Leo asubuhi kulitokea mabishano home

Ndoa ina muda gani na mnawatoto wangapi na wa umri gani? Je mumeo macho juu juu au hana ibilisi?
 
N jambo dogo tu hilo, lisikuumize kichwa, mwache ashindie, Cha muhimu angalia usalama wa ndoa yako.
 
Binafsi naona uyo house girl wako kaona bora awe anaivaa iyo nguo coz unajua fika mabeki tatu wengi huwa awatoki home so unazani uyo dada iyo nguo ataivaa wapi so kaona bora awe anakashindia kihome home japo na yeye aonekane bhana embu mwache basi japo naye aonekane amependeza ila angaliz kuwa makini baba asije akamgeuza mke mdogo si unajua tena ahahaha just jokes mama
 
Upuuzi mtupu mnapost sasa nguo ndo Nini

Vitu vya ovyo ovyo tu yaani nyie wanawake was siku hizi nimabogasi jitu Zima unagombania midosho
 
Una gubu na unavyoendelea kumsema house girl ndio Mr anazidi kumuonea huruma kwa tabia zako na mwishowe ataanza kumpa pesa ajinunulie mwenyewe na binti atataka kurudisha fadhila na ndipo ndoa yako utaona Chungu!

Chakufanya wewe mpotezee na usiongee tena chochote kuhusu iyo nguo na anza kutafuta binti mwingine kimya kimya uyo kashaweka doa tayari!
Wewe kweli cute wife.
Je bado wewe ni cute wife??
 
Mkisha maliza kubishana ntarudi,ni bora muendekee kubishana na huyo dada wa kazi mumpe kazi ya kuwaoa maji ya koo
 
Mdada yuko kwenye adolescence, tambua tabia zake akiwa kwenye huo umri.Anataka na jamii hasa rika lake,inataka kumuona kapendeza muda wote.Mwache awe huru,ainjoi wakati wake,kikubwa msihi asijiachie kwa mumeo sana,yawezekana akamla,kwani sifa ya wadada kwenye umri huo,wanafeel kufanyafanya kilamara.
 
Mmeo yupo sahihi sana,, msikilizie alichokuambia....

Msaada ni sadaka,,UKIPEWA USISAHAU NA UKITOA, TOA BILA KUKUMBUKA
huyo sio mwanao ndio maana ana uwezo wa kuamka Asubuhi na kusema mimi kazi basi narudi kwetu... Je ukienda huko kwao utamuelekeza pia wapi pa kuvaa hio nguo..??

Hicho unachofanya ni Kero kwa Dada wa kazi,,,asije akaanza kulipiza kwa Watoto wako kipindi wewe haupo...

Shemeji Yajue ya kuzingatia,, ili uachane na yasiyokuhusu.....

Thank me later.
 
Kweli Kama mama nimeshangaa Sana kwa hizo kauli. Je Mimi makosa yangu ni yapi au ni kweli mtoto ndani ya nyumba hupaswi kumshauri
Kwanini unahisi unamakosa ilihali naona mmeo amekueleza tu kawaida..??? na kwanini umeita mabishano..?? Ulimjibisha mmeo au??

Nakukumbusha tena Beki tatu sio mtoto ndani ya familia,, ni mfanyakazi...(independent person),,kinachomuweka hapo ni huo Mshahara,, hio ni kazi kama kazi zingine...siku na saa yoyote atakayotaka anaweza kuondoka na hakuna lolote mtafanya....

SIJAOA lakini naamini hili sio jambo la wanandoa kubishana
 
Habari waungwana.

Habari ipo hivi. Nyumbani tuna House gal ambaye Kama kawaida husaidia kazi za Nyumbani pamoja na kulea watoto .Sasa wkt anakuja nikagundua Hana nguo za kutokea kwa maana mfano kutokea tukienda mahali au akiumwa au akienda tembelea ndugu ZAKE weekend.

Nilichofanya nikampa nguo yangu moja NZURI ambayo hata Mimi ni zile za kanisani au kwenda sehemu special na pia nikamuongezea na za kushindia kwa maana za Nyumbani Kama anafanyafanya shughuli ndogo ndogo ,lakini wkt Nampa nilimfafanulia na Tena siku iyo nakumbuka alifurahi Sana na ni siku alikuwa anaenda kusalimia ndugu zake ilibidi avue Ile aliyokuwa ameivaa na kuvaa ile niliyompa akisema anashukuru Sana na ameipenda Sana .

Na alipovaa ni Kama alipimwa ilimpendeza Sana. Baada ya Kama wiki nikagundua Ile nguo ameigeuza ya kushindia na NDO anafanyia usafi.Nikamwita nikamwelekeza kwa Nini asivae zile zingine kwa maana Ile uwe Kama nilivyomuelezea.Akaelewa akaivua na kuifua.

Sasa Leo asubuhi naamka nikamkuta ameivaa anaifagilia nje na hata Jana yake aliivaa anamenyea nduzi(nikiongelea hivyo nduzi Zina utonvu na ni nyeupe) Nikamuuliza mbona umerudia kuifubaisha nguo NZURI na nilikuelezea? Nikamwambia vua ntampa hata ndugu yangu atakayeithamini.

Sasa Baba watoto akasema Kwanza Iyo nguo kumpangia masharti aivae vipi umekosea kwa kuwa wakati unampa hakukuomba ulimpa mwenyewe na kanuni ya kumpa mtu kitu chochote ukishampa umempa matumizi ni juu yake hata angeamua kudekia kufanyaje ni yeye maana imekuwa yake.

Kweli Kama mama nimeshangaa Sana kwa hizo kauli. Je Mimi makosa yangu ni yapi au ni kweli mtoto ndani ya nyumba hupaswi kumshauri(Huyo msichana Ana miaka 18 kwenda 19) Na ikumbukwe ni mista huyo huyo aliyenilalamikia kwamba huyo msichana tangia aje anavaa vinguo vyepesi na khanga tu akijua na yeye yupo kwa maana Kama Ana majaribu na akimfananisha na dada mwingine ambaye aliondoka ambavyo hakuwa na majaribu Kama ya huyu wa Sasa kwa maana kujipitisha Mara kajilaza ovyo Yaani Mambo Kama hayo.

(Kwa hayo malalamiko yake nikaongea na Dada nikamshauri jinsi ya kuvaa na hasa azingatie nguo za heshima.Walau akabadirika.
Sasa Leo NDO hayo.

Naombeni maoni na mista atawasoma Mana kajaa tele humu
Unamuona tu maana hajui value ya nguo. Kuna watu hawajui thamani ya vitu. Anaweza kitu cha thamani ndogo akaona ndicho kizuri na cha maana.
Sasa yeye huenda ulizosema za kushindia ndizo anaona kali. Next time mnunulie nguo zinazoendana na taste yake
 
Mr yupo kwenye timing kali sana za kumla huyo mtoto anacheza tu na akili yako!...mfute kazi mara moja kabla hajaliwa aisee!
 
Umesoma vizuri toka mwanzo?kwa Nini Kama ni hivyo huwa watoto wakitoka na nguo kanisani au na nguo special mahali husema vua Kwanza hiyo nguo Na Mimi sijamchukulia Kama mtu Bali au jirani au mtu nisiyekaa Naye na sijawahi mwambia asivae Ila asiifanyie kazi mfano wkt anafagia au wkt anamenya ndizi.Na wkt Nampa nilimwambia hii ya kutokea .

Na SIO hivyo tu nikamuongezea zingine za kufanyia kazi asubuhi kwa maana hata akivaa iyo nguo Nyumbani wkt hafanyi zile kazi za kuifubaza Haina shida.Nikisema kuifanyia kazinunaelewa NDO Mana hata shambani KUNA nguo zake usijifanye hujaelewa
Nguo ni yake, kwani ikifubaa wewe inakuhusu nini shemeji?? Mumeo yupo sahihi mno! Binti ameipenda hiyo nguo ndo mana anatamani aivae kila siku. Mambo ya nguo ya safari na nguo ya kushindia ni mambo ya kishamba ya watu wa mashambani huko.
 
Nimependa Sana ushauri wako ni NZURI
Lkn nimegundua KUNA baadhi ya watu huchangia madam haraka haraka bila kuangalia dhima kuu ya mwandishi.Narudia Tena jamani I wish niipige picha halafu anachoifanyia.Hata wewe ungeumia kwanza ni dharau kwa nguo ya thamani na kwa kuifubaza huko lengo lake lisingekuwepo au Kama msemaji mmoja alivyosema labda mista alimsifia wakiwa wawili Mimi nitajuaje
Acha wivu shemeji
 
Nimekuelewa Ila kwa hapa dear lengo langu nashukuru umenielewa na ni kawaida hata ukitoka kanisani na watoto ukaona wanaendelea kuchezea nguo zile NZURI za kanisani utasikia vua kwanza hiyo.Sijawahi ona mtu akisema amewapangia maana yangu ilikuwa hiyo.Walau asigeuze Kila nguo ya kushindia
Binti wa 19 yrs sio mtoto na hivyo hupaswi kumwambia akavue nguo alotoka nayo kanisani. Atavua mwenyewe akijisikia. Huyo ni mtu mzima.
 
Kijinguo kimoja na malapulapu mawili
😆😆😆
Una anzishiwa uzi jf.
Umaskini huu hauna adabu kbsa,
 
Una Gubu shoga angu,
Kitendo cha kumwambia aivue utampa hata nduguyo ataithamini ni wazi ulimpa ili umsimange yaan haikutoka moyoni,

Huyo Binti hiyo nguo ni wazi kaipenda ndio maana anataka aivae kila mara ila wewe kwa Gubu lako umeona haithamini,

Ushauri wangu mnunulie nguo nyingi zaidi atazoea na kujua ipi ya kushindia ipi ya kutokea.
 
Back
Top Bottom