Licha ya uzuri na elimu, dada yangu hapati mwanaume wa kumuoa

Maleven

JF-Expert Member
Sep 8, 2019
627
2,788
Namuona kabisa dada angu sasa anamawazo sana, anamiaka 28 sasa, kila anaemfata hayuko serious au ni mume wa mtu, wapo wengine sema sasa dada anasema anakosa hisia nao kabisa, anaogopa kujilazimisha.

Alifikia hatua ya kutaka kupanga akakae mwenyewe, kitu ambacho baba na familia nzima haijakubaliana nalo kwakua bado hajaolewa.

Nami najitahidi kwa maombi apate mwanaume aolewe, wenzake wote walokua karibu wa rika moja, wameolewa na wana watoto.

Dada yangu imefika hatua hata kazini anaona anahatibu tu.

Eeh Mungu mpe dada angu hitajio pa moyo wake, asije akadata au akazalishwa nyumbani.

N.B
Wanaume wa mtandaoni labda awatafute mwenyewe,mimi siwezi muunganisha nao watu nisio wajua, hivyo siwezi tuma namba wala picha yake. Nimeleta hapa kwakua nami linanishughulisha nikimuona akiwa hayuko sawa

Update: Dada amepata mchumba
 
Wanawake wote waliokua na presha ya kutaka kuolewa Wameishia kuwa singo maza kuzaa na wanaume tofaut tofaut kama kuku, mwisho wa siku wanatelekezwa wanaanza kuita wanaume mbwa 😂😅.

Ni hivi wanaume sikuhiz Wanazalisha wanapitw kushoto... KATAA NDOA UISHI KWA AMANI UIMARIKE KIUCHUMI
 
Namuona kabisa dada angu sasa anamawazo sana, anamiaka 28 sasa, kila anaemfata hayuko serious au ni mume wa mtu, wapo wengine sema sasa dada anasema anakosa hisia nao kabisa, anaogopa kujilazimisha...
Mwangalie tu asijezaa na mume WA mtu😀😀mi na binamu yangu mtoto WA uncle, Naye alikuwa ivyo ivyo nahisi kinachowaponza ni kutopenda kujishusha Kwa wanaume,dharau na kuchagua chagua mwisho WA siku umri ulienda Hadi 30 na kitu wanaamua kutafuta tu mtoto Hadi na watu wasioeleweka, kama uyo binamu yangu ni msenge sana😀ana mtoto sa hivi mkubwa mkubwa tu ila baba yake mtoto, watu wote hatambuliki kwenye ukooyaani anamficha ila watu wameshazinyaka za chini kuwa ni jamaa mwenye familia yake.
 
Namuona kabisa dada angu sasa anamawazo sana, anamiaka 28 sasa, kila anaemfata hayuko serious au ni mume wa mtu, wapo wengine sema sasa dada anasema anakosa hisia nao kabisa, anaogopa kujilazimisha.

Alifikia hatua ya kutaka kupanga akakae mwenyewe, kitu ambacho baba na familia nzima haijakubaliana nalo kwakua bado hajaolewa.

Nami najitahidi kwa maombi apate mwanaume aolewe, wenzake wote walokua karibu wa rika moja, wameolewa na wana watoto.

Dada yangu imefika hatua hata kazini anaona anahatibu tu.

Eeh Mungu mpe dada angu hitajio pa moyo wake, asije akadata au akazalishwa nyumbani.
Mkuu una maanisha?
Unataka dada yako ajae furaha?
Muunge nami hakika hutojuta...atajaa furaha hutaamini
 
Back
Top Bottom