Leo nimeondoka rasmi jijini Dar es Salaam baada ya kupata mchongo Jehanamu

Objective football

JF-Expert Member
Oct 21, 2023
1,195
2,758
Hakika dar es salaam ni Mji ulionipa marafiki wengi, network kubwa na hata pesa ya kuishi japo kuna siku mji huu ulinilaza njaa.

Asubuhi ya leo wakati natoka mbezi kuja huku mkoani chozi limeni tililika sana(fear of new changes)

Doh! nimefika mkoani , nikaenda kuripoti kituo changu cha kazi nilichopangiwa na shirika moja binafsi hapa nchini! ni aibu sana kwakweli!.

Wafanyakazi wenye certificate,diploma wanavimba ofisini na kipupwe mimi wamenipeleka kijijini wastani wa kilomita 120 kutoka mjini,hakuna makazi bora,maji ya tabu,usafiri wa shida na network inashika haloteli tu.

Nimeikuta jamii ni walevi mno, sura zao zimekosa nuru, najiona kabisa napotea kwenye ulevi wa kupindukia huku kijijini, wanatumia punda kwenda kuchota maji ya kunywa kweli!
 
wafanyakazi wenye certificate,diploma wanavimba ofisini na kipupwe mimi wamenipeleka kijijini wastani wa kilomita 120 kutoka mjini,hakuna makazi bora,maji ya tabu,usafiri wa shida na network inashika haloteli tu.
Wanakulipa Shilling ngap? Tuanzie hapo ili usipige sana kelele hapa wakati watu hata huko bush hawajafanikiwa kupata kazi wewe umepata unaanza kuleta ngebe, wanakulia Shilling ngap?
 
Back
Top Bottom