
Mheshimiwa Lisu hebu sasa tumia utaalamu wako kuishauri serikali badala ya kulaumuuu kulaumuuu kila kukicha,
haipendezi kwa msomi kulaumulaumu kila wakati.
Hiyo mikataba ilishasainiwa kimakosa, tufanyeje sasa ?
Tugange yajayo.
Alishashauri. Wakakaidi. Rais akipoke ripoti ya pili alosema wazi watu km Lissu hawatashirikishwa kwenye majadiliano wala kwenye kuzipitia sheria. Ndo uone kuwa hao ni sikio la kufa.........

Kama haitoshi, rais alisema kuna mtu anaongea sana ila wamekamata simu zake akichukua taarifa Acacia. Lissu akasema kama wana hayo mawasiliano waweke hadharani watz wamjue mbaya wao. Umeshawahi kuyasikia?

Ukiunganisha dots na namna mambo yanavyoungana utagundua wamekosa single itakayohit mda mrefu kama ya SAMUNGE. So wanatoa nyinginyingi kuchanganya watu.

Ishu hapa uchumi unadorora balaa, serikali imeelemewa hasa. Hayo ni mambo hampaswi kujadili sana mtasumbua. So mnapewa decoys.

La mashapo limeisha. Tusubiri Bashite atakuja na nini akitoka SA. Au pengine single itatokea mtwara
 
Andiko hilo na hoja ya Lissu ni kuona nchi inashindwa ili Lissu apate sifa. Aliyofanya Magufuli na heshima aliyoipata hakuna wa kuichukua. Ninachoona hapa ni kujitambulisha kwa msimamo wa viongozi wa CHADEMA. Wale walioko kwenye migodi na wanaooumia ndio watakaowahukumu vyema 2020 mtaona kama mtapata Jimbo lolote eneo hilo. Tena ni bora asiwe Lissu maana atashindwa vibaya sana.
Uwoga mnaouweka kwa Lissu ndo utawacost.
 
Nyie mtaendelea ku-suffer intellectual subjugation. Miswad siyo siri, ilisambazwa kwa umma na ofisi ya Bunge siku ya Alhamis Jume 29. Kwa wanaojua kusoma kama mimi tuliisoma (jumla page 110; 68+11+11) na tunajua kilichomo. Hiyo habari ya kucheza ngoma ya Acacia chezeni ninyi na Lissu wenu, siyo wazalendo kama sisi tunaojitambua. Tangu lini makampuni ya kigeni yakawa na viti bungeni katika nchi/dola yenye mamlaka? Inaelekea hata hamjui mnasema nini. Kwenye comment yangu hapo juu miwenukuu hata vifungu mahsusi; chukua mswada husika, soma, siyo kutegemea vijimaneno vya Lissu. Tundu Lissu ni Mwanasheria msomi kwa nini kwenye bandiko lake hanukuu hata kifungu kimoja Zaidi ya blah blah? Kuna mambo mengine ya kufanya siyo huo uwakala wenu kwa Acacia. Mmekwishashindwa!
Mliambiwa mtoe hayo mawasiliano ya huyo wakala wa acacia. Tangu mshindwe hilo kii yenu ya uwakala haina mashiko. Kilicho wazi ni kwamba hakuna udhati kushulika na tatizo la mali asili
 
Kwann kila mnapojibu hoja zake mnahisi anajichukulia kuwa mwanasheria makini zaidi nchini?

Kimjazacho mtu ndicho kimtokacho. Mnamkubali rohoni, mdomoni mnaongea tofauti. Lahaula!! Sura zenu zinawakana

Ukisoma nilichoandika utagundua kuwa sijakataa kuwa Lisu ni mwanasheria mahiri, ila haina maana kuwa ni yeye tu aliye mahiri (kuna wengi sana wabobezi ktk sheria zaidi yake lkn wao si wanasiasa ). Mtizamo wangu ni kuwa mara zote anawasilisha maoni yake kwa mtizamo hasi ambao wakati mwingine unatia shaka dhamira yake. Na pia uwasilishaji wake wa mambo hauwezi kumuonyesha kama Rais wa wanasheria.
 
kama nilivyosema Lisu alikuwa anaisoma kwa makini kinyume cha wale wabunge wa ndio waliokuwa wanashangilia tu,kila lisemwalo ili mradi anaesema ni mtu wa ccm kama alivyosema Polepole
 
Back
Top Bottom