Leo asubuhi kulitokea mabishano home

Wanawake wa siku hizi ni pasua kichwa ndio maana wanaoshia kuachwa..hawasikilizi waume
Hakuna kuachwa kwa mwanamke makini hizo family matters ni za kawaida.Ila nawakumbusha ndani ya nyumba KUNA kuelekezana na mama NDO kiongozi NDO Mana Mimi Mista wangu kaniachia majukumu yote mpaka ya kuchukua Kodi za nyumba tulizopangisha.

Maamuzi mengine Kama biashara ni yeye lkn lazima atanishirikisha Sasa ndani ya nyumba Napo napenda maagizo yafuatwe na watoto akiwepo huyo Dada.Hii nguo nimekununulia ya outing sawa na hii ya kufanyia usafi sawa.Simple like that Sasa wanaosema ulimpa mtu usimfatilie ni kweli akiwa mtu tu mfano rafiki jirani mpita njia.

Mlichoshindwa kutofautisha ni ndani ya nyumba kwa Kila mama kuna masharti Sasa hii ni tofauti pesa yake ya mwezi ataifanyia chochote Wala siingilii.Mfano natoa samaki kwenye friji pika yeye akarudisha akapika maharage ni kosa japo kuna wkt humwambia Leo chagua Cha kupika.Mpate SoMo kidogo na nyie.
 
Ukiona anaivaa kilasiku ujue anaipenda Sana kuliko nguo zote kwaiyo hutakiwi kumzui
Na ni kweli but ya kutokea SIO kuiweka utonvu kumbuka ni mtoto wa kumwelekeza
 
Nyeye alikuwa anapenda pensi kwaiyo hakufanya kosa kila mtu ana penda nguo za tofauti na wengine
Aiseeee sio kweli Mapensi yaliyojaa Kila Kona mpaka ya buku buku akakate jeans ya gharama. Nyie why mnatetea Mambo Kama haya??
 
MKE WANGU HAYA MAMBO TUMEJADILI NYUMBANI KAMA FAMILIA, NI KWANINI UMEAMUA KUYALETA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII HUKU?
Haaa haaaa lilinikaba kooni nikaona nije kutoa la Rohoni ajabu Sasa watu wamenipiga na kitu kizito kichwani.Kuweni na huruma jamani moyo wangu mdogo.
 
Zinazoitwa changamoto za ndoa mnazishughulikia vipi ikiwa jambo dogo kama hili limeleta mpasuko ndani ya nyumba?
Ni kweli nguo uliompa ndio ameipenda na zingine kaziona tambara kama wewe ulivyoona ni nguo za kuburuta kwa shughuli za nyumbani.
Hao ndugu zako hukuweza kuwapa hiyo nguo kabla ya kuona kuwa house girl anaiharibu?
Pengine Mr kamwambia avae hiyo badala ya vipande vya matambara ya kanga au nguo za ajabu alizokuwa anavaa ili kuepusha balaa ndani ya nyumba.
Swala halipo hivyo.Wala issue sio kubwa.Unajua Mambo madogo madogo kwenye nyumba NDO huleta sintofahamu tusipuuzie.Hapa Mimi nilichoona ni wengi kutoelewa Shana nzima ilivyo.Mimi nilipompa nilimwambia hii ya kutokea na hizi zingine thou nazo NZURI tu za ile unafanya shughuli kumbuka ni Kama maagizo ndani ya nyumba.

Sio mtu baki mbona niliwahi mpa mtoto wa jirani nguo NZURI nikidhani mama yake atakuwa anamvalisha sehemu muhimu but NDO akawa anashindia na haikuwa moja nilizowapa kwa wkt tofauti sijawahi hoji.Hapa ni ndani kwa maana maelezo ya nyumbani Nyie Nyumbani kwenu hakunana kanuni wala maelezo watoto wanajiamulia tu Mambo yao? Malezi ya wapi hayo
 
Kama ni mimi ningekurudishia nguo yako. kama unaipenda sana ungebaki nayo.
Unaweza kuona kitu ni cha thamani sana kumbe mwingine anakiona cha kawaida sana.
Halafu kuhusu mavazi, wengine tumetofautina. Kuna watu hawana kanuni ya mavazi kwamba hii ni ya kutokea na hii ya kushindia. Ni akijisikia yeyote anaivaa.
 
Heloo, nadhani unasahau kuwa huyo HG anatoka katika familia gani. Hapo alipo ni kama yupo 5 star hotel na anaona ni vyema akawa smart kila wakati.
Usisahau, ukimtuma HG dukani, lazima aingie bafuni kuoga na ajikwatue. Huo ni umri unasumbua na mazingira aliyomo yanamzuzua. Kwa mantiki hiyo ndo maana kila siku anapenda kuivaa hiyo nguo hata akiwa anamenya ndizi zenye utomvu.

Kwa wengine wote, usitoe zawadi kwa mtu yeyote awe mtoto, mpenzi etc zawadi yenye thamani kubwa! Kwa kawaida zawadi huwa ni ile ambayo hata mkiachana au mkakasirikiana hutaitumia kama fimbo. Hata kama ni rafiki, urafiki ukikoma unamwachia na haitakuuma. Ndiyo maana humu tunaambiwa Mchumba hasomeshi. Ukimpa mtu zawadi usiifuatilie! Mfano ukimjengea mwanamke nyumba, hata mkiachana unaondoka bila kinyongo na hata ukikuta njemba imetanua miguu, usiumie. Kama unadhani utaumia acha usimjengee nyumba maana hiyo si zawadi bali CHAMBO.
Nailed.
But my friend labda kilichosumbua kwangu ni vile wkt Nampa nilimpa na kasharti kidogo.But all in all nimeelewa.Na Mimi kweli niliumua maana ni nguo ya bei
 
Nawashukuru wote mlioshauri na Kila kitu.

Ila nimejifunza nilipokosea wapi na nilipopatia wapi Ila nasisitiza wkt nagawa Ile nguo nilimwambia na masharti yake na nikitambua ni mtoto wa ndani ya nyumba Ila Kama wengine walivyosema eti huenda anaipenda Sana na huenda pengine hajui japo nilimwambia lengo la kumpa kwangu nilichukulia Kama(mazarau)unajui na sisi akina Mama tuna Mambo Mambo yetu yale ya kupenda kuheshimika au kuona ulichosema kinafuatwa nakumbuka hata hapo zamani mama akisema hii nguobya kanisani au ya Christmas huwezi vaa kabla ya hiyo siku au ukaamua kufanya ambavyo hajasema utafanya but NDO itakuwa mwisho wa kupewa vitu vizuri.Is like I remember my late sister Kissa may Lord rest her soul in heaven, Gave me her favorite suit.

Guess what she always wanted me to wear on special events that all about.
Na kuhusu mista wangu kafurahi Sana mlivyonipiga na kitu kizito kichwani.Mungu anawaona
 
Unachofanya ni sahihi. Inaonekana huyo dada bado hajajua anapaswa kuvaa nini wakati gani na wapi. Mfundishe.
Waoooh! What a nice advise.Hii sms sikuiona mapema.Sasa wewe NDO umenielewa vizuuuuuri.
Mana wengine walikuwa wananipiga na kitu kizito kichwani.
 
Mista yuko sahihi, kwa mtazamo wangu. Umempatia mtu kitu, mwache akitumie kwa kadri anavyotaka yeye.. kumpangia pangia namna ya kukitumia means bado hiyo ni mali yako na yeye umemwazima tu.
Hapo napingana na wewe. Unajua kwa jamii zetu zilivyo, mdada wa kazi akionekana yupo rough, lawama na shutuma huwa zinaenda kwa mama, yeye ndo ataonekana anamnyanyasa Binti. Mwonekano mzuri wa dada wa kazi, unareflect jinsi anavyokuwa treated ndani ya hiyo nyumba.

Hata sisi wakati tupo wadogo, nguo zetu tulikuwa tunanunuliwa na wazazi, na Mama ndio alikuwa anapanga, nguo ipi tushindie, na ipi ni ya mtoko, japo zilikuwa Mali zetu. Na ikitokea umeshindia nguo ya mtoko ulikuwa unapigwa.

So acheni double standard wakuu
 
Mi nilinunua jeans kali 25000 enzi hizo ikanibana kiuno ikiwa mpya kabisa nikampa ndugu yangu mtoto wa ba mdogo kesho yake akaikata pensi,kidogo nimpe kesi ya kuhujumu uchumi
Mimi nilimtumia simu dada yangu kijijini baada ya kuniomba sana hata simu used. Mimi nikaenda kumnunulia mpya, ile imefika kijijini tu kaiuza, tena kamuuzia dada mkubwa.
Nikakausha tu hata sijamuulizia hilo jambo.
Watu wengi ni wahuni
 
Upo sahihi kwa % fulani, usahihi wako ni kumfundisha binti ajue nguo ipi ivaliwe wapi na katika mazingira gani.

Kifupi watu wengi, hata watu wazima hawajui kugawanya nguo za kuvaa, hivyo kwa binti mdogo ni vizuri kunfundisha, ajue nguo ipi ivaliwe katika mazingira gani.

Ukiona hafundishiki unaachana nae tu, utajifunza kuwa huna haja ya kumpa nguzo zako nzuri hadi atakapojua kuzipangilia.
 
Issue iliyopo hapo ni zaidi ya kuvaa hiyo nguo nzuri,
Huyo Mista sio Kila kitu Cha kutoa MAONI najua umjisikia vibaya alipomtetea huyo dada suala la hiyo nguo, if you have a bad feeling mtoe huyo dada
 
Back
Top Bottom