Lissu: Makampuni yaliyotunyonya tangu 90's hayapo kwenye sheria ya madini

Nilitegemea Tundu Lisu kama Rais wa chama cha wanasheria angeongea tofauti na alivyofanya, amejikita ku-criticize kama kawaida yake. Waziri wa sharia alisema kuwa sharia mpya huanza kuwa applied pale inapotungwa na kupishwa (haiendi nyuma), na kuwa kwa mikataba ya madini iliyokwishaingiwa kabla ya sharia hii (miswada ya madini iliyo ktk mjadala) basi itabidi waongee na hao wawekezaji ili kukubaliana na baadhi ya mambo.

Kwa hiyo Rais wa wanasheria baada ya kuisoma hiyo miswada na kuzingatia kauli ya waziri wengi tulitegemea angekuja na hoja za kisheria (kutokana na weredi wa members wa hicho chama) ambazo zingeonyesha au kuhalalisha sharia mpya kutumika hata kwa mikataba ya huko nyuma. Kwa ufupi angeshauri ni nini cha kufanya ili maoni hayo yahusishwe ndani ya sharia kabla haijapitishwa.

Badala yake amekuja kuongea kama watu wengine wa kawaida tu. Hapo ndo huwa nashindwa kumwelewa kabisa Lisu; anapenda kuonyesha makosa na umbumbu wa wengine akijichukulia kama ndo mwanasheria mahiri pekee hapa nchini.
 
matusi ya nini? unatabia kama za lissu kutukana wenzie,sikushangai mkawekwa sero mnaanza kulia lia
Na sisi hatushangai mnvobanduliwa mmojammoja kule kibiti,ngoma droo sero na kifo ipi inakolea?
 
Narudia kusema,watu aina ya Tundu Lissu hakupaswa kuzaliwa katika nchi kama hii bali walipaswa kuzaliwa katika nchi za wenzetu ambako bila shaka wangekuwa wameshapata recognition.

Bahati mbaya sana, maoni haya ya kina Lissu yanaishia tu mitandaoni ila ya bwana yule ndio yanatangazwa dunia muzima na bahati mbaya sana sisi binadamu wengi hatutafuti habari za siasa na wanasiasa kama tunavyotafuta habari zinazohusu gossip,sex,soccer,jokes,etc na badala yake tunasubiri kuletewa/kutangaziwa habari hizi na bahati mbaya zaidi kwa hapa kwetu habari zinazotangazwa zaidi na media ni zile za watawala na sio hizi za kina Lissu tunazopaswa kuzitafuta mitandaoni na kwingineko.

Angalieni hata magazeti yetu siku hizi yalivyojaa ushabiki.

Tundu Lissu nakushauri angalia uwezekano wa kuongea na wahariri wa vyombo vya habari ili wakusaidie kufikisha kwa wananchi haya unayosema na kuyaandika mitandaoni maana wengi hayawafikii.
Kwani kuna aliyemnyima kuita press conference?
 
UTAFITI HURU UMEBAINI KWAMBA MH TUNDU LISSU NDIYE MWANASHERIA BORA KABISA KUWAHI KUWEPO KWENYE ENEO LA MAZIWA MAKUU TANGU KUUMBWA KWA MBINGU NA ARDHI .
Huu utafiti utakuwa umefanywa mitaa ya ufipa
 
Magazeti wanaogopa KUFUNGIWA baada ya KUTISHWA MAJUKWAANI NA KWENYE HOTUBA KALI.
KUJIDANGANYA NI KUENDELEA KUFICHA MOTO HUKU WAKIZIMA MOSHI!
Hata vituo vya TV naona wamegwaya-labda muujiza utokee-sioni wa kumwalika atuelezee kwa kina haya mambo, tunamsikia bwana yule tu.
 
Ripoti aliyopewa rais itakuwa ni fake yakutuzuga. Wabunge wetu nao ni vilaza, ilikuwaje wakakubali kujadili na kubadilisha sheria kwa hati ya dharura pasipokuiona ripoti ili warekebishe mapungufu katika sheria na mengineyo?
 
Kuifuta mikataba iliyokwisha sainiwa na viongozi waliopita si jambo jepesi la kulifanya kwa haraka.
Ni jambo linalohitaji sio tu umakini bali pia kuwapata wataalamu wa kushauri kama mheshimiwa Lisu, kuhusu kipengele gani kinaweza kuondolewa, kusahihisha au kuongezwa kwenye mikataba hiyo.
Jambo hilo inabidi lifanyike kwa makubalino na hao wawekezaji kama tulivyokubaliana
nao awali.
Ikumbukwe kuwa biashara ni makubaliano ya pande mbili na mwisho mikataba
inasainiwa.
Kama mikataba hiyo inatoa mwanya wa nchi kuibiwa au kuwapa faida kubwa wawekezaji hapo haijalishi kwani mikataba hiyo ilishasainiwa.
Lisu angefanya vizuri kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu nini kifanywe kwa sasa ili kurekebisha mikataba hiyo na sio kilawakati
kulaumu.
Viongozi waliopita ndo walisha tuingiza kwenye mikataba mibovu na tukijawa na jazba za kuwazuia wasifanya kazi sheria za kimataifa zita tubana maana tulishawaruhusu wenyewe kufanya
biashara.
Tuki amua kutaifisha miradi hiyo pia tutaonekana wakosaji na itatulazimu kama nchi kuwalipa wawekezaji kwa hasara tuliowasababishia.
Ndo maana,
sheria ya mpya ya madini iliyopelekwa Bungeni na mheshimiwa waziri Paramagamba Kabudi haiwezi kuingilia taratibu za makampuni ambayo yanafanya kazi
kabla ya hapo.
Kampuni kama Geita Gold Mine, inafanya kazi kwa taratibu na kanuni zilizosainiwa kwenye mikataba ya awali, hapa inabidi tungoje mpaka muda wa mkataba utakapoisha, watakapo omba ku re-new leseni zao hapo ndipo tunaweza kuwaingiza kwenye sheria mpya za
Kabudi.
Kama lawama tuwalaumu viongozi wetu waliopita kwa kukosa umakini kwenye mikataba ya awali.
Yaliyopita si ndwele hata hizi juhudi za kupeleka Bungeni sheria mpya za mikataba ni jambo la kujivunia na linapaswa kuungwa mkona na sisi sote pamoja na mheshimiwa
Tundu Lisu.
Lisu akumbuke kuwa sheria mbovu za mikataba hazijaanza juzi.
Udhaifu huu upo toka enzi za Chifu Mangungo, alipo ingia mikataba na wajerumani ya kutoa Almasi akibadilishana na Nguo, Mbegu za mazao, Magari na pesa,
Mheshimiwa Lisu hebu sasa tumia utaalamu wako kuishauri serikali badala ya kulaumuuu kulaumuuu kila kukicha,
haipendezi kwa msomi kulaumulaumu kila wakati.
Hiyo mikataba ilishasainiwa kimakosa, tufanyeje sasa ?
Tugange yajayo.
 
Anaandika Mhe. Tundu Lissu

Leo Bunge linajadili Muswada wa marekebisho ya sheria za madini na za kodi katika sekta ya madini.

Makampuni ya kigeni ambayo yametunyonya tangu miaka ya mwisho ya '90, na yanaendelea kutunyonya hadi sasa, hayapo kwenye mjadala huu.

Acacia Mining PLC, ambayo Magufuli na maprofesa wake wamedai imetupiga zaidi ya shilingi trilioni 139 wakati haina hata leseni ya uchimbaji madini, nayo haipo kwenye mjadala huu.

Kama nilivyotabiri mwezi uliopita, Magufuli amesalimu amri mbele ya makampuni haya na mbele ya Acacia Mining PLC.

Naomba kufafanua.

Muswada unaojadiliwa leo umetamka wazi kuwa mikataba ya uendelezaji madini iliyopo sasa itaendelea.

Hii ni pamoja na mikataba ya Acacia Mining PLC kuhusu Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara. Kwa Muswada huu, mikataba hii ni halali.

Kusalimu amri huku kwa Magufuli kuna maana kubwa sana.

Mjadala wa makinikia ya dhahabu sasa ndio umezikwa rasmi.

Kama mikataba ya Acacia Mining PLC ni halali, maana yake ni kwamba usafirishaji wa makinikia ulikuwa halali muda wote. Watayarudishiwa makinikia yao kimya kimya.

Sidhani kama tutamsikia mtukufu Rais wetu akizungumzia makinikia tena. Na mtakaong'ang'ania tuyajadili mtaanza kutishwa ili mnyamaze.

Hayo matrilioni ya akina Prof. Mruma na Prof. Osoro ndio hatutayasikia tena. Yalikuwa ni ya uongo, 'professorial rubbish', tangu mwanzo.

Ndio maana hata wabunge wameambiwa Taarifa za hao wasomi wabobezi ni mali ya Rais peke yake. Wengine haturuhusiwi kuziona.

Kama mikataba ni halali kwa mujibu wa Muswada wa leo, maana yake nyingine ni kuwa waliohusika kuiandaa au kuisaini hawana kosa lolote.

Hoja ya kuwashtaki akina Chenge, Ngeleja, Muhongo na wengineo waliotajwa kwa majina na Kamati ya Prof. Osoro, nayo sasa ni marehemu.

Kama mikataba ni halali watakamatwa na kushtakiwa kwa kosa gani???

Kwa hiyo, kwenye signature issue yake kubwa juu ya rasilmali zetu, huyu anayeitwa mtetezi wa wanyonge na mlinzi wa rasilmali zetu, ameshindwa vibaya. Magufuli ameshindwa, kama nilivyosema atashindwa.

Kwa Muswada huu, Magufuli ameendeleza na kuhalalisha matendo ya watangulizi wake Mkapa na Kikwete ya kugawa rasilmali zetu kwa wageni.

Kwa Muswada huu, waliotunyonya na kutuibia juzi na jana na wanatuibia leo, wataendelea kutunyonya na kutuibia kesho na kesho kutwa.

Muswada wa leo unafanya mabadiliko makubwa ya kisheria kwa makampuni yatakayokuja miaka ijayo.

Sawa kabisa. Lakini naomba Magufuli na wapambe wake watusaidie hili: hivi ni sehemu gani ya nchi yetu ambayo ina madini na hayana mwenyewe tayari???

Ni sehemu ipi ya eneo letu la bahari au eneo maalum la kiuchumi ambalo bado halina mikataba ya kutafuta au kuchimba mafuta au gesi asilia???

Nchi hii ilishagawanywa vipande vipande na kupewa wawekezaji wakati wa Mkapa na Kikwete.

Muswada huu ni mzuri kwenye karatasi, kiuhalisia sheria yake haitatekelezeka kwa sababu mali tayari ilishauzwa na Muswada huu umebariki biashara hiyo.

Magufuli na watu wake hawataki watanzania wajue hili. Ndio maana Muswada unaletwa kwa dharura, ili kusiwe na mjadala wowote wa kuna.

Baadae kidogo nitazungumzia Sheria mpya zilizopitishwa jana kwa mpigo na kwa Hati ya Dharura. Sheria hizo ni uongo mwingine mkubwa kwa watanzania.
Andiko hilo na hoja ya Lissu ni kuona nchi inashindwa ili Lissu apate sifa. Aliyofanya Magufuli na heshima aliyoipata hakuna wa kuichukua. Ninachoona hapa ni kujitambulisha kwa msimamo wa viongozi wa CHADEMA. Wale walioko kwenye migodi na wanaooumia ndio watakaowahukumu vyema 2020 mtaona kama mtapata Jimbo lolote eneo hilo. Tena ni bora asiwe Lissu maana atashindwa vibaya sana.
 
Kuifuta mikataba iliyokwisha sainiwa na viongozi waliopita si jambo jepesi la kulifanya kwa haraka.
Ni jambo linalohitaji sio tu umakini bali pia kuwapata wataalamu wa kushauri kama mheshimiwa Lisu, kuhusu kipengele gani kinaweza kuondolewa, kusahihisha au kuongezwa kwenye mikataba hiyo.
Jambo hilo inabidi lifanyike kwa makubalino na hao wawekezaji kama tulivyokubaliana
nao awali.
Ikumbukwe kuwa biashara ni makubaliano ya pande mbili na mwisho mikataba
inasainiwa.
Kama mikataba hiyo inatoa mwanya wa nchi kuibiwa au kuwapa faida kubwa wawekezaji hapo haijalishi kwani mikataba hiyo ilishasainiwa.
Lisu angefanya vizuri kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu nini kifanywe kwa sasa ili kurekebisha mikataba hiyo na sio kilawakati
kulaumu.
Viongozi waliopita ndo walisha tuingiza kwenye mikataba mibovu na tukijawa na jazba za kuwazuia wasifanya kazi sheria za kimataifa zita tubana maana tulishawaruhusu wenyewe kufanya
biashara.
Tuki amua kutaifisha miradi hiyo pia tutaonekana wakosaji na itatulazimu kama nchi kuwalipa wawekezaji kwa hasara tuliowasababishia.
Ndo maana,
sheria ya mpya ya madini iliyopelekwa Bungeni na mheshimiwa waziri Paramagamba Kabudi haiwezi kuingilia taratibu za makampuni ambayo yanafanya kazi
kabla ya hapo.
Kampuni kama Geita Gold Mine, inafanya kazi kwa taratibu na kanuni zilizosainiwa kwenye mikataba ya awali, hapa inabidi tungoje mpaka muda wa mkataba utakapoisha, watakapo omba ku re-new leseni zao hapo ndipo tunaweza kuwaingiza kwenye sheria mpya za
Kabudi.
Kama lawama tuwalaumu viongozi wetu waliopita kwa kukosa umakini kwenye mikataba ya awali.
Yaliyopita si ndwele hata hizi juhudi za kupeleka Bungeni sheria mpya za mikataba ni jambo la kujivunia na linapaswa kuungwa mkona na sisi sote pamoja na mheshimiwa
Tundu Lisu.
Lisu akumbuke kuwa sheria mbovu za mikataba hazijaanza juzi.
Udhaifu huu upo toka enzi za Chifu Mangungo, alipo ingia mikataba na wajerumani ya kutoa Almasi akibadilishana na Nguo, Mbegu za mazao, Magari na pesa,
Mheshimiwa Lisu hebu sasa tumia utaalamu wako kuishauri serikali badala ya kulaumuuu kulaumuuu kila kukicha,
haipendezi kwa msomi kulaumulaumu kila wakati.
Hiyo mikataba ilishasainiwa kimakosa, tufanyeje sasa ?
Tugange yajayo.
Watakubali ushauri wake kweli?
 
Tujiondoe kwenye MIGA kwanza ili tufanye yetu pia hamtaki mkidhani Lissu atashinda; zungukeni wee mtarudi palepale kwa Lissu. Akina Paramagamba wanakufa na ushauri kifuani kisa the Boss ataki kusikia yaliyosemwa na Lissu ndo yamechukuliwa.
 
Watakubali ushauri wake kweli?
Ushauri wa Lisu utapokelewa na kufanyiwa kazi kwa asilimia mia moja.
Ashauri tu kwa nia njema hakuna wa kumkatalia ukichukulia anaweza hata kwenda binafsi kumwona na kushauriana na mwalimu wake
Bwana Kabudi.
 
Back
Top Bottom