Lema ukicheza utapoteza Arusha mjini for good

Asante kwa kuleta mada hii, kwa mtazamo wangu kama mkazi wa Arusha na supporter wa CHADEMA. Lema anapoteza umaarufu na umuhimu na hii ni dalili ya kulipoteza jimbo hili 2015. HAjaweza kugusa matumaini ya wapiga kura. Hajawatembelea kusikiliza shida zao, hajui vizuri jiographia ya watu wake hivyo hawezi kujua shida zao na kuzibeba wala kuzizungumzia. Watu wanachangishwa michango ya visima vya maji huku hakuna umeme katika eneo husika lakini hajawahi kulisemea. Ataje amehudhuria mkutano gani la wapiga kura wake kujua kero zake? Madiwani wana mwitikio mzuri kwa wananchi kuliko lema coz wako karibu na wananchi. Si kila malumbano yana tija. Mwalimu Nyerere alicopromise lkn tulipata uhuru

Wacha upuuzi miaka 50 ya upuuzi wa CCM la laghai za amani ndiyo unashadidia KWA KUJIPACHIKA USEMAJI wa watu wa Arusha. Hapa siyo suala la hisia za wana Arusha. Hapa ni issue ya "PRINCIPLE". Taratibu zimekiukwa lazima zisahihishwe si kwa lubuni na kampeni za kutumia ujinga wa watu.

NI AFADHALI KUPOTEZA JIMBO MADIWANI KULIKO KUWA NALO KWA LUBUNI

Mimi kama mwana-arusha ambaye sitaki kusemewa naunga mkono msimamo wa CDM na hao madiwani wapuuzi waondoke
 
Asante kwa kuleta mada hii, kwa mtazamo wangu kama mkazi wa Arusha na supporter wa CHADEMA. Lema anapoteza umaarufu na umuhimu na hii ni dalili ya kulipoteza jimbo hili 2015. HAjaweza kugusa matumaini ya wapiga kura. Hajawatembelea kusikiliza shida zao, hajui vizuri jiographia ya watu wake hivyo hawezi kujua shida zao na kuzibeba wala kuzizungumzia. Watu wanachangishwa michango ya visima vya maji huku hakuna umeme katika eneo husika lakini hajawahi kulisemea. Ataje amehudhuria mkutano gani la wapiga kura wake kujua kero zake? Madiwani wana mwitikio mzuri kwa wananchi kuliko lema coz wako karibu na wananchi. Si kila malumbano yana tija. Mwalimu Nyerere alicopromise lkn tulipata uhuru

Samahani lakini naona hayo ni mawazo duni, nadhani ni mapema mno kumtahmini Lema. Miezi nane tu ya kuwa mbunge unategemea awe ametembelea kila kona. Mawazo hayo yangoje mpaka 2014 ndio uyaseme. Nani mbunge ambaye ameshafanya chochote toka achaguliwe. Hili la madiwani wa Arusha ni lazima lichukuliwe kwa nguvu zote, na watimuliwe tu hata kama itakuwa kwa gharama ya kupoteza hizo kata. CDM ILIPOFIKIA SASA KUFA NI NDOTO NA LAZIMA ICHUKUE DOLA 2015
 
Ndugu zanguni, mtoa mada hii kaeleza jambo la msingi sana. Hebu tujifunze kutoka kwa NCCR- Mageuzi na sasa TLP. Tujifunze kutatua matatizo kwa mtizamo chanya kisha tusonge mbele.
 
Utakua umeongea na wananchi 29 na wewe ni wa 30 mliohudhuria pale ofisi za halmashauri kwa kile mlichokiita tamasha la muafaka ili hali muafaka ni hewa. Watu 30 kujitokeza inadhihirisha wananchi wa arusha hawajaridhika na muafaka hewa na wana imani na Mh Lema.
 
Aisee mwanakwetu umenigusa hasa. Jana nilisikitika sana nilipoangalia TV kumbe hawa madiwani wetu bado hawajaanza kazi. Barabara walizoahidi kutengeneza ziko taabani na ahadi nyingine nyingi bado hata kuanza kuzitendea kazi bado. Wananchi ni kweli tumechoka kusikia magomvi na sasa tunataka kusikia mipango na mikakati ya utekelezaji. La sivyo tutawaweka kiporo hadi 2015 tuashangaze CDM tuwape CUF nao wajaribu.[/QUO

Kama kuna diwani alikuahidi kukujengeeni barabara nanyi mkamchagua basi kuna tatizo la uelewa miongoni mwenu, tangu lini diwani akajenga barabara kama si serikali inayojenga??

Labda uniambie RA ndiye aliwaahidi barabara hapo nitakuelewa, hebu jaribunji kuelewa majukumu ya mbunge badala ya kukurupuka na allegations zisizo na kichwa wala miguu!!
 
Ni vigumu kuelewa wanachofanya CDM Arusha kama wewe si mpambanaji halisi. Mavazi ya CMD yenyewe yanamaanisha ''Man at Work''. Tukubaliane tu mafanikio hayaji bila pain. Hicho ndicho CCM wamekua wakitushinda nacho kila wakati. Mkichagua mpinzani wanabana maendeleo ya eneo husika mpaka mgawanyike/mjutie then next election wanawabeza mlichagua upinzani mlipata nini! Hata hiyo Southern Sudan isingekua nchi kama wangetarajia mafanikio kila baada ya miezi 7 baada ya uchaguzi. CMD wasipokua strong ktk maamuzi dhidi ya wanachama including Madiwani CCM itawarubuni wananchi kirahisi kuwa mnaona mmechagua upinzani na hasara zake? Mbona wao wameongoza majimbo mengi tu toka uhuruna yananuka umaskini wa kutupa
 
Nilijua sitaungwa mkono katika hili na najua historia inaonyesha watu wengi walioleta changes walikuwa very unpopular kwa sababu upeo wao ulikuwa juu ya wengine na kufikiri kwao hakukuwa motivated by ushabiki. Ukitumia hisia badala ya akili lazima comments zako zitakuwa kama ulizotowa. Hata kama ametumwa na kamati kuu yeye ni sehemu ya hao watoa maamuzi. Kama utaendea kutoa utumbo basi wajaribu kuwafukuza wenyewe mtaona ninayo yasema.
Mpaka sasa sijaona official statement ya CHADEMA ,inayoclear doubts zote kuhusu suala hili.Lakini hii haikupi ww sababu tosha ya kujipambanua kama mwenye upeo wa juu kuliko wengine, labda uje na data zinazotosha kuwa prove wrong wengine walioamua kuwa na subira kama ilivyo tokea kwa mambo yaliyopotoshwa kama vile EPA,na ufisadi mwingine ndani ya sisiem,baadae chadema ikaonekana ime simama katika UKWELI!
 
Nazungumza kama supporter mkubwa wa CHADEMA na niliyemchagua Godbless Lema kama mbunge wangu. Niko mjini na niko mobile sana huwa nazunguka katika kata kadhaa za hapa mjini. Wananchi wengi ukiwasikia wanasema lazima waonyeshe support kwa madiwani wao waliowachagua kutokana na uamuzi waliotangaza jana. Mambo ya kamati kuu ya CDM haimsaidii mwananchi wa Kata ya Kimandolu, Sekei, Kaloleni n.k. ambao wanachotaka ni maendeleo na si migogoro ambayo haimaliziki. Wananchi walio wengi including viongozi wa dini wanaunga mkono muafaka na dhamira safi ya madiwani ya kutaka kuendelea mbele katika kuwatumikia wananchi na kuachana na malumbano.

Kutokana na mgogoro huu Lema ameanza si tu kupoteza umaarufu bali hata ushawishi kwa wakazi wa manispaa ya Arusha. Wengi tunaanza kumwona yeye na CHADEMA taifa kama watu wanaotafuta mambo yao binafsi na si kuwatumikia waliowachagua.
Naomba wajue wananchi wamechoka na hakuna mtu yuko tena interested na mvutano ambao siyo tu hauna mwisho bali ambao hauchangii hata asilimia 1% ya maendeleo katika kata zao.
Madiwani wameshikamana na wananchi kuliko Kamati kuu ya CDM inavyofikiri na kama watakosea wakawafukuza hawa madiwani basi wajue wamepoteza jimbo la Arusha kwa sababu watu hawa hawa ndio waliompigia Lema kura na hawatakuwa tayari kumpigia tena 2015.

Watu wanataka iwepo way forward na wasahau ya nyuma tujenge manispaa yetu na siyo kila wakati kutaka kuonyeshana misuli ya kisiasa kana kwamba ndilo lengo kuu la kuingia madarakani.

Please Lema anza kushughulikia malengo makuu ya maendeleo kama mbunge kwa mustakabali wa watu waliokuchagua kinyume na hapo tutakuona uliingia kwenye ubunge kwa personally motivated agenda na si vinginevyo. Kama hautafanya kazi kwa matakwa ya wananchi ndugu yetu hatutakuwa na jinsi zaidi ya kumtafuta mtu atakayeweza kufanya hiyo kazi.

Lastly but not the least namuomba sana Dr. Slaa asiwatishe tishe madiwani tuliowachagua kwani hakuwachagua yeye na hii ni sawa na kututisha sisi tuliowachagua. Dr. Slaa ni mtu mzima na atumie hekima na busara kulishughulikia hili suala haraka iwezekanavyo na kwa manufaa ya wananchi waliowachagua hawa madiwani. Tutaendelea kumheshimu Dr. Slaa kama atatuheshimu na kuelewa wale madiwani wana watu nyuma yao waliowachagua.

Sioni dhambi kukaa meza moja na CCM wakati huko bungeni mko na CCM na mnacheka nao. Sisi tuko nao pia huku mitaani, mahotelini, kwenye mabasi, kwenye nyumba za ibada n.k. Hawa ni wenzetu na tumetofautiana tu itikadi lakini hatuna uadui mkubwa kiasi hicho ambacho Lema anataka kuonyesha hapa Arusha. Ninamuomba Lema akue na aache mambo ya kuonyeshana ubabe ili tujenge nchi yetu kwani safari iliyoko mbele ni ndefu na kazi bado ni kubwa. Nitakuwa na uchungu mkubwa sana kama uzembe wa CDM utalifanya jimbo hili kurudi tena mikononi mwa CCM na mtakuwa mmepoteza sana credibility na support kwa jinsi ambayo itakuwa ngumu ku- reverse.

Mungu Ibariki Tanzania
Nakubaliana na usemayo mwanawane.
Malumbano yasiyoisha hayana faida kamwe.
Mwambie huyo ndugu yako Mr Lema awape maendeleo wananchi waliomchagua kama madiwani wake walivyoamua.
 
Mnaounga mkono hoja hii hamjui siasa. Uchaguzi wa Arusha haukufuata taratibu, hilo ndilo tatizo. Utatuzi wake ni kwamba diwani wa sasa hivi na uongozi wote waachie ngazi, kisha uitishwe uchaguzi wa huru na wa haki. atayeshinda baada ya hapo basi!

Wewe ndio mbumbumbu mkubwa wa siasa. Bora ungekaa kimya.
 
Nawahurumia wale waliopoteza kura zao na kumpa kinda wa kisiasa Lema.
Matokeo yake mmeanza kuyaona. Lakini bado, mtayaona mengine mengi. Tulishasema hapa kuwa shule ni kitu muhimu sana kwa kiongozi. Lema hana hiyo kitu. Akishangiliwa na machalii...kichwa kinavimba, anatoa maamuzi ya kipuuzi.

Very sorry mliompa kura...imekula kwenu.
Now you know!
 
You are dreaming a folitle dream, Lema na mjomba wake Mbowe hawana mbele wala nyuma, mjomba mtu alimpandikiza ili avae magwanda ya mtu fulani hapo kwenu cdm, ila mwipwa mtu kapwata ile mbaya, hahaaa, kwa hiyo kumuongelea lema, 'you are dreaming a folitle dream'
 
Chadema wasipokuwa makini 2015 wanaweza kurudi bungeni si zaidi ya watu sita kutoka majimboni, ambao wanaweza kuwa ni Mzee Ndesamburo kama atagombea, Mbowe kama hatagombea urais, Zitto, Halima Mdee, Mnyika na jembe la ukweli Tundu Lissu.
 
Jamani tunaomba tupate ripoti ya kamati ya Marando ili tujue kilichobainiwa huko otherwise ni porojo tu hapa.Kwa nini Slaa na wenzie wamekuja tu na agizo ukweli uko wapi?.Bila shaka hata hawa wakubwa watakuwa na matatizo tena makubwa katika hili.

Haiwezekani utetezi wa Lema dhidi ya Pinda uliangikwa kwenye website ya Chadema na tukasoma hii inayohusu umma inakuwaje.Hapa sitaki kuwa judgemental katika yote yaani ''wana makosa au hawana makosa''.Wengi mnaotetea kuwa wakubwa hawakushirikishwa hamna uthibitisho zaidi ya kuwaona wakidai hivyo hence ni maneno ya kuambiwa.

Kama ripoti hiyo,itaendelea kuwa confidential basi ni dhahiri madiwani wako right.
 
Jamani tunaomba tupate ripoti ya kamati ya Marando ili tujue kilichobainiwa huko otherwise ni porojo tu hapa.Kwa nini Slaa na wenzie wamekuja tu na agizo ukweli uko wapi?.Bila shaka hata hawa wakubwa watakuwa na matatizo tena makubwa katika hili.

Haiwezekani utetezi wa Lema dhidi ya Pinda uliangikwa kwenye website ya Chadema na tukasoma hii inayohusu umma inakuwaje.Hapa sitaki kuwa judgemental katika yote yaani ''wana makosa au hawana makosa''.Wengi mnaotetea kuwa wakubwa hawakushirikishwa hamna uthibitisho zaidi ya kuwaona wakidai hivyo hence ni maneno ya kuambiwa.

Kama ripoti hiyo,itaendelea kuwa confidential basi ni dhahiri madiwani wako right.

nipe sikio la kushoto nikuume kidogo,
wakubwa wao ni wanafiki sana, juzi juzi tu mzee slaa alikua anaropoka kwenye media kuwa atawafukuza, sasa leo anajing'ata ulimi, hahaa amefullia tu huyu mzee, pinda alisema na membe walisema kuwa uongozi wa cdm umeridhia hayo tena pinda akamtaja mbowe na hakubisha. hizo kamati ni a kuwafumba macho wananchi....ushee........zi kabisa.
 
Jana nimemsika Dr Slaa akiongea na TBC anasema CDM watatoa tamko rasmi siku ya Ijumaa, na ukimsikia naibu meya wa CDM anavyosema utaona kabisa kuna mvutano mkubwa ndani ya CDM sujui mwisho wake utakuaje!
 
Muafaka kati ya ccm na magwanda ni kwa maendeleo ya watu wa arusha mjini na kata zake sasa mambo ya kamati kuu ya nini imagine ungekuwa hai karatu au kwa lisu hayo mambo madiwani pekee wanaweza kutatua hata bila kumshirikisha huyo lema wa kishumundu sijui ni uru tokea awe mbunge arusha vurugu tupu je wakichukua nchi je si ndo kabisaaaaa any way amebakiza miaka minne sijui atarudi kuwaambia nini wananchi atajivunia toka amechaguliwa migogoro ameongeza jijini arusha ina boa sasa tunataka maendeleo kama vipi municipal iendeshwe na tume tumechoka hatutaki migogoro siye
 
Siungi mkono hoja, hakuna mtu anashida na muafa. Makao makuu ya CDM yanasema ni batili sasa wewe unayefikiri hao madiwani ni popular kuliko chama unajidanganya. Arusha sehemu gani ulifanyia analysis yako ?????????? mimi niko Arusha pia bado wananchi hawautambui muafa.

Pia viongozi wetu wanasema kama ccm wanaongoza manispaa basi waongoze na CDM wawe wapinzania. Kama CDM wanatakiwa kuongoza basi ccm wapinzani. Kwa kifupi ni kwamba hakuna kushea madaraka Malah na wenzako mjue hilo!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mnaong'ang'ania muafa wa Arusha mna maslahi binafsi. Manispaa ya Arusha imeoza inatakiwa ishughulikiwe ipasavyo lakini si kwa kushea madaraka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom