Katika hili baby mamas mnafeli

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,520
6,503
Jua kali mida ya mchana kuelekea al asiri, mwamba mmoja anaonekana akiongea na simu yake ya mkononi,na hakika amezama hasa katika maongezi yake.

Wazee wa Cuba huwa hatukawii kung'amua kwamba kuna kitu hakiko sawa kwa jinsi mwamba alivyokuwa anaongea, ilinichukua sekunde zisizo zidi thelathini kujua hakika mwamba yuko katika wakati mgumu na baby mama wake.

Alisikika mwamba kwenye line "ina maana huyo mtoto mpaka leo bado anaumwa tu? Haijafika hata miezi minne tayar ameumwa Mara kadhaa"

Kuhusu baby mama wake kajibu nini anajua mwamba mwenyewe, lkn ilionekana mwamba ana maswali mengi kuliko Majibu kwani aliendelea kuhoji mambo mengi kuhusu afya ya mwanae.

Hii ikanikumbusha kisa cha jamaa yangu mmoja ambaye yuko katika ile taasisi ambayo wanavaa Nguo zenye mabaka mabaka ambazo endapo ukakutwa umevaa nguo zao na wakati wewe si mmoja wao hakika maji utaita mma!

Mwamba nae alikuwa anapata habari za mwanae kuwa anaumwa mara Kwa mara, akapatwa na machale basi akafanya safari ya kushtukiza kwenda kumcheki mwanae na kujua hali yake.

Alichokiona huko hakika hakujuta kufanya ziara ya ghafla, kwani alimkuta dogo yupo mtaani anavumbi kibao Kama kiongozi wa msafara wa mwenge, kwani ni bukheri wa afya na anatimiza majukumu yake ya kucheza na wenzake kama kawaida.

Kilichoendelea na baby mama wake baada ya tukio lile wala sitaki kujua na hata Kama ningejua nisingewaambia humu ndani.

Madam zangu hii tabia ya kusingizia mtoto anaumwa ili tu upate chochote sio poa coz ipo siku mtoto ataumwa kweli na kujikuta unashindwa kupata msaada kwa wakati.

Kama umekwama mwambie tu mzazi mwenzako kuwa baba fulani leo sielewi elewi kuna mambo nataka niyaweke sawa msaada wako ni muhimu Sana, hakika kwa mwanaume mwenye busara zake atakubusti tu.

Nayasema haya kwa roho saf tu kwani Sina baya na Mtu hata kidogo.

Ni hayo tu!
 
Hospitali zote nowdays wanalipa kwa control number..... Akikuambia mtoto anaumwa mwambie aende hospitali kisha malipo yote utafanya kwa control number atakazokutumia✅
 
Chief
Umetisha Sana,,, ila watatafuta namna yoyote ile ya kukupiga.

Ila wazo lako litapunguza kupigwa hela ndefu
 
Mie mtu akiniongopea ili apate pesa yangu, namchukia kwa kiasi kikubwa mnoo, umekwama we niambie tu kuna 1,2,3 mie nijikune mkono wangu unapofika, sasa ukiongopa mwishowe naweza fosi kujikuna hata na jiti mwishowe najitoa ngozi.

Chief
Umetisha sana
👇👇👇

"sasa ukiongopa mwishowe naweza fosi kujikuna hata na jiti mwishowe najitoa ngoz"
 
Jua kali mida ya mchana kuelekea al asiri, mwamba mmoja anaonekana akiongea na simu yake ya mkononi,na hakika amezama hasa katika maongezi yake.

Wazee wa Cuba huwa hatukawii kung'amua kwamba kuna kitu hakiko sawa kwa jinsi mwamba alivyokuwa anaongea, ilinichukua sekunde zisizo zidi thelathini kujua hakika mwamba yuko katika wakati mgumu na baby mama wake.

Alisikika mwamba kwenye line "ina maana huyo mtoto mpaka leo bado anaumwa tu? Haijafika hata miezi minne tayar ameumwa Mara kadhaa"

Kuhusu baby mama wake kajibu nini anajua mwamba mwenyewe, lkn ilionekana mwamba ana maswali mengi kuliko Majibu kwani aliendelea kuhoji mambo mengi kuhusu afya ya mwanae.

Hii ikanikumbusha kisa cha jamaa yangu mmoja ambaye yuko katika ile taasisi ambayo wanavaa Nguo zenye mabaka mabaka ambazo endapo ukakutwa umevaa nguo zao na wakati wewe si mmoja wao hakika maji utaita mma!

Mwamba nae alikuwa anapata habari za mwanae kuwa anaumwa mara Kwa mara, akapatwa na machale basi akafanya safari ya kushtukiza kwenda kumcheki mwanae na kujua hali yake.

Alichokiona huko hakika hakujuta kufanya ziara ya ghafla, kwani alimkuta dogo yupo mtaani anavumbi kibao Kama kiongozi wa msafara wa mwenge, kwani ni bukheri wa afya na anatimiza majukumu yake ya kucheza na wenzake kama kawaida.

Kilichoendelea na baby mama wake baada ya tukio lile wala sitaki kujua na hata Kama ningejua nisingewaambia humu ndani.

Madam zangu hii tabia ya kusingizia mtoto anaumwa ili tu upate chochote sio poa coz ipo siku mtoto ataumwa kweli na kujikuta unashindwa kupata msaada kwa wakati.

Kama umekwama mwambie tu mzazi mwenzako kuwa baba fulani leo sielewi elewi kuna mambo nataka niyaweke sawa msaada wako ni muhimu Sana, hakika kwa mwanaume mwenye busara zake atakubusti tu.

Nayasema haya kwa roho saf tu kwani Sina baya na Mtu hata kidogo.

Ni hayo tu!
Kataa ndoa, kataa mahusiano
 
Back
Top Bottom